Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 38,399
- 47,802
Dhana ya makabila na ukabila huwa inafanyiwa upotoshaji kwa makusudi au kukosa uelewa hasa na wanasiasa kwamba watu kutambuana kwa makabila yao, kusemwa kwa makabila yao na kufurahiwa kwa makabila yao ni makosa makubwa au dhambi.
Huu ni upotoshaji mbaya sana, kote duniani kuna nchi nyingi tu watu wanatambuana, wanasemwa au kufurahiana kwa makabila yao au nasaba zao bila ubaguzi wowote. Ubaguzi ndio jambo baya, watu kutambuana kwa tofauti zao za makabila au nasaba sio jambo baya.
Hapa Tanzania Polisi kabila ni mojawapo ya utambulisho wa mtu, watu wamekuwa wakitaniana kwa makabila yao kwa muda mrefu tu bila shida yoyote.
Ubaguzi kwa misingi ya ukabila, siasa, dini, rangi n.k ndio jambo baya.
Mtu anaweza kujivunia kabila lake bila kuwa mbaguzi, mtu kujivunia kabila lake hakumfanyi kutokuwa Mtanzania mzalendo. Mtu anaposema yule Msukua, Mnyakyusa, Mchaga au Mzaramo ni tajiri sana hajafanya ubaguzi, pia akisema ni mkatili sana hajafanya ubaguzi pia, tuachane na upotoshaji na "petty issues".