Kufungua pharmacy

chicharito 97

Member
Feb 11, 2024
6
2
Ndugu zangu habari,mwezi wa 4 nitafungua pharmacy kwa mtaji wa kama mil 30,kuhusu location am sure nitaipata nzuri hofu yangu kubwa ni kwamba mimi kazi yangu ni ya kusafiri safiri sana.

Nilitaka kujua je ninaweza kufungua halafu ni control duka langu kwa kutumia camera ntakazofunga dukani mke wangu angeweza kulisimamia lakini naye yupo bize na kazi zake ni muajiriwa serikalini

Naombeni ushauri ndugu zangu kama itawezekana kufanya ivo navofikiria ama sivyo mnisaidie hata kwa ushauri nifanye nini ili koboresha na ku control biashara yangu hiyo tarajiwa

Mwenye wazo karibu kwa ushauri,kwa wale wanaomiliki biashara hii msiniache tafadhali ndoto yangu ikafa

Mnishauri nawaombeni
 
Mwanzon unalazimika kuwa karibu na biashara yako, baadae ndio unakuwa free kuzurula
 
Tatizo maboss mnawaza kukaba hadi penalty, sisi tutakula wapi?
Ajiri wataalamu na mifumo ya biashara wasimamie, wataiba na wewe utapata.... sio mambo ya kuweka mkeo sijui ndugu wasio na sifa.
 
Tafuta ndugu au mtu unayemfahamu akawe mkusanya maokoto yaan (cashier) wa mauzohapo hautaibiwa
 
Tengeneza mfumo mzuri tu; ndio maana kwenye taasisi kuna wakaguzi n.k; si lazima kila biashara uwepo wewe; muhimu tengeneza mfumo wako.
 
naombani ushauri ndugu zangu kuna binti nimekuwa naye kwenye mahusiano miaka 3,nikawajulisha nyumbani wakamkubali na tukapanga tarehe ya kwenda kulipa mahari,lakini cha kushangaza wazazi wamebadilika hawamtaki tena binti kisa dini,kuhusu dini binti alikubali kubadili dini kunifuata familia imeshaanza dalili zote za kunitenga baada ya kuonesha msimamo wangu wakubakia na binti,na sijamueleza binti chochote kuhusu yanayoendelea kwenye familia yangu,naombeni ushauri ndugu zangu kuhusu hili linanichanganya sana,kwani hata kwenda kutoa mahari wamekataa
 
Embu maliza kwanza haya mambo ya mwanamke ndo ufungue biashara. Alafu vipi umepagawa mbona thread mbilo ndani ya thread moja?
 
Back
Top Bottom