Kufanya kazi TAMISEMI shida tupu, kila ukilala unaota uko jela

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,712
36,171
TAMISEMI aidha uwe muadilifu wa kiwango cha SGR ili ustaafu salama au uwe na tamaa za kula vizuri, kupata usafiri bora na kupeleka watoto private school ili uishie jela.

TAMISEMI hata ukiiba elfu 50 jiandae kufukuzwa kazi au kufungwa.

TAMISEMI ukifanya kazi kuwa makini, unaweza kuingizwa mkenge na wahuni bila kujua dakika yoyote.

TAMISEMI kuna mabosi wengi na kila bosi ni spy mnoko . Yaani wa juu kazi yake kubwa ni ku mzoom wa chini Ili ampeleke jela.

Serikali boresheni maslahi ya watumishi wa TAMISEMI, wana hali ngumu sana.

Rafiki yangu yuko huko TAMISEMI kasimamishwa kazi kwa vikesi uchwara hajui afanye nini.
 
TAMISEMI aidha uwe muadilifu wa kiwango cha SGR Ili ustaafu salama au tamaa za kula vizuri, kupata usafiri bora na kupeleka watoto private school zikupande uishie jela...
kuna mshikaji wangu yupo TAMISEMI,,ameniomba nimtrain kunywa MNAZI manake asilimia 75 ya kamshahara kake kanaishia kulipa madeni ya MASANGA bar!

{ingawa alikuwa akinisema sana niachane na pombe ya mnazi kwani imenifanya niwe na nywele kama rafiki yangu PREMJI wa pale kisutu!

Pia kaniomba nimpeleke ninaponunua viwalo vya bei chee,shati buku,,,nafikiria kumpeleka pale KARUME kwa mshakaji wangu RAMA MAPENSI

Maisha ni rahisi na mepesi sana kama na wewe ukijifanya mwepesi,ukiwa mzito utazama lakini ukiwa mwepesi unakuwa kama BOYA yaani unaogelea tu!!!!!!
 
TAMISEMI huku kumejaa uchawi,kusemana na kuingizana mkenge
Hivi ukisema Tamisemi unazungumzia Wizarani au Kwenye halmshauri au manispaa au mahospitalin maan kwa navyojua Tamisemi ndo wizara yenye ukubwa sana maana ofisi nyingi ziko chini yake.
Sasa wapi kwenye shida na wapi kwenye afadhali, iwe mashuleni huko, kwenye maofisi ya kata huko
 
Hivi ukisema Tamisemi unazungumzia Wizarani au Kwenye halmshauri au manispaa au mahospitalin maan kwa navyojua Tamisemi ndo wizara yenye ukubwa sana maana ofisi nyingi ziko chini yake. Sasa wapi kwenye shida na wapi kwenye afadhali, iwe mashuleni huko, kwenye maofisi ya kata huko
Tamisemi ni Halmashauri kimsingi. Ambapo kuna idara za afya, mahospitalini, Elimu ni shule zote, mifugo na kilimo maafisa kilimo na mifugo na uvuvi si unasikia Ulega juzi kala kichwa Kigoma huko.

Maafisa mendeleo wote kuanzia katani, maafisa afya, maafisa biashara na idara zote za pale makao makuu ya halmashauri zote za Wilaya na Town Councils nchi nzima. Imagine zilivyo nyingi na upuuzi wanaofanya.
 
TAMISEMI aidha uwe muadilifu wa kiwango cha SGR Ili ustaafu salama au tamaa za kula vizuri, kupata usafiri bora na kupeleka watoto private school zikupande uishie jela.

TAMISEMI hata ukiiba elfu 50 jiandae kufukuzwa kazi au kufungwa.

TAMISEMI ukifanya kazi kuwa makini, unaweza kuingizwa mkenge bila kujua dk yoyote.

TAMISEMI kuna kuna mabosi wengi na kila bosi ni spy . Yaani wa juu kazi yake kubwa ni ku mzoom wa chini Ili ampeleke jela.

Serikali boresheni maslahi ya watumishi wa TAMISEMI, wana hali ngumu sana.

Rafiki yangu yuko huko TAMISEMI kasimamishwa kazi kwa vikesi uchwara hajui afanye nini.
Ni mungu tu atupiganie mpaka mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kitongoji ni boss wako na anakufanya atakalo, aisee hii nchi ngumu sana, ni kudra za mungu tu.
 
Kufanya kazi halmashauri inabidi uwe na roho ngumu sana na ujitoe akili kama wafuasi wa ccm
Hakuna sehemu zenye wachawi, wanafiki, watu wa roho mbaya, kijicho, husda, fitina kama watu wa halmashahuri, ndio maana nyuso zao zimekosa nuru kwa unafiki na uchawi, kufanya kazi tamisemi ni sawa na kujivisha boom muda wowote linaweza kukulipikia, huku ndio wanasiasa wanapotafutia umaarufu, utasikia daktari fulani tumemfukuza kzazi, mara mwalimu mkuu tumemfukuza kwa kuimba wimbo wa zuchu n.k.....mambo ni mengi...
 
Changamoto ya kazi nyingi hasa hizi ambazo njaa nyingi ni mifumo uchwara ambayo unakuta imeundwa ili kumnufaisha fulani na chawa wake

Kwa hiyo unakuta kila ofisi ina kigenge fulani ambacho bosi na baadhi ya wafuasi wake wamejiundia kamfumo, hapo ndio watajipangia fursa na ulaji kisha walio nje ni kalenda na kupishana na maokoto

Hapo hata kama wanafanya ndivyo sivyo usithubutu kuhoji au kuwakosoa, watatumia kila nyenzo utolewe ndani ya mchezo

Ukiwa kwenye ofisi fulani ridhika na mshahara na nafasi uliyonayo, ukiwaza cheo, posho, marupurupu, vikao, semina na safari utapata ugonjwa wa moyo maana kuvipata lazima uwe chawa kichizi na kujipendekeza kupitiliza kitu ambacho wenye kujielewa wengi hawawezi kufanya.
 
Ehehhehe
 
Back
Top Bottom