Kufahamiana [JF Identities] - Faida na Hasara [?]

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,076
2,445
Well:: Well:: Well::

Kumekuwepo na ongezeko kubwa sana la wana-JF kufahamiana "kiuhalisia" kadri siku zinavyokwenda...

Kiuhalisia namaanisha - kwa majina halisi na kupeana namba za simu na hata kufika mahali pa makazi yao...

Ni jambo jema kama lina nia njema ... Sitaki kulinganisha JF na Facebook lakini zidhani kama inafaa ziwiane par se! ...

Sina tatizo la watu kuwa na mahusiano ya kijamii, lakini, ninaposoma "posts" za "new members" inanipa wasiwasi kuwa kuna uwezekanao wa kuwepo "negative consequences" pale "members" wanapofahamiana "kiuhalisia" halafu wakatofautiana in one way or another!

Heri ya Mwaka Mpya kwa wote wenye "mapenzi mema"
 
Hhmm binafsi sioni tatizo, labda kama hao watu wamezoea na wanapenda kuuungwa mkono na kusifiwa tu.

Mimi nnaowafahamu tunapingana kwa hoja jamvini na bado urafiki unaendelea. Hamna haja ya kumbadilikia mtu kisa mmetofautiana hoja.
 
Baba Enock hata hao wanaofahamiana sidhani iwe ndio kisa cha kutoleana matusi au kutukanana kisa unamfahamu mtu
Kumfaham unaweza umfaham na ikaishia hapo na hapa mnapotezeana kama hamfahamiani
Kuna trend ya watu wanaingia na wanataka wapate ile attention ya wengi humu wanaanzisha mambo yao ya ajabu ambayo sio ya kistaarabu
Kufalhamiana kupo na unamfaham mtu na inaishia huko huko mtaani na hapa tunaingia na kujibizana kama hatufahamiani
Heri ya mwaka mpya mkuu
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hhmm binafsi sioni tatizo, labda kama hao watu wamezoea na wanapenda kuuungwa mkono na kusifiwa tu.

Mimi nnaowafahamu tunapingana kwa hoja jamvini na bado urafiki unaendelea. Hamna haja ya kumbadilikia mtu kisa mmetofautiana hoja.

Ngoja tufahamiane halafu unijie na GX. Lazima nikuanzishie uzi tuu.
 
.. Hiyo ndio social networking..safari moja huanzisha nyingine,new member atashangaa mwanzoni tu kuwa kwanini huyu kamzoea sana yule but akishapazoea jamvini ataelewa tu kisa na maana..
 
Baba Eno, mtu akiamua kukuchafua au kukufanyia mbovu muonane msionane hilo lawezekana!
Mioyo inaficha mengi sana na siku ikifunguka kuna watu watazimia kama si kufa kabisa.
Muujiza ulishawahi kunitokea mimi, heri yangu...
 
Hadi ufahamiane na mtu kiuhalisia inabidi umwamini mtu huyo
Bila kuwa na uaminifu kati ya hao wanaofahamiana
Wanaweza dhuriana bada hasa wakitofautiana

Ni kuwa makini tu na type ya mtu unayepanga kukutana naye.
 
So far kwangu mimi niliofahamiana nao hapa JF nimepata faida nyingi sana hao tunaofahamiana nao wanazijua hizo faida na bado tunaendelea kubishana na kupingana humu humu JF kila siku na hata tukiwa nje ya JF tunabishana na kuwa na healthy arguments na maisha yanaendelea bila kuwapo hard feelings..
 
Baba Eno, mtu akiamua kukuchafua au kukufanyia mbovu muonane msionane hilo lawezekana!
Mioyo inaficha mengi sana na siku ikifunguka kuna watu watazimia kama si kufa kabisa.
Muujiza ulishawahi kunitokea mimi, heri yangu...
Kweli kabisa... Haya na wewe ulitokewa na muujiza gani? Nataka nijifunze kupitia kwako.
 
Kweli kabisa... Haya na wewe ulitokewa na muujiza gani? Nataka nijifunze kupitia kwako.
Hehehee muone...
Muombe Bikira maria akutokee kama wale wakina Lucia wa Lurdi!
Just one general advice from your homegirl...'be careful'
 
tatizo la watu wehu sio tu kukutana nao na kufahamiana nao

humu kuna watu wameshaanzisha thread juu ya mtu ambae hawajawahi kukutana nae
na hawamjui.....

wengine obssession zao kwa mtu zinawatuma tu kuandika chochote wanachokihisi....
 
So far kwangu mimi niliofahamiana nao hapa JF nimepata faida nyingi sana hao tunaofahamiana nao wanazijua hizo faida na bado tunaendelea kubishana na kupingana humu humu JF kila siku na hata tukiwa nje ya JF tunabishana na kuwa na healthy arguments na maisha yanaendelea bila kuwapo hard feelings..

Na hii ndio spirit ya kumfahamu mtu maana mnafahamiana mnajenga urafiki na unapata faida kutokana na urafiki huo
Sio biashara ya kuja kujibizana na kupeana matusi
Na mkikutana humu ndani mnabishana kiungwana na kumaliza mambo yenu hata kama hamjuani
Na wengine ninaowafahamu hapa najibizana nao kama hatujuani ila ni healthy arguments za kujenga na sio kubomoa
 
tatizo la watu wehu sio tu kukutana nao na kufahamiana nao

humu kuna watu wameshaanzisha thread juu ya mtu ambae hawajawahi kukutana nae
na hawamjui.....

wengine obssession zao kwa mtu zinawatuma tu kuandika chochote wanachokihisi....

Labda wanajiunga na JF wakidhani labda is primarily a dating site?
 
Back
Top Bottom