Kuendesha biashara yako mwenyewe ni kazi ngumu sana

The River

Senior Member
Dec 27, 2015
127
83
Wasalaamu wadau,, nimekuwa kila nikianzisha biashara sitoboi kabisa,..kwa mfano nilikuwa namiliki saloon yangu ya kiume lakini cha ajabu sipati wateja,..yaani unaweza kukaa kutwa nzima ukaambulia vichwa viwili tu,,,siku nikipata wengi ni watatu mwisho,..

Vivyo hivyo hata biashara zingine nilizowahi kuanzisha kama vile kuuza nguo na mahindi,...je mimi nakosea wapi wadau? au wengine huwa munafanyeje?

Karibuni kwa ushauri maana hapa nahisi kushindwa,. sijui bora kuajiliwa tu,..daah
 
Usijali Mkuu
Pambana sana,Mungu ni mwema atakufanikisha
Kuna siku thread kama hii ilichachamaa sana hapa jukwani! wengi walielezea either uwe mtu wa Mungu sana! au Nguvu za giza na ideas nyingine tofauti tofauti..
Kwa msaada na thread yenyewe hii hapa
 
Ahsante kwa knitia moyo,. lakini inavunja moyo sana
Mkuu pambana.
Jaribu kuangalia site unayofanyia biashara zako.
Pia competition from your colleagues.
Usikate tamaa pambana.
All the best
Ahsante kwa kunitia moyo lakini inakatisha tamaa sana mkuu
 
wasalaamu wadau,, nimekuwa kila nikianzisha biashara sitoboi kabisa,..kwa mfano nilikuwa namiliki saloon yangu ya kiume lakini cha ajabu sipati wateja,..yaani unaweza kukaa kutwa nzima ukaambulia vichwa viwili tu,,,siku nikipata wengi ni watatu mwisho,.. vivyo hivyo hata biashara zingine nilizowahi kuanzisha kama vile kuuza nguo na mahindi,...je mimi nakosea wapi wadau? au wengine huwa munafanyeje? karibuni kwa ushauri maana hapa nahisi kushindwa,. sijui bora kuajiliwa tu,..daah
Mwanzo mgumu mkuu
 
Badili style unayotumia
Pia aangalie location,,ukishakosea location,biashara itakufa ama itadumaa,kwasababu hakuna mzunguko wa pesa,
Pia customer care ni muhimu sana,jinsi unavyohudumia,,ajitahidi kwa siku awin japo mteja mmoja,,
Yaani kumfanya awe royal kwake na avuke mitaa mingi kufuata huduma yake..
 
wasalaamu wadau,, nimekuwa kila nikianzisha biashara sitoboi kabisa,..kwa mfano nilikuwa namiliki saloon yangu ya kiume lakini cha ajabu sipati wateja,..yaani unaweza kukaa kutwa nzima ukaambulia vichwa viwili tu,,,siku nikipata wengi ni watatu mwisho,.. vivyo hivyo hata biashara zingine nilizowahi kuanzisha kama vile kuuza nguo na mahindi,...je mimi nakosea wapi wadau? au wengine huwa munafanyeje? karibuni kwa ushauri maana hapa nahisi kushindwa,. sijui bora kuajiliwa tu,..daah
mkuu kwanza hongera sana kwa mpambano!
#pili nikushauri yafuatayo
mosi kaa chini jitathmini wewe kama wewe wapi unakosea, zungumza na majiran na wateja wako hapo ulipo juu ya huduma unayotoa, angalia eneo unapofanyia hiyo biashara,tizama mienendo yako mwenyewe means kauli zako kwa wateja zikoje,,tizama mazingira ya ufanyaji kazi yako yanavutia wateja kwa kulinganisha na washindani wako!,angalia bei zako na huduma zako,,tizama marafiki zako maeneo hayo ulipo(ikibidi jenga urafiki na watu unaohisi ndo wateja wako) ikibidi mda mwingine wape offer moja moja na wasikilize shida zao..kiufupi zipo factor nyingi mno kwenye kuendesha biashara na inategemea na biashara yenyewe kwangu mimi hakuna kazi nina yo enjoy kama kuendesha biashara yangu japokua kuna muda napitia magumu mno ila uvumilivu ndo kitu cha msingi na maamuzi magumu kwa wakati sahihi
kwangu mimi nina miaka mitatu kwenye biashara ila cjawahi badilisha biashara ila sijawahi badili aina ya biashara na had napokueleza biashara ndo kwanza nimeanza kuona matunda ya uvumilivu
 
Mkuu hiyo hali inatokea watu wengi hasa wanaonza biashara kuumbuka hiyo biashara unayofanya wapo wengi wanaifanya pia so hapo ni kitendo cha kubadili mawazo ya wateja waje kwako wasiende kwa wengine na kuwatafta wapya na hiyo ndio kazi zenyewe wala usifkirie eti sjui mikosi hamna iyo skushauri ufkirie kuajiriwa kwan maana yake umeshindwa kujismamia wataka ukasimamiwe pambana mkuu utatoboa
 
ahsante mkuu kwa ushauri wako
 
nas

nashukuru sana kuna umenisaidia mkuu
 
Mkuu komaa usikate tamaa. Mimi ninapofanyia biashara frame ya pembeni yangu alifungua mtu biashara kama yangu, kodi ilivyoisha akafunga biashara. Same fremu kafungua mwingine nae anasema akimaliza kodi harudi.

Kama sio kukomaa ningeshafunga biashara kitambo kabisa. Imagine wenzio wanakuja wanakata tamaa ila sio kwamba kuna siku sikosi. Nakosa lakini naamini kwenye kupata na kukosa kwamba sio kila siku nitapata tu.

Komaa mkuu. Biashara inayoanza ngumu sana. Nina mwaka now ila bado naona kama nimeanza jana biashara ila sikati tamaa kuona haikua kama nilivyodhani itakua ndani ya muda niliodhani mimi biashara itakua.

Nina rafiki yangu anabiashara ya mihogo. Anasema yeye ilimchukua miaka mitatu kusimama vizuri.

Mimi nikiwaza ndo kwanza mwaka nasema bado nina muda wa kusimama vizuri
 
Mchawi ni location akisindikizwa na rafki yake ajulikanaye kama ubora wa huduma unazotoa , narudia tena mchawi ni location.....ukikosea location wafaaaaaaaaaaa no mercy and no compromise....!!! Yaan hyo factor inastand alone haihtaji mbwembwe za kusali ama kuroga ......
 
Mkuu hiyo hali inatokea watu wengi hasa wanaonza biashara kuumbuka hiyo biashara unayofanya wapo wengi wanaifanya pia so hapo ni kitendo cha kubadili mawazo ya wateja waje kwako wasiende kwa wengine na kuwatafta wapya na hiyo ndio kazi zenyewe wala usifkirie eti sjui mikosi hamna iyo skushauri ufkirie kuajiriwa kwan maana yake umeshindwa kujismamia wataka ukasimamiwe pambana mkuu utatoboa
Mkuu ni kweli ulichosema!
Ila cha kujiuliza kwa mfano location za mjini kuna kujuana??
Kule nina imani kuna watu tofauti tofauti..Lakini Mr X ana msururu wa wateja hadi kero chanzo haswa ni nini???

Asilimia kubwa sana ya wafanyabiashara wanatumia nguvu za giza/Mungu/ ni nyota ya Mtu.
 
Mchawi ni location akisindikizwa na rafki yake ajulikanaye kama ubora wa huduma unazotoa , narudia tena mchawi ni location.....ukikosea location wafaaaaaaaaaaa no mercy and no compromise....!!! Yaan hyo factor inastand alone haihtaji mbwembwe za kusali ama kuroga ......
Mkuu ujaficha kitu
 
Mkuu ni kweli ulichosema!
Ila cha kujiuliza kwa mfano location za mjini kuna kujuana??
Kule nina imani kuna watu tofauti tofauti..Lakini Mr X ana msururu wa wateja hadi kero chanzo haswa ni nini???

Asilimia kubwa sana ya wafanyabiashara wanatumia nguvu za giza/Mungu/ ni nyota ya Mtu.
Connection zipo kila sehemu mkuu.
 
BIASHARA ya salon.....
Mambo ya msingi ya kuzingatia
Kama upo uswahilini....usiirembe Sana salon yako...wabongo wakiona umeremba Sanaa wanakimbia kwa kujua bei ni kubwa.

Shusha bei,kama wenzio wananyoa buku jero,wewe nyoa buku,

Wahi kufungua...... Chelewa kufunga.

Customer care nu muhimu....

Kinyozi akimyoa MTU asimuondoe haraka haraka,labda kuwe na vichwa nje....mteja akimaa mda mtefu akinyolewa ndio anaamini kuwa jamaa amenyoa vizuri...Ila faster faster anahisi amelipuliwa

Kinyozi awe na uongo Fulani wenye faida, mfano kuna Saloni moja hivii,kila MTU akimyoa utamkuta anasema" hivi nywele zako kwa jinsi zilivyo angekuwa kinyozi wasiwasi...lazima akunyoe vibaya....maana kinasehemu zimekaa vibaya ...inamaana anamuaminisha kuwa yeye ndio Bora ,hivyo asiende kwingine.....kumbe anamjazaa tuu.

Piaa kinyozi awe mpiga Stori Sanaa na watejaa,mteja akija anapiga stor Sana za siasa na zinginee,basi jamaa anajikuta kesho analud hapo hapoo.

Piaa kinyozi MTU akija kunyoa basi amnyoe na ndevu kwa pesa yake ile ile.

Huu ndio ushauri wangu.....japo napata kvant hapa,Sasa siajua NI ushaur wangu au NI akiri za kvant.
 
Back
Top Bottom