Kuendesha biashara yako mwenyewe ni kazi ngumu sana

Endelea kupambana usikate tamaa.
Kuwa mbunifu, pia sio mbaya ukaongeza huduma nyingine ambayo haitoathiri shughuli za unyoaji.
 
Kwanza sehemu ya kufanyia biashara pia UBORA wa huduma, tatu usilazimishe faida kubwa


Ucheshi kwa wateja na mbinu za kuwaweka kuwa wakudumu
 
Fanya SWOT analysis ikusaidie kujua unakwama wapi. Kama huwezi tafuta mtu anayefahamu akuongoze. Bila hii utakuwa unakomaa kama ntu anayekomaa chumba chenye giza akimsaka paka mweusi ambaye hayupo!
 
Mkuu fanya hivi

Jitafakari kwa kina sana(mf. Wewe ni nani unamadhaifu yapi unanguvu gani).

Njoo jiangalie ni wapi unafanya vizuri ufanyapo jambo mpka watu wanasema yes. Iangalie familia yako/yenu (baba mama dada kaka wadogo zako wajomba baba wakubwa kwa wadogo mama wakubwa kwa wadogo shangazi) wamefanikiwa kwenye upande upi? KUAJIRIWA AU KUJIAJIRI? Utapata jibu. Amini sio kila mtu ni wa biashara sio kila mtu wa kujiajiri na kinyumeche.

NYONGEZA;
Usisukumwe na peer pressure usione umri unasogea bila mafanikio usione marika wamefanikiwa nawe haufanikiwi haya huwaongoza vijana wengi kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Nikuambie tu kuna mahusiano madooooogo sana kati ya UMRI & MAFANIKIO.

Kila la kheri mkuu
 
BIASHARA ya salon.....
Mambo ya msingi ya kuzingatia
Kama upo uswahilini....usiirembe Sana salon yako...wabongo wakiona umeremba Sanaa wanakimbia kwa kujua bei ni kubwa.

Shusha bei,kama wenzio wananyoa buku jero,wewe nyoa buku,

Wahi kufungua...... Chelewa kufunga.

Customer care nu muhimu....

Kinyozi akimyoa MTU asimuondoe haraka haraka,labda kuwe na vichwa nje....mteja akimaa mda mtefu akinyolewa ndio anaamini kuwa jamaa amenyoa vizuri...Ila faster faster anahisi amelipuliwa

Kinyozi awe na uongo Fulani wenye faida, mfano kuna Saloni moja hivii,kila MTU akimyoa utamkuta anasema" hivi nywele zako kwa jinsi zilivyo angekuwa kinyozi wasiwasi...lazima akunyoe vibaya....maana kinasehemu zimekaa vibaya ...inamaana anamuaminisha kuwa yeye ndio Bora ,hivyo asiende kwingine.....kumbe anamjazaa tuu.

Piaa kinyozi awe mpiga Stori Sanaa na watejaa,mteja akija anapiga stor Sana za siasa na zinginee,basi jamaa anajikuta kesho analud hapo hapoo.

Piaa kinyozi MTU akija kunyoa basi amnyoe na ndevu kwa pesa yake ile ile.

Huu ndio ushauri wangu.....japo napata kvant hapa,Sasa siajua NI ushaur wangu au NI akiri za kvant.
Nmekusoma mkuu, uko sawa kabisa.!
 
Usikate tamaaa...watu wengi wanapitia kama hali yako......Fanya tathimini kama wakuu wanavyokushauri huko juu...Muombe mungu sana pia...
 
Vitu ninavyozingatia kama mteja kwanza ni usafi wa salon yenyewe, sterilizer, ubora wa mashine, after shelv liquor, uwezo wa kinyozi. Nikipata hivyo vyote basi huwa
Nanyoa salon moja, kinyozi yule yule na kama anamyoa mtu mwingine nitamsubiri amalize na kama hayupo nipo radhi niahirishe. Nikikaa kwenye kiti sina haja ya kumuelekeza nanyoaje ni story mwanzo mwisho yani anaanza mtoto huyu, yule wa pale unamuonaje bro aah yule fresh.. poa bro nakusawazishia au yule ni grid au kama kuna pisi naielewa nampa kazi kwakweli hawajawahi kuniangusha.
Kutokana na mazoea haya akihama salon huwa wananiambia bro nimehamia mahali fulani na mimi nawafuata huko kuwaunga mkono. Soma kwa makini nilichokiandika
 
wasalaamu wadau,, nimekuwa kila nikianzisha biashara sitoboi kabisa,..kwa mfano nilikuwa namiliki saloon yangu ya kiume lakini cha ajabu sipati wateja,..yaani unaweza kukaa kutwa nzima ukaambulia vichwa viwili tu,,,siku nikipata wengi ni watatu mwisho,.. vivyo hivyo hata biashara zingine nilizowahi kuanzisha kama vile kuuza nguo na mahindi,...je mimi nakosea wapi wadau? au wengine huwa munafanyeje? karibuni kwa ushauri maana hapa nahisi kushindwa,. sijui bora kuajiliwa tu,..daah
Location, convicing power
 
Utafiti ...Mtaji.... Location....Bidhaa....Bei... customer care....hapo wewe ni kupiga pesa tu.
 
Mchawi ni location akisindikizwa na rafki yake ajulikanaye kama ubora wa huduma unazotoa , narudia tena mchawi ni location.....ukikosea location wafaaaaaaaaaaa no mercy and no compromise....!!! Yaan hyo factor inastand alone haihtaji mbwembwe za kusali ama kuroga ......
Nakazia hapa
 
Back
Top Bottom