Elections 2010 Kuelekea uchaguzi mkuu.... SAUT FM yafungiwa....!

katika uchambuzi wa magezeti leo Asubuhi wanasema REdio SAUTI imefungiwa kwa sababu frequency zake zinaingilianana na za mawasiliano ya ndege kwa hiyo wameagizwa kununua kifaa maalumu kwa ajili ya kuzuia tatizo hilo, inasemekana kifaa walichoagizwa kununua hakuna redio yoyote ya FM Tanzania mambayo inakitumia
 
Hii ni Redio ya chuo na huwa wanatangaza mambo mbalimbali ya kijamii na ni zaidi ya kufundishia. Nasikia eti imejiingiza kwenye siasa. Masha atakuwa nyuma ya yote haya. Mbona haijafungiwa kwa kuongelea mambo ya dini au mahusiano ya vijana? CCM at work!
 
CCM ni balaa. Wanaweza kuifungia JF wakidai inaingiliana na mawimbi ya mawasiliano ya ikulu. Yaani hadi wataalam wetu wanasababishwa kuongea mambo ya kipuuzi yanayodhalilisha taaluma zao. Kwa nini wasijiuzulu watafute kazi nyigine kuliko kukubali CCM idhalilishe taaluma zao????
 
Eti kuna ukweli wowote kuhusu habari kwamba kuna wachapishaji wanaochapisha karatasi za kupigia kura ambazo zimeandaliwa kwa namna ambayo zenyewe humchangua yule ambaye wachapishaji karatasi hizo wameambiwa zimchangue? Na kwamba ukimpigia mgombea unayemtaka bado karatasi hiyo ina uwezo wa kumkataa na kumchagua yule usiyemtaka ?

Na, je, CCM haioni inachezea fedha za umma kwa kuwa na kitu kama redio Uhuru na gazeti la Uhuru? Redio hiyo inajipaka matope kwa kiasi ambacho karibu wasikilizaji wote wamekimbia labda wanaCCM wasiojua kuchuja kati ya nafaka safi na chuya au pumba. Na gazeti ambalo watu wanalazimishwa kununua huku fika wahariri wake wakijua kuwa wanavunja miiko na maadili ya uandishi lakini kwa kuwa wanategemea kuwa wakuu wa Wilaya na Mkoa wanalazimika kuandika uongo na uzushi na kupotosha kile kinachosemwa na wanasiasa wasiokuwa wanasiasa wa CCM.

aklili
 
katika uchambuzi wa magezeti leo Asubuhi wanasema REdio SAUTI imefungiwa kwa sababu frequency zake zinaingilianana na za mawasiliano ya ndege kwa hiyo wameagizwa kununua kifaa maalumu kwa ajili ya kuzuia tatizo hilo, inasemekana kifaa walichoagizwa kununua hakuna redio yoyote ya FM Tanzania mambayo inakitumia
UNARETA MCHEZO NA SISIEM MURA!:mad2:
 
Radio ya SAUT imefungwa eti kwa sababu walikua wanawasema mno CCM kwa ukweli kuhusu ufisadi unaoendelea? Mbona radio ya chama inapewa hio ruksa pamoja na Clouds FM?

Alafu Baregu (campaign chairman CHADEMA) si anafundisha kwenye hio shule? Yani mengi yatafanyika kipindi hii ya uchaguzi.
 
Alafu eti Mhariri ni wa chama upinzani. Sijui lipi lakini nimeambiwa kwamba walikua wanaongea sana juu ya siasa. Alafu kumbuka kwamba Mwesiga Baregu (Campaign Chairman CHADEMA) ni Professor pale.
 
Nimejaribu kupata habari hii kwenye Nipashe (online version) bila mafanikio, ningependa kuipata habari hii kwa undani naomba mdau aliye na Nipashe ya leo atuwekee sisi ambao tuko nje ya nchi ili tuweze kuchangia mada
 
Radio ya SAUT imefungwa eti kwa sababu walikua wanawasema mno CCM kwa ukweli kuhusu ufisadi unaoendelea? Mbona radio ya chama inapewa hio ruksa pamoja na Clouds FM?

Alafu Baregu (campaign chairman CHADEMA) si anafundisha kwenye hio shule? Yani mengi yatafanyika kipindi hii ya uchaguzi.

Sasa Baregu,kufungiwa kwa SAUT Which is which?,

Lete story kwa undani tujadili,tuwekee ilivyoandikwa,kwani taarifa ni kuwa redio hiyo imefungwa kwa sababu masafa yake yanaingilia mawasiliano ya ndege,sasa siasa zinatoka wapi
 
Ooops!! Uhuru wa vyombo vya habari mashakani. Hii ni dalili kuwa Watawala wetu na virusi vya udikteta. Hao wengine ni "Darlings" (angalau kwa wakati huu) wanatumika kama vuvuzela wakati huu wakuelekea uchaguzi mkuu ila wakae wakielewa fungate lina mwisho wake. Kuna siku watakuja kukinywea kikombe siku watakaposema jambo linalowakera watawala. Mtu akiathiriwa na virusi vya udikteta yuko tayari hata kumnyonga mtoto wake pindi anapomhisi ni tishio kwa utawala wake. Asomaye na afahamu!!
 
Radio ya SAUT imefungwa eti kwa sababu walikua wanawasema mno CCM kwa ukweli kuhusu ufisadi unaoendelea? Mbona radio ya chama inapewa hio ruksa pamoja na Clouds FM?

Alafu Baregu (campaign chairman CHADEMA) si anafundisha kwenye hio shule? Yani mengi yatafanyika kipindi hii ya uchaguzi.

Kuna siri kubwa iliyosababisha naogopa kuiandika sababu ya uadilifu wa wamiliki Radio hiyo, lakini amini usiamini mwaka huu ni mwaka wa shetani kuumbuka, kumbuka wachungaji wa makanisa waliombea sana amani wakati wa uchaguzi,Amani maana yake ni pamoja na kuumbuka kwa shetani na mitego yake.Wanaharakati tulieni bwana mungu anatenda kazi yake kama walivyoomba waumini wa madhehebu mbalimbali na pia mkumbuke shetani anapopagawa huwa anaropoka ropoka.Kuna mtumishi wa mungu mmoja aliwahi kutoa usemi kwamba Shetani amepewa uwezo wa kutengeneza chungu kikubwa na kuweza kuingia na kujificha lakini amenyimwa uwezo wa kutengeneza mfuniko wa chungu hicho na hivyo anapoingia juu panabaki wazi na baadaye siri zote ndani ya chungu zinabaki wazi.Ya RADIO SAUTI tutayajua tu tusiumize vichwa.Mbona Dr.Slaa kagundua siri ya Waraka wa serikali kwenda kwa vibaraka wanaoongoze selekali ya kifisadi
Wewe tulia utasikia mengi zaidi.
 
Ebana wewe uko anonymous, naomba ututangazie hapa hapa sababu basi kwa nini walifunga.
 
Back
Top Bottom