Ujenzi wa Chadema ya ushindi 2015 hautafanikiwa kwa siri bali kwa uwazi; kwa maana nyingine, siri ya mafanikio katika ushindani wa siasa chini ya demokrasia ya uliberali sio siri bali uwazi;I am not sure MMM kama sincere members wa CDM watatoa siri zao in public kuijenga CDM!
Mkuu nilishangaa sana Dr slaa alipotoa comment kuhusu uchanguzi wa ccm week mbili zilizopita,je ilikuwa sawa au ni makosa,nafikiri kiongozi mkubwa kama Dr slaa anatakiwa kuwa na washauri kwa ukaribu na lolote atakaloleta publick wahakikishe wamelipitia na kuangalia reaction itakuwaje
Dr. Slaa yupo makini; pamoja na uanachama wangu wa CCM, i have to admit kwamba watu kama Mnyika, Lissu na Slaa ni hazina kubwa sana kwa taifa letu;
Dr. Slaa yupo makini; pamoja na uanachama wangu wa CCM, i have to admit kwamba watu kama Mnyika, Lissu na Slaa ni hazina kubwa sana kwa taifa letu;
sawa Mkuu naona umeamua kuja kutusaidia,lakini vilevile hatuna imani na wewe nahisi unataka mambo yawekwe peupe,usisahau nyie ccm mna hamu sana ya kujua mienendo ya Chadema
Well said mkuu. Lakini nimeupitia uchambuzi wako kwa kina na ninasita kuamini kwamba wewe ni CCM kweli!!!
Katika kuangalia changamoto hizo nina presume kuwa watu wanakubaliana katika mengi mazuri ambayo yamekwisha fanya hadi hivi sasa na CDM.
Unaamini kuna changamoto kubwa....
Ni kweli sana. Watu wanafikiria kujadili changamoto za CDM hadharani ni kuisaidia CCM; kivipi mimi sielewi bali ni woga usio na sababu.Ujenzi wa Chadema ya ushindi 2015 hautafanikiwa kwa siri bali kwa uwazi; kwa maana nyingine, siri ya mafanikio katika ushindani wa siasa chini ya demokrasia ya uliberali sio siri bali uwazi;
Ni mawazo yangu tu mkuu, ila kimsingi naelewa hoja juu ya umuhimu wa kufanya mikakati ya chama kuwa ya siri hasa katika mazingira haya ya siasa za kuviziana; Mimi nilikuwa nazungumzia tu kwa ujumla wake ambapo ushindani wa siasa katika mfumo wa demokrasia ya uliberali hauendeshwi kwa siri bali mikakati iliyo wazi hasa kutokana na uwepo wa ushindani unaotegemea sana tofauti za itikadi; Lakini ndani ya mazingira yetu ya ombwe la itikadi miongoni mwa vyama vyote vya siasa Tanzania (including CCM), hoja ya usiri katika mikakati ina mashiko kwani ushindani upo based on mambo mengine ambayo yanakaribia kuwa ya udaku;
Nilikuwa naamka alfajiri saa 10 kuangalia zile debate tatu za Obama na Romney. Romney wa Republicans alikuwa hafichi kitu juu ya nini atafanya akiingia madarakani. Hapa tunawachagua watu hata ambao hawajui kwa nini wanautaka UONGOZI wa nchi yetu!Ni kweli sana. Watu wanafikurua kujadili changamoto za CDMhadharani ni kuisaidia CCM; kivipi mimi sielewi bali ni woga usio na sababu.
Nashukuru kwa kuliona hilo, kwani inanishangaza sana kuona makamanda wangu kama kina Samson Mwigamba wakiwa hawaelewi wala kusikia neno lingine zaidi ya Chadema 2015 Ikulu njia ni nyeupe; Binafsi nitafurahi hilo kutokea nikiwa bado hai kwani itakuwa ni ukomavu mkubwa wa demokrasia katika taifa letu, na sio jambo la ajabu kwa vyama kupeana vijiti kutokana na matakwa ya umma; Huo ndio msingi wa demokrasia; CCM tukishindwa, tujipange, and actually tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kujipanga kwani watakaobakia CCM iwapo itaanguka 2015 watakuwa ni wale wenye mapenzi ya dhati na chama hiki;Mchambuzi....Muhimu: Chini ya kanuni ya sasa ya mshindi ni mshindi - CCM hata ikimsimamisha Sofia Simba 2015 itapita kwa uhalali;.....
Asante kwa maneno mazuri, ingawa najua walio ndani ya CDM hawatapost wala kujibu haya hapa hadharani, inawezekana kwa nia na sababu njema, ila sisi wapenda maendeleo tunasema "msg send" cha ajabu hata mashabiki wao wamekaa kimya.
Mchambuzi, kwa nini umemtumia m/kiti wa UWT?
Mkuu umesahau na USALAMA WA TAIFA1.KATIBA
2.TUME YA UCHAGUZI
3.MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA(TENDWA)
4.JESHI LA POLISI(JWTZ nao ni-kama wameanza kuingia kwenye huo mkumbo)
...hizo ndo changamoto zinazokikabili chama kilichobeba matumainia ya watanzani "CHADEMA"...
Nilikuwa naamka alfajiri saa 10 kuangalia zile debate tatu za Obama na Romney. Romney wa Republicans alikuwa hafichi kitu juu ya nini atafanya akiingia madarakani. Hapa tunawachagua watu hata ambao hawajui kwa nini wanautaka UONGOZI wa nchi yetu!