Kuelekea 2015: Changamoto Kuu za CHADEMA ni nini?

Sina shida na heading,no contents,ningeomba ujibu nilichouliza.Kama ni changamoto mbona wanazo nyingi tu?Hakuna chama cha kisiasa chenye kujitambua na chenye wanachama na ambacho bado kinakuwa na kisiwe na changamoto.

Swali langu la msingi umeliona,ungelijibu badala ya kung'ang'ania kwamba sijaelewa maana ya changamoto.

Mbali na ukweli kuwa kuna maelfu ambao hawajakikubali kama ulivyoainisha,pia kuna changamoto kwamba maelfu walioko vijijini bado hawajafikiwa na chama hicho.

swali lako lina dalili ya kutokuelewa nilichosema; nikijaribu kulijibu itabidi nianze kukuelewesha kwanza.
 
swali lako lina dalili ya kutokuelewa nilichosema; nikijaribu kulijibu itabidi nianze kukuelewesha kwanza.
Ok,lets say chadema hawatakikosoa ccm wala kukipa ushauri kama unavyotaka,halafu badala yake wakasema sisi tutafanya hivi ama vile,whats the difference?Swali rahisi tu.
 
Mzee Mwanakijiji punguza hofu!2015 tunaipa chadema nchi.ni vyema tukaipima chadema kuanzia 2015 kuliko kuendelea kuiamini ccm iliyoshindwa kwa miaka 50.kinachotakiwa na wananchi ni mabadiliko ya mfumo wa uongozi uatakayowajengea heshima.kwa sasa mwanaccm anaamini akishapita kwenye chama basi hakuna wa kumhoji,tunachotaka wanasiasa wakielewe ni kimoja tu kwamba wananchi ndio mabosi wao tofauti na sasa .
 
Mzee Mwanakijiji unafanya kazi nzuri sana ya kuijenga CDM hata kama wewe si CDM. Naomba niwakataze kulinganisha CDM na TANU kwani mazingira ya vyama hivi na agenda zake ni tofauti sana. Wakati wa mkoloni wahenga wetu walisahau tofautio zao na kumuangalia mkoloni kama adui yao mkubwa, na kwa hiyo colomialism was a unifying factor to the blacks and colloured. Ingawa na wakati huu tunayo agenda ya kuondoa ufisadi na kulinda rasilimali zetu kwa manufaa yetu sote lakini tunalokundi kubwa ambalo mfumo huu unawanufaisha na hao tuko nao karibu sana katika maisha yetu ya kila siku tofauti na mkoloni wa wakati huo. Nini changamoto kwa CDM kwa sasa?
  1. Wanawake hawajapewa nafsi kama BAVICHA ili wawafikie wanawake wenzao
  2. Nini dira ya kisiasa ya CDM
  3. CDM ni vizuri ikaanza kuandaa itikadi yake na ikaelezwa kwa wananchi na namna wananchi wanavyolindwa na itikadi hiyo
  4. Maadili ya kitaifa -azimio la arusha lazima lirudishwe
 
Ok,lets say chadema hawatakikosoa ccm wala kukipa ushauri kama unavyotaka,halafu badala yake wakasema sisi tutafanya hivi ama vile,whats the difference?Swali rahisi tu.

Kuna mambo ambayo yanahusu CDM kama chama na mambo ambayo CDM itakuja kufanya ikishika madaraka kwa taifa. Changamoto zinazoulizwa hapa siyo changamoto za baada ya kushika utawala. Ni changamoto za jinsi ya kujiandaa kuelekea kushinda mwaka 2015. Kwamba ili iweze kushinda yawezekana kuna vikwazo ambavyo vitafanya CDM isishinde kirahisi (vinaweza kuwa vya ndani au nje ya chama). Hizi ndizo changamoto.

Unafikiri ni vitu ambavyo viko ndani ya CDM au kuhusiana na CDM ambavyo vinaweza kuwa vizuizi vya kuweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa na ule wa Rais na wabunge?
 
Mzee Mwanakijiji punguza hofu!2015 tunaipa chadema nchi.ni vyema tukaipima chadema kuanzia 2015 kuliko kuendelea kuiamini ccm iliyoshindwa kwa miaka 50.kinachotakiwa na wananchi ni mabadiliko ya mfumo wa uongozi uatakayowajengea heshima.kwa sasa mwanaccm anaamini akishapita kwenye chama basi hakuna wa kumhoji,tunachotaka wanasiasa wakielewe ni kimoja tu kwamba wananchi ndio mabosi wao tofauti na sasa .

Kwani 2010 ilikuwaje? CCM haijaanza kushindwa kutawala mwaka huu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Je mfumo wa kuchuja na kupata wagombea wa ngazi mbalimbali ni mzuri ba unapaswa kuendelea ulivyo?

MM mfumo huu ni mzuri kwa watu wanaokubali kushindana na kukubali kushindwa kama sehemu ya demokrasia, pili mfumo huu ni mzuri kama kuna fair play, kwa sasa tuwaache washindani wachujwe na umma kwa kupitia vikao halali kwa utaratibu wa kuwa na 'first vote round' kwa ajili ya kuwachuja na kura ya pili wabaki wawili ambao watashindana na mshindi atakuwa wa halali.
 
Kwani 2010 ilikuwaje? CCM haijaanza kushindwa kutawala mwaka huu.
ccm hajaanza kushindwa kutawala mwaka huu ni kweli kabisa!wengi wa wapiga kura hawakupata ufafanuzi wa jambo hili,sasa hivi wananchi especially vijana wamefunuliwa kupitia operesheni mbalimbali za CDM na wameelewa kwa kiasi cha kuiangusha ccm 2015.uelewa huu wa wananchi ndio chachu ya ushindi wa chadema.
Labda nikueleze kuwa anayeamua nani atawale ni mwananchi pekee iwe kwa kupiga kura,kulinda kura au ikishindikana kabisa kwa mapinduzi/maandamano.
Wanaoongoza libya ya leo hawakujiaandaa lakini wananchi waliamua kuwapa nchi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
MM mfumo huu ni mzuri kwa watu wanaokubali kushindana na kukubali kushindwa kama sehemu ya demokrasia, pili mfumo huu ni mzuri kama kuna fair play, kwa sasa tuwaache washindani wachujwe na umma kwa kupitia vikao halali kwa utaratibu wa kuwa na 'first vote round' kwa ajili ya kuwachuja na kura ya pili wabaki wawili ambao watashindana na mshindi atakuwa wa halali.

kama watu wanakumbuka baadhi ya wagombea waliopendekezwa na CDM mwaka 2010 waliingia mitani na kutoa nafasi kwa wagombea wa CCM kuwa "wagombea pekee". Na wakati mwingine baadhi ya wagombea wamekuja kuwa matatizo makubwa sana kwa chama baadaye. Kwa vile mfumo uliopo sasa bado ni ule ule haitawezekana kweli kupata matatizo yale yale 2014 na 2015?
 
ccm hajaanza kushindwa kutawala mwaka huu ni kweli kabisa!wengi wa wapiga kura hawakupata ufafanuzi wa jambo hili,sasa hivi wananchi especially vijana wamefunuliwa kupitia operesheni mbalimbali za CDM na wameelewa kwa kiasi cha kuiangusha ccm 2015.uelewa huu wa wananchi ndio chachu ya ushindi wa chadema.
Labda nikueleze kuwa anayeamua nani atawale ni mwananchi pekee iwe kwa kupiga kura,kulinda kura au ikishindikana kabisa kwa mapinduzi/maandamano.
Wanaoongoza libya ya leo hawakujiaandaa lakini wananchi waliamua kuwapa nchi.

Wrong; walijiandaa sana wengine tena kwa miaka. Na katika kujiandaa huko utaona waliweza kutengeneza ile Baraza la Mpito na hatimaye kuandaa uchaguzi na sasa wanajiandaa kumaliza kuandika Katiba ya kudumu. Muslim Brotherhood kule Misri tayari ilikuwa inajulikana itafanya nini na hivyo ulipokuja uchaguzi watu waliichagua kwa sababu walijua inasimamia nini, wapi na kwanini.
 
Kwa lugha fupi leo katika mjadala huu Mzee Mwanakijiji unawashauri CDM waanze 'so quickly the exercise of a planned neglect'. While in politics there are so many things that demand their time and attention. Any attempt to give attention to all things that come into their way will not take them to the destiny we wish them and this country to be, you cant be a jack of all trade, list a few challenges to embark on for bigger results. here we gooooooooo for baraza la wanawake revive it by facilitate election or fill gaps and asign them with tasks to acomplish.
 
Kujiimarisha vijijini, vitongojini, katani na tarafani ni changamoto kubwa
Ukosefu wa ofisi za kutosha hata katika maeneo ya mijini ni changamoto kubwa
Ukosefu wa taarifa za chama kwa wanachama kutokana na mtandao kuwa mdogo
Nyaraka nyingi za chama hata zile muhimu hazipatikani hata katika ofisi za wilaya
Ukosefu wa watenda kazi (full time) ambao wako tayari kuifanya kazi ya siasa
 
Wrong; walijiandaa sana wengine tena kwa miaka. Na katika kujiandaa huko utaona waliweza kutengeneza ile Baraza la Mpito na hatimaye kuandaa uchaguzi na sasa wanajiandaa kumaliza kuandika Katiba ya kudumu. Muslim Brotherhood kule Misri tayari ilikuwa inajulikana itafanya nini na hivyo ulipokuja uchaguzi watu waliichagua kwa sababu walijua inasimamia nini, wapi na kwanini.
inawezekana!je unaweza kuniambia walijiaandaa kwa miaka mingapi?
Je kwa miaka waliyotumia kujiandaa(kumbuka Cdm ina miaka 20) ilitosha kuwafanya wananchi wawaamini?
Ina maana hadi leo hujajua chadema wanasimamia nini?
Je unakubali kuwa mwenye uamuzi wa mwisho ni mwananchi?
 
nionavyo mimi changamoto kubwa kwa chadema ni moja tu.kwamba ni vipi inaweza kuendelea kuwafumbua macho wananchi wengi zaidi juu ya uovu wa ccm huku ikikabiliwa na serikali ya ccm na vyombo vyake vya dola.(hapa naongelea sustainability ya operesheni zao dhidi ya nguvu ya ccm na dola)
 
ni kweli; lakini vipi itasaidia kuwaingiza madarakani katika mfumo uliopo (ndani ya CDM na nje yake)?
 
ni kweli; lakini vipi itasaidia kuwaingiza madarakani katika mfumo uliopo (ndani ya CDM na nje yake)?
ndani ya CDM naamini wamejipanga ndio maana leo hii tuko hapa tulipo.nje ya CDM siwezi kuongelea sana lakini naamini unaona yanayotokea kwenye chaguzi za ndani za ccm au hata kampeni za cuf!
Ukweli ni kwamba CDM inaendelea kuvuka vikwazo vya wapinzani wake huku ikiweka lengo la kuchukua nchi.
Punguza hofu mkuu,tafuta taarifa zaidi juu ya hali ya kisiasa nchini,ongea na watendaji serikalini na wananchi wafanya maamuzi utapata ukweli.
 
Niliwahi kuandika huko nyuma mada ya kwamba jukumu la chama cha upinzani siyo kusaidia serikali kutawala bali ni kuhakikisha wanaiangusha serikali iliyoko madarakani ili wao wapate nafasi ya kuingia kwenye uongozi huo na kutekeleza sera zao. Mada hiyo ya Aprili 2011 inaeleza kwa kina kuwa siyo jukumu la CDM kuikosoa serikali ili itawale vizuri. Lengo lolote la kukosoa serikali ni kuidhoofisha ili hatimaye ianguke (collapse) au wananchi waikatae kwenye uchaguzi mkuu.

Mawazo kama haya yanaongozwa na falsafa ya scarcity, watu wanaongozwa na falsa ya abundance waanamini tofauti,

Falsafa ya scarcity inaamini kwamba Mwanakijiji akishindwa mimi nitapata, Au Mwanakijiji Akifeli mtihani mimi nitafaulu, Au Mwanakijiji Akipata mavuno mengi kwenye shamba lake mimi sitavuna, mjukuu wa mzee mwanakijiji akishindwa wa kwangu atafaulu... etc. etc... Mawazo kama haya huwa yanaishia mtu kuwa mchawi, mzandiki, kuandamana consectively for 5 years. etc. Ngoja nisiwashauri ili wafeli, lakini ukipata uraisi/ukiunda utaanzia chini zaidi kuliko kama ungeendelea kushauri matatizo fulani fulani yatatulia kila uchaguzi utakuwa na changamoto zake na vipaumbele vyake na kila wakati yapo ambayo yatahitaji kutatuliwa maana chama kilichokuwa madarakani kimeundwa na wanadamu! Wakati mwingine wenye mrengo wa namna hii wanaishia kujenga mazingira mabaya zaidi wakati wa Utawala wao... Mifano iko mingi sana.

Falsafa ya Abundance inaamini kwamba Mwanakijiji awesha shinda na wewe pia ukashinda, Mwanakijiji anawezapata Mavuno na wewe pia ukapata mavuno! Falsa ya namna hii ndio inayoleta maendeleo, na inafanya unafanya aliyeko madarakani akazane... lakini pia utapokea kijiti wakati unayepokea akiwa na speed nzuri hivyo kuweza kushinda mbili mara uchukuapo kijiti... tofauti na kupokea kijiti kwa mwenzako ambaye inabidi ufuate mita 80 akiwa ameanguka chali. Falsafa hii inafanywa na watu wanaona mbali... na mmojawapo ni Mh. Zitto Kabwe... anapenda apokee kijiti kutoka kwa mkimbiaji ambaye ana nguvu bado, hivyo itamfanya yeye akimbie zaidi na kushinda mbio... eventually wote watakuwa washindi na wananchi watakuwa washindi zaidi. Kuna kabila moja limeendelea hapa Tanzania nadhani yako mengi... lakini ni kwa sababu ya-believe on abundance... kwamba mtoto wa fulani akipata na wakwangu pia atapata... kwa hulka hii wanaishia ku-support each other... b'se no body believe resources are scarce... mawazo... mbinu mpya etc.

Hii ni mitazamo tu... Mzee wetu Mwanakijiji amependa mtizamo wa ku-believe the world has scarcity, mimi na-believe hata tukiwasaidia CCM vipi wafanikiwe come 2015 tutakuwa na changamoto zingine kabisa na ambazo zitashindaniwa na mwenye uwezo wa kueleza namna ya kuzitatatua na huyo ndiye apewe uongozi.

Let Think BIG, let think as 21 Century mambo ya TANU na mazingira tuliyonayo is totally different.... and think there is a lot there, that can satisfy you, him and me and that our nation will continue be here for 100 of years... there is no need stop supporting those who are in charge now...
 
Dr. Slaa yupo makini; pamoja na uanachama wangu wa CCM, i have to admit kwamba watu kama Mnyika, Lissu na Slaa ni hazina kubwa sana kwa taifa letu;

I have to admit kwamba watu kama
1.jerry Silaa
2.Magufuli
3.Mwakyembe

Ni hazina kubwa sana kwa taifa letu.
 
Let Think BIG, let think as 21 Century mambo ya TANU na mazingira tuliyonayo is totally different.... and think there is a lot there, that can satisfy you, him and me and that our nation will continue be here for 100 of years... there is no need stop supporting those who are in charge now...

if you have scarcity you can't behave as if you have plenty. The world in fact has scarcity. It is this which is the fundamental prerequisite in understanding of economic theory. Katika siasa ni tofauti zaidi. Kama waliopewa nafasi kusimamia the scarce resources that we have wanaplunder au squander kuwasaidia hawa ili wapate muda zaidi wa kuharibu ni kujiharibu wenyewe. NI jukumu letu kuhakikisha kuwa tunawasaidia kuondoka ili waje wengine.

CCM ilivyo sasa haisaidiki. Isipokuwa kama kunatokea a revolt ndani ya CCM. Siyo uasi huu wa sasa ambao unahusiana na nafasi na maslahi bali uasi unaotokana na tofauti za mtazamo, fikra na maono. Kwa sasa CCM haina tofauti hizo za maono wala fikra; ina tofauti ya nani apate nini na kwanini.

CDM haipaswi hata kidogo kuisaidia CCM kuponya mgongano wake wa maslahi ili wakae vizuri wale zaidi.
 
Kuna mambo ambayo yanahusu CDM kama chama na mambo ambayo CDM itakuja kufanya ikishika madaraka kwa taifa. Changamoto zinazoulizwa hapa siyo changamoto za baada ya kushika utawala. Ni changamoto za jinsi ya kujiandaa kuelekea kushinda mwaka 2015. Kwamba ili iweze kushinda yawezekana kuna vikwazo ambavyo vitafanya CDM isishinde kirahisi (vinaweza kuwa vya ndani au nje ya chama). Hizi ndizo changamoto.

Unafikiri ni vitu ambavyo viko ndani ya CDM au kuhusiana na CDM ambavyo vinaweza kuwa vizuizi vya kuweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa na ule wa Rais na wabunge?
Kuhusu vizuizi vya ndani,kikubwa(ambacho kina indirect correlation na maadui wa nje),ni hilo suala la udini na pengine ukanda(hili halina nguvu).

La udini linapokuwa exploited na kiongozi wa ndani,ni tatizo kubwa sana.Ni tatizo kwasababu utakuta kiongozi huyo badala ya kujaribu kuzifuta hisia hizo kwa wananchi,basi anazitumia kwa manufaa yake binafsi kwasababu tu ya kupata nafasi ya kugombea urais.

Kwa mfano kumekuwa na almost in a simultaneous kind of fashion,kuona kiongozi akicapitalize kwenye issue ya udini kwa maneno ambayo yana mwelekeo wa kuwaaminisha wananchi kuwa ni kweli kuna udini.Na hilo linatokea sambamba na wakati ambao kuna shughuli ambayo ni muhimu kwa chama kujijenga.(mfano uchaguzi,m4c nk)

Hapo tatizo ni kubwa kabisa kwa uongozi kwasababu sioni kama kuna jitihada makini na za makusudi kabisa za kujaribu kulidhibiti hilo.

Viongozi wenye dini ambazo inasemekana haipewi nafasi kwenye chama,ndiyo hao ambao walitakiwa wawe msitari wa mbele kukanisha taarifa ama hisia hizo,yani wawe kama mabalozi wa kupingana na hilo kwa nguvu zote(kama ni kweli wanaamini hakuna udini).Lakini imekuwa tofauti.

Hilo linanipa mashaka sana given the fact kwamba uongozi kwa ujumla hawaonyeshi dhamira ya kupambana na hali hiyo.

Kukiwa na umoja ndani ya chama (uongozi),basi ni rahisi kujipanga(badala ya kulumbana kugombea madaraka),na kujikita zaidi kupeleka ujumbe kwa wananchi wengi kwa kadri ya uwezo wao.(especially vijijini)

Kwa upande wa mambo ambayo ni nje ya chadema,kubwa ni la serikali ya ccm kutumia dola kudhibiti ukuaji wa chama hicho.Tumeona wanavyotumia polisi,usalama wa Taifa pamoja na makundi kama green guard,na wakati mwingine kutumia makundi ya dini ili kuleta mvurugano.

Yote hayo ni kujaribu kuidhibiti demokrasia na kuwanyima wananchi kuitumia haki yao ya kuwachagua viongozi na vyama wanavyovipenda ama wanavyoviona kuwa vitawaletea mabadiliko kwenye maisha yao.

Ninaamini hata kama chadema watakuwa na sera na itikadi nzuri kiasi gani,kama hawapewi nafasi na uhuru wa kuwafikia wananchi ili kuwaelewesha kuhusu mipango yao kwa Taifa,basi haijalishi,kwasababu kitakachokuwa kikizungumziwa ni hayo ya unyanyasaji na umwagaji damu,chama tawala kikijaribu kuitumia nafasi hiyo kuwa pakazia chadema kuwa ni chama cha fujo,pia hilo linaondoa ile focus.(mfano toka yale mauwaji ya Iringa na Morogoro,ni kama m4c imeyumba)

Na ukishawaingizia wananchi hofu,basi kwa namna moja ama nyingine,utakuwa umepunguza kasi ya wananchi hao kujitokeza kukiunga mkono chadema.

Sasa sijui hilo litakuwa fixed kwa kutumia katiba mpya ama ni kitu gani?

Kwasababu ndiyo maana niliamini kuwa kupigania katiba mpya ndilo jambo la kwanza na la msingi kabisa.Inavyoonekana,ni kama vile tuko chini ya utawala wa chama kimoja.
 
Back
Top Bottom