Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,642
Wanabodi, Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is nothing to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...
  • Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
  • Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama vile ni mbali, unless wamsimamishe their one and only jewel!.
  • Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakiichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu!.
  • Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu, sasa wameichoka, hivyo uchaguzi wa 2015, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
  • Hakuna ubishi kuwa Chadema, ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kuliko CCM, hivyo ule mtaji mkubwa wa CCM iliyoutegemea kwa miaka nenda miaka rudi, sasa umehamia Chadema!.
  • Kama ambavyo CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea tuu, na sasa CCM imechokwa, vivyo hivyo kwa sasa Chadema haina lolote la kukifanya kipendwe, bali kinapendwa kwa sababu "watu" wameichoka CCM!.
  • Kama uchaguzi utaitishwa leo, Chadema itashinda kwa kishindo kikubwa cha ajabu, lakini ukiwauliza hao watakaokipa Chadema ushindi, ni sababu zipi za kuichagua Chadema, hawatakupa sababu yoyote zaidi ya kuichagua Chadema kwa sababu wameichoka CCM!.
  • ili Chadema iweze kupata ushindi wa Tsunami kwa uchaguzi wa 2015, lazima Chadema ikubali kubadilika, isiendelee kuutegemea huu umaarufu wa muda kwa kushangiliwa na umati wa watu walioichoka CCM, bali Chadema sasa lazima iwape Watanzania sababu za kuichagua Chadema!.
  • So far so good, Chadema is doing a good job chini ya Uongozi Shupavu wa Kamanda Mbowe na kinara wa M4C, Dr. Wibroad Slaa, Chadema is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
  • Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kuzifanyia kazi hizi hoja na tatu mkubali kubadilika!.
Naomba kumalizia kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanachama wetu humu jf.
Nitasema jambo moja zito- labda mbeleni nitaliangalia zaidi - ni wagumu sana kushaurika. Wametengeneza cocoon ya kujilinda kiasi kwamba ni vigumu sana kuweza kutoka ndani. Na kama kuna kitu kitakachosababisha waendelee kuwa wapinzani wa kudumu siyo kukosa ushauri au mawazo mapya bali kutokukubali kubadilika.
Kwa wale wapenzi wa Chadema, for sure, Uchaguzi wa 2015, Chadema inaweza kabisa Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If "Itabadilika" and provided that CCM haitamsimamisha yule mgombea wangu!. Japo ni vema kuwa na great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best na kama Chadema haitabadilika, you better get prepared for the worst kwa sababu 2015 itakuwa ni CCM Tena!.NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.Naomba kuwasilisha.Pasco.
UP DATE 1.Kufuatia maswali mengi kuhusu Chadema wabadilike nini, naomba kumnukuu mmoja wa great thinkers wetu humu jukwaani
‘The Country is Suffering From CCM Fatigue'. Kuna tofauti kubwa baina ya "Doing the Right Things" na "Doing things Right", na ili ufanikiwe, nilazima kufanya yote mawili. Chadema has been doing the right things ambayo ni kutumia kikamilifu mapungufu ya CCM kujijenga kisiasa. Lakini tatizo linakuja kwenye "doing things right" Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na CoherentKwanza Chadema wanastahili pongezi kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwa politically active majira yote. Lakini pamoja na mafanikio haya, bado Chadema kinaonyesha udhaifu mkubwa kwenye mbinu inazotumia kuendesha siasa za upinzani. Mbinu za Chadema kwa kiasi kikubwa hazina consistency (uthabiti) na coherence kwani zinabadilika mara kwa mara. Hili ni tatizo, hasa pale chama kinapokuwa hakina mvuto unaotokana na itikadi bali masuala ya mpito Upinzani dhidi ya Itikadi ya CCM, lakini bila ya kutoa dira na itikadi mbadala iliyo practical – Chadema wamekuwa wanapinga sera nyingi za CCM bila ya kutoa itikadi na dira mbadala Ni muhimu nisisitize kwamba tatizo sio mbinu hizi za upinzani bali the inconsistency na incoherence katika hilo.

Leo hii masuala ya uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya Ukanda, Ukabila na Udini. Inawezekana baadhi ya watu wasikubaliane na mimi katika hili, Ni vigumu kwa sasa kubaini masuala la udini, ukabila na ukanda yata ‘play out' vipi katika siasa za CCM na Chadema 2015. Vinginevyo ni muhimu Chadema ikafanya marekebisho ya maana kwenye itikadi yake, kwani nje ya uchovu wa wananchi na CCM, nje ya agenda ya serikali ya CCM kutokuwa na maamuzi magumu kutatua matatizo ya nchi, na pia nje ya agenda ya ufisadi, Chadema haina ammunition ya kutosha kisera kuitoa CCM magogoni. Hili linahitaji kubadilika na ndio kete kuu ya Chadema 2015 itakayowaletea mafanikio yenye mashiko zaidi mbali ya vita dhidi ya ufisadi ambayo sio mwarobaini (panacea) ya matatizo ya wananchi walio vijijini.

Ni mambo haya ambayo nadhani yakifanyiwa kazi na Chadema, basi yatazidi kujenga mazingira ya utayari kwa Chadema kushika madaraka ya nchi 2015 – kwani mbali ya "doing the right things", pia watakuwa wametekeleza dhana ya "doing things right"

NB. Kwa maswali yoyote kuhusu haya mambo ambayo Chadema inahitaji kubadilika, naomba uyaelekeze moja kwa moja kwenye thread husika hapa.CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015
UPDATE 2: Input ya Mchambuzi.
Ningependa kuchangia kidogo kuhusu suala hili la rushwa, hasa kwa kujaribu kujengea hoja kwanini rushwa ni hoja ya ukombozi. Naungana na wewe kupinga hoja kwamba Ufisadi sio hoja ya kuwakomboa watanzania. As a matter of fact, vita dhidi ya Ufisadi/Rushwa na ile dhidi ya umasikini lazima viende kwa pamoja, vinginevyo kuendeleza vita dhidi ya umaskini huku vita dhidi ya ufisadi vikilega lega, juhudi za kutokomeza umaskini hazitazaa matunda na tutaishia tu kupoteza resources nyingi sana pamoja na muda mwingi bure kwenye vita dhidi ya umaskini ambavyo havitamalizika.

Mabadiliko yoyote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yenye kulenga kuletea faida wananchi walio wengi hayawezi kufanikiwa bila ya kutokomeza rushwa; Rushwa/Ufisadi ni ‘an infection' kwenye juhudi za Maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ndio maana hata kwenye kwenye international development community, Suala la Rushwa/Ufisadi limeanza kuchukuliwa kama ‘a development issue' & ‘a development imperative';

Kwanini Rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania?

Rushwa covers a wide spectrum, kuanzia rushwa ndogo ndogo/petty corruption to large scale/grand corruption. Tukianza na Petty corruption, ili mtanzania aweze pata huduma za msingi kabisa zinazosimamiwa na Bureucrats/Administrators kama vile Uhamiaji, Polisi, Ardhi, Elimu n.k, bila ya kutoa ‘kitu kidogo', normal bureaucratic procedures can't be accomplished; Mwalimu Nyerere alipokuja na kauli mbiu ya TANU dhidi ya Rushwa kwamba RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA, aliliona hili kwani MASKINI HAWEZI KUPATA HAKI katika jamii inayoendeshwa kwa rushwa, na maskini tanzania ni zaidi ya 80% na hawa wanasubiria ukombozi kwa miaka 50 sasa;
Mpaka hapa, hoja kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi?

Tukiangalia aina nyingine ya rushwa - Large scale/Grand Corruption, hii inatokea pale ambapo a considerable amount of money inatolewa kama hongo ili kuwapatia watu fulani fulani preferential treatment au access kwa Rasilimali za watanzania ambazo walipewa na Mungu. Nyerere alitueleza kwamba ili kufanikiwa katika Maendeleo, moja ya vitu muhimu tunavyohitaji ni ARDHI, vingine vikiwa ni watu, siasa/sera safi, uongozi bora n.k. Tumeshuhudia jinsi gani wageni wanajinyakulia ardhi kwa kutoa rushwa huko kwa watawala; tunazidi kuona jinsi gani wawekezaji wanawawekea watawala mamilioni ya dola kwenye mabenki huko Uswisi na kupewa miradi ya madini, mafuta, gesi….miradi ambayo ina kila sura ya kijambazi na unyang'anyi kwani HAKI YA MUNGU aliyopewa mtanzania (rasilimali) inakuwa HAKI YA MZUNGU.
Pia kwa mfano mwingine huu mdogo tu, hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi.

Mtu anayetoa hoja kwamba rushwa sio hoja ya kumkomboa watanzania ni dhahiri anawatusi mamilioni ya watanzania waliotaka mabadiliko mwaka 1995 wakati wa Augustine Mrema na NCCR Mageuzi kwani nchi ilikuwa inanuka rushwa, jambo ambalo hata Nyerere alilisema sana; Kama tunaamini katika demokrasia, hasa katika dhana ya nguvu ya umma, umma ule kumuunga mkono Mrema kutokana na msimamo wake dhidi ya Rushwa ni maana kwamba Rushwa ni Hoja ya kumkomboa Mtanzania; Vile vile, katika nyakazi hizi, Chadema imejinyakulia umaarufu na kuungwa mkono na watanzania wengi sana (kwa mamilioni) kwani watanzania wengi wanaona hoja ya rushwa ina mashiko;vile vile the fact kwamba CCM inazidi kupoteza mapenzi mioyoni mwa watanzania wengi ni ushahidi tosha kwamba rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania;

Nchini Tanzania rushwa imeshaota mizizi, na its ‘negative effects' imesha – multiply kwenye jamii. Katika Tanzania, Rushwa/Ufisadi umepelekea mamilioni ya watanzania kupoteza matumaini na hali zao za maisha, umezaa cynicism, hali ya kutoaminiana kwani watanzania wengi sasa wanaamini kwamba rushwa/ufisadi is a ‘norm'. Ufisadi/rushwa unazidi ku-undermine our social values kwa sababu watu wengi wanaona ni rahisi na inalipa kujiingiza katika shughuli za ufisadi/rushwa kuliko kutafuta shughuli au ajira halali;

Rushwa/ufisadi umeshapelekea mmomonyoko wa uhalali wa serikali ya CCM in the eyes ya watanzania wengi kwani mbali na madhara ya Ufisadi ambayo yanawanyang'anya watanzania ile HAKI YA MUNGU na kugeuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU, vile vile petty corruption inapunguza kwa kiasi kikubwa sana ‘effective delivery' ya huduma za kijamii, na ni ahadi juu ya upatikanaji wa huduma za namna hii ndio ilipelekea watanganyika wengi kuiunga mkono TANU miaka ya 1950s na hatimaye kuisaidia TANU kutekeleza malengo yake ya ukombozi wa nchi;

Given all this, mtu anaweza vipi kuja na hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania? Wakati tunazidi kushuhudia madhara ya rushwa/ufisadi katika upatikanaji wa huduma za kijamii kwa watazania walio wengi? Na pia jinsi gani ufisadi/rushwa unapelekea watanzania kuporwa HAKI YAO KUTOKA KWA MUNGU (Rasilimali) na inageuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU?
Cha kuzidi kushanganza zaidi ni pale CCM (tofauti na TANU) kinapogeuka kuwa ni chama cha kujiuma uma kuhusu suala la rushwa/ufisadi. Pengine tunapoteza muda kujadili hoja hii kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania bila ya kujua kwamba kumbe ina mahusiano na kujiuma uma kwa CCM; I don't know, Lakini yetu macho na masikio.
UPDATE 3: CLOSING REMARKS YA MKUU NGURUVI3

Mkuu, kama nilivyoahidi nipo. Ingawa mjadala unaonekana kufungwa hakika sitasita kutupa neno moja au mawili hasa kujibu hoja yako ya kuwa inaonekana nakubaliana na Pasco.

Ni kweli nakubaliana naye kwa asilimia kubwa sana hata kama si mia moja. Na sababu za kufanya hivyo ni:
1. Kama alivyosema CCM imechokwa, si tu imechokwa bali imechokwa na matendo yake. Chama kilichopo madarakani miaka 50 hakionekani kuwa tumaini kwa Wananchi, badala yake kimegeuka kuwa genge la waporaji na waporaji hao kulindwa kwa kura za wananchi licha ya kuwa uporaji ni wa kodi zao.

2.Wananchi wametafuta mbadala kwa miaka mingi na hakika 'ndele' ya kupendwa imeangukia Chadema.
Ndele hiyo inatokana na jitihada hasa zilizofanyika bungeni kuuonyesha umma wapi tatizo lilipo.
Yule mama aliyehojiwa Iringa yeye alisema 'Anaipenda chadema kwasasababu kama si wao, yeye asingejua uhuni na udhalimu unaoendelea nchi hii'.Hadi hapo Chadema wame win nyoyo za watu kwa kutambua kuwa wapo wanaosimama nao.

3.Mikutano inayoendelea ya M4C ni jambo sahihi, lakini haitoshi tu kuwa sahihi ni lazima ifanyike kwa usahihi.
Mfano, je kila baada ya mkutano kuna ufuatiliaji wa kuimarisha chama eneo husika? Au ni kugawa kadi tu na kukusanya watu na kama ni hivyo je huo ni usahihi hata kama jambo lenyewe ni sahihi?

4.Juzi tumeona picha za CDM mji mwema. Tena viongozi wakionekana kuwa makini. Aliyeleta picha ni mkereketwa wa Chadema na haikuwa na maelezo nini kimesemwa. Mkutano ni jambo sahihi, je, wamelifanya kwa usahihi? Jibu ni hapana kwasababu hawajawasiliana na umma kama ilivyokuwa mwazoni.
Wamekuwa 'out of touch' kwa public kama walivyo kwa JF.
Tayari wameshau ngazi iliyowapindisha na hiyo tu ni tatizo.

5.Pasco amesema lazima wawe tayari kukubali ushauri, na ushauri tuliwahi kutoa kwa kitengo cha mawasiliano ya umma 'public relationship' na ni wazi hawajaufanyia kazi. Hapo nakubaliana na Pasco kuhusu hoja hiyo.

6.Uwajibikaji; Tumeona panga la Arusha na Mwanza kwa madiwani.Uamuzi huo ni sahihi, lakini je wameufanya kwa usahihi? Jibu ni ndiyo na hapana. Ni ndio kwasababu wale wanaoleta vurugu wanapaswa kushughulikiwa.
Ni hapana kwasababu sheria au taratibu zinapindwa kila mara. Kama CDM ilikuwa tayari kupoteza madiwani wa Arusha na wa Mwanza hadi kufikia kupoteza hatamu za umeya katika grassroot level, imeshindikanaje kwa CDM kukubali kupoteza ubunge kwa utaratibu ule ule wanaoutumia? Mbunge mmoja na madiwani 9 ni nani muhimu katika kuimarisha chama.

7.Taratibu zinazowaangukia madiwani kwanini zisitumike kutuliza mtafaruku uliopo BAVICHA?
Ikifika hapo tofauti kati ya CDM na CCM inayowafukuzu makatibu wa matawi na kuwaacha wahalifu NEC na CC haipo.
Inaonekana kama Chadema wanafanya kazi kwa template ya CCM.
Kwa staili hiyo wananchi wataonaje tofauti ya vyama hivi katika kusimamia taratibu zao kabla ya kupewa madaraka!

Hapo ndipo niliposema Chadema lazima iwe na clear demarcation iliwatu waone mbadala walio na matumaini nao.
Ni lazima kuwe na demarcation katika kutoa misimamo ya mambo ya kitaifa. Chadema kama chama pinzani na tegemo kwa wakati mfupi ujao inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujibu, kupendekeza na kunyumbulisha hoja zinazohusu utaifa.
Mfano, nini msimamo wa Chadema kuhusu muungano?

8.Chadema wanapaswa kusimama kama taasisi na si kundi la watu fulani maarufu. Taasisi ina namna ya kupanga na kushughulikia mambo yanayohusiana nayo. Suala la Iringa ni mfano mzuri tu. Imewachukua wiki moja kukabiliana na uharibifu wa taswira ya chama uliohusishwa na tukio. In fact kauli ya Mbowe ilikuwa 'damage control' badala ya statement. Tatizo lisiloonekana kwa wengi ni hili la kutokuwa taasisi kikamilifu na ni ngumu kuliona kirahisi.

9.Kama Chadema hawatajipambanua kama Chama kinachosimamia na kueleza sera zake basi ipo siku wananchi watasema tofauti iko wapi? Hawa wanatenda wale wanakosoa nini kilitakiwa kifanyike!
Kwa maneno mengine ukosoaji pekee hautoshi ni lazima kuwepo na makusudi ya kueleza sera zao.

Chadema isimamie sera zake na kuzieneza na si kubaki katika makabrasha au kukaa kimya zikiporwa.
Hoja kama ya katiba, utawala wa majimbo wameziacha zimeporwa na sasa kuonekana kama za CCM.
Kwanini hili linatokea? Hoja ya katiba ilikuwa sahihi, je ilifanywa kwa usahihi?

Kwa ufupi, Chadema sasa kimekuwa na ni wakati kiongoze. Hoja za kukubaliana na CCM kama ya katiba haionyeshi mbadala. Kwangu mimi CDM walikuwa na hoja na waliwaacha wananchi porini. Nitty gritty!
Pamoja na ukosaoaji sasa ni wakati waeleze wao wana matarajio gani kwa njia gani, rasilimali gani na kipaumbele gani.

Vinginevyo wananchi watasema 'better the devil you know than the angel you don't know'.
The simple way CDM could counter act this arguement is to set a clear goal, and make a clear distinction between the past and the future.

CLOSING REMARKS.
Wababodi, baada ya 25 pages each with twenty posts, with a total 500 Posts Plus, imethibitika pasi shaka kuwa uchaguzi wa 2015, Ikulu ni ya Chadema, hivyo sasa kuelekea 2015, kila dalili zinaelekeza Chadema kuchukua nchi, ila kwa maoni ya wengi serious waliochangia thread hii (ukiondoa wale wa ushabiki), wengi wamekubali Chadema iko on the right track, ila ili kutimiza lengo hilo la kubisha hodi ikulu, na kukubaliwa kuwa mpangaji rasmi wa jengo lile, lazima Chadema ikubali kubadilika, apart from doing the right thing kama inavyofanya sasa, it got to do things right!.

Baada ya maneno haya, sasa kwa heshima na taadhima naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa hawa wafuatao.
  1. Mkuu Mkandara, topic yako ya ndio was the inspiration ilionifanya kuanzisha hii thread na niliepuka kukutaja wala kukuquote popote kwa sababu maalum. Asante kwa kujitanabaisha kama mwana Chadema ambaye uko tayari kusimama na ukweli, "no matter what"
  2. Mzee Mwanakijiji , ile quote yako niliyoitumia humu, imekuwa kama ndio "colabo" ya hit single kwa mwanamuziki mchanga, kumshirikisha "star mkubwa" ili atoke!, ndivyo ilivyokuwa hii thread, imefikisha record hits kwa mada yangu yoyote kufikisha posts 500 in two days, hii ndio mara yangu ya kwanza, na naamini kuna wachangiaji walichangia thread hii kwa ajili ya quotation yako. Ingawa wewe binafsi hukuchangia kwa sababu ambazo ninazifahamu fika, thanks for being you, who you are!.
  3. Mkuu Mchambuzi, ule uzi wako wa ndio the subject matter ya hii mada, kwa jinsi ninavyokusoma humu, naamini wewe ni genius kwenye politics zetu, kama Chadema wanakusoma na kuzifanyia kazi hoja zako, 2015, hatuzungumzii ushindi wa Chadema, bali how big the margin is, kati ya mshindi na mshindwa!.
  4. Mkuu Nguruvu3, wewe ni other political genius wetu humu, nilikufahamu kupitia theory yako ya "demage control" na kuendelea kukufuatilia kule kwenye Jukwaa lako, hii closing remarks yako, ni faraja kubwa kwangu, kuendelea kuibua topic ambazo sio popular kwa wana jf wengi, ila huu ndio ukweli halisi ambapo siku zote, kweli itasimama.
  5. Na mwisho, napenda kuwashukuru, wachangiaji wote mlioungana nami katika mada hii, ni vigumu kumtaja kila mtu, lakini shukrani za pekee ziende kwa wachangiaji changamoto akiwemo Mag3, J Mushi, Nicholas, na wengine wengi ambao japo hatukubaliani, lakini tumeishia kukubali kutokubaliana na hii ni healthy kwenye mjadala wowote. Mimi pia ni binadamu kama binadamu wengine, huwa nakwazika na kuwakwaza wengine, na especial kwenye mada yoyote inayomhusu "yule mgombea wangu"! tusameheane na tuzidi kusonga mbele kwa maslahi ya taifa.

Nakufikia hapa, naomba sasa ku declare rasmi, mjadala huu, umefungwa rasmi!
this Topic is officially Closed by the thread starter!!
 
Maneno mazito sana haya, viongozi wa Chadema wanapaswa kuyafanyia kazi, lakini si wa dizaini ya ya yule Genius Zitto Kabwe.
 
Nimeipenda hii nukuu ya Mwanakijiji

Nitasema jambo moja zito- labda mbeleni nitaliangalia zaidi - ni wagumu sana kushaurika. Wametengeneza cocoon ya kujilinda kiasi kwamba ni vigumu sana kuweza kutoka ndani. Na kama kuna kitu kitakachosababisha waendelee kuwa wapinzani wa kudumu siyo kukosa ushauri au mawazo mapya bali kutokukubali kubadilika.
 
Last edited by a moderator:
Pasco umetumia neno "Hakuna ubishi" kama tayari umeshafanya research ya kutosha, ikiwa hivyo ni kheri.

Lakini ukweli ni huu, kwa miaka mingi CCM imejaribu kujenga matumaini ya maisha bora kwa watanzania bila mafanikio. Jambo hili ndiyo ambalo limekuwa chukizo kubwa kwa wapiga kura wa rika zote. Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanywa na CDM ni mazalia ya matendo ya CCM toka miaka mingi kuongoza nchi pasi kuwa na malengo serious.

Lakini huo ni upande wa mmoja, upande wa pili ili CDM iweze kuingia 2015 madarakani ni kuomba upepo wa kusiasa uvume vizuri mpaka 2014 - 2015 ambapo wapiga kura wengi watakuwa wameshatoa maamuzi ya chama gani kishinde.

Lakini naona CCM nao wamejipanga vya kutosha kuhakikisha hilo nalo halitokei kwa kuanza kukipaka CDM matope kuwa ni chama cha vurugu na mauaji!!!!!

Zaidi ya hapo CCM ipo nyuma ya Jeshi la Polisi kuhakikisha mambo hayaendi mrama.
Hayo ni maoni yangu.

Kuingia CDM 2015 madarakani itategemea na karata wabunge wake watavyozichanga vizuri mpaka 2015 nakujiandalia mazingira mazuri ya kushinda.
 
Hakuna ubishi kama magamba wamekuwa wakishinda chaguzi nyingi kiharamu kwa kuwahonga wapiga kura ubwabwa, pesa, matandiko, fulana, kanga na kofia za rangi ya Yanga, kilevi kunyanyasa vyama vya upinzani hasa Viongozi wa Chadema na wafuasi wao na pia kutumia vyombo vya dola katika kuchakachua matokeo ya uchaguzi katika majimbo mbali mbali nchini.

Kamwe unaposhinda katika mazingira kama haya ushindi wako hata siku moja hauwezi kuitwa ni wa halali.


Wanabodi,
Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!

Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...

  • Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.



 
hadi leohujajua sababu za watz kukichagua chadema? sababu ni hiz hapa
1.wananchi waliahidiwa maisha bora lakin imekuwa kinyume chake

2.ccm kimekua ni chama cha maficho ya majambaz wa kalam(ufisadi)

3.serikali ya ccm imeshindwa kuwakamata mafisad na imekaa kuwakumbatia

4.kwa miaka 50 tangutupate uhuru chama kukaa madarakan kimeshindwa kutatua kero mbalimbali za wananchi kama vile ujenzi wa shule,nyumba za watumishi,zahanati,upatiakanaji wa dawa na watumishi.
sababu hizo zinatosha kukipigia kura
 

NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.




Mimi kama Muhusika (Mwanachama hai) hujanishirikisha naona kama hunitakii mema, tubadirike nini plz?
 

NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.

Ati??

Sasa ndugu yangu kwa nini usishirikishe jukwaa hili kuhusu hicho wahusika walichoshauriwa??
 
haya mawazo ni mazuri sana, hata mm ni mpenzi wa CDM tusipojirekebisha katu Ikulu hatuioni!!! tusiwe wepesi wa kuwaambia wezetu wameongea pumba ili hali mawazo ni mazuri na ya kutujenga.... ni hayo tu kwa leo!!!
tujirekebishe kwalipi?liweke waz sio unasema tujirekebishe halafu husem wapi tunatakiwa kujirekebisha.acha umbea.
 
Hakuna ubishi kama magamba wamekuwa wakishinda chaguzi nyingi kiharamu kwa kuwahonga wapiga kura ubwabwa, pesa, matandiko, fulana, kanga na kofia za rangi ya Yanga, kilevi kunyanyasa vyama vya upinzani hasa Viongozi wa Chadema na wafuasi wao na pia kutumia vyombo vya dola katika kuchakachua matokeo ya uchaguzi katika majimbo mbali mbali nchini.

Kamwe unaposhinda katika mazingira kama haya ushindi wako hata siku moja hauwezi kuitwa ni wa halali.
Mkuu BAK, determinant factor ya ushindi wowote kupitia ballot box ni idadi ya kura halali!. Matokeo yakishatoka, "the end justify the means", kama mshindi alihonga ili apigiwe kura au alichakachua, kura batili zika its way into ballot box, mshindi ni aliyeshinda no matter what!. Hao wanahongwa pilau, t-shirt na kofia na kupiga kura zao in favour ya CCM, kura zao ni halali kwa sababu hiyo ndiyo ridhaa yao!.
 
Back
Top Bottom