Kueleke miaka 50 ya uhuru, mmh

Leornado

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,529
196
Maskini watoto hawa, tena wapo eneo nyeti linaloingizia hii nchi mamilioni ya shilingi kwa mwaka. Watoto wa umasaini wakiwa darasani. Nini cha kujivunia miaka 50 ya uhuru kama hali bado mbaya hivi? hizo fedha wanazoandalia sherehe ya uhuru ( nimeona vijana wa bongo fleva wanjifua uwanja wa taifa mahususi kwa sherehe hii) zingetumika kutatua matatizo kama haya.

Hii siku ipite kimya kimya tu maana so far hamna cha kujivunia zaidi ya majuto. Hata ile amani CCM wanayojidai nayo imetoweka.

179313_157352860981857_100001214312304_319376_2304488_n.jpg
 
Mpelekeeni Kikwete hii picha aone maendeleo anayojivunia; hata akiiona huyu ****** hatajali kwani watoto wake wanashiba pale magogoni wanakula na kusaza na siku hizi wamejifunza hata kufunga tai!!
 
Hiyo ni kweli kabisa. Lakini kuna usemi usemao masikini akipata, ****** hulia mbwata. Ndiyo maana, licha ya kuwa na kipato kidogo, tunapenda kujitutumua na kuonyesha kuwa na sisi tuna kitu!
 
Inasikitisha sana, viongozi wetu wanayajua haya bali ni kwamba hawapo kwa maslahi ya wananchi na nchi hii, wao ni kulimbikiza mali tu na familia zao
 
Natamani kama watoto wa Rostam, Lowasa, Chenge nao wakasoma shule wanazosoma watoto wetu..
 
Maskini watoto hawa, tena wapo eneo nyeti linaloingizia hii nchi mamilioni ya shilingi kwa mwaka. Watoto wa umasaini wakiwa darasani. Nini cha kujivunia miaka 50 ya uhuru kama hali bado mbaya hivi? hizo fedha wanazoandalia sherehe ya uhuru ( nimeona vijana wa bongo fleva wanjifua uwanja wa taifa mahususi kwa sherehe hii) zingetumika kutatua matatizo kama haya.

Hii siku ipite kimya kimya tu maana so far hamna cha kujivunia zaidi ya majuto. Hata ile amani CCM wanayojidai nayo imetoweka.

179313_157352860981857_100001214312304_319376_2304488_n.jpg

Mkuu picha nyingine zinatia simanzi sana hata kuziangalia machozi yanaweza kukutoka
 
Hivi hilo ni darasa au zizi?

JK na familia yake, hata zizi haliko katika hali hiyo. Mifugo ya JK iko kwenye hali nzuri sana kuliko hawa malaika waliolundikwa kwenye hilo banda eti wanasoma. Hizi picha zinazidi kunifanya nichukie CCM.
 
Hicho kiboxi ni cha nini?

"Donation Box" ili ukitembelea hapo uchangie malipo ya mwalimu na kuwawezesha wapate uji shuleni. Hii naona ni shule ya Chekechea, ila hali inaonyesha sio mbaya kwa watoto hawa, pamoja na shule kuwa mbaya, afya zao (physical appearance) sio mgogoro.
 
JK na familia yake, hata zizi haliko katika hali hiyo. Mifugo ya JK iko kwenye hali nzuri sana kuliko hawa malaika waliolundikwa kwenye hilo banda eti wanasoma. Hizi picha zinazidi kunifanya nichukie CCM.

mkuu kama hao watoto ndo wanasomea kwenye hilo banda na wako hivyo huyo mwalimu mwenyewe kweli anajua dunia inaendaje na hata mshahara wake anaujua kweli au anaupata
 
kweli kuna haja ya kuinyima kura ccm
ni dunia gani tuliyopo?kwanini wasipunguze mavx,semina za kifalafala
ambazo brekfast tu ni mamilion ya hela?wangewapeleka watoto zao humo
siku mbili tu kushnehi... naichukia ccm from ma heart
 
Maskini watoto hawa, tena wapo eneo nyeti linaloingizia hii nchi mamilioni ya shilingi kwa mwaka. Watoto wa umasaini wakiwa darasani. Nini cha kujivunia miaka 50 ya uhuru kama hali bado mbaya hivi? hizo fedha wanazoandalia sherehe ya uhuru ( nimeona vijana wa bongo fleva wanjifua uwanja wa taifa mahususi kwa sherehe hii) zingetumika kutatua matatizo kama haya.

Hii siku ipite kimya kimya tu maana so far hamna cha kujivunia zaidi ya majuto. Hata ile amani CCM wanayojidai nayo imetoweka.

179313_157352860981857_100001214312304_319376_2304488_n.jpg

Mmh hali inatisha sana kwa kweli,unaweza kufikiri kuwa wakubwa hawajui mambo haya, wanafanya hivi makusudi ili watoto wao wanaosoma nje waje waendelee kututawala maana kwa hali hii mtoto anayesoma katika mazingira kama hayo ataweza vipi kuhimili ushindani katika sekta yeyote inayohitaji akili zisizolala.
 
Worse zaidi ni kwamba pamoja na kusomea humo bandani unaweza ukakuta hata mwalimu hawana maskini.
 
Binafsi sikubaliani kabisa na sherehe ya mabilioni ya kuazimisha miaka 50 ya uhuru, hizo hela zipelekwe kwenye kujeng shule ambazo bado ni za udongo, nyumba za walimu, na sekta ya afya.
Jamani ni aibu kubwa sana miaka 50 halafu bado tuna madarasa na nyumba za walimu zimejengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi na hamna vyooo wanafunzi wanaenda kujisaidia porini, bila aibu usoni mnakusanya bilioni 200 kufanya sherehe, yaani naomba siku hiyo mungu awadodoshee bomu hapo uwanjani au kwenye dhifa
 
Nimeamini kila shule ya msingi itakuwa na kompyuta.

Baba wa taifa (RIP) alisema ikifika miaka 10 ya uhuru tutawaita mje muone maendeleo yetu. Leo tunaweza kusema hayo maneno kweli?

Hatuna jeuri hiyo, miaka 50 baada ya uhuru ni kama vile tuko enzi za kina mkwawa, kimweri, milambo , halafu mtu na akili yake anasimama kusema tutumie mabilioni kusherehekea uhuru.
 
Mkuu kuna Halmashauri moja wanapanga kufanya sherehe za kuukaribisha mwana mpya wakati tumefikia kati kati ya mwaka na hapo watatumia mamilioni wakati kwenye wilaya husika shule hazina madawati wala vitabu
 
Tunatumia mabilioni kwa ajili ya chai kwenye ofisi za serikali, michezo ya wizara, ziara za mafunzo, Magari ya kifahari yasio ya lazima, tafrija za kila namna wakati wanachi wako hivi. Hio ni shule bado hatujaona hospitali, barabara mahakama, huduma za maji, ustawi wa jamii.

Halafu inafika tunaenda kwa wafadhili kuomba fedha za kuendesha nchi.

Kwa kweli hii ni nchi ya masihara.
 
Back
Top Bottom