Tahadhari yatolewa Bonde la Rufiji, baada ya bwawa la JNHPP kufunguliwa maji yake

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,321
24,228
Serikali mkoani Pwani nchini Tanzania yatoa tahadhari kwa wakaazi na wakulima waliopo katika bonde la mto Rufiji

Mh. Abubakar Kunenge mkuu wa mkoa wa Pwani amesema taarifa hiyo muhimu ni kuweka tahadhari kutokana na wingi wa maji katika bwawa la mradi wa umeme wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo Rufiji mkoa wa Pwani.

Mh. Abubabar Kunenge ameongeza kuwa taarifa kutoka wizara ya Nishati na shirika la TANESCO zinasema imelazamu kufungulia maji yaliyokwisha jaa kufikia kikomo cha usalama wa bwawa ili, bwawa hilo liweze kuwa salama kwani linauwezo wa kuhimili kiasi kadhaa za ujazo wa maji na yakizidi ili lisipate madhara yoyote inabidi kufungulia maji ya ziada.
 
Kila kitu kikizidi kinakuwa harmful......khaa tuwe makini mafuriko ya kutengenezwa
 
Mkuu wa mkoa wa Pwani ametoa tahadhari kwa wananchi waishio mwambao wa mto Rufiji kwani mto huo umefurika na maji kuanza kuvamia makazi ya watu baada ya bwawa la kufua umeme la mwalimu Nyerere kufunguliwa maji yake.

Ikumbukwe bwawa hilo baada ya kukamilika lilitakiwa kufungwa mashine tisa ili zizalishe umeme wa megawatts 2115 lakini mpaka sasa baada ya kukamilika limefungwa mashine moja tu inayozalisha megawatts 235! ,hali hiyo imepelekea maji yafunguliwe tu na kuenda bure ili kuzuia bwawa lisiendelee kujaa zaidi.

My take. Chadema mpo?
 
Ndiyo sisi hao, laana zingine tunazitafuta wenyewe, ipo siku hayo maji tutayakumbuka, jamii yetu haijawahi kuwa na akili ya kuangalia kesho yetu
 
Serikali mkoani Pwani nchini Tanzania yatoa tahadhari kwa wakaazi na wakulima waliopo katika bonde la mto Rufiji

View: https://m.youtube.com/watch?v=1Fgt6WMmHEI

Mh. Abubakar Kunenge mkuu wa mkoa wa Pwani amesema taarifa hiyo muhimu ni kuweka tahadhari kutokana na wingi wa maji katika bwawa la mradi wa umeme wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo Rufiji mkoa wa Pwani.

Mh. Abubabar Kunenge ameongeza kuwa taarifa kutoka wizara ya Nishati na shirika la TANESCO zinasema imelazamu kufungulia maji yaliyokwisha jaa kufikia kikomo cha usalama wa bwawa ili, bwawa hilo liweze kuwa salama kwani linauwezo wa kuhimili kiasi kadhaa za ujazo wa maji na yakizidi ili lisipate madhara yoyote inabidi kufungulia ili ni jambo la kawaida mkuu.

Hili ni jambo kawaida mkuu. Sasa tahadhari ya nini?
 
Hili ni jambo kawaida mkuu. Sasa tahadhari ya nini?

Upo sahihi hata kabla ya mradi wa bwawa la JNHPP mafuriko yamekuwa yapo eneo hilo la Rufiji, Ikwiriri n.k

Maji haya yalitakiwa yavunwe kutumika kwa umwajiliaji na matumizi ya kijamii mijini pia vijijini. Wameshindwa kutafuta namna kujenga bwawa la ziada pembeni kilometa kadhaa kutoka bwawa la JNHPP badala ya kuyafungulia yote kwenda kusababisha mafuriko na maji yote kuingia baharini bahari Hindi.

TOKA MAKTABA:
MASWALI YA MBUNGE MCHENGERWA KUHUSU MAFURIKO YA RUFIJI KUJIRUDIA

https://www.parliament.go.tz › polis
Supplementary Questions from Hon. Mohamed Omary Mchengerwa (15 ...

... wa Jimbo langu la Rufiji hususan Tarafa ya Ikwiriri? ... Rufiji imekuwa ikikumbwa na mafuriko ya mara ... Rufiji, Mkoa wa Pwani Tanzania
 
Back
Top Bottom