Wenza wa vigogo kulipwa mafao

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Hakika inasikitisha sana na inaumiza sana kuona watumishi wa umma na wazee wastaafu wakiendelea kulipwa mafao kiduchu huku wenza wa vigogo wakiandaliwa sheria ya wao pia kulipwa mafao kama waume/wake zao wanapostaafu.

Mafao ya hao vigogo ambao ni rais, makamu wa rais na waziri mkuu wanapo staafu tayari ni makubwa sana lakini bado serikali inataka na wenza wao nao walipwe.

Japo sina uhakika kuna tetesi kuwa wazee wa mjengoni tayari wameongezewa ulaji kimya kimya huku watumishi wa umma wakisota na wazee wetu wastaafu wakiendelea kulipwa pensheni zisizokithi hata mshahara wa house girl licha ya kuitumikia nchi hii kwa uadilifi mkubwa.

Ombi kwa serikali
Pamoja na mabadiliko ya sheria inayotaka kuyafanya ili wenza wa vigogo walipwe mafao ni vema mabadiliko hayo yakawahusu watumishi wa umma na wazee wetu wastaafu kinyume chake huu utakuwa upendeleo wa wazi kwa kundi la vigogo.

Tanzania ni yetu sote.
758718553.jpg
 
Namtafakari sana Madeleka,Hasa ukizingatia amewahi kuwa mtumishi wa Polisi tena afisa.Kinachoshangaza zaidi Polisi wenzake hawajifunzi kwamba katika hali kama hii iko siko na wao yatawafika na itawapasa kujibu maswali magumu sana kwa watanzania wote
 
OMBI kwa SERIKALI
Pamoja na Mabadiliko ya Sheria inayotaka kuyafanya ili WENZA wa VIGOGO walipwe MAFAO ni vema Mabadiliko hayo Yakawahusu WATUMISHI wa UMMA na WAZEE WETU WASTAAFU kinyume chake huu utakuwa UPENDELEO wa WAZI kwa KUNDI la VIGOGO.
Huhitaji kuomba ni kuwaambia openly, huo ni wizi na uhuni, hiyo serikali haitakiwi kurudi madarakani uchaguzi ujao kwakuwa ni genge la wahuni, huwezi kuwalipa watu wasio watumishi wa umma wakati watumishi wanasota wala hakuna anayewasemea

Hii akili ni laana inayotokana na viongozi kula viapo ambavyo mwisho wa siku wana visaliti matokeo yake ndiyo huko kupumbaa akili na kuja na maamuzi ya kijinga kama hayo,
 
Hakika inasikitisha sana na inaumiza sana kuona Watumishi wa UMMA na Wazee WASTAAFU wakiendelea KULIPWA MAFAO KIDUCHU huku WENZA wa VIGOGO wakiandaliwa Sheria ya Wao pia KULIPWA MAFAO kama WAUME/WAKE zao WANAPOSTAAFU.

MAFAO ya hao VIGOGO ambao ni RAIS, MAKAMU wa RAIS na WAZIRI MKUU wanapo STAAFU tayari ni MAKUBWA sana lakini Bado SERIKALI inataka na WENZA wao nao WALIPWE.

Japo sina Uhakika kuna TETESI kuwa Wazee wa Mjengoni tayari Wameongezewa ULAJI Kimya KIMYA huku WATUMISHI wa Umma Wakisota na WAZEE Wetu WASTAAFU wakiendelea kulipwa PENSHENI zisizokithi hata MSHAHARA wa HOUSE GIRL licha ya kuitumikia NCHI hii kwa UADILIFI MKUBWA.

OMBI kwa SERIKALI
Pamoja na Mabadiliko ya Sheria inayotaka kuyafanya ili WENZA wa VIGOGO walipwe MAFAO ni vema Mabadiliko hayo Yakawahusu WATUMISHI wa UMMA na WAZEE WETU WASTAAFU kinyume chake huu utakuwa UPENDELEO wa WAZI kwa KUNDI la VIGOGO.

Tanzania ni YETU SOTE.View attachment 2743744
Hii ndiyo tunayoiita, aliyenacho ataongezewa maradufu!🙆
 
Hii inonyesha jinsi viongozi wa kiafrika walivyo walafi na wabinafsi.Madaraka walionayo ni ya kujinufaisha wao na familia zao.Aibu kubwa.Hivi hawaoni wananchi wanaowaongoza wanaishi kwenye Lindi kubwa la umaskini?Hakika Kuna siku si ajabu watajimilikisha nchi kwa jina la wawekezaji.
 
I don't understand why you're getting angry with me.

Mimi nimekukumbusha wajibu wako.

Wewe ni chawa na kazi ya chawa ni kusifia mabwana zake.

Sasa wewe unavuka mipaka unapata wapi ujasiri wakukosoa maamuzi ya mabwana zako?

Fikiria vizuri, uchawa ndiyo kazi inayokupatia ujira. Je, ukipoteza hii kazi utapata wapi kipato?
 
Barikiwa sana mtumishi! sema acha walipwe tu sasa tutafanyaje.Binafsi nlipendekeza kila mtu afundishwe matumizi sahihi ya Ak47 na awe na umiliki pia lakini naona watanzania hawako tayari,basi tuishi tu
Misitu iko mingi, ebu anzisha kundi la kigaidi uone kama hutapata watanzania walio tayari kukamata AK 47.
 
Huyo jamaa kwenye picha ana kichwa kama taahira fulani hivi.
Anyways, ndiyo Afrika na maajabu yake. Yapo mengi ya gizani. Hayo ni sehemu tu ya gizani.
 
Back
Top Bottom