Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Mwanahalisi walikuwa wanataja mafisadi ndani ya ccm wakiwemo mapacha wa3 na ccm wamekubali kwamba kweli hao ni mafisadi sasa we unataka waandike nini tena kuhusu hao mapacha wa3. Kazi iliyobaki ni kuwakumbusha magamba mengine mana RACHEL ime-expire.
 
Kijembe ambacho mmoja wa mapacha watatu wa ufisadi, Rostam Aziz Abdulrasul, alikirusha kwa Saed Kubenea kuwa anaweza kumnunulia mtambo wa kuchapishia gazeti lake la MwanaHalisi mapema mwaka huu, kimegeuka kuwa "azma iliyotimia" baada ya mwandishi huyo machachari aliyejizolea sifa kemkem kwa ujasiri kutiwa mfukoni na sasa ni sehemu ya majeshi ya Rostam ya kumlinda na kuwasambaratisha wabaya wake!

Kubenea ambaye mwaka juzi alishambuliwa na watu "wasiojulikana" na kumwagiwa tindikali machoni karibu apofuke, kasahau yote hayo na sasa ni silaha ya kuaminika ya Rostam katika kujihami dhidi ya kampeni kali ya CCM inayoongozwa na Katibu Mwenezi Taifa Nape Nnauye ili mkuu wake mpya Rostam abakie na gamba lake.

Taarifa za ndani kwenye duru za mwanahabari huyo zinasema kijembe kile cha kumnunulia Kubenea mtambo wa kuchapishia magazeti kimefanyiwa kazi na Kubenea yuko mbioni kupata mtambo mpya wa kisasa lakini kwa sharti la kuachana na habari hasi za Rostam na Lowassa kwenye gazeti lake na kuendesha kampeni kali dhidi ya msururu wa watu aliopewa katika miaka mitatu ijayo. Baadhi ya watu hao ni JK na familia yake, "Mtoto wa Mkulima", Magufuli, Chilligati, Nape, Sitta, Anne Kilango, Ole Sendeka, Lembeli, Mwandosya, Membe, Kinana, Mwakyembe, Mkuchika, Chatanda na Kigoda. Kubenea kakubali dili hilo ambalo tayari limemwingizia zaidi ya sh. milioni 20.

Gazeti la MwanaHalisi ambalo limekuwa kwa muda mrefu msumari wa moto kwa mapacha watatu wa ufisadi kutokana na Kubenea kuamini kwamba wawili kati ya mapacha hao watatu walihusika na mpango wa kumtoa roho au kumpa kilema cha maisha, halitabeba taarifa tena za Lowassa wala Rostam ila za wabaya wao hao.

Mathalan, toleo la kesho kutwa la MwanaHalisi tayari lina taarifa ndefu ya Daniel Porokwa akiwamwagia sumu "maadui" wa RA na EL bila kujali kuwa gazeti lake lilimwandika Porokwa mwaka jana kuwa kibaraka wa Lowassa baada ya kujitoa kugombea Ubunge jimbo la Monduli. Porokwa "alizawadiwa" kazi ya Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya, gari mpya aina ya NOAH, shilingi milioni 2, na ng'ombe kadhaa baada ya kujisalimisha na kukubali Lowassa amkanyage kichwani kwa mila eti ya Kimasai kama siyo ya kishirikina.
 
HTML:
Kubenea kakubali dili hilo ambalo tayari limemwingizia zaidi ya sh. milioni 20.
Milioni 20 ndio iuze uhuru wa mtu anayeheshimika na jamii?..Kwani angeshindwa kupata fedha hiyo kwa mtu msafi?
 
Kama ni kweli basi money can buy anything except peoples' power!!! Lakini nina wasiwasi mkubwa na mtoa mada hivi ni mtambo wa aina gani unaouzwa mil.20 labda tupe ufafanuzi kidogo!!
 
Kwahiyo hao jamaa uliowaorodhesha wasiandikwe kwenye Mwanahalisi wakiandikwa ETI kubenea katumwa.
 
Wewe lazima ni mtu wa Rostam na Lowassa. Futa kauri yako na omba msamaha kwa kumdhalilisha Kubenea. Haingii akilini eti mil.20 ni sawa na gharama ya maisha yake aliposimamia haki kupambana na tindikali.
 
Hayo kweli majungu wanaJF.lazima tujihadhali na hawa wavua magamba,coz kwanini wao wamewapa RA&ER plus mzee wa kuroga bunge zima siku zote hizo halafu leo wanakuja na story za KUBENEA,no no no no no no no no !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! mimi nasema no..hebu kesho tuamke na kauri kutoka kwa hilo kundi lililoorozeshwa hapo juu ikisema kwamba RA amenyang'wanywa uraia wake wa mda na amepewa masaa 24..na washikaji wake siyo tena wanachama wa ccm...hapo ndiyo ntaamini kuwa kweli KUBENEA kanunuliwa mtambo.....la sivyo wacheni longolongo bwanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.:dance:PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS!!!!!!!!!!!!!!!!!!! POWER.:dance:
 
MAFISADI HAWANA JIPYA WAMEDODA NA WAMEFULIA KISIASA..........................., bado naendelea kuamini kwamba mafisadi hawana jipya na watazidi kuchemsha na kundi lao lote na vijana wao wote wao ndio wanaopanga njama na kumuingiza madarakani kijana wao kutoka visiwani JAMAL KASSIM kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mh Masauni(Mb) naamini hawatafanikiwa hata kidogo....nasema hata kidogo.

-wacha wamnunulia Kubenea hata JUMBO MASHINE PRINTER nini hicho kikoroboi cha milioni 20-30, ila njama wanazozipanga hazitafua dafu hata kidogo wanaplan nyingi kuliko uwezo wao wa kufikiri, wanahela nyingi hawajui wazifanyie nini, wanakundi kubwa lisilo kuwa na tija, hakuna watakalofanikiwa hao. plan wanazotumia kumuingiza JAMAL KASSIM kuwa mwenyekiti UVCCM hazitafua dafu ni bora litibuke tusubiri mwakani 2012 kuliko hizo njama zao, kikao kilichokaliwa na hao vijana wao wa mwmvulia chini ya HUSSEN BASHE BASHE wasidhani havijulikani vinajulikana na wanayoyafanya yanajulikana.

-WANAPINGO KAMA IFUATAVYO: kama LOWASA hawi rais 2015 basi kijana wao EMENUEL NCHIMBI awe rais na LOWASA kuwa WAZIRI MKUU TENA hiyo ndio hesabu yao hata hili wataula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua, leo wamemgeuka mwanamama wao MARY CHATANDA kwa kuwa hakuweza kumsaidia demu wao BATILDA BURIAN kuwa mbunge ARUSHA MJINI sasa imekula kwao waendelee kuvurugana tu na kijana wao JAMES MILLYA mwalimu sijui shule ipi ya sekondari aendelee kutumika utadhani sio mmasai halisi.

-wanamthumu kijana wa watu bure MRISHO GAMBO bila sababu yeyote japo naye mwanzo alikuwa wao lakini hawakumpenda na baadae amejua ukweli sasa wanamuona mbaya, nchii kila aliyekataliwa na BABA W TAIFA MWALIM JULIUS KAMBARAGE NYERERE HAKUNA ATAKACHOFANYA KIKAKUBALIKA MILELE hata kama utamfanyia mtu madhali ni ww unafanya itakula kwako na hao unaowafanyia.

-LOWASA ALISHAKATALIWA NA BABA WA TAIFA watanzania wanajua hilo....................., Mzee kambarage alishawahi toa hundi ya DOLLA LAKI TANO AMBAYO LOWASA ALIHONGWA NA WAHINDI KUKIUZA KIPANDE CHA ARDHI LEO NDIO KUNA SHULE YA AGKHAN MZIZIMA PRIMARY SCHOOL, hii lilikuwa MKUTANO MKUU WA HALMASHAURI KUU 1995 watanzania hawajasahau na hawatasahau hilo. wakati huo alikuwa WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO.

-KUBENEA ATAKULA NAO SAHANI MOJA PAMOJA NA KUNUNULIWA HUO MTAMBO na hao aliotajiwa kuwashughulikiwa haita tokea mbona wanamiliki MAGAZETI YAO YA TAZAMA linatoka kila JUMANNE NA LIMESHINDWA KUFUA DAFU, WANAMILIKI MKAKATI linatoka kila IJUMAA nalo limeshindwa kufua DAFU? NINI WANATAPA TAPA HAWA WATU? WAMEFULA.

-WAMEKULA YA MBUZI WATAOTA MAPEMBE.............................!!!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Milioni 20? Si angelisema tu Chadema wakamchangia? Na tena Wabunge tu wachache wangelimpa.

Huu ni uwongo wa hali ya juu kuwa mitambo kama hiyo iuzwe kwa bei ya Euro 10,000/-
 
Milioni 20? Si angelisema tu Chadema wakamchangia? Na tena Wabunge tu wachache wangelimpa.

Huu ni uwongo wa hali ya juu kuwa mitambo kama hiyo iuzwe kwa bei ya Euro 10,000/-

Homeboy

Jamaa anauza story hakuna kitu kama hicho! Ni vita wanapigana Magamba hao wanajaribu kumtumia Kubenea kama AK47. Kubenea is not that much cheap. Wanajua Magazeti yao ya Uhuru, Mzalendo, Habari leo hayauziki.
 
Huyu mtoa mada katumwa na wanaotuhumiwa kutaka kujiunga na ccj.haiingii akilini issue ya parokwa kuandikwa kwenye mwanahalisi ni mpango wa rostam.nasema hivi wote wameandika issue ya parokwa lakini s.kubenea jumatano atahitimisha.
 
Back
Top Bottom