Kubadili sheria kuwa kwa Kiswahili hakuna budi kwenda sambamba na kubadili mitaala iwe ya Kiswahili

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,111
Huwezi kutaka sheria ziwe kwa lugha ya Kiswahili, halafu wakati huohuo unawatrain wanasheria wako kwa Kiingereza, kufanya hivyo ni kujaribu kuweka mkokoteni mbele ya punda ausukume kwenda mbele.

Kitu cha kuzingatia katika maamuzi haya ni Je, Taifa limejiandaa kikamiifu kutunga sheria na kuendesha kesi hasa zile zenye kuchangia rejea ya kisheria kwa kiswahili?

Je, huko vyuo vyetu vikuu na shule za sheria (Law schools) wamejiandaaje kutoa wahitimu ambao mazingira yao ya kazi ni kwa lugha tofauti na ile wanayowafundishia?

Ninachokiona uamuzi huu japo ni mzuri, lakini unahitaji mabadiliko makubwa sana ya kimfumo ili uweze kuleta tija. Tusipobadili mitaala ya masomo ya sheria tutaishia kupata KISWANGLISH kwenye majadiliano ya mahakama zetu na pia KISWANGLISH kwenye hukumu.

Lakini hofu yangu nyingine ni je, iwapo mahakimu wetu watafanya rejea ya kesi za nje kwa kuzitafsiri ili tafsiri hizo ziwe msingi wa hoja za maamuzi yao, ni mahakimu wangapi wamesomea lugha ili tuweze kuthibitisha kuwa tafsiri zao hizo ni sahihi ii ziweze kuwa rasmi?. Maana kujua lugha ya kuongea ni jambo moja lakini kuwa na tafsiri sahihi ya jambo la kisheria kwenye lugha mpya ni jambo jingine! Ndiyo maana sheria huandikwa kuwa panapotokea changamoto ya tafsiri kwenye vifungu fulani basi tafsiri kwenye Lugha X ndiyo Final!

Nimebahatika kuisoma hukumu ya yule Jaji aliyoitoa kwa Kiswahili, Jaji amejitahidi sana hata hivyo ndani yake bado kuna VISWANGLISH.

Sasa tuamue moja, tusiwe uvuguvugu. Tukamilishe mzunguuko mzima unaofundisha sheria, unaotunga sheria, unaosimamia sheria na unaotafsiri sheria vyote hivyo viwe kwenye lugha Moja. A sivyo hukumu za majaji wetu zitashindwa kufanywa rejea na wenzao duniani kwa sababu zitakuwa katika lugha isiyotumiwa na wengi duniani. Lakini hata wao itakuwa vigumu kufanya rejea katika hukumu za wenzao na kuziandika katika lugha ya pili ambayo rejea hiyo haikuandikwa pindi ilipoandikwa!
 
Hofu yangu ni kuwa tutaenda kuwa kisiwa katika zama hizi za utandawazi.

Mawakili wetu hawatapata kazi za kimataifa.Uelewa wetu wa sheria za kimataifa utapungua.

Mimi ningependa tutumie lugha zote mbili.Na hata ikiwezekana tuongeze lugha nyingine m9ja ya kimataifa.
 
Hofu yangu ni kuwa tutaenda kuwa kisiwa katika zama hizi za utandawazi.

Mawakili wetu hawatapata kazi za kimataifa. Uelewa wetu wa sheria za kimataifa utapungua.

Mimi ningependa tutumie lugha zote mbili. Na hata ikiwezekana tuongeze lugha nyingine m9ja ya kimataifa.

Siku akitoka rais huyu madarakani tutarudi kwenye utaratibu wa kawaida. Ni suala la muda tu.
 
Siku akitoka rais huyu madarakani tutarudi kwenye utaratibu wa kawaida. Ni suala la muda tu.
Kuna kitu Magufuli alisahau kutoa maagizo kuwa hata madaktari waandike madawa kwa kiswahili na pia dawa ziandikwe Kiswahili.
 
Mwalimu amewahi kusema kuwa "nia njema yaweza kuwa na maangamizi tele"

Haya masuala ya kufanya mambo kwa jina la uzalendo baadae yanaweza kuwa counter productive

Huwezi Kutaka Majaji na Mahakimu watoe hukumu kwa Kiswahili wakati wamesomea sheria kwa Kiingereza!

Ili twende sawa, Masomo yote yanayozalisha wanasheria kuanzia Masomo ya Arts inabidi yafundishwe kwa Kiswahili
 
Hii yote ni kwa sababu mwenyekiti wa chama hajui lugha ya malkia, what a shame
 
Kiswahiri kikirudi shuleni kwa ajiri ya kufundishia, namimi narudi shule kusoma! Lazima nitakuwa electric eng mzuri na kujiajiri mwenyewe.
Hongera magufuri.
 
Back
Top Bottom