Kuachana au kutengana??

Duuh! Lizzy kwani we Sheikh Yahya!?

Nimekutana na kisa kama hiki last week.
na yuko desperate anataka kuoa,ana mtoto wa miaka 8 mke kamkimbia kasema amechoka.hawajaachana kisheria..

Mi hapo naona huyo bado ni mume/mke wa mtu..
siki mwenza wake atakapoamua kubadili mawazo na kutumia kigezo kuwa hawakuachana kihalali huna chako hapo
na wengine hufanya hivyo makusudi kumkomoa mwenzake.
SD hiyo wala haisumbui,njemba kama inataka kuoa iende tu kwa Pilato iombe talaka,atapewa tu maana mahakama hazina utamaduni wa kulazimisha ndoa hasa pale inapong'amua maji kwenye ndoa yamezidi unga. Baada ya talaka yeye aoe tu wala haina shida.Ila kama ni wakristu hasa wakatoliki hataweza kukomunika for life, in that case apime imani vs utashi wa roho na mwili wake.
 
Habari zenu wapendwa!
Leo naomba niwaulize swali.Umekutana na mwanamke/mwanaume ambae aliwahi kua kwenye ndoa na anakwambia bila maelezo ya ziada!Baada ya kua karibu sana unaona uulize kidogo chanzo cha kuachana..muda waliokua pamoja na muda gani tangu wameachana!Unapata majibu yako ila la tatu anakujibu kwamba imepita muda fulani tangu tumetengana..labda tuseme zaidi kidogo ya mwaka!Ndoa haijavunjwa kisheria ni wao tu hawaishi pamoja!

Je mtu kama huyo achukuliwe kama bado ni mke/mume wa mtu?
Naomba maelezo zaidi ya kuvunjwa kwa ndoa kisheria kwako inamaanisha nini labda. Kabla sijachangia maana ndoa ni za aina nyingi kweli na kuachana kwake si lazima iwe kama wengi tunavyofahamu na hata neno ndoa lenyewe lina maana nyingi kwa kila mtu.
 
Hapo sasa SweetDada!Na mimi nna mawazo kama yako ila imebidi niulize baada ya mtu kunibishia!Imagine mtu akija kukwambia achana na mume wangu sijui utatumia kigezo gani kumbishia!
So long as kuna talaka hiyo lugha ya 'achana na mme wangu' itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,haitakuwa na maana yoyote labda naye akushawishi utoe talaka kwa huyo mpya ili muoane mu remarry.
 
hao bado ni mke na mume tena ukizingatia mafundisho ya dini kama ya kwangu talaka haipo,siku wakiamua kurudiana sijui utasemaje dear.labda uwe na bahati ya kukutana na wale wenye misimamo wakiamua hawarudi nyuma nao ni moja kati ya kumi wengi wanatafuta mahali pa kutuliza stress zao zikiisha wanarudi nyuma.
Kisheria talaka ipo,kiimani ndo inategemea,legally unaweza kuachika tu no problem.
 
Naomba maelezo zaidi ya kuvunjwa kwa ndoa kisheria kwako inamaanisha nini labda. Kabla sijachangia maana ndoa ni za aina nyingi kweli na kuachana kwake si lazima iwe kama wengi tunavyofahamu na hata neno ndoa lenyewe lina maana nyingi kwa kila mtu.
Kuvunjwa kwa ndoa kisheria...pande zote mbili kusaini kwamba hawako pamoja tena!Kutotambulika kisheria kama wanandoa!
 
So long as kuna talaka hiyo lugha ya 'achana na mme wangu' itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,haitakuwa na maana yoyote labda naye akushawishi utoe talaka kwa huyo mpya ili muoane mu remarry.

Kama talaka haijatolewa ndo tatizo sasa...kuachana kienyeji kwa maana nyingine!
 
Utanitoa lunch kesho!Haya mwaga mabusara!
asavali siku hizi umekuwa mwanafunzi mtiifu. ok kamata kalam na karatasi uandike hii.

separation/kutengana ni situation ambayo mke na mume wanapeana distance lakini kisheria wanabaki kuwa bado ni wanandoa, mnaweza mkaifanya separation yenu kuwa "legal separation" kwa kwenda kusaini mkataba flani mahakamani, mkiwa kwenye separation right za ndoa zinabaki pale pale. Divorce inavunja rights zote za kindoa na kiurithi baina ya wanandoa. Hivi vitu kwa bongo ni tabu kuona effect yake lakini kwa europe vina athari kubwa sana kwavile wengi wanawekeza kwenye "ndoa" na "government social benefits"

naomba nisiulizwe suali la ziada. haya endelezeni sredi
 
Haya tena
Duuhh hilo sikufahamu
Wa weza ni ambia sehemu ipi ya
bible nikasoma
Na mie nipate ujuzi zaidi..
Ni kweli AD,yapo mazingira ambayo wakristu (hususani wakatoliki na waluteri) hutoa talaka.Kwa wakatoliki iko mahakama maalum Vatican ambayo husikiliza kesi hizi na kutoa hukumu itakayomruhusu mke/mme kuoa au kuolewa tena.
 
Kama talaka haijatolewa ndo tatizo sasa...kuachana kienyeji kwa maana nyingine!
Lizzy na hayo ndo makosa makubwa sana ambayo huwa tunayafanya.X anaachana na Y kisha hawaendi mahakamani kuomba talaka.X anavuta kimwana mpya anaishi naye.Jamii nzima inawatambua kuwa ni 'mke' na 'mme'.Wanazaa watoto,wanalea na wakati huo huo wanafungua biashara wanajenga ,mradi maisha yanakuwa muruuuwa. Siku ya siku tena ghafla bin vuu mme ndee presha anadondoka chini na kurudi kwa muumba wake.Pekua pekua makabrasha mzee hakuacha mirathi.Hapo ngoma inogile maana so called ex-wife atatinga msibani na cheti chake cha ndoa, utake usitake yeye na wanae watarithi kila kitu na huyu aliyetafuta mali na marehemu ataambulia sifuri na wanae,law is an ass,mambo ya sheria hayo! Ushauri wa bure njemba/dem akikuzengua tafuta makaratasi kabisaa mahakamani,ikitokea baby come back hakuna kizuizi kaoaneni upya kwa DC.
 
me nadhani anakua ni mketu linapokuja suala la recognition.yani mfano mmoja wao anataka kugombea ka nafasi fulani, au recognition kisheria lakini tukija katka sense ya mke/mme huwezi sema huyo ni mke wako mtu ambae moyo wako upo mbali nae, humhitaji kimwili wala kimawzo, hamjaonana wala hamtamani kuonana kwa mda wote mnaokua mmetengana n.k.

sasa mtu kama huyo ukaja kumkuta na mimba/mtoto utamlaum kua alikusaliti?
 
majibu yamepatikana kama alikuwa anataka kukufuata ww baada ya kutengana na mke wake mwambie yeye bado ni mume wa mtu
 
Ni kweli AD,yapo mazingira ambayo wakristu (hususani wakatoliki na waluteri) hutoa talaka.Kwa wakatoliki iko mahakama maalum Vatican ambayo husikiliza kesi hizi na kutoa hukumu itakayomruhusu mke/mme kuoa au kuolewa tena.

Ninachotaka kueleweshwa
ni kama ipo kwenye bible
Maana haya makanisa siku hizi yana zidi
kuongeza sheria fulani fulani hivi..

Ninachoomba nikuelezwa kama iko kwenye bible
Na ni sehemu gani ?

Ps...samahani lizzy
Kwa kuchakachua thread..
 
me nadhani anakua ni mketu linapokuja suala la recognition.yani mfano mmoja wao anataka kugombea ka nafasi fulani, au recognition kisheria lakini tukija katka sense ya mke/mme huwezi sema huyo ni mke wako mtu ambae moyo wako upo mbali nae, humhitaji kimwili wala kimawzo, hamjaonana wala hamtamani kuonana kwa mda wote mnaokua mmetengana n.k.

Japo kihisia sio sahihi kisheria inahusu zaidi maana mtu akikufata akakwambia huyu ni mke/mume wangu huwezi kupinga!
 
Ninachotaka kueleweshwa
ni kama ipo kwenye bible
Maana haya makanisa siku hizi yana zidi
kuongeza sheria fulani fulani hivi..

Ninachoomba nikuelezwa kama iko kwenye bible
Na ni sehemu gani ?

Ps...samahani lizzy
Kwa kuchakachua thread..
Niko njiani sasa hivi mpnz...ngoja nikitulia ntakwambia!
 
Back
Top Bottom