Kuachana au kutengana??

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,778
59,133
Habari zenu wapendwa!
Leo naomba niwaulize swali.Umekutana na mwanamke/mwanaume ambae aliwahi kua kwenye ndoa na anakwambia bila maelezo ya ziada!Baada ya kua karibu sana unaona uulize kidogo chanzo cha kuachana..muda waliokua pamoja na muda gani tangu wameachana!Unapata majibu yako ila la tatu anakujibu kwamba imepita muda fulani tangu tumetengana..labda tuseme zaidi kidogo ya mwaka!Ndoa haijavunjwa kisheria ni wao tu hawaishi pamoja!

Je mtu kama huyo achukuliwe kama bado ni mke/mume wa mtu?
 
haswa ni mke/mume given that muda sio mrefu tokea watengane na sio kisheria.
Kidini ndoa haitengani.
 
Duuh! Lizzy kwani we Sheikh Yahya!?

Nimekutana na kisa kama hiki last week.
na yuko desperate anataka kuoa,ana mtoto wa miaka 8 mke kamkimbia kasema amechoka.hawajaachana kisheria..

Mi hapo naona huyo bado ni mume/mke wa mtu..
siki mwenza wake atakapoamua kubadili mawazo na kutumia kigezo kuwa hawakuachana kihalali huna chako hapo
na wengine hufanya hivyo makusudi kumkomoa mwenzake.
 
Hapo sasa SweetDada!Na mimi nna mawazo kama yako ila imebidi niulize baada ya mtu kunibishia!Imagine mtu akija kukwambia achana na mume wangu sijui utatumia kigezo gani kumbishia!
 
hao bado ni mke na mume tena ukizingatia mafundisho ya dini kama ya kwangu talaka haipo,siku wakiamua kurudiana sijui utasemaje dear.labda uwe na bahati ya kukutana na wale wenye misimamo wakiamua hawarudi nyuma nao ni moja kati ya kumi wengi wanatafuta mahali pa kutuliza stress zao zikiisha wanarudi nyuma.
 
bado yupo ndani ya ndoa unless wangeachana kisheria....................kusoma hujui hata picha tu kwamba ni mbuzi au mbwa,we vp
 
Lizzy! Hao bado ni mke na mume, walichofanya ni kujipa nafasi ya kujiachia kivingine. Hata wataaram wa mambo ya familia huwa wanatoa option ya distancing for sometimes up to 2yrs
 
bado yupo ndani ya ndoa unless wangeachana kisheria....................kusoma hujui hata picha tu kwamba ni mbuzi au mbwa,we vp

Hahaha umenifurahisha kweli!Ila tatizo utakuta mtu anadai sisi tumeachana bwana...ukiwaambia wametengana wanasema sio!
 
Lizzy! Hao bado ni mke na mume, walichofanya ni kujipa nafasi ya kujiachia kivingine. Hata wataaram wa mambo ya familia huwa wanatoa option ya distancing for sometimes up to 2yrs
Inabidi watu wajifunze tofauti ya kuachana na kutengana!Wengine wanadhani ni kitu kimoja!
 
Daahh huyo lazima bado atakuwa mume/mke
Wa mtu kisheria
Kidini hao mpaka kifo (Christian)
 
Kifo na kesi ya kucheat"!!!

Kwa mimi ninavyoelewa
Watu kama walikuwa wamefunga ndoa
yaani ndio hivyo mpaka
kifo kiwatenganishe..
Wanaweza waachane au kutengana
Kwa sababu mbali mbali za maisha
kama kucheat, ugomvi, abusing, seek of seeing
each other every day etc ..

Lakini hayo ni ya dunia ,Mbele za Mungu
Wako pamoja ...

Wanaweza wapeane divorce na hizo ni rules nyingine
tu za dunia..
 
kuna tofaut gan tupe darasa

Kutengana mnakua mbali physically ila ndoa bado inaexist kwenye makaratasi!Hapo watu wanakua bado ni mume na mke na kurudiana ni kiasi cha kuitana tu...mke/mume wangu rudi nyumbani!Kuachana ni pale kila mmoja anachukua njia yake rasmi bila kua na chochote kuwatambulisha kama wanandoa! Mnapoitana ex wife and hubby!
 
Mmmh wametengana hao, hasa ukizingatia na mtoto wanaye.
 
Kwa mimi ninavyoelewa
Watu kama walikuwa wamefunga ndoa
yaani ndio hivyo mpaka
kifo kiwatenganishe..
Wanaweza waachane au kutengana
Kwa sababu mbali mbali za maisha
kama kucheat, ugomvi, abusing, seek of seeing
each other every day etc ..

Lakini hayo ni ya dunia ,Mbele za Mungu
Wako pamoja ...

Wanaweza wapeane divorce na hizo ni rules nyingine
tu za dunia..
Biblia inatambua kuvunjika kwa ndoa kama uaminifu hamna!
 
separation na divorce ni vitu viwili tofauti katika sheria. naomba rushwa ili nitoe ufafanuzi zaidi
 
separation na divorce ni vitu viwili tofauti katika sheria. naomba rushwa ili nitoe ufafanuzi zaidi

Siku yako imeisha, hata hukunialika nije kusherehekea na wewe!!
Rushwa inaua, usipende kupokea rushwa.
Lete mchango huko.
 
Back
Top Bottom