Kuacha kazi kufanya ujasiriamali

Ndugu Chasha suala la kuongeza elimu while doing business ni jambo la kawaida,wengi imewezekana na jamaa kasema wife yupo nyumban so ni msaada tosha...kuongeza elimu kuna faida nying,kama ni muajiriwa utazijua,baadhi tu ni kipato kuongezeka,heshima,kukuza uelewa na assurance ya kuongeza mafao pale utakapostaafu.

Ma prof ndo maprof tunawaona wanalilia kuongezewa mikataba baada ya muda kufika, so kumbe watu wanaongeza elimu ili waheshimiwe na wapate mafao mengi? Dah nilikuwa silijui hili
 
Mkuu kujitosa katika kitu chochote bila preparation sio ujasiri bali ni upunguani..., katika kila maisha yako inabidi kuwa na plan B, na kufanya calculated risks.., na hapa tunaongelea miradi na kujiongezea kipato ila wewe unachanganya na running multi million corporations.., hivi kuna ubaya gani kama huyu mtu anavuta mkwanja wa kutosha kazini kwanini asianze kwanza part time (gaining experience) na kufanya investments kwenye vitu kama real estate n.k. vitu ambavyo anaweza kutumia leverage (efforts of others) to make money, pia kufanya investments tofauti (not putting ones eggs in one basket) hence anakuwa ame-hedge risk, baada ya hapo hata atakapoacha kibarua chake will have somewhere to fall upon...,

Akifukuzwa kazi amefukuzwa kazi hio ni part ya maisha sio sababu anaweza kufukuzwa kazi ndio aache kazi leo kabla ya kujitayarisha.., cha maana narudia (kama kazi yako ina kipato cha kutosha) tumia hicho kipato ku-hedge risk kwa investments ndogo ndogo hata utakapoacha kazi kunakuwa na fedha ya kujihifadhi in a rainy day..., sio unaamua kuacha kazi leo wakati hata pesa ya mwenye nyumba hujamalizia kumlipa.

Huu msemo wa kuchoma meli ni just msemo.., huyo jamaa yako alichoma kabisa na vyeti vyake au ?..., sababu anaweza akakwambia hivyo ila deep down when push comes to shove angeweza kuanza kutuma applications tena (if he is employable), pia cha maana ni kwamba aliacha nini na kwenda kufanya nini ? (hapo keyword ni kufanya nini.., sio kuamua kuacha kazi kama CEO fulani alafu kuamua kwenda kuendesha bodaboda yake.., sababu hata hii ni biashara)

Hapa tubaisha hadi mwaka ujao, Ila ukweli ndo huo, na Kwanza elewa ishu ya kuacha kazi haihitaji ushauri make ndo kama huyu jamaa anakuja kukutana na waajiriwa halafu wamshauri, unatakiwa kujilipua mwenyewe,

Hivi kwako biashara ni ipi? Hizi kampuni zote unazo ona leo zilianza chini kabisa, hakuna kampuni hata moja hapa Duniani iliyo ibuka ghafla, makumpuni yametoka mbali sana, Tatizo wewe unazani biashara ya Toyo sio biashara, hakuna biashara kubwa wala ndogo, mtu anaweza anza hata kuuza karanga na baadae akaja kuwa msambazaji wa karanga hata Africa nzima, ishu ni wewe uko commited kiasi gani,

Wewe ma CEO kwako ndo unaona watu wasio takiwa kuacha kazi ila wafagiaji ndo wanatakiwa kuacha, Mkuu naomba mimi niishie hapa make hutakaa unilewe milele

In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure. – Bill Cosby
 
Mkuu swala la kuacha kazi si kwamba ni mpaka uwe na uhakika wa 100% wewe hutakaa uelewe na najua wewe ni moja wa wahanga wa kazi, ni vigumu sana na mwajiriwa kutoa ushauri wa mtu kuacha kazi, ni kitu ambacho hakipo.

Mkuu hivi nikikwambia sijawahi kuajiriwa maishani mwangu utakubali ?, thats the reality..., ndio narudia yule mtu anaruka au kukanyaga kwenye shimo bila kuangalia kuna nini au kama kuna kitu cha kumuumiza basi ana matatizo..., vilevile in business word mtu anayeingia kwenye biashara fulani bila kujua ile biashara (uhakika na hio biashara) kwa kufanya due diligence na kujua Strength, Weaknesses, Opportunities, na Threats za hio business.., basi sio mfanyabiashara bali ni gambler.., hakuna tofauti na kufanya betting au kucheza kamali (pata potea), sasa huyu mtu akiamua kuacha hata alichofanya sasa ili kujaribu hiki kingine bila kuwa na uhakika anachokifanya basi atakuwa punguani.

Jaribu kusoma story ya MUGUKU, huyu jamaa sasa marehemu aliacha kazi ya ualimu na kila mtu alimshangaa nan kufikia mhali Wazazi wake kuamini kabisa mtoto wao kachanganyikiwa but yeye alikuwa amekwisha amua moja.
Again point yangu ipo pale pale aliacha huo ualimu ili aende kufanya nini (biashara ipi), sababu hata mimi ninamjua mwalimu mmoja aliacha kazi akaamua kuanza kuuza electronics, matokeo yake sababu ya biashara ya huku ilivyo watu wasumbufu, wanataka bei ndogo na uduni wa products za China hivi sasa anagongea hata nauli..., wakati kipindi kile alikuwa anafanya biashara ya kufundisha hata tuition na hata angeweza labda kutunga na kuuza materials ya masomo yake ingekuwa a better alternative, pia kumbuka huyo Muguku kuacha kwake Ualimu angeweza anytime akaenda sehemu na kupata kazi sio kwamba alichana vyeti vyake.

Ukikalia kwamba mimi ni bosi, natumia gari la shirika na kazalika huta kaa uwe na hii spirit, Watu wanaacha kazi za mamilioni na kwenda kuanza kazi za kuingiza elfu kadhaa badala ya mamilioni, usikalie kwamba uache kazi leo halafu wiki ijayo uwe tajiri make ndo za wabongo, anataka aanze leo then kesho awe biulionare, MUGUKU pamoja kwamba watu walimshangaa ila baadae mpaka anafaliki alikuwa kwenye top 5 ya matajiri wakubwa kabisa nchini Kenya,
Yees hao watu wanaoacha kazi za mamilioni wanakuwa tayari wameshaweka a plan in hand wanakuwa na plan B tayari sababu baada ya kusave hayo mamilioni hata kwa miaka mitano wanakuwa tayari wamesave vya kutosha na kuweka investments nyingine ndogo ndogo za kuweka mambo sawa.

Ujasirinali ni process ni safari ndefu sana na uoga ndo adui mkuwa sana, mbona wakina Edson walifeli mara nyingi but walikuja kufanikiwa, usikae kuwaza mishahra mikubwa kwamba ndo ikufanye usiache kazi,
Ofcourse ni process na safari ndefu that's why plan ni ya lazima, alafu hao wa kina Edson alikuwa ni inventor ambaye alikuwa na team ya watu wabunifu (at one time even Tesla alimfanyia kazi) kwahio kuanza kumfananisha willy nilly na mtu aache tu kazi for the sake ya kuacha kazi nadhani ni silly.., Pia inabidi tuangalie kwanini mtu anafanya kitu in the first place.., mwingine mapenzi ya kitu (feel good factor) mfano kufundisha..., mwingine mfano anachokifanya kinahitaji institution fulani ili akifanye..., au utasema pia mtu kama Messi aache kucheza mpira aende akafanye biashara yake (ni biashara ipi ambayo ataingiza pesa kama ile yeye kama Messi) au utamshauri aendelee kucheza huku anatumia kujulikana kwake yeye kama product ili aendelee kuingiza pesa through sponsorship na matangazo
 
Hivi kwako biashara ni ipi? Hizi kampuni zote unazo ona leo zilianza chini kabisa, hakuna kampuni hata moja hapa Duniani iliyo ibuka ghafla, makumpuni yametoka mbali sana, Tatizo wewe unazani biashara ya Toyo sio biashara, hakuna biashara kubwa wala ndogo, mtu anaweza anza hata kuuza karanga na baadae akaja kuwa msambazaji wa karanga hata Africa nzima, ishu ni wewe uko commited kiasi gani,
Kwahio labda unamshauri mtu aache kazi ili kwanza aanze kuuza karanga ili baadae akue na kusambaza africa nzima ?, Au hii kazi anaweza kufanya research ya masoko na kutafuta mauzo na kuweza ku-supply kwa watu in container loads na polepole kujenga mahusiano na watu..., nadhani mkuu inabidi ujiulize tofauti ya kufanya kazi effective na kufanya efficiently...

Wewe ma CEO kwako ndo unaona watu wasio takiwa kuacha kazi ila wafagiaji ndo wanatakiwa kuacha, Mkuu naomba mimi niishie hapa make hutakaa unilewe milele

In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure. – Bill Cosby
Mkuu nasema tena inategemea unaacha nini na kwenda kufanya nini wewe kama CEO unaweza kuacha kazi yako na kufungua firm yako na kufanya kile kile kwa makampuni tofauti kwa ku-outsource kazi yako ila sio uache kazi ya kipato kikubwa na kwenda kufungua genge la kuuza nyanya (hio sio efficiency)..., ila kama wewe ni mama lishe umeajiriwa unapika na kuuza chakula kwa wateja (mtaji sio mkubwa) ni bora na rahisi kuanza kupika na kuwasambazia wateja walewale chakula kilekile ila tofauti hapa profit itakuwa kubwa.

Hapana usiishie hapa..., hapa tueleweshane kwa hoja.., naomba ujifanye wewe ndio huyu Bwana mwenye laki tano yake kwa mwezi unamwambia aache kazi leo akafanye biashara gani hio inayohitaji muda wake 100%, ambayo asingeweza kuanza polepole na kwa kujitayarisha kwa investments ndogo ndogo part time
 
Kwahio labda unamshauri mtu aache kazi ili kwanza aanze kuuza karanga ili baadae akue na kusambaza africa nzima ?, Au hii kazi anaweza kufanya research ya masoko na kutafuta mauzo na kuweza ku-supply kwa watu in container loads na polepole kujenga mahusiano na watu..., nadhani mkuu inabidi ujiulize tofauti ya kufanya kazi effective na kufanya efficiently...

Mkuu nasema tena inategemea unaacha nini na kwenda kufanya nini wewe kama CEO unaweza kuacha kazi yako na kufungua firm yako na kufanya kile kile kwa makampuni tofauti kwa ku-outsource kazi yako ila sio uache kazi ya kipato kikubwa na kwenda kufungua genge la kuuza nyanya (hio sio efficiency)..., ila kama wewe ni mama lishe umeajiriwa unapika na kuuza chakula kwa wateja (mtaji sio mkubwa) ni bora na rahisi kuanza kupika na kuwasambazia wateja walewale chakula kilekile ila tofauti hapa profit itakuwa kubwa.

Hapana usiishie hapa..., hapa tueleweshane kwa hoja.., naomba ujifanye wewe ndio huyu Bwana mwenye laki tano yake kwa mwezi unamwambia aache kazi leo akafanye biashara gani hio inayohitaji muda wake 100%, ambayo asingeweza kuanza polepole na kwa kujitayarisha kwa investments ndogo ndogo part time

Kwani Nyanya sio Biashara? Usikalili kwamba biashara ya heshima ni lazima uwe unauza Magaru Used kutoka Japani, Uuze sijui simu, inategemeana Idea yake imekee vipi, anaweza hata akaanza project ya kuuza karanga, ila all in all inategemeana yeye anamalengo gani,

Wewe unazania akianza kuuza nynya ataonekana mjinga?
 
Hivi umesoma nilichoandika au ? Wapi nimesema kuuza nyanya sio biashara ? Rudia tena kusoma..., kuacha kazi inayomuingizia kipato kikubwa ili auze genge la nyanya anaweza akaziuza effectively ila hio sio efficiency (why ?, sababu angeweza akaweka mtu pale akamuuzia hizo nyanya na yeye kuendelea na kazi yake). Its all about opportunity cost
 
Aongeze elimi ili iweje? apate mshahara mkubwa au, Ujasirimali si ishu ya kitoto huwezi practise vitu viwili at the same time ni lazima uamue moja,

Kwa hiyo utaniambia pia huwezi kuanzisha biashara zaidi ya moja kwa wakati mmoja!?? Hivi Mengi anaendeshaje biashara zake? Cocacola, itv, radio one, mambo ya madini nk? Inategemea wewe ni smart kiasi gani ktk kuplan mambo yako, unaweza ukaanza huku unafanya kazi then as the business grow unajicomit 100% kwenye biashara tu.
 
Wakuu, endeleeni kubishana wengine tunanufaika sana na mbishano huu.. Pande zote mbili Zinaongea point zenye kujenga... Tafadhari Rudini tena tuendelee na shamba darasa.
 
Wakuu, endeleeni kubishana wengine tunanufaika sana na mbishano huu.. Pande zote mbili Zinaongea point zenye kujenga... Tafadhari Rudini tena tuendelee na shamba darasa.

Hata mimi natamani waendelee na mjadala wao una manufaa sana.
 
Asikwambie MTU.hakuna biashara ambayo unatia pesa yako alafu unamuacha MTU.pesa itapotea na utabaki kama mwanzo.biashara haitaki ukae mbali na pesa yako.kama umeamua moja simama na uamuzi wako.pigs chini kazi komaa na unachokiamini.last matunda utayaona tu.
 
Mleta post kulingana na maekezo yako sikushauri kuacha kazi cha msingi ambacho naona apo dom na kwa akiba ulionayo fanya utafiti wa mahali apo then fungua tigo pesa na Mpesa (kulingana na mtaji wako) before that fanya uchunguzi wa eneo husika kuhusu hyo business ata kama utapatapa commission ya laki 3 deducting running cost unakuta unasave kama laki 2 (this is minimum approximation)
 
Mkuu nisha sema kuacha kazi na kuingia kwenye ujasirimali si ishu ya kitoto, najua watu wanahofia kuchekwa, kutengwa, kuachwa na kazalika, hivyo kama hizo ndo sababu ni bora mtu akakomaa na kazi tu, Kwenye biashara kuna risk hata ukisema biashara ikue kwanza ipo siku unaweza jikuta biashara yako imesambaratika unatakiwa kuanza mwanzo, je hapo familia haitasambaratika? hizo ni sababu mfu.

Kinacho takiwa ni kukaa na kuelimisha familia yako, kwa sababu kama ishu ni familia kusambaratika je ukifukuzwa kazi itakuwaje?

Kuchoma Meli moto ni kazi moja ngumu sana yenye uchungu wa hali ya juu, nakumbuka kuna jamaa angu alifanya zoezi kama hili la kuacha kazi na kuingia kwenye business huku akilia sana, ila alisha amua moja, hivyo ni lazima uamue moja,
Unaonekana ni muoga saana
 
Kaka kauli ya kusema mtaji ni mdogo sii nzur lakin kwa hapa imebeba maana kubwa kama ume weza kukusanya 1m kwa miaka 3 inamaanisha matumizi yako yanafikia 540000 kw mwenzi je kuna biashara utakayo weza kuanzisha kwa 1m na ikupatie faida 540000 kwa mwezi ili ukithi mahitaji ya kila siku nyumban jibu ni jepes hapo fikiria ishu nyinge abayo haita kulazim kuacha kaz kwa sasa
 
Karibu kampuni ya Rifaro Africa ujipatie kipato cha ziada..mm ni mfanyakaz kama ww mshahara wangu ni sh. Lk4 lakin tangu niingie katika biashara hii napata sh lak 5 au 6 katika week mbil au tatu na sijaacha kaz kilicho nifanya nifike hapa ni juhud pia kujiamin kwa kile nacho Fanya..
Karibu ujaribu
Maelezo zaid 0765650028watsaap
0652703803call ntakueleza juu ya biashara na maamuz yatabak kuwa yako.asante
 
Mtu mwenye wazo la kuacha kazi ya kuajiriwa si la kuomba ushauli maana hakuna hata mmoja atakaekushauli uache hiyo kazi cha msingi simamia unachokiamini na niwatu wachache waliokua majasiri wa kuacha kazi za kuajiriwa lakini hao wengi wamefanikiwa kwa sababu ya kua na malengo na moyo wa kufanya wanachokiamini.
 
Hii mada ingetakiwa tupate mrejesho... Kama je mshikaji aliacha kazi au aliamua kufanya nini baada ya kushauriwa ni takribani miaka miwili now tangu a post ...huenda mke alipata kazi au alimtimua au aliongezewa mshahara au ...
 
Usiache kazi;jitahd kwa namna yyte upate kianzio/mtaji toka kwenye kazi hyo;mtaji waweza kua kwa kukopa bank au saving za kila mwisho wa mwezi;Buni biashara kulingana na mazingira uliyopo;then wekeza juhudi ktk kuikuza hyo biashara;USISAHAU KUMWOMBA M.MUNGU KILA SIKU
 
Kwa wale wajasiriamali wanaohitaji kujiunga na group ya WhatsApp kwa masuala ya kijasiriamali nicheki 0762600100
 
Back
Top Bottom