Jinsi ninavyopata Faida ya 45,000/= kwa siku, huku nikiendelea na kazi zangu kila siku

Evans Richard Arsenal

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
365
750
Jinsi mimi ninavyopata faida ya 45,000 kwa siku.

Kwasasa nina pikipiki aina ya Fekon na Huoniao jumla zote zipo 15 mtaani kwa mkataba wa miezi 12. Nilianza na mtaji wa 8,300,000/= mwaka Jana November 2021 ambao ulinisaidia kununua pikipiki 3 mpya aina ya Fekon na baada ya hapo nikawa naongeza pikipiki nyingine kwa marejesho ya pikipiki nilizonazo na hela kidogo kutoka kwenye mshahara wangu.

AINA ZA PIKIPIKI:
Kwa nini hizi pikipiki ni kwasababu ya aina ya eneo ambapo mimi nipo, kiuhalisia ni kwamba Boxer huku nilipo hazifai kwasababu ya barabara zilizopo sio rafiki. Boxer inahitaji barabara tambarare ambayo haina mabonde mengi maana ni rahisi kuharibika tofauti na Fekoni, Huoniao, Sinoray, Haojue etc

BEI ZA PIKIPIKI NA FAIDA ZAKE:
Fekon ni mkataba wa miezi 12, inauzwa 2.3m na kwa miezi 12 yaani mwaka mzima napata jumla ya 3.6 millions kwa maana hiyo faida yangu ni 1.3 millions kwa mwaka mzima (miezi 12) na kwa mwezi napata faida ya 108,000/= gawanya kwa siku 30 kwa siku kwa pikipiki moja ni faida ya 3,600/=.

Huoniao nafanya kwa mkataba wa miezi 11, inauzwa 2.1 millions na kwa miezi 11 nitapata jumla 3.3 millions kwa maana hiyo faida yangu ni 1.2 millions kwa miezi 11 tuu, na kwa mwezi mmoja napata faida ya 100,000/= gawanya kwa siku 30 kwa pikipiki moja ni faida ya 3,300/=

Kiufupi ni kwamba pikipiki moja inazalisha faida ya 3,000/= kwa siku hivyo kwa pikipiki zangu 15 kwa siku moja napata faida ya zaidi ya 45,000/= yaani (3,000/= x 15). Na kwa mwezi mmoja pekee napata Faida ya pikipiki 15 sio chini ya 1,350,000/=.

MAREJESHO:
Marejesho ya pikipiki moja kwa siku ni 10,000/= kwa hiyo kwa pikipiki 15 kwa siku nakusanya 150,000/= na kwa mwezi nakusanya jumla ya 4,500,000/= kwa pikipiki zote 15.

Kiufupi nina kazi yangu, so kwa mwezi kwa marejesho ya pikipiki nilizonazo nina uwezo wa kuongeza pikipiki mpya 2 kwa kila mwezi. Kwa maana hiyo kwa mwaka mzima nina uwezo wa kufunga pikipiki mpya 24 huku faida inaongezeka na makusanyo ya kila mwezi na siku yanaongezeka.

Faida ya pikipiki moja ni milioni moja na kuendelea inategemea wewe na dereva wako mtakubaliana vipi kuhusu mkataba wenu. Kuna sehemu nyingine mkataba wa pikipiki ni miezi 10, kwingine miezi 11 na wengine mpka miezi 13 hapa ni makubaliano ya pande mbili.

Hapa natumia tu mshahara wangu kiasi na 10% ya makusanyo naweza nikaweka kama akiba pembeni.

CHANGAMOTO:
Changamoto zipo nyingi kwenye bodaboda hasa kwa vijana kushindwa kurudisha hesabu ya siku lakini ukiweka mkataba vizuri na ukikaza hamna kinatoshindikana. Kingine ni kuwa na maelewano mazuri na madereva wako maana sio kila dereva anauwezo wa kupata elfu 10 kwa siku so kuna maelewano binafsi yafanyike.

MKATABA:
Mkataba wa pikipiki lazima uwe mkali usainiwe na pande zote mbili, kuwe na sehemu ya mashuhuda wa pande mbili na lazima usainiwe na mwenyekiti wa kijiji pamoja na mwanasheria wa serikali.

Kukata tamaa sio suruhisho dereva asipotoa hela kwa siku kadhaa unaongea nae kwa maelewano ya kurudisha tarehe fulani, weka MFUMO mzuri wa Microsoft Excel ambao utakuwa unaonyesha hela ya kila dereva iliyoingia na hela ambayo ipo nje anayodaiwa. Lazima Excel yako iwe na Formula ambayo itafanya majumuisho ya hela zinazoingia na kutoka kwa madereva wote wakiwa wengi bila ya hivyo utakosea mahesabu yako.

KUPATA VIJANA WAAMINIFU:
Mtafute mtu sahihi ambaye yupo uraiani unayemuamini awe anakusaidia kutafuta vijana waaminifu na ambao wana pikipiki zao walizomaliza mkataba. Kuna madereva wakongwe katika kila sehemu ambaye umezoeana naye mueleze na yeye atakusaidia kucontrol pikipiki zote na madereva wako maana yeye anajua wanapoishi na maisha yao kiujumla.

Vijana waaminifu wapo ila tu hamna ambaye ni mkamilifu zaidi asikose hela kwa siku fulani. Sio kwamba kila dereva muaminifu wa pikipiki ana uwezo wa kupata hiyo hela elfu 10 kila siku hapana.


ONYO:

Usimpe pikipiki, kijana ambaye anategemea pikipiki moja kurudisha 10,000/= kwa siku. Jaribu kutafuta vijana wenye pikipiki zao walizomaliza mkataba uwape wakuletee hesabu maana na yeye pikipiki yake atampa mtu mwingine kama DEWAKA ambapo yeye atapewa 7,000/= kwenye pikipiki yake na yeye atatafuta 3,000/= kwenye pikipiki yake mpya ya mkataba ili ajazie ifike 10,000/= kwa siku kama hesabu ya boss. Bila hivyo utafeli katika hii biashara

Usimpe pikipiki ndugu yako au rafiki yako eti kwasababu tu amekwambia atakupa hiyo hela 10,000/= kila siku. Hawa hawaaminiki utashindwa hata kusaini nae mkataba, usikubali undugu au urafiki kwenye biashara. Hauwezi kumpeleka rafiki yako mahakamani au polisi so kataa undugu katika kazi. Tafuta mtu ambaye utamuweza katika hizi biashara.

MAELEWANO BAADA YA MKATABA KUISHA:

Nina mwaka mmoja sasa kwenye hii biashara, dereva akimaliza mkataba wake na ana deni unauwezo wa kumuongezea siku kadhaa mbele za kumaliza deni lake.

Biashara sio vita kwamba dereva asipomaliza deni basi unampokonya tu pikipiki. Kama ameweza kulipa 3 millions na ana deni la 300k kwann usi pe siku kadhaa amalize hata kama ni mwezi mmoja tu.

Mnaelewana kama ana deni unamuongezea miezi miwili pamoja na riba ya 20% mpaka 40% ya deni lake. Ni maelewano ya pande mbili.


RIBA YA KUMUONGEZEA MUDA WA KUMALIZA DENI LAKE:

Mfano kama dereva alikuwa anadaiwa 300,000/= baada ya mkataba wake kuisha mnaongea kwa makubaliano yenu, unaweza ukamuongezea miezi 2 mbele kwa riba ya 30% ambayo itamfanya alipe tena 390,000/= kwa miezi miwili inayofuata. Ambayo hapo wewe utakuwa na faida nyingine ya 90,000/= kwa miezi inayofuata.

Pikipiki ya kwanza kabsa mnamo November 2021.
IMG_20211129_172952_6.jpg


Kwenye comments chini nimeweka Microsoft Excel inayoonyesha jinsi pikipiki zote ninavyozifanyia mahesabu kwa excel kuweka kumbukumbu sawa pamoja na majina ya madereva wote. Utaona mpaka sasahivi wapo 15 na 16,17.... etc ni mwezi unaofata January 2023
 
Hongera kwa upambanaji, ila mada imekaa kama vile ni marketing tu ya hizo pikipiki.
Mkuu nimetaja pikipiki zote hapo juu kuna Fekon, Huoniao, Huaojue, Boxer etc hizi zote zipo hapo juu ila kwa maeneo nilipo hizi ndio pikipiki ngumu zaidi.

Dar bila kuwa na Boxer haufanyi kazi vzuri ila huku vijijini kwetu tunatumia hizi nyingine
 
Changamoto madereva, ukiwekeza kwenye pikipiki faida yako iko kwa dereva. .

Ukiwa na dereva sio umeingia changa na pesa yako imewaka na moto., Hence changamoto

Nina mwaka mmoja sasa kwenye hii biashara, dereva akimaliza mkataba wake na ana deni unauwezo wa kumuongezea siku kadhaa mbele za kumaliza deni lake.

Biashara sio vita kwamba dereva asipomaliza deni basi unampokonya tu pikipiki. Kama ameweza kulipa 3 millions na ana deni la 300k kwann usi pe siku kadhaa amalize hata kama ni mwezi mmoja tu.

Au mnaelewana kama ana deni unamuongezea miezi miwili pamoja na riba ya 20% mpaka 4p% ya deni lake. Ni maelewano ya pande mbili.

Mfano alikuwa anadaiwa 300,000/= na mkataba umeisha unamuongezea miezi 2 kwa riba ya 30% ambayo itamfanya alipe tena 390,000/= kwa miezi miwili inayofuata.
 
Nilibahatika kuwa na pikipik moja, bahati nikaenda likizo nikawa mbali na yule boda, akawa haleti pesa had nikamuambia shahid wake ndo ikawa inatumwa lkn changamoto ni nyingi
Nilikuw na bajaji tatu, nilienda mpaka polisi kwenye kesi ya ujambazi. Huyu jamaa Mungu kambariki Sana akumbuke kutoa sadaka kanisani. .
 
Shukrani mkuu.

Changamoto kama hizo zipo sana tu ila mpaka sasa sijawai kukutana nayo ktk hii biashara. Ni mara mbili nilisikia vijana wangu wamepata Ajali nikatoa hela ya service za pikipiki na inahesabika katika Rxcel kwamba ni deni kwao na watalipa ndani ya muda fulani
 
Mshukuru Mungu wako unapata madereva wanaojielewa. Hawa madereva wanyoa viduku na kuvaa sendo nusu mbona ungelia kufwatilia hesabu za siku. Yaani unakuwa kama unafwatilia deni kwenye mali yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mm nipo juu kama Boss lakini chini yangu yupo kijana niliyemuajiri kunitafutia madereva wote wa pikipiki zangu mfano nikitaka kufunga pikipiki yeye ndiye anayetafuta dereva. Jamaa ana uzoefu wa miaka 10 kwenye kuendesha pikipiki za abiria.

Yeye ni mpole lakini kwenye marejesho yeye ni mtata anahakikisha kila dereva analeta hesabu kamili labda dereva akiwa na changamoto zake binafsi ndio anamuelewa zaidi ya hapo huyu ndiye anayecontrol mipango yote then mimi ndio namaliza.
 
Back
Top Bottom