Kuacha kazi kufanya ujasiriamali

yenyewe

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
621
94
Hbr wadau?

Mimi nimeajiriwa nina mshahara wa 570,000. ni mwaka wa tatu sasa tangu nianze kazi lakin sioni mafanikio yoyote zaidi ya kulipa kodi, kununua chakula na kumhudumia kidogo mke wng mtarajiwa ambae nimekuwa nae mda mref kwenye shida na raha na ajapata kazi tangu ahitimu chuo.

Nimekuwa nikisevu hela kidogo na sasa nimefikisha kiasi cha milion moja. Sasa wadau naombeni ushauri wenu kwa kiasi hiki kidogo nlichonacho shuguli zipi au biashara ipi naeza kufanya (tuachilie mbali kufuga kuku) kwa hapa Dodoma ukizingatia umri unakimbia kwa kasi majukum nayo yanaongezeka.

Nafikiria pia niache kazi au hii hela nimfungulie mpnz wng biashara tushirikiane kutafta riziki.

Ushauri wenu wadau.
 
Wekeza kwenye kilimo popote siyo lazima iwe dodoma. Unaweza kulima mazao haya; kitunguu swaumu, kitunguu maji au tangawizi.
 
mkuu kuacha kazi ni kuzuri lalini si sasa ,mfungulie mkeo biashara ,usiache kazi,sio sasa!

Kwani wakati wa kuacha kazi ni upi? ni wakati umezeeka? ni wakati unapo npewa barua ya kupunguzwa? ni wakati conract inapo isha au,

Wakati wowote unaweza acha kazi, ila ni kwamba kuacha kazi kuna hitaji spirt ya kipekee na ni wachache sana wenye hiyo sprit ya kuacha kazi wengi huishia kusema wakati bado na mwishowe hujikuta wanalazimishwa kuacha kazi kwa nguvu.
 
Mkuu sipingi wewe kuacha kazi lakini pia sishauri uache kazi kwa sasa kwasababu huko mbele kwa maelezo yako japo mafupi kunauwezekano wa wewe kukwama japo si lazma ukwame.

Ushauri wangu swala la wewe kuacha kazi kama itaonekana inafaa linahitaji maandalizi,jambo hilo ni process.

Kwanza kabisa mtaji ulionao si mkubwa kiivyo kuweza kuhimili mikiki ya matumizi yako lakini pia huezi kuacha kazi ukajifunze biashara, nasema ukajifunze biashara kwani kwa maelezo yako huna uzoefu kwenye biashara. Biashara ina changamoto moto zake hasa kipindi cha mwanzo.

Cha kukushauri tafuta mtaji wa kutosha kisha buni mradi na uanze biashara ukiwa kazini, tizama mwenendo wa biashara yako kwa muda then utapata maamuzi sahihi eidha uache kazi ufanye biashara au uafanye vyote kwa pamoja, kikubwa usikate tamaa ukiwa na malengo na juhudi lazma njia itaonekana.
 
Kwani wakati wa kuacha kazi ni upi? ni wakati umezeeka? ni wakati unapo npewa barua ya kupunguzwa? ni wakati conract inapo isha au,

Wakati wowote unaweza acha kazi, ila ni kwamba kuacha kazi kuna hitaji spirt ya kipekee na ni wachache sana wenye hiyo sprit ya kuacha kazi wengi huishia kusema wakati bado na mwishowe hujikuta wanalazimishwa kuacha kazi kwa nguvu.
Its all about kipato...., wakati muafaka ni pale kile anachokiacha ni duni kuliko kile anchokifuata...

Kwahio mpaka pale kile atakachofanya kitamuingia kipato zaidi au kinahitaji muda wake zaidi..., kumbuka kuna miradi anaweza kuanza huku bado anafanya kazi iki-take off au pale itakapohitaji muda wake 100% basi ataacha kazi, ila sio kuacha kazi tu.., sababu ya kuacha kazi, mambo yakienda kombo itapelekea frustrations na mwisho wa siku hata kuvunja familia, tena ukizingatia hizi biashara zetu za kibongo za misimu na za kuigana hazina guarantee
 
Ujasiriamali nayo ni kazi. Tatizo la watanzania mnaona ujasiriamali siyo kazi.

Tumia neno zuri .utofauti ni kuwa moja kazi ya kujiajiri nyingine kazi ya kuajiriwa.

Ila zote ni kazi. Wewe kama unasema unaacha kazi sijui unamaanisha unataka kulala tu na kuhijaza dunia
 
Umesoma content jamaa aliyoweka au umesoma heading peke yake ?
 
Kwani wakati wa kuacha kazi ni upi? ni wakati umezeeka? ni wakati unapo npewa barua ya kupunguzwa? ni wakati conract inapo isha au,

Wakati wowote unaweza acha kazi, ila ni kwamba kuacha kazi kuna hitaji spirt ya kipekee na ni wachache sana wenye hiyo sprit ya kuacha kazi wengi huishia kusema wakati bado na mwishowe hujikuta wanalazimishwa kuacha kazi kwa nguvu.

atleast pale atapoanzisha miradi tofauti ikawa na sustainable income generation!
 
Kama we ni muajiriwa wa serikali jaribu kuongeza elimu,omba kusoma ili ulipiwe ada,..halafu kuhus ujasiliamali kwann usimshirikishe wife msaidiane,kwa mfano dodoma unawezakuwa unanunua mazai km maharage kipind cha uvunaji af unayastore vizur mpk bei inapokuw nzuri unauza..usiache ajira,itakusaidia kupata mkopo wa kusupport biashara,pia kuongeza elimu ni muhim sana.
 
Aongeze elimi ili iweje? apate mshahara mkubwa au, Ujasirimali si ishu ya kitoto huwezi practise vitu viwili at the same time ni lazima uamue moja,
 
atleast pale atapoanzisha miradi tofauti ikawa na sustainable income generation!

Miradi tofauti ni ipi? mkuu kama huna spirt hiyo hakika ni ndoto kuacha kazi belive me, watu wengi huwa si kwamba wanaacha kazi ila unakuta huko wameisha hari bu au ndo kama hivyo mkataba umeisha anaamua sasa kuinfia kwenye Dunia nyingine.

Huwezi fanikiwa kibiashara ukiwa vile vile ni mfanya biashara kama kuna mfanya kazi mfanya biashara aliye fanikiwa mtaje, Wewe kuanzisha project inatakiwa uwepo full time na si kuongoza kwa simu,

Ishu ya kuacha kazi na kuingia kwenye biashara inaweza fanywa na watu wa chache sana na wengi wao kikwazo kikubwa ni uoga na si kingine
 
mkuu chasha nakuelewa sana,lakin biashara imejaa risks kibao(of course ndio uoga uliotaja),lakin ni busara kutokuingia kwenye mto usiojua kina chake,kwa ss aanze mrad na ampe wife asimamie uzdi kukua uzoefu ukitosha anaingia kwenye ujasiriamal moja kwa moja!
 
Its all about kipato...., wakati muafaka ni pale kile anachokiacha ni duni kuliko kile anchokifuata...

Kwahio mpaka pale kile atakachofanya kitamuingia kipato zaidi au kinahitaji muda wake zaidi..., kumbuka kuna miradi anaweza kuanza huku bado anafanya kazi iki-take off au pale itakapohitaji muda wake 100% basi ataacha kazi, ila sio kuacha kazi tu.., sababu ya kuacha kazi, mambo yakienda kombo itapelekea frustrations na mwisho wa siku hata kuvunja familia, tena ukizingatia hizi biashara zetu za kibongo za misimu na za kuigana hazina guarantee

1. Mkuu kwenye msatari wa kwanza, kwa staili hiyo huwezi acha kazi kamwe, labda ustafu.

2. Kama unafanya for substance unaweza fanya project ukiwa kazini na ndo biashara zetu ila you can do competetive business ukiwa kazini, wewe kama initiator wa Idea ni lazima uwepo full time kwenye project yako, na kipindi ambacho unatakiwa kuwepo full time ni kipindi ambacho ndo biashara inaanza, unatakiwa kuwa Maneja, mkurugenzi, salles, purchasing officer, na kila aina ya kazi, sasa sisi mtu anafungua project kesho anatafuta shemeji/mjombo/mke/mme/mchumba/kaka/dada/shangazi/mtoto na kumkabidhi majukumu, ni kosa kubwa sana na kufanikiwa ni vigumu sana, wale hawajui chochote, ni wewe pekee ndo unaye jua biashara yako inataka nini.

3. Kuacha kazi maana yake usha jua what will hapeni, unaweza ona biashara yako sasa imefikia pazuri na kujidanganya kwamba sasa uache kazi na baadae ukajikuta unarudi kwenye 0, unapo choma meli moto unabakia na optional moja tu, ishu kwamba familia itasambaratika ni uoga wa kijinga, kwani kusambaratika ni kitu gani? kwa hiyo mke wako alikupenda kwa sababu ya kazi yako? Ingawa ukweli ndo huo kwamba hapendwi mtu bali kinacho pendwa ni pesa uliyo nayo.

ILA UNAPO AMUA KUACHA KAZI NI HUTAKIWA KUANGALIA NYUMA, NA UKIJARIBU KUANGALIA NYUMA KAMWE HUTAACHA
 
Mkuu in life there is more than on way to skin a cat...., sio kweli kwamba biashara is the only way to make it.., unaweza ukawa CEO wa kampuni kubwa au unafanya kazi UN ambapo mapato yake na pension yake ni kubwa kuliko wewe mwenyewe kujaribu kufungua kampuni yako (doing same thing, au kuanzisha UN yako).

Ni tofauti kama mtu umeajiriwa unaendesha Bodaboda na unauza bidhaa fulani kusema kwamba ngoja nipate mtaji badala ya kumuuzia huyu boss au kumuendeshea boss nianze kuendesha mwenyewe au na mimi nifungue mradi wa watu kuniendeshea..., Vile vile wewe kama ni lawyer, Dr au specialist (sababu watu wanakufata wewe kwa ujuzi wako) unaweza ukasema let me open my own firm..., Hii ni tofauti labda na Sir Alex Ferguson kusema ahh ngoja na mimi nianzishe timu yangu ya mpira huku kupewa contract na Man United ni utumwa... Kwahio tukirudi kwenye ushauri kwa mleta mada ni biashara gani hio hapa Bongo ambayo anaacha kazi yake ili aifanye inayohitaji 100% (ukizingatia mazingira ya hapa home business zinafail usiku na mchana kulingana na mazingira duni)

Kumbe hapa unaongelea kwamba mtu amekuja na idea which pays a unique business ambayo ana competitive advantage na ameshafanya SWOT analysis na amegundua inalipa..., now a million dollar question is mleta mada ana hio idea au anataka kufanya ambacho wengine labda wanafanya ? na vingi wengine wanavyofanya anaweza kufanya part time....

Mpaka mleta mada amekuja kuuliza hapa it shows kwamba hajajua what will hapen, risks bado ni zile zile alafu issue ya kwamba familia ikisarambatika its okay naona sio busara..., huyu ni mtu anategemewa sasa watoto watakapokosa karo sababu ya gambling ya huyu jamaa (taking un-calculated risks) itakuwa ni upuuzi kwa jamaa..., yeye kama baba ana wajibu wa ku-take care of his family first and foremost.
 
Mkuu nisha sema kuacha kazi na kuingia kwenye ujasirimali si ishu ya kitoto, najua watu wanahofia kuchekwa, kutengwa, kuachwa na kazalika, hivyo kama hizo ndo sababu ni bora mtu akakomaa na kazi tu, Kwenye biashara kuna risk hata ukisema biashara ikue kwanza ipo siku unaweza jikuta biashara yako imesambaratika unatakiwa kuanza mwanzo, je hapo familia haitasambaratika? hizo ni sababu mfu.

Kinacho takiwa ni kukaa na kuelimisha familia yako, kwa sababu kama ishu ni familia kusambaratika je ukifukuzwa kazi itakuwaje?

Kuchoma Meli moto ni kazi moja ngumu sana yenye uchungu wa hali ya juu, nakumbuka kuna jamaa angu alifanya zoezi kama hili la kuacha kazi na kuingia kwenye business huku akilia sana, ila alisha amua moja, hivyo ni lazima uamue moja,
 
Mkuu swala la kuacha kazi si kwamba ni mpaka uwe na uhakika wa 100% wewe hutakaa uelewe na najua wewe ni moja wa wahanga wa kazi, ni vigumu sana na mwajiriwa kutoa ushauri wa mtu kuacha kazi, ni kitu ambacho hakipo.

Jaribu kusoma story ya MUGUKU, huyu jamaa sasa marehemu aliacha kazi ya ualimu na kila mtu alimshangaa nan kufikia mhali Wazazi wake kuamini kabisa mtoto wao kachanganyikiwa but yeye alikuwa amekwisha amua moja.

Ukikalia kwamba mimi ni bosi, natumia gari la shirika na kazalika huta kaa uwe na hii spirit, Watu wanaacha kazi za mamilioni na kwenda kuanza kazi za kuingiza elfu kadhaa badala ya mamilioni, usikalie kwamba uache kazi leo halafu wiki ijayo uwe tajiri make ndo za wabongo, anataka aanze leo then kesho awe biulionare, MUGUKU pamoja kwamba watu walimshangaa ila baadae mpaka anafaliki alikuwa kwenye top 5 ya matajiri wakubwa kabisa nchini Kenya,

Ujasirinali ni process ni safari ndefu sana na uoga ndo adui mkuwa sana, mbona wakina Edson walifeli mara nyingi but walikuja kufanikiwa, usikae kuwaza mishahra mikubwa kwamba ndo ikufanye usiache kazi,
 
Mkuu nisha sema kuacha kazi na kuingia kwenye ujasirimali si ishu ya kitoto, najua watu wanahofia kuchekwa, kutengwa, kuachwa na kazalika, hivyo kama hizo ndo sababu ni bora mtu akakomaa na kazi tu, Kwenye biashara kuna risk hata ukisema biashara ikue kwanza ipo siku unaweza jikuta biashara yako imesambaratika unatakiwa kuanza mwanzo, je hapo familia haitasambaratika? hizo ni sababu mfu.
Mkuu kujitosa katika kitu chochote bila preparation sio ujasiri bali ni upunguani..., katika kila maisha yako inabidi kuwa na plan B, na kufanya calculated risks.., na hapa tunaongelea miradi na kujiongezea kipato ila wewe unachanganya na running multi million corporations.., hivi kuna ubaya gani kama huyu mtu anavuta mkwanja wa kutosha kazini kwanini asianze kwanza part time (gaining experience) na kufanya investments kwenye vitu kama real estate n.k. vitu ambavyo anaweza kutumia leverage (efforts of others) to make money, pia kufanya investments tofauti (not putting ones eggs in one basket) hence anakuwa ame-hedge risk, baada ya hapo hata atakapoacha kibarua chake will have somewhere to fall upon...,
Kinacho takiwa ni kukaa na kuelimisha familia yako, kwa sababu kama ishu ni familia kusambaratika je ukifukuzwa kazi itakuwaje?
Akifukuzwa kazi amefukuzwa kazi hio ni part ya maisha sio sababu anaweza kufukuzwa kazi ndio aache kazi leo kabla ya kujitayarisha.., cha maana narudia (kama kazi yako ina kipato cha kutosha) tumia hicho kipato ku-hedge risk kwa investments ndogo ndogo hata utakapoacha kazi kunakuwa na fedha ya kujihifadhi in a rainy day..., sio unaamua kuacha kazi leo wakati hata pesa ya mwenye nyumba hujamalizia kumlipa.

Kuchoma Meli moto ni kazi moja ngumu sana yenye uchungu wa hali ya juu, nakumbuka kuna jamaa angu alifanya zoezi kama hili la kuacha kazi na kuingia kwenye business huku akilia sana, ila alisha amua moja, hivyo ni lazima uamue moja,

Huu msemo wa kuchoma meli ni just msemo.., huyo jamaa yako alichoma kabisa na vyeti vyake au ?..., sababu anaweza akakwambia hivyo ila deep down when push comes to shove angeweza kuanza kutuma applications tena (if he is employable), pia cha maana ni kwamba aliacha nini na kwenda kufanya nini ? (hapo keyword ni kufanya nini.., sio kuamua kuacha kazi kama CEO fulani alafu kuamua kwenda kuendesha bodaboda yake.., sababu hata hii ni biashara)
 
Aongeze elimi ili iweje? apate mshahara mkubwa au, Ujasirimali si ishu ya kitoto huwezi practise vitu viwili at the same time ni lazima uamue moja,

Ndugu Chasha suala la kuongeza elimu while doing business ni jambo la kawaida,wengi imewezekana na jamaa kasema wife yupo nyumban so ni msaada tosha...kuongeza elimu kuna faida nying,kama ni muajiriwa utazijua,baadhi tu ni kipato kuongezeka,heshima,kukuza uelewa na assurance ya kuongeza mafao pale utakapostaafu.....kwa kuongezea ajira hasa ya serikalini ni advantage kubwa sana kwa waajiriwa sema tu watu weng hawajui,ukiwa na ajira unaweza kupata loan ambayo kama umejipanga vzr ikabadilisha maisha yako..kumbuka financial institution nyng hazitoi mkopo km huna collateral,...ujasiriamali unawezekana katika hali yoyote ile tatzo ni expecttn za watu huwa kubw kupitiliza,start slow,Mwenyezi Mungu muweza yote aliumba dunia na vilivyomo polepole japokuwa angeweza kusema vyote vitokee na vingetokea,sisi ni mfano wake kumbuka,hatupaswi kushindwa kitu kama nia ipo!
 
Back
Top Bottom