Kosa la Mwangosi: Waandishi warudia Makosa

Status
Not open for further replies.
Ndugu zangu, tusimshambulie mleta mada kwa matusi na maneno ya kejeli, hayo maswali yatatakiwa kupatiwa majibu wakati wa kesi...of course yanaweza kuibuliwa while trying to justify the validity of the killing.

Naomba ufafanuzi ndugu...Una maana kwamba kuna mazingira ambayo mauji yanaruhusiwa endapo mhanga kafanya technical mistake?

Hapa naomba tuweke pembeni hukumu ya kifo. Mbali ya hapo, unieleze ni mazingira yapi ambao kifo ninaweza kuwa fair punishment!
 
Kisheria kuna plea maarufu ya "Contributory Negligence" Kwamba mtu anakiri kutenda kosa lakini anahamishia lawama kwa muathirika kwa kudai kuwa uzembe wa muathirika ndio umechangia kudhuriwa kwake.
 
Ndugu yangu ukitukanwa usishangae wakati wenzako wanaomboleza mwenzao kawatoka wewe unaingiza upumbavu wako wa kuvaa sare hivi unajua uchungu wa kufiwa wewe? Mwangosi amekufa kwa amri ya RPC Kamuhanda na si zaidi ya hapo hata wewe pamoja na upumbavu wako unajua hilo.
Usichanganye mada. Msiba hutoa fursa kwa waliobaki kutafakari kilichotokea. Msiba huwa hauzuii kutafakari.
 
Wakati mwingine unapotaka kuleta uzi humu ndani unatakiwa kujipanga, hata hivyo naamini mleta uzi umejifunza.

Binafsi waandishi wa habari kwa leo nimeona mshikamano wao na busara lakini wakati mwingine lugha ya kujikomba kwa watawala kwa baadhi ya waandishi waache. Nimemsikia Meena wa gazeti la mwananchi alivyokuwa anaongea kama kujikomba kwa Bw. Nchimbi baada ya kuwa amefukuzwa na wanahabari si jambo la afya, wakati mwingine inabidi watawale waambiwe ukweli bila kumung'unya maneno.

Kwa ujumla waandishi wameonyesha busara vinginevyo Nchimbi alitakiwa hata kutemewa mate, lakini kwa kule tu kumzomea inatosha
 
Kisheria kuna plea maarufu ya "Contributory Negligence" Kwamba mtu anakiri kutenda kosa lakini anahamishia lawama kwa muathirika kwa kudai kuwa uzembe wa muathirika ndio umechangia kudhuriwa kwake.

Kwa maana hiyo, wewe binafsi unaamini kuwa Mwangosi asingeuawa na polisi kama angekuwa amevaa hicho kivazi cha waandishi wa habari?
 
Sijawah dhan kuwa bado kuna wagonjwa wa akili kama ww mtoa mada hii, anyways utakuwa yule polisi aliyemuua Mwangosi, hivi ni sheria ipi inayosema m2 asiye mwaandishi wa habari auliwe kwenye halaiki kisa hajatambulika kama ni mwandishi???!! Hivi unaijua katiba ww, au unaishi kwa bahati mbaya, ok, hiv huna dini? Humuogopi Mungu? Na unasema hakuwa na sare??! Ile camera je? M/kiti wa waandishi asitambulike ktk mji mdg km iringa, lastly, jaribu kuimagine Mwangosi angekuwa baba yako/kaka/mjomba/ndugu/rafiki yako au wewe mwenyewe! Akili yako inahitaji kufanyiwa uchunguzi, sio bure
 
Wakati mwingine unapotaka kuleta uzi humu ndani unatakiwa kujipanga, hata hivyo naamini mleta uzi umejifunza. Binafsi waandishi wa habari kwa leo nimeona mshikamano wao na busara lakini wakati mwingine lugha ya kujikomba kwa watawala kwa baadhi ya waandishi waache. Nimemsikia Meena wa gazeti la mwananchi alivyokuwa anaongea kama kujikomba kwa Bw. Nchimbi baada ya kuwa amefukuzwa na wanahabari si jambo la afya, wakati mwingine inabidi watawale waambiwe ukweli bila kumung'unya maneno.
Kwa ujumla waandishi wameonyesha busara vinginevyo Nchimbi alitakiwa hata kutemewa mate, lakini kwa kule tu kumzomea inatosha

Kwa taarifa yako, katika kazi zinazohitaji kujikomba, ni uandishi. Hii ni kwa sababu wanategemea vyanzo ambavyo inabidi wavibembeleze ili viwape news. Na huwezi kuandika kinyume na matakwa ya media owners. We acha tu.
 
Sijawah dhan kuwa bado kuna wagonjwa wa akili kama ww mtoa mada hii, anyways utakuwa yule polisi aliyemuua Mwangosi, hivi ni sheria ipi inayosema m2 asiye mwaandishi wa habari auliwe kwenye halaiki kisa hajatambulika kama ni mwandishi???!! Hivi unaijua katiba ww, au unaishi kwa bahati mbaya, ok, hiv huna dini? Humuogopi Mungu? Na unasema hakuwa na sare??! Ile camera je? M/kiti wa waandishi asitambulike ktk mji mdg km iringa, lastly, jaribu kuimagine Mwangosi angekuwa baba yako/kaka/mjomba/ndugu/rafiki yako au wewe mwenyewe! Akili yako inahitaji kufanyiwa uchunguzi, sio bure

Angekuwa ndugu yangu pia ningetafakari pande zote mbili nijue namna ya kushinda changamoto alizotuachia.
 
we jamaa inaonekana ni moja ya polisi wachache wenye uwezo wa kutumia kompyuta. maana hicho ulichokiandika hakika unajaribu kutetea maslah binafsi. au mshua wako ni polisi?
 
Ndugu wakati unaendelea na lawama zako juu ya polisi, tumia fursa hii kutazama upande wa pili wa shilingi kwa kujiuliza swali lifuatalo: Je angevaa sare angukuwa treated kama hivyo?

Mkuu, mbona unakuwa mbishi bila mantiki?
Umeambiwa Mwangosi alikuwa anajulikana sana kule Iringa, na hata RPC naye alikuwa anamjua.

Pili yule askari aliyekumbatiwa na Mwangosi wakati anapigwa naye pia alimfahamu ndiyo maana alikuwa anawazuia wenzake wasimpige.

Na tatu, nadhani unafahamu kwamba haki ya kuishi ni kwa kila binadamu, bila kujali ni kibaka, mwandishi wa habari au yeyote awaye. Sasa suala la uniform linakujaje?

Na mwisho kama ungeiangalia clip ya video ya lile tukio ungegundua kwamba hakukuwa na fujo ya aina yoyote ya kuweza kusababisha Mwangosi achukuliwe kama ni mmoja ya waliokuwa wanaleta vurugu, kwa sababu hazikuwepo.
 
Kwani polisi walisema kuwa waliua nani? Polisi awali si walisema kuwa mwandishi alikuwa na bomu? Iweje walimtambua kama ni mwandishi ilhali hajavaa kizibao? Maswali ni mengi

Jamaa anasema kuwa ilibidi Mwangosi auawe kwa sababu hakuvaa sare ya waandishi wa habari....

May be na polisi akipita mtaani bila sare hata kama anafahamika tumchome kama kibaka....au nakosea?
 
Mkuu, mbona unakuwa mbishi bila mantiki?
Umeambiwa Mwangosi alikuwa anajulikana sana kule Iringa, na hata RPC naye alikuwa anamjua.

Pili yule askari aliyekumbatiwa na Mwangosi wakati anapigwa naye pia alimfahamu ndiyo maana alikuwa anawazuia wenzake wasimpige.

Na tatu, nadhani unafahamu kwamba haki ya kuishi ni kwa kila binadamu, bila kujali ni kibaka, mwandishi wa habari au yeyote awaye. Sasa suala la uniform linakujaje?

Na mwisho kama ungeiangalia clip ya video ya lile tukio ungegundua kwamba hakukuwa na fujo ya aina yoyote ya kuweza kusababisha Mwangosi achukuliwe kama ni mmoja ya waliokuwa wanaleta vurugu, kwa sababu hazikuwepo.

Hayo unayasema wewe,

Kama keshahitimisha kuwa lilikuwa ni kosa la marehemu.....Very pathetic!

Hata hivyo, wote tunajua kuwa nguvu ya pesa (tena hapa Tanzania) ni kubwa kuliko kila kitu. Nadhani kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa pesa sasa inamzidi hata Mungu!
 
Angekuwa ndugu yangu pia ningetafakari pande zote mbili nijue namna ya kushinda changamoto alizotuachia.

Mkuu, samahani. Lakini, huoneshi kama una watu wanaokutegemea au kwamba una majukumu makubwa. Vinginevyo usinge andika na kubisha ki-hivyo.
 
AKILI NDOGO HAWEZI KUONGOZA AKILI KUBWA......
Kalikinya...wewe mwenyewe umeshuhudia,UMEANZISHA UZI NA KUTHIBITISHA AKILIYAKO NDOGO KULINGA NISHA NA AKILI ZA WATU WA JF...wewe jifunze kutoka katika hili.....kwamaana umewachikoza sasa wanakushangaa kua labda umshilikishe mkeo katika kupata ushauri kabla ya kubonyeza ENTER.....
FOGY OF WAR MKUU
 
hv wachangiaji wengine ni wapuuzi? au mnatumika hv mbona askari wetu hamuwathamini? angekufa askari ktk maandamano hayo ndo mgefurahi? acheni kutetea mambo ya kijinga hapa pamoja na kulaani tukio la kuuwawa mwangosi lakini lazima tulaani tabia ya kukaidi amri za jeshi la polisi, kwa nn hTujiulizi huu ujasili wa wananchi kudharau vyombo vya dola umetoka wapi? wenye akili watanielewa lkn wajinga watashindwa kunielewa, kaeni na upuuzi wenu ipo cku nchi itangia kwenye machafuko kwa kuezandekez CDM
 
kalikenye

Hoja yako imepwaya kwa hoja zangu zifuatazo:
  • Polisi si mahakimu wa kutoa hukumu ya papo kwa papo
  • Polisi wamejichukulia sheria mkononi
  • Polisi wameteka kazi za mahakimu
  • Polisi haruhusiwi kuua isipokuwa wa bahati mbaya kama ni sababu za kujilinda ikionekana kutishia uhai wake
  • Hakuna sheria inayoainisha kwamba raia avae aina fulani ya kitambulisho ili asiadhibiwe na polisi kwa vile polisi hawana mamlaka ya kuadhibu ila mahakama pekee.
  • polisi wana mamlaka ya kumthibiti na kumkamata mtu ye yote anayekiuka sheria na kumfikisha mahakamani, si kuua.
  • Polisi anawajibika kumwuliza kwanza raia ni nani, anafanya kazi gani kabla ya hatua zaidi iwapo kuna uvunjaji sheria.
  • Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi amefanya makosa kwenda kuteka maandamano ya wanahabari wakati hakualikwa, la sivyo angekuwa waziri wa Habari ingeleta mantiki ya kueleweka.

Hoja yako imepwaya, utetezi wako umekosa hoja za kuivutia audience kwako kwa kuwa umejenga hoja za kutetea udhalimu wa polisi dhidi ya raia badala ya haki ya raia dhidi ya vyombo vya usalama.
 
Last edited by a moderator:
kalikenye

Mkuu Kama bado unazo hivyo Vizibao vya Journalist,sema tukusaidie kuuza. Camera pekee ni kitambulisho, kama uliangalia picha vizuri, Marehemu Camera yake ilikuwa mkononi. Je hao mapolice hawakuiona? mbona haijapatikana mpaka leo?
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom