Korti yazuia EWURA kudhibiti 'ufisadi'

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
09.10.2008 0025 EAT

Korti yazuia EWURA kudhibiti 'ufisadi'

Na Ramadhan Libenanga, Morogoro
Majira

MAMLAKA ya Usimamizi wa Nishati, Madini na Maji (EWURA), imezuiwa kufunga vituo sita vya mafuta ya petroli mjini hapa, baada ya wamiliki kukimbilia mahakamani na kuweka pingamizi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Petroli wa EWURA, Bw. Cyril Massay, alisema hatua hiyo ilishindikana baada ya kufika katika vituo hivyo na kukuta wamiliki hao wakiwa na hati za pingamizi, hivyo kuendelea na biashara ya mafuta kama kawaida.

Alisema kuwa vituo hivyo viliweka pingamizi la Mahakama lililosainiwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Bw. Amir Msumi.

Awali Mkurugenzi huyo alieleza kushangazwa kwake alipokuta vituo hivyo vikiendelea kufanya kazi licha ya Mamlaka hiyo kuweka vifungo (seal) ili visiendele na biashara hadi taratibu zitakapozingatiwa.

"Nashangaa kuona wamekata seal za EWURA na kuendelea kufanya biashara ya mafuta katika vituo vyao kinyume na sheria," alisema.

Bw. Massay alisema uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo haufanyiki kwa lengo la kumkomoa mfanyabiashara, bali ni sheria zilizotungwa na Serikali kwa mujibu wa kanuni za nchi.

Hata hivyo alishangazwa na kiburi kilichooneshwa na na wafanyabiashara wa vituo vya mafuta hasa kwa kukata seal hizo na kuendelea kufanya kazi.

Sambamba na hilo, alisema ofisi yake itaendelea na operesheni yake ikiwa ni pamoja na kutaka kujua kama Mahakama ndiyo iliyotoa ruhusa kwa wamiliki hao kukata seal hizo.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema ofisi yake haitakuwa tayari kuwanyamazia mafisadi hao wenye tabia ya kuchafua mafuta kwa maslahi binafsi na hivyo kuvuruga utaratibu uliowekwa na idara ya viwango.

Vituo vilivyokuwa katika orodha ya kufungiwa kutokana na kudaiwa kuchafua mafuta ni Oilcom katika barabara ya Dodoma, maeneo ya Kihonda; Kobil Msamvu na Abdulatif Twalib katika barabara ya Iringa.

Vingine ni Oilcom maeneo ya Nane Nane na Petro ya Sokoine, ambapo vituo vyote hivyo jana vilibandika notisi ya pingamizi kutoka Mahakamani dhidi ya EWURA.
 
Back
Top Bottom