EWURA: Nchi ina hifadhi ya Mafuta inayojitosheleza, Petrol inatosha kwa siku 19 na Diesel siku 18

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,023
Mkurugenzi mkuu wa EWURA Dr James Andilile amewataka hofu Wananchi kwa kusema Nchi ina hifadhi ya kutosha ya Nishati ya Mafuta

Dr Andilile amesema kuna Hifadhi ya Petrol ya kutosha siku 19 na Diesel ya kutosha siku 18.
---

Mkurugenzi wa EWURA Dkt. James Andilile
Mamlaka ya udhibiti wa Nishati nchini Tanzania (EWURA) imekifungia kituo vya MATEMBA kilichoko Tuliani na CAMEL OIL kilichopo Msamvu Mkoani Morogoro kwa kipindi cha miezi sita kujihusisha na Biashara ya uuzaji mafuta kwa kile ambacho EWURA imedai ni kwenda kinyume na taratibu zinazoendesha Biashara ya mafuta.

Mkurugenzi wa EWURA Dkt. James Andilile amesema Nchi ina hifadhi inayojitosheleza kwa Nishati ya mafuta ambapo amesema kwa upande wa Petrol nchi ina akiba ya Nishati hiyo ya kutumika kwa siku 19 na upande wa Diesel Nchi ina akiba ya kutumika kwa siku 18 hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu upatikanaji wa Nishati hiyo.

Source: Jambo TV
 
Huyo bila shaka Hana akili au anatufanya wananchi hatuna akili na ni wajinga..

Kama yapo ya kutosha iweje sasa kuna maeneo ya nchi hayana nishati hii kwa zaidi ya wiki 4 na kule ambako yanapatikana bei iko juu kuliko kawaida..!

Hawa viongozi wetu Wana shida gani kwenye vichwa vyao??
 
Mkurugenzi mkuu wa EWURA Dr James Andilile amewataka hofu Wananchi kwa kusema Nchi ina hifadhi ya kutosha ya Nishati ya Mafuta

Dr Andilile amesema kuna Hifadhi ya Petrol ya kutosha siku 19 na Diesel ya kutosha siku 18

Source: Jambo TV
Hizi tantalila tu watu wamefungia mafuta hawauzi wanasubiri bei ipande. wameshindwa kusimamia hii sekta.
 
Mkurugenzi mkuu wa EWURA Dr James Andilile amewataka hofu Wananchi kwa kusema Nchi ina hifadhi ya kutosha ya Nishati ya Mafuta

Dr Andilile amesema kuna Hifadhi ya Petrol ya kutosha siku 19 na Diesel ya kutosha siku 18

Source: Jambo TV
Sijasikia vizuri amesema siku 19 au miezi 19 maana ukiwa chini ya miezi 4 mpaka sita Tayari unakuwa na shortage sasa unapokuja hadharani na kusema kuhusu siku dah inafikirisha sana
 
Mkurugenzi mkuu wa EWURA Dr James Andilile amewataka hofu Wananchi kwa kusema Nchi ina hifadhi ya kutosha ya Nishati ya Mafuta

Dr Andilile amesema kuna Hifadhi ya Petrol ya kutosha siku 19 na Diesel ya kutosha siku 18

Source: Jambo TV
Kwa hio zikiisha siku 19 na hizo 18 ukame wa mafuta unaendeleaje au sijamwelewa?

Nilijua miaka/miezi 18 au miaka/miezi 19 kumbe siku
 
Mafuta yenyewe wananunua kwa ‘bulk procurement’ wote wanatoa order kwa siku moja.

Lead time ya kuleta mafuta ni siku 26, halafu wewe unaweka inventory ya siku 16.

Hela yenyewe ya kuagizia mafuta wafanya biashara hawana, kwa hivyo volumes za kuagiza pia zinapungua.

Soon tunaenda tengeneza matatizo ya Bangladesh kukosa hadi hela ya kuagiza mafuta kabisa.

Amtoe na huyo Majaliwa, hilo jumba bovu lianguke haraka. Si anataka vijana yeye, hawa-hawa waliotengeneza shida ya umeme TANESCO halafu wanamuongopea wananchi wameilewa sana TANESCO mpya huku wakimuonyesha upuuzi wao kwenye TV na kupeana tuzo za upuuzi eti shirika lililofanya turnaround.

Hakuna raisi wa nchi hapo, hilo ndio tatizo halisi; mengine matokeo tu ya uongozi wake.
 
Back
Top Bottom