Kondomu zilizotumika zakithiri stendi ya Same, polisi waamrishwa kufanya doria usiku kuwakamata wanaotumia stendi vibaya

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,822
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amemwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo kuanza doria nyakati za usiku katika stendi ya mabasi Same mjini, ili kuwabaini na kuwakamata wanaotumia stendi hiyo kufanya mambo yasiyo na maadili.

Amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakilitumia eneo hilo la stendi vibaya na kwamba kila siku zimekuwa zikikutwa kondomu zilizotumika zimezagaa ndani ya stendi hiyo.

Mgeni ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya stendi hiyo, wakati akisikiliza kero mbalimbali za wananchi wa wilaya hiyo.

"Hili eneo la stendi kuna watu wanalitumia vibaya sana, tunakumbana na kondomu kila siku hapa stendi, kuna kitu gani kinafanyika hapa, OCD nikuombe fanya doria kamata wote weka ndani uwachukulie hatua kwa mujibu wa sheria," amesema DC Mgeni.

Ameongeza: "Wanatuharibia sana watoto wetu hapa Same, mimi kama mkuu wenu wa wilaya na mwakilishi wa Rais katika wilaya hii ya Same na kama mwanamke, nina uchungu sana na hawa watoto, niwaombe sana wazazi timizeni wajibu wenu,"

"Sitaki kusikia tena kuna kondomu hapa, na kila mzazi awe mlinzi wa mwenzake hata kama mzazi unaona yule mtoto sio wa kwako anarandaranda maeneo ya hapa stendi nyakati za usiku, mtoto wa mwenzake ni wa kwako, mweleze mzazi mwenzako usione kama una kiherehere unakuwa umeokoa taifa la kesho,"
 
Wakianza kupiga kavu?

images (2).jpeg
 
Wapare wenzangu wananiaibisha 😂 Anyway kukulana sehemu isiyo sahihi kuna utamu wake bhana
 
Kabla ya DC kupongeza watu kutumia Kinga yeye kama kawaida ya politicians wetu ni kutumia dola, my DC unatakiwa usambaze refuse bins hapo stendi, weka taa hapo uwanjani yaani kimbiza giza, mambo mengine hayahitaji nguvu, kwani ukitia ndani utawashitaki kwa kosa gani?
 
tunakumbana na kondomu kila siku hapa stendi, kuna kitu gani kinafanyika hapa
Wanastahili pongezi kwa kutumia kinga sawa na maelekezo ya wataalamu wa afya
"Sitaki kusikia tena kuna kondomu hapa..
Huyu atasababisha watu wakulane nyama kwa nyama maambukizi ya virusi yaongezeke.
Inawezekana kwenda gesti hawawezi kwa sababu ya ukata au ubahili
 
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amemwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo kuanza doria nyakati za usiku katika stendi ya mabasi Same mjini, ili kuwabaini na kuwakamata wanaotumia stendi hiyo kufanya mambo yasiyo na maadili.

Amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakilitumia eneo hilo la stendi vibaya na kwamba kila siku zimekuwa zikikutwa kondomu zilizotumika zimezagaa ndani ya stendi hiyo.

Mgeni ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya stendi hiyo, wakati akisikiliza kero mbalimbali za wananchi wa wilaya hiyo.

"Hili eneo la stendi kuna watu wanalitumia vibaya sana, tunakumbana na kondomu kila siku hapa stendi, kuna kitu gani kinafanyika hapa, OCD nikuombe fanya doria kamata wote weka ndani uwachukulie hatua kwa mujibu wa sheria," amesema DC Mgeni.

Ameongeza: "Wanatuharibia sana watoto wetu hapa Same, mimi kama mkuu wenu wa wilaya na mwakilishi wa Rais katika wilaya hii ya Same na kama mwanamke, nina uchungu sana na hawa watoto, niwaombe sana wazazi timizeni wajibu wenu,"

"Sitaki kusikia tena kuna kondomu hapa, na kila mzazi awe mlinzi wa mwenzake hata kama mzazi unaona yule mtoto sio wa kwako anarandaranda maeneo ya hapa stendi nyakati za usiku, mtoto wa mwenzake ni wa kwako, mweleze mzazi mwenzako usione kama una kiherehere unakuwa umeokoa taifa la kesho,"
Kina ambieree wanakamuana mpka stand...kweli mpare noma
 
Back
Top Bottom