Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,815
- 11,992
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ameagiza kufungwa kwa Shule ya Msingi Kigulunde, iliyopo katika Kata ya Mtii, Tarafa ya Gonja kutokana na kutishia usalama na uhai wa wanafunzi pamoja na walimu wao.
Shule hiyo iliyojengwa mwaka 1975, licha ya kukabiliwa na uchakavu wa majengo yake, imejengwa kwenye mkondo wa maji.
Hofu hiyo inatokana na historia mbaya ya shule hiyo ambapo mwaka 2011, ilizingirwa na mafuriko ya maji, yaliyokuwa yakitiririka kutoka safu za milima ya Upare, na hivyo kusabisha uharibifu wa miundombinu yake ya madarasa.
Amri ya kuifunga shule hiyo ambayo ina jumla ya wanafunzi 49 na walimu wawili, imetolewa, Desemba 5, 2023 wakatiDC huyo alipoitembelea shule hiyo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.
"Nimeagiza shule hii ifungwe, nimeitembelea na iko kwenye mkondo wa maji, na mwaka 2011 iliwahi kukumbwa na mafuriko na wataalam wangu wa udhibiti ubora wamenithibitishia kwamba pale hapafai na walishatoa huo ushauri kwa mamlaka husika kwamba hiyo shule ifungwe," amesema DC Kasilda.
Pia soma - Muonekano wa Shule ya Msingi Kugulunde, miundombinu yake ni hatari kwa Wanafunzi na Walimu
- Kilimanjaro: Serikali yasema inasubiri Wananchi watenge eneo ili ujenzi wa Shule ya Kigulunde uanze