Komandoo Salmin: Nini kilichojiri akaanguka 2000?

Pakacha,
Hebu tuwe wakweli kidooooooooogo tu!
Pindipo (nasisitiza tena, Pindipo) zanzibar ufanyike uchaguzi (angalau wa majaribio) halafu uchaguzi huo uwe huru na haki, ufanyike kihakkki lillahi. Vyama vyote visifanye haya maigizo wanayofanya saivi wakiyaita uchaguzi. Niagulie matokeo.

He! panataka tochi hata hapo??
 
Na ile ya Bilali na Amani karume je?

hii ya Bilali Na Amani naomba uni fahamishe wewe ndugu yangu. Kilicho tokea ni nini haswa? Maana najua kidogo sana kuhusu hawa wawili. Nilicho sikia mimi ni kua Amani aliombewa na mama ake kwa wakubwa waliokua na ushawishi wa kupeleka mambo upande wake.
 
MwanaFA1,

"Sheria za CCM ni kuwa mtu kua mgombea wa CCM lazima ashinde kwa zaidi ya 50%(yani majority). Mgombea mmoja asipo pata hizo asilimia zinazo hitajika kuna kua na runoff kati ya wagombea wawili walio pata kura nyingi zaidi"

Sasa sku ile kule machinjioni(dodoma) nilishangaa niliposikia Mw'kiti (Mkapa wakati ule) akimlazimisha kistaarabu na kumtisha tisha Dr. Bilal aondowe jina lake katika kinyan'ganyiro cha urais kwa kisingizio eti kumwachia Karume amalize temu ya pili (utafikiri kaikodi), wakati huku wanaume tulishajitayarisha kupiga rusha roho kuanzia bandarini dsm hadi zenj, sasa hapa ule utaratibu wa demokarasia ya kuchagua na kuchaguliwa ndani ya CCM ulienda wapi siku ile. Na mm najua mpaka hapo unapojuwa ww kuwa "maza" alienda kulialia na kumwaga michozi eti "ooooh watu wameanza kusahau jitihada za marehemu bwana kwa kumpuuza mwanawe"
Sisi wengine kuanzia pale ndo tukabwaga manyanga eti...
 
- Pamoja na mengine mengi Salmin pia aliponzwa sana na tamaa zake za kua rais wa Muungano, kiburi na ubabe wake dhidi ya rais Mkapa, vlichangia sana katika kuwaudhi waamuzi ndani ya CC,

- The bottom line ni kwamba wafadhili wanaotupa michango mizito special kwa ajili ya kusimamia demokrasia bongo, wasingeweza kabisaa kukubali huu muigizo wa Salmin.

Respect.

FMES!
 
Tusisahau kuwa kiboko ya CUF alikuwa si mwingine bali KAMANDOOO

hilo CCM wanalijua

vile vile tusisahau kuwa CUF na CCM have one thing in common:

wote hawaupendi muungano...the only question nani atakuwa na guts za kusema hilo wazi wazi
 
Pamoja na mengine mengi Salmin pia aliponzwa sana na tamaa zake za kua rais wa Muungano, kiburi na ubabe wake dhidi ya rais Mkapa, vlichangia sana katika kuwaudhi waamuzi ndani ya CC...

Msaada kwenye tuta Mkuu FMES.

Salmin kuendelea na urais ingebidi Baraza la Wawakilishi wabadili katiba ya Zanzibar. CC ya CCM inahusika vipi?

KATIBA YA JAMHURI, 104 ( 1 )
``Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atachaguliwa na wananchi katika Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar, na kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi la Zanizibar inayohusu uchaguzi kwa ujumla au uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.``
 
G.T,
clarification.
kama unakusudia c.c.m zanzibar (siwasemei) ila kwa c.u.f ninachokifahamu kuwa sera yao katika suala la muungano ni serikali tatu, hii si kutokuupenda muungano bali ni kuwa na muungano bora unaoeleweka kimaslahi.
Hapajapatwapo kusemwa au kutendwa na yeyote zanzibar kuonyesha kuwa muungano haupendwi ila watu wanataka "reforms" tu.
 
Dilunga,
ww hujuwi mpaka leo kuwa katiba ya ccm inakuja mwanzo halafu ndo ya nchi!
 
MwanaFA1,

"Sheria za CCM ni kuwa mtu kua mgombea wa CCM lazima ashinde kwa zaidi ya 50%(yani majority). Mgombea mmoja asipo pata hizo asilimia zinazo hitajika kuna kua na runoff kati ya wagombea wawili walio pata kura nyingi zaidi"

Sasa sku ile kule machinjioni(dodoma) nilishangaa niliposikia Mw'kiti (Mkapa wakati ule) akimlazimisha kistaarabu na kumtisha tisha Dr. Bilal aondowe jina lake katika kinyan'ganyiro cha urais kwa kisingizio eti kumwachia Karume amalize temu ya pili (utafikiri kaikodi), wakati huku wanaume tulishajitayarisha kupiga rusha roho kuanzia bandarini dsm hadi zenj, sasa hapa ule utaratibu wa demokarasia ya kuchagua na kuchaguliwa ndani ya CCM ulienda wapi siku ile. Na mm najua mpaka hapo unapojuwa ww kuwa "maza" alienda kulialia na kumwaga michozi eti "ooooh watu wameanza kusahau jitihada za marehemu bwana kwa kumpuuza mwanawe"
Sisi wengine kuanzia pale ndo tukabwaga manyanga eti...

Mimi nilicho sikia ni kwamba kamati kuu ya CCM ikiwa chaired by Mkapa walimuomba(sijui walimuomba kweli au ilikuwa by force) kuwa ampishe Karume. Nakubaliana na wewe hapo kidogo inaleta utata. Kwa nini wamzuie Bilali kuwania nafasi hiyo? Sielewi kama ilikua a tactical move on behalf of CCM au ni kumpendelea tu bwana AK. Lakini ndiyo yale yote ya watu kubebana. hata uraisi Amani kaupata kutokana na jina(na mama ake kumuombea).
 
Msaada kwenye tuta Mkuu FMES.

Salmin kuendelea na urais ingebidi Baraza la Wawakilishi wabadili katiba ya Zanzibar. CC ya CCM inahusika vipi?

KATIBA YA JAMHURI, 104 ( 1 )
``Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atachaguliwa na wananchi katika Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar, na kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi la Zanizibar inayohusu uchaguzi kwa ujumla au uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.``

Ahh Dilunga Mwanazuoni mwenzangu, leo unajifanya kusahau kuwa Katiba ya Tanzania na ya Zanzibar zinafuata amri ya CCM?

CCM wakiamua jambo, ndipo hubadili Katiba ifanye kazi kwa matakwa yao.

Sasa hili la Zanzibar linakushangaza vipi?

Umesahau ni CCM iliyoridhia kwanza kuwa na Vyama vingi ndipo Katiba ikabadilishwa?

Labda nikusaidie kwa mara ya mwisho, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hupitishwa kuwa Wagombea na kuchujwa na nani kabla ya kwenda kwa Wananchi kupigiwa kura? Jibu ni kwanza Kamati Kuu ya CCM, kabla ya kwenda NEC na hata Mkutano Mkuu wa Taifa!

CC ya CCM ndio nguvu ya nchi na si chombo kingine ati!
 
- Mchungaji naona hakuna cha kuongeza tena maana umempa jamaa darasa zito sana, la siasa ya taifa lake mwenyewe alikuwa haijui? Kaaazi kweli kweli!

FMES
 
- political miscalculations, yeye alikuwa ana bank on mkapa, kwmaba kwa sababu alimsaidia mwalimu, kumpa urais mkapa over kikwete basi mkapa hana ubavu wa kumzuia kuwa rais tena wa term tatu,

- wafadhili wasingekubali huu ujuha, ccm siku zote wako careful kuwa on line na wafadhili, ndio maana siku ya kumfundisha adabu salmin kule cc dodoma, salmin aliitwa mbele ya kikao na cc wakamuomba mkapa atoke nje, ili wamshughulikie wenyewe, na kwa hasira ya wajumbe wengi dhidi ya salmin, wakamwambia wazi kwamba hata mgombea wake bilali wanamtwanga na kumpa karume, aliyeshindwa naye!

Respect.

fmes!
mkapa hakutoka nje kwani ndiye aliyeongoza kikao cha kumuondoa jamaa katika tamaa zake hizooo..

Wajumbe wengi walishangazwa na ujasiri wa mkiti (bwm) katika kushughulikia jambo zito kama lile kwa diplomasia ya halii ya juu..na kikao kikisonga na maamuzi safiii wakafikiaaa..

Bwm alimaliza kazi kilainiii sanaa...jamaa ana ujasiri wa uongoziiii
 
- Sawa sawa mkuu huenda vilifanyika viako viwili tofauti katika jengo moja la "White House", CCM makao makuu Dodoma, maana walioshiriki kikao kimoja kati ya hivyo viwili walionipa dataz, Mkapa hakua na uwezo wa kumwambia Salmin anything katika urais wake wote, siku zote ilikuwa ni lazima Mkapa amuombe rafiki wa karibu wa Salmin mpaka leo, jm peke yake na ndiye alimpa bad news kwenye hicho kikao cha siri cha CC,

- Kwamba sio tu hatapewa term ya tatu, bali amewaudhi sana wajumbe na tabia zake za kibabe kama kukataa kuhudhuria vikao vya Cabinet, maneno machafu against Mwalimu, kutomuheshimu rais Mkapa na ukandamizaji wa CUF, infact at one point jm alimuonya Salmin kwamba kama hataki kusikia, CCM iko radhi kumpa uongozi Maalim Seif na CUF ili tu kumkomoa yeye Salmin, alipomaliza Salmin aliomba radhi kwa kikao na kukubali kufuta mawazo yake,

- CC hawakumalizia hapo, walimpa more bad news kwamba kutokana na ujeuri wake, wamamua kwamba hata mtu wake Bilali hatapitishwa kugombea urais wa Zanzibar wakampiga chini, hivi karibuni Salmin alioa dogo dogo, kwenye hiyo harusi alimkaribisha kiongozi mmoja tu kutoka bara jm basi.

Respect.

FMES!
 
Tusisahau kuwa kiboko ya CUF alikuwa si mwingine bali KAMANDOOO

hilo CCM wanalijua

vile vile tusisahau kuwa CUF na CCM have one thing in common:

wote hawaupendi muungano...the only question nani atakuwa na guts za kusema hilo wazi wazi

Discussion za JF huwa zinanipa raha sana. Mana watu wanamgeuza samaki kama inavyotakiwa. Huu muungano inawezekana unalindwa na mazoea na siyo dhamira ya dhati ya kuuona unakua na kuendelezwa ndo mana kashikashi haziishi
 
Komandowa chuma alisema ATARUDI IKULU KWA MIGUU.. Nasubiri siku tu nijionee... sijui atauona mlango wa ikulu?
 
Back
Top Bottom