whizkid
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 357
- 240
Wakati "mwananchi wa kawaida" anakandamizwa kwa rungu kubwa la kodi, mfumuko wa bei na gharama za juu za maisha kiujumla, serikali ya CCM muda huu ipo uwanja wa Uhuru inatumbua fedha kwa shughuli za "kipuuzi". Haingii akilini. Huu mwenge wa Uhuru una manufaa gani kwa mtanzania? Nadhani maana ya kuukimbiza mwenge wa Uhuru ilishapita miaka mingi, CDM walikuwa sahihi na hoja ya kuupeleka mwenge makumbusho ya taifa! Sioni faida yake. Wewe unaonaje?