Kodi zetu na mwenge wa Uhuru

whizkid

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
357
240
Wakati "mwananchi wa kawaida" anakandamizwa kwa rungu kubwa la kodi, mfumuko wa bei na gharama za juu za maisha kiujumla, serikali ya CCM muda huu ipo uwanja wa Uhuru inatumbua fedha kwa shughuli za "kipuuzi". Haingii akilini. Huu mwenge wa Uhuru una manufaa gani kwa mtanzania? Nadhani maana ya kuukimbiza mwenge wa Uhuru ilishapita miaka mingi, CDM walikuwa sahihi na hoja ya kuupeleka mwenge makumbusho ya taifa! Sioni faida yake. Wewe unaonaje?
 
Juzi hapa wamekuja kukusanya Tsh.10,000/= eti za mwenge
 
Du hoja yako imenigusa nimepigwa panga kamshahara kangu,tena nadunduliza hela watoto waende shule mapema mwakani;But dont wory my brother salvation shall come from our blood
 
Inapofika kwenye swala la mwenge kwa kweli nashindwa kuelewa nini haswa mantiki ya kutumia kodi ya mtanzania maskini kuzungusha mwenge,
wanasema umulike mipaka, wameshajiuliza hawa wahamiaji haramu wanapitia wapi wakati mwenge upo?
Wasema ulete tumaini, lipi wakati watanzania wameshalipoteza zamani hali yao sasa ni tia maji tia maji?
eti ulete upendo, upi wakati watanzania sasa wanachuki ya kupita kiasi juu ya serikali yao kwa uozo unaofanywa na hao wenye dhamana? eti heshima mahali palipo na dharau, hii ndio kabisa waifute katika list maana viongozi ndio wanaongoza kwa dharau kwa wananchi, hakuna anaesikiliza kilio chao tena, ni dharau mtindo mmoja kwa kua wao wanacho na hawa hawana, lol

Kweli mwenge umepitwa na wakati
 
Mimi naona wangeupeleka jumba la Makumbusho tu, mshahara wenyewe kidunchu, TRA, NSSF, SACCOS, wote wanaangalia hapo bado familia, halafu eti unaambiwa changia mwenge, hizo walizochukua hao MAFISADI hazijawatosha? Jamani, kwa nini hamuwaonei huruma watanzania wale wa kima cha chini?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom