Kodi ya Maendeleo(kichwa), Uzembe na Uzururaji...

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
3,277
5,514
Enzi hizo bwana mgambo wanakamata watu kodi ya kichwa.....yaani watu walikua wanakimbia balaa...tukiwa wadogo wakija mtaani kwetu basi tunakaa kona ya mtaa na kuanza kushtua watu kuwa kuna mgambo wanakamata watu kodi weee.wengine wabishi bwana ilikua balaa..

hata hivyo hakuna kitu nilikua sipendi kama sanya sanya ya polisi kwa kutumia magari yao (karandinga) actualy yalikua Leyland comet.....we mnakamatwa ijumaa mnaachiwa jtatu ...kama huna hela imekula kwako....ile ilikua unyanyasaji.....

Wadau mnakumbuka nn kuhusu hayo mambo mawili? je ilikua sawa?
 
Kwa suala kubwa na zito kama kodi, labda uniambie kuna mchakato wa kupeleka hoja Bungeni; hilo linawezekana lakini sio kienyeji; ila kwa magamba pia usishangae.

Well, vyovyote iwavyo, iwe kodi ya kichwa au wa-introduce hata ya masaburi muda sio mrefu kitaeleweka kama alivyowahi kusema mlalahoi fulani kwenye tamthilia moja - "yana mwisho haya".
 
Kila mwisho wa mwezi mi nakatwa PAYE ambayo ni bajeti yangu ya nusu mwezi. Nitashangaa kama watawadai kodi wazazi wangu ambao ni walalahoi kule kijijini, itakuwa sawa na kumnyonya nzi damu.
 
kila mwisho wa mwezi mi nakatwa paye ambayo ni bajeti yangu ya nusu mwezi. Nitashangaa kama watawadai kodi wazazi wangu ambao ni walalahoi kule kijijini, itakuwa sawa na kumnyonya nzi damu.

usishangae selikari jk ina weza kufanya watakavyo.
 
Nilikuwa sijui kwa nini watu(hasa akina baba) walikuwa wanakimbia pale kijijini na kurudi usiku. Baadae nikajua ni mambo ya kodi eti ya kichwa. Tukio kubwa lililotokea kipindi kile nilikuwa na babu nyumbani, ghafla bibi akaja akamwambia ajifiche. Babu akaingia darini, mgambo walipofika wakaambiwa kaenda shamba. Hakutoka huko hadi jioni.....
 
heee heeee heee!hizi story babu yangu alinihadithia yalimkuta siku moja akajikuta ameshinda juu ya mwembe kutwa nzima! hivi ingerudishwa miaka hii ingekuwaje loh!
 
miaka hii ikija hii..
ukimbie uachie mgambo mkeo..
looh..watamtumia kama kodi ya kichwa...mpsixxxxx
 
hahahahaaah!!! Yaani huwa nikikumbuka namna watu walivyokuwa wanakimbizana na mgambo.....navunjika mbavu!

mi nakumbuka kuna siku ma anko zangu walibebwa mzega mzega na mgambo kisa hiyo kitu,nilibaki kutoa macho tu,ila zamani maisha yalikuwa swadakta sana,tofauti na enzi hizi za jk
 
heee heeee heee!hizi story babu yangu alinihadithia yalimkuta siku moja akajikuta ameshinda juu ya mwembe kutwa nzima! hivi ingerudishwa miaka hii ingekuwaje loh!

Irudi ili pato la serikali liongezeke.....lol.
 
Nilikuwa sijui kwa nini watu(hasa akina baba) walikuwa wanakimbia pale kijijini na kurudi usiku. Baadae nikajua ni mambo ya kodi eti ya kichwa. Tukio kubwa lililotokea kipindi kile nilikuwa na babu nyumbani, ghafla bibi akaja akamwambia ajifiche. Babu akaingia darini, mgambo walipofika wakaambiwa kaenda shamba. Hakutoka huko hadi jioni.....
Kaka salama?
Du!nahisi hii kitu ilisumbuaga sana watu miaka hiyo,
Mie hata sikumbuki km niliwahi kuishuhudia ua vp zaidi yakusikia story tu kwa watu!!
Nahisi ilikuwa inafanana na hii ya siku hizi ya mgambo kukimbizana na wamachinga na mama lishe.
 
Hahahaaa Katavi umenikumbusha na ile Kodi ya baiskeli....dah ni maisha ya zamani yanayokumbusha hisia fulani za ukweli...
enzi za viatu vya CHACHACHA na SAA NANE UTANIKOMA....Duh unakumbuka???
 
mi nakumbuka kuna siku ma anko zangu walibebwa mzega mzega na mgambo kisa hiyo kitu,nilibaki kutoa macho tu,ila zamani maisha yalikuwa swadakta sana,tofauti na enzi hizi za jk

Kuna siku walinikosakosa na ndio nilikuwa nimemaliza kidato cha nne, kitambulisho kiliniokoa!
 
Kaka salama?
Du!nahisi hii kitu ilisumbuaga sana watu miaka hiyo,
Mie hata sikumbuki km niliwahi kuishuhudia ua vp zaidi yakusikia story tu kwa watu!!
Nahisi ilikuwa inafanana na hii ya siku hizi ya mgambo kukimbizana na wamachinga na mama lishe.

Mzima wewe?............ilikuwa ni sawa au zaidi ya hii ya machinga na mgambo. Sina hakika kama wanaume wa Dar walipata misukosuko ya kodi ya kichwa!
 
Mie mzima sana aiseee,
Kuna mahali nimekuona alafu!!

Inawezekana ile kodi ilikuwa ikitozwa vijijin tu?
Basi walikuwa na raha!
 
Back
Top Bottom