Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,820
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 19/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
=======


Kufahamu ilipoishia, soma hapa:Yaliyojiri mahakamani kwenye Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Kesi imeahirishwa hadi 19/01/2022

Jaji ameingia, kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa.

Jaji: Shahidi Nakukumbusha Upo Chini ya Kiapo Bado na Wakili wa Mshtakiwa Namba Mbili Ilikuwa Unaendelea, Karibu

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba nikumbushwe niliishia wapi

Jaji: Uliishia Wakati anakusomea Kielelezo H


Freeman Mbowe.jpg

Mallya: Shahidi tusomee hii ni Tarehe

Shahidi: Imeandikwa 05 August 2020

Mallya: Kuna Entry imeandikwa Owner of Article, Kwenye PF Je imeandikwa Jina gani?

Shahidi: Nashindwa Kusemea Sana Mheshimiwa Jaji sababu Siyo Mimi Niliyeandaa

Jaji: Hujaambiwa Uisemee Umeambiwa Usome

Shahidi: Imeandikwa Mohammed Abdallah Ling'wenya.. Lakini sijaandaa mimi

Mallya: Kwa Hiyo nani kaleta Mahakamani

Shahidi: Ni Mimi

Mallya: Kwa hiyo tuiondoe Mahakamani?

Shahidi: Hapana

MALLYA: Soma Sasa

Shahidi: Mwisho Imeandikwa DOYI

Mallya: Kutoka Tarehe 05 August 2020 Mpaka Tarehe Uliyo letewa Kwenye Ofisi yako Kuna Interval ya Siku Ngapi

Shahidi: Kuna Interval Ya Siku 08

Mallya: Na wewe Ulifanyia Kazi Tarehe Ngapi

Shahidi: Mwezi Wa July 2021

Mallya: Tarehe Ngapi

Shahidi: Sikumbuki Tarehe

Mallya: Kutoka Muda Umeletewa Mpaka Unafanya Uchunguzi Kuna Muda gani

Shahidi: Angalau Miezi 10

Mallya: aliyekuletea hiyo Item "H" alikwambia alikamata katika Physical Condition gani

Shahidi: Hakuniambia

Mallya: Alikwambia alikuwa Amehifadhi Siku gani

Shahidi: Hakuniambia

Mallya: alikwambia Kwamba aliondoa au Kutumbukiza Physically Kitu gani

Shahidi: Hakuna Kitu kama hicho Unachosema, kuwa alitoa chochote, Utaratibu Wa Kutunza Kielelezo Unajulikana, Kwa Utaratibu Wa Polisi Kielelezo Umapo Ki Seize unapaswa Umantain Kilivyo

Mallya: aliyekuletea alikwambia alifuata Utaratibu au Haku fuata Utaratibu huo

Shahidi: Ni Askari Polisi ni Imani yangu alifuata

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu Swali Langu

Shahidi: Mheshimiwa Jaji swali linahitaji Maelezo,

Jaji: Nani sasa, Maelezo ya Wakili au Ya Kwako?

Shahidi: Mimi Naamini Kuwa Utaratibu ulifuatwa

Jaji: Swali lake Halipo Huko kama Utaratibu ulifuatwa au Lah Bali Je alikueleza

Shahidi: Mheshimiwa Jaji hakunieleza

Mallya: Ndiyo Jibu ndiyo Nilikuwa nayafuata

Mallya: Kwenye Kielelezo H Kuna Physical Damage inaonekana hapa, Kuna gaps, Je Macho yangu ya naona sawasawa

Shahidi: Condition Siwezi Kuzungumzia hapa

Mallya: Hilo Sijakuuliza, Nauliza Kuna Damage hapa Inaonekana, Je Kinachoonekana ni nini

Shahidi: Kinachoonekana ni Simu

Mallya: Siulizi simu hapa Mahakamani, usilete mahakamani michezo yako..

Mallya: Unachokiona ni Kitu gani

Shahidi: Ninachokiona ni Simu Mheshimiwa Jaji

Mallya: Ngoja Nichukue Simu F tulinganishe na H, Zote Umeleta Wewe, Swali langu hii yenye haya Ma gaps unahitaji?

Shahidi: Mhe Jaji Hizi ni simu Mbili tofauti, Siyo lazima zifanane..

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Wakili amebakia Muda Mrefu na Majibu yameshatolewa, Swali lake limeshajibiwa

Mallya: Mheshimiwa Jaji Swali langu halijajibiwa bado

Jaji: Muulize swali tena

Mallya: Kwenye Kielelezo H Kuna Ma' gaps, Je kitaalamu Unayaitaje?

Shahidi: Miye siwezi Kuongelea chochote

Mallya: Hii difference ya Kuwa hii ina button Kwenye simu na hii haina, unasemaje?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji siwezi Kuzungumzia kuhusu tofauti

Mallya: Kwenye Riport yako Kwenye Kielelezo F Je aina Positive Results..?

Shahidi: Ndiyo Ilikuwa na Positive Results

Mallya: Kuna Simu Ulizo letewa ukakuta Hazina Positive Results Kama Ulivyoletewa kwenye Terms of reference

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa Mujibu wa Sheria Askari Polisi anaruhusiwa Kukamata simu.?

Shahidi: ndiyo Kwa Mujibu wa Sheria

Mallya: Kama Askari Polisi anataka Kujiridhisha Juu ya Kitu anachotafuta analeta Forensic?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Unafahamu Simu ni Personal Property ya Mtu?

Shahidi: Inaweza Kuwa Simu ya Ofisi

Mallya: Yapo Mazingira Mtu anaweza Kuwa na Simu Kama Mali yake Binafsi.?

Shahidi: Kama amenunua ni Mali yake Binafsi

Mallya: Je Yule ambaye amekamata kama Hajakuta Kitu anatakiwa kumrudishia Simu yake..?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Unafahamu Kwenye Simu ya Mtu Binafsi ambayo kanunua Kwa Pesa Yake, Inaweza Kuwa na Taarifa zake Binafsi?

Shahidi: Simu ya Mtu anaweza Kuweka Taarifa ambazo anahisi anaweza Kuhifadhi

Mallya: Kuna uwezekano Kuwa Mtu akahifadhi Taarifa au Nyaraka ya Utetezi kwenye Simu?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Taarifa Uliyompelekea huyo aliyekuomba Umfanyie Uchunguzi, Je akipokea Kwa Mkono au Kwa Email?

Shahidi akipokea Kwa Mkono

Mallya: Je alisoma hiyo Taarifa Yako ya Uchunguzi

Shahidi: Naamini alisoma

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 23 Samahani

Mallya: Shahidi Interest yangu Katika Riport Yako ni Ukurasa Wa Sita Unapozumgumzia Kuhusu Kielelezo A, B, C, D

Shahidi: Vielelezo Tajwa A, B, C, D hazina Taarifa Zenye Maudhui

Mallya: Kwenye Hicho Kielelezo namba C ulikuta ni Cha Nani

Shahidi: Ni Cha Khalfani Bwire

Mallya: Kwa hiyo Katika simu ya Khalfani Bwire hukukuta Jambo Lolote?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Ulifanya Uchunguzi Wako Lini

Shahidi: July 2021

Mallya: Ulikuja Kutoa Ushahidi wako lini

Shahidi: Juzi January 2022

Mallya: Kuna Interval ya Muda gani kati ya Wewe Kufanyia Uchunguzi Mpaka Kutoa Ushahidi

Shahidi: Usio Pungia Miezi Mitano

Mallya: Hiyo Content ambayo ulikuta negative Results upo wapi

Shahidi: Sikuona Haja ya Kuweka Kwa sababu sikukuta Kitu

Mallya: Bwana Bwire alikuwa anataka Negative Results ambayo Ingekuja Mahakamani Kuonyesha Kuwa Hakuna Maswala ya Ugaidi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Nilipewa Terms of Reference, Kwa Hiyo Kama Haipo siwezi Kutoa

Mallya: Shahidi Umesha wahi Kupima Malaria

Shahidi: Hilo swali Limeingiaje hapa

Mallya: Kwa Sababu Wewe ni Mtu wa Laboratory na Malaria inapimwa Laboratory?

Shahidi: Sioni likihusiana

Mallya: Kwa Sababu Wewe ni Mtu wa Laboratory na Malaria inapimwa Laboratory

Shahidi: Sioni likihusiana

Mallya: Lina husiana Kwa Sababu Malaria Ukipimwa Wakikuta Negative Results wanakupa Majibu Yako

Shahidi: Kuna Baadhi ya Simu Zina Taarifa zaidi ya GB 20 huwezi Ku Print zote

Mallya: Je ulitoa taarifa Kwamba hukukuta kwa sababu ni Kubwa

Shahidi: Kwa sababu ni Out of Context

Mallya: Ulishajibu Kuwa Hukuona Haja

Shahidi: Siku Jibu hivyo

Jaji: Hapo Ndipo Mr. Malya Unapotuchanganya, Ni wapi Tutaona Huku uliza

Mallya: Nilikuwa namkumbusha Majibu Yake

Jaji: Basi Kama Unaulizwa Swali Hakuna Haja ya Kuongea Yote hayo

Mallya: Shahidi Nilisikia Unasema Mnatumia Legitimate Software Ku Updates yenu, Je Ulizungumzia Mnapewaje

Shahidi: Hapana Sikuzungumzia

Mallya: Mheshimiwa Jaji Naomba Barua ya Airtel na Ya Tigo

Mallya: Nakuonyesha Kielelezo P15 na Interest yangu ni Mtu aliyepewa hii Barua

Shahidi: Barua hii Imeelekezwa Kwa Kamishina wa Uchunguzi wa Kisayansi

Mallya: wewe sasa hivi ni Inspector Wa Polisi, Je Mwaka 2021 uliwahi Kuwa Kamishina wa Polisi

Shahidi: Mimi Sijawahi Kuwa Kamishina

Mallya: Kwenye hii Barua wapi Umekuwa Adressed.?

Shahidi: imekuwa Adressed Kwa Kamishina wa Uchunguzi Wa Kisayansi

Mallya: Naomba na ya Tigo

Mallya: Umesema Ofisini Kwenu Mkubwa wa Command ni Nani

Shahidi: Anaitwa CP SHABANI

Mallya: Kuna Departments Ngapi katika Forensic Beaural

Shahidi: Tuna Units Mbalimbali Ka Cyber crime ambayo Natoka Mimi, Toxicology, DNA, Pathology, Fingerprints, Ballistic, Documents, Crime scenes

Mallya: Kwa Mahesabu yangu ni Nane, Kwa Kiswahili zinaitwaje?

Shahidi: Kamisheni ya Uchunguzi Wa Kisayansi

Mallya: Zote hizi Ukubwa Wake Kwa Maana ya Commanding Ofisa wake ni CP SHABANI.?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Naomba uniseme Adress ambayo Tigo Wameitumia

Shahidi: UCHUNGUZI WA KISAYANSI
S. L. P 9094
DAR ES SALAAM
TANZANIA

Malya: naomba Mwenzangu Wakili Faraji Mangula aendelee

Mangula: Shahidi Pole na kuuguq Kichwa Siku ya Kwanza

Mangula: Ni sahihi ulisema Kuwa umesema Advanced Diploma ya Computer Science

Shahidi: Ndiyo

Mangula: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali, Ulielezea Kuwa Baada ya Masomo Ulipata Award gani

Shahidi: Nilisema nilikuwa napata Certificate

Mangula: Wakati Unafanya Uchunguzi Ulisema Ulikuwa una cheo Gani

Shahidi: Mkaguzi Msaidizi

Mangula: kwa sasa Una cheo Gani

Shahidi: Inspector

Mangula: Wakati Mawakili Wanakuongoza Hapa Mahakamani, Je ulisema Kuwa Ulipata Mafunzo gani Mpaka Ukapanda Cheo

Shahidi: Unakuwa Awarded siyo Kwa Kwenda Kozi

Mangula: Cheo chako umekipata wakati awamu ya 5 au ya 6?

Shahidi: Sijaelewa logic ya swali lako

Jaji: Swali la nani alikuwa Rais, unataka kujenga nini

Mangula: Mhe Jaji kuna premise nataka kutengeneza

Jaji: hiyo premises ndiyo utengeneze kupitia Rais aliye madarakani?

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mahakama Ilisha wahi Kutoa Maelekezo Juu ya Kutaja Majina ya Watu ambao Hawapo Mahakamani

Jaji: nilitoa Maelezo Kuhusiana na Kutaja Majina ya Watu ambao Hawapo Mahakamani, lakini pia nataka Kujiuliza Kuhusu Kuuliza Maswali ya Rais wa Awamu ya Tano au Lah

Sasa Unachotaka hapo ni nini.?

Mangula: Ngoja Niulize Kwa Namna Nyingine

Mangula Naomba Kielelezo Namba 23,Shahidi Naomba Usome Kwa Sauti Kichwa Cha Habari cha Hicho Kielelezo

Shahidi Kamisheni ya Uchunguzi Wa Kisayansi, ya Makosa ya Kimtandao Chini ya Sheria ya Mtandao namba 14

Mangula: Je ni kifungu Kipi ambacho umekitumia?

Shahidi: Mimi siyo Mtaalamu wa sheria, Ila nilifanya kwa sheria ya mtandao

Mangula: Mwambie Mheshimiwa Jaji sasa ni kifungu kipi ulitumia

Shahidi: Mheshimiwa sikutumia kifungu

Mangula: Nikikupa hiyo sheria, unaweza Kunitajia kifungu ulichotumia

Shahidi: Mimi sina UFAHAMU WA MAMBO YA KISHERIA

Mangula: Kwa hiyo nyie Ofisini kwenye mnafanya bila ufahamu wa Sheria

Shahidi: Nishasema mheshimiwa SINA UFAHAMU WA SHERIA

Mangula: Fungua sasa Ndani, Ieleze Mahakama ni Kielelezo Kipi Ulichofanyia Kazi Ukagundua Kuna Makosa ya Ugaidi Uliyaona, Ni wapi Umeandika hivyo..

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Jibu linahitaji Maelezo, Mimi nililetewa tu Kufanya Uchunguzi.

Mangula: Kwa hiyo wewe hujui Kuwa Kuna Ugaidi au Hakuna Ugaidi kwenye hicho Kielelezo?

Shahidi: Sahihi

Mangula: bado unataka Mahakama ichukue Kielelezo Hiki Kama Kielelezo Cha Umuhimu?

Shahidi: Nimesema ni Kazi ya Mpelelezi

Mangula: Umesomeshwa na Serikali?

Shahidi: Ni Sahihi

Mangula: Na Umelipiwa Masomo Kwa Kodi ya Watanzania

Shahidi: Sahihi

Mangula: wewe Umesomea Udukuzi

Shahidi: Nimesomea Ethical Hacking

Mangula: Ulisema Mwanzo Kuwa Vifaa Vyako Vya Uchunguzi Vina Uadilifu

Shahidi: Ndiyo

Mangula: Na Kila Unachotaka Kwenye hiyo Simu, Mambo wako Unakuonyesha

Shahidi: Yes

Mangula: Kama Kuna video inakuomyesha.?

Shahidi: Inaonyesha Vile Vitu ambavyo Inaweza Ku Extract Kwenye Kielelezo

Mangula: Inakupa kila Kitu ambacho Kipo Kwenye simu?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Mangula: Mheshimiwa Jaji Naomba Extraction Report

Mangula: Katika huo Mambo unaosema Ulikuwa upo Sawa Kukupa Kila Kitu, Ukisoma Kielelezo Cha Kwanza hicho namba 25

Mwambie Mheshimiwa Jaji kwenye hicho Kifaa Ulichofanyia Uchunguzi Kulikuwa na Content gani

Shahidi: Kukikuwa na Proxy Ya Chat ya WhatsApp

Mangula: Kulikuwa na Picha Kwa Maana Images

Shahidi: Picha Hakuna, Zipo Profile Picture

Mangula: ambazo ni za nani

Shahidi: Sijui za nani

Mangula: Katika hivyo Vielelezo ambavyo Vimepokelewa Mahakamani, Palikuwa na Mazungmzo ya Simu kati ya Watuhumiwa

Shahidi: Hakuna ila kwenye Kielelezo namba 26 zipo

Mangula: apewe Namba 26,,tuchagulie Mazungmzo Marefu Kuliko yote

Shahidi: Kuna Mazungmzo ya Dakika 9

Mangula: Bila Shaka Ndipo walikuwa wanapanga Ugaidi, Haya Mwambie Mheshimiwa Jaji Walizungumza nini hawa Watuhumiwa

Shahidi: Kuna Call Logs tu

Mangula: zile Sauti zipo wapi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kama Mahakama Yako itaniruhusu Kwa sababu za Ki Usalama nisijibu Hilo swali

Mangula: Swali langu ni Juu ya Watuhumiwa Ukiwa Mchunguzi wa Hizo Simu, Nauliza Mazungmzo ya Watuhumiwa Wale Wanne, Narudia Swali Sauti zao Watuhumiwa Zipo wapi ndugu shahidi?

Shahidi: Sababu za Kiusalama huwezi Kuzungumzia suala la Sauti

Mangula: Shahidi Nimesikia unasema Kuwa huwezi Kuzungumzia Kwa sababu ya Kiusalama, Je Sheria gani inakuzuia Usizungumzie hilo Suala?

Shahidi: Sijataja Sheria

Mangula: haya Sasa Mwambie Mheshimiwa Jaji, Sauti za Watuhumiwa Zipo wapi????

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Hazikuwa zinahitajika katika Terms Of Reference

Mangula: Ni sahihi nikisema Kuwa Katika Extraction Uliyo fanya, Kuna Vitu Uliviondoa sababu hazikuhitajika?

Shahidi: Swali linahitaji Maelezo, Mwanzoni Nilisema Kuwa Tunafanya Kwa Hatua tatu, Aquisation, Analysis na Extraction

Mangula: Kwa hiyo ni sahihi Kuwa Kwenye Mtambo Kuna Baadhi Ya Taarifa Hukutoa Sababu Hazikuhitajika?

Shahidi Wa Jamhuri: Kimya

Mangula: Kwa Mujibu Wa Kielelezo Namba 22, Mwambie Mheshimiwa Jaji Vitu gani Viliombwa Kwa ajili ya kufanyia Uchunguzi

Shahidi: Kwa Mujibu wa Barua yako Yenye Reference........

Mangula: Hoja ya Barua Ilikuwa unahitaji Ufanyie nini

Shahidi: Pamoja na Taarifa Hii Nakuletea Uchunguzi Niliofanya .... Mimi Inspector Innocent Ndowo

Mangula: Ni wapi Walikutaka Wewe Usitoe Sauti za Watuhumiwa?

Shahidi: Mimi nilifuata Terms of reference

Mangula: Nikisema Kuwa Wewe Inspector Ndowo na Viongozi Wako wa Polisi Kwa Makusudi Mliamua kuficha Baadhi ya Taarifa katika
Kesi hii kwa Maslahi yenu Itakuwa sahihi au siyo Sahihi Ukizingatia Kuna Taarifa Hazipo hapa?

Shahidi: Siyo Sahihi, Hatufanyi Kazi kwa interest zetu

Mangula: Fungua Kielelezo H, na Umwambie Mheshimiwa Jaji IMEI namba ya hicho Kielelezo Ni namba Ngapi Kwa Mujibu wa PF 145

Shahidi: Kwa Mujibu wa PF Hakuna IMEI namba

Mangula: Soma huo Mstari Wa Pili Kwa Sauti Umeandikwaje

Shahidi: Simu TECNO IMEI imefutika

Mangula: Wakati Unaongozwa Kwenye Ushahidi Ulisema nani aliyefuta hizo IMEI namba

Shahidi: Si Kuulizwa hilo swali

Mangula: Wewe unafahamu aliye futa hiyo IMEI namba

Shahidi: Simfahamu

Mangula: Katika hicho Kikaratasi Umeeleza IMEI namba Imefutwa Wapi.?

Shahidi: Sikusema

Mangula: ukiacha Kielelezo namba 35 ambacho kimechezewa na Watu wasiojulikana , Ni Kielelezo Kipi Kingine Mlichochezea

Shahidi: Hakuna Kielelezo Kilichochezewa

Mangula: Fungua Kielelezo namba 23, Mheshimiwa Jaji Namuonyesha Kielelezo namba 23

Mangula: Nataka Majibu ya Riport Yako ya Uchunguzi

Mangula: Mwambie Mheshimiwa Jaji ni wapi Katika Report Yako ya Uchunguzi Umeandika IMEI namba Imefutika

Shahidi: Hakuna Mahala Nilipo andika

Mangula: Nilisikia Unasema Ulichukua simu Ukiweka Katika Mtambo Wa Uchunguzi, Ule Mtambo utakuonyesha Kuwa Simu ni Original au Feki

Shahidi: Mtambo hauonyeshi Kuwa Simu ni Feki au Original

Mangula: Kitu gani Kinaonyesha kuwa Simu ni Feki au Original

Shahidi: Kitu nilichosema Kuna Kama zile Simu za Kichina, Mtambo una Operate kwa OS

Mangula: Kwa hiyo nini Kina onyesha ni FEKI Au ORIGINAL?

Shahidi: Nilichosema naomba Unisikie Vizuri, Mtambo una Option ya Kufanya Kazi hata Kwa kutumia Chip

Mangula: Mheshimiwa Jaji naomba NIISHIE Hapo

Shahidi: Samahani Mheshimiwa Jaji NAOMBA KWENDA WASHROOM (CHOONI)....

Shahidi anatoka na kuelekea katika vyoo vya nje..

Mahakama Ipo kimya inasubiri arejee kizimbani.

Shahidi amerejea kizimbani kutokea kwa fasii ya chooni.

Kihwelo: Shahidi Nilisikia Unazungumzia Kuhusu Celebrite Physical analyser Je ni Software Au.?

Shahidi: Ni software

Kiwhelo: nani alifanya Development ya Software

Shahidi: Celebrite Wenyewe

Kiwhelo: Nilisikia Umesomea Kuhusu Penetration Test

Shahidi: Ndiyo

Kihwelo: Je Penetration Testing, Ni sawa na Fazzing

Shahidi: Sifahamu

Kiwhelo: Je Wakati Unafundishwa Kuhusu Penetration Testing, Walikufundisha Kuhusu Mashambulizi ya Hali ya Juu ya Kimtandao (High Tech Cyber Attack)

Shahidi: Sijafundishwa hiyo

Kiwhelo: kwakuwa Ujafundisshwa kuhusu Mashambulizi ya Hali ya Juu ya Kimtandao, Ni sahihi Celebrite Ingeweza Kuingiliwa

Shahidi: Haiwezi Kuingiliwa

Kiwhelo: pale Ofisini kwenu ni nani Network Provider

shahidi: ni TTCL

Kiwhelo: Ni sahihi Kuwa Network Services Provider anaweza Kuingilia Data Zako

Shahidi: Hawezi

Kiwhelo: Nyinyi Kama Jeshi la Polisi Mnatumia Nini Kujilinda na Mashambulizi ya Hali ya Juu ya Kimtandao

Shahidi: Naomba nisijibu sababu za Kimtandao

Kiwhelo: Nilisikia Kuwa unazungumzia kuhusu DECORDING

Shahidi: Ndiyo

Kiwhelo: Shahidi Pegasus Technology ni Moja ya Technology mnayotumia?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji naomba Nisijibu Sababu za Kiusalama

Kiwhelo: Mheshimiwa Jaji naomba anijibu sababu Baadae Nitataka kujua Intergrity ya Technology Wanayotumia

Jaji: Shahidi ame raise suala la Security, Au mnasemaje Upande wa Serikali?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesha Sema kuwa awezi Kusema Sababu za Kiusalama, Sisi tunaona Sababu hizo ni Valid, lakini siyo kutulazimisha

Kiwhelo: Mheshimiwa Jaji Shahidi Wakati Shahidi anataka Ushahidi Wake Jana Alitaja Hapa Kuhusu Microsoft na Celebrite, alitaja hizo Mbili Maana yake ameshataja

Jaji: Sasa Shahidi Kaja na suala la Security kwa hii Uliyotaja

Kiwhelo: Basi Ngoja Niendelee na Kingine, Shahidi Wakati Una Extract Data Kwenye Celebrite Ulihifadhi Kwenye nini

Shahidi: Nili hifadhi Kwenye Computer

Kiwhelo: Vipi kuhusiana na Usalama wa computer yenyewe

Shahidi: Kimya

Kiwhelo: Uliandika Taarifa ya Simu Nne..?

Shahidi: Simu zote Nane

Kiwhelo: Siku ya Tarehe 09 July 2020 Uliingia Saa ngapi

Shahidi: Niliingia Saa 1 na Nusu Asubuhi

Kiwhelo: na Ulitoka Muda gani

Shahidi: Unatoka Muda wowote, hupangiwi kwa Sababu tunafanya Kazi Masaa 24

Kiwhelo: Mwambie Mheshimiwa Jaji ulikuwa unaandika summary kisha unafuata extraction

Shahidi: Siyo sahihi

Kiwhelo: Soma hapo kwenye report yako

Shahidi: Inaanza na summary kisha extraction

Kiwhelo: Kwa hiyo imeanza na summary

Shahidi: Ni sawa, imeanza na Summary

Kiwhelo: Tuzungumze Kidogo Kuhusu Kampuni ya CELEBRITE Ukasema Kuwa Ni Moja ya Kampuni inayodevelop Software

Je unafahamu Celebrite Ni Kampuni Ya Kijasusi wa Kidigitali ya Nchi Israel

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kiwhelo: Je Unafahamu Kuwa Hiyo Kampuni inahusishwa na Unyanyasaji wa Waandishi Wa Habari na Wana Harakati Duniani

Shahidi: Sifahamu

Kiwhelo: na Je Unafahamu Kuwa Celebrite Mashine Inaweza Kuingiliwa.?

Shahidi: Haiwezi Kuingiliwa

Kiwhelo: Je Nitakuwa Sahihi Nikisema Kuwa Celebrite Mashine Inaweza Kuingiliwa na Kubadili Taarifa Zilizotamgukia na zilizopo

Shahidi: Hapana Siyo Sahihi

Kiwhelo: Mheshimiwa Jaji naomba nimkabidhi Shahidi Nyaraka asome Kuhusiana na Celebrite

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba wakili azuiwe Kusoma hiyo Nyaraka

Kiwhelo: Mheshimiwa Jaji Kwa ajili ya Muda nitaomba Kuachana na hiyo

Naomba nipatiwe P23 na P35

Naomba Sasa Nimkabidhi Shahidi

Kiwhelo: naomba Unisomee description hapo Juu

Shahidi: Imeanza Neno Station, Date 05 August 2020, CF imeandikwa. Simu Imeandikwa Tecno IMEI imefutika, Ilipatikana Maungoni (Mwilini)

Kiwhelo: Mwambie Mheshimiwa Jaji Wewe Umetoa wapi Namba kwa Mujibu wa IMEI namba ambayo Imefutika

Shahidi: Inawezekana Physically Isionekane ila akuna Namna unaweza Kuona, au Kwenye Barua

Kiwhelo: hiyo Barua Ipo Hapa Mahakamani

Shahidi: Haipo Mahakamani

Kiwhelo: Ulizungumzia Kuwa IMEI namba ulitoa Kwenye Barua.?

Shahidi: Nili zungumza Kwa Ujumla

Adv. @FrederickWakili
: Mheshimiwa Jaji nimeishia hapo na naomba kurudisha vielelezo

Anasimama Wakili Msomi Peter Kibatala.

Kibatala: Inspector Ndowo Mambo Vipi

Shahidi: Salama

Kibatala: Siku ya Kwanza Uliomba Kusitisha Ushahidi Kwa sababu uliumwa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Ulipitia Hospitali.?

Shahidi: Nilienda Ofisini, nikarudisha Vielelezo

Kibatala: Kwa hiyo Baada ya Kutoka Hapa Hukwenda Hospitali Moja kwa Moja

Shahidi: Si kwenda Hospitali Moja Kwa Moja

Kibatala: Ulisema Kichwa Kilikuwa Kinafanya nini Vile

Shahidi: Kilikuwa Kinaniuma Kadri nilivyokuwa natoa Ushahidi

Kibatala: Na Kwa hiyo Ofisi Yako Ilikuwa wapi Vile

Shahidi: Posta

Kibatala: na Baada ya Hapo Ukaenda Hospitali Wapi

Shahidi: Kilwa Road

Kibatala: Twende Kwingine, Shahidi Je Uliwahi Kufanyiwa Training na Watu wa CELEBRITE

Shahidi: Yes Wawakilishi Wao

Kibatala: Unakumbuka Kozi Mbalimbali Ulizo taja Siku ya Kwanza Ukiwa unataja Mafunzo mbalimbali uliyopata.

Kibatala: Je kwa Kumbukumbu yako Ulitaja Mafunzo Yaliyo endeshwa na Celebrite au Wawakilishi wao

Shahidi: Jibu Lina hitaji Maelezo, Nilitaja Kozi Mbalimbali na Baadhi walitoka Nairobi.

Kibatala: Maelezo Ambayo Umeyatoa, Kuna Mahali Umesema Kuna watu Walitoka Nairobi Kuja Kuku train Kuhusu Celebrite.%?

Shahidi: Nilipata Kozi Mbalimbali, sikudadavua

Jaji: Swali Lake Ulisema Kuwa Kuna Wataalamu Kutoka Nairobi Kuja Kuku Fundisha Kuhusiana na Celebrite.

Shahidi: Sikutaja Mheshimiwa

Kibatala: Katika Maelezo yako, Ulisema Ulienda Training Mahala Mbalimbali, Je Ulisema Kuwa ulienda Israeli.?

Shahidi: Israel Sikutaja

Kibatala: Unafahamu Kuwa Makao Makuu ya CELEBRITE Yapo Nchini Israel

Shahidi: Nafahamu Yapo Israel

Kibatala: Je Unafahamu Kuwa Israel Kwa Wivu na Technology yao Hawaja Outsource kwa Mtu Kuhusiana na Training wala Technology?

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kuwa Nairobi Hakuna Wakala Wa CELEBRITE?

Shahidi: Hapana Sifahamu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakili anataka Misamiati Migumu ya Technology shahidi anaweza asijue ni nini Kinaongelewa.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji hakuna hoja hapo, Mbona shahidi anajibu, Eti ndugu shahidi, ni kweli huelewi Kitu?

Shahidi: Ndiyo sielewi

Kibatala Kwanini sasa ulikuwa unajibu?

Shahidi wa Jamhuri: Kimya

Kibatala: unafahamu sababu ya Wivu Wa Technology, Israel Hawana Mwakilishi wa CELEBRITE Duniani katika Nchi yoyote

Shahidi: Yupo Nairobi

Kibatala: Anaitwa Nani

Shahidi: SAM

Kibatala: Unafahamu Kuwa Technology ya Pegasus ni Technology ya Israel Pia

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: una Cornfirm kwetu bila kwenda kwenye details kuwa Jeshi la Polisi mnatumia pegasus?

Shahidi: Naomba nisijibu hilo swali kwa sababu za Kiusalama

Kibatala: Baadae Nitakuja hapo na nitakutaka kwa lazima ujibu hilo swali, kwa sasa ngoja niende kwingine.

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Celebrite unatumia Software Mbili UFET na physical analyser?

Shahidi: Ndiyo ni baadhi ya product za kwake

Kibatala: UFEN kazi yake I naingia katika Simu au Computer kisha Inatengeneza Back up

Shahidi: Inategemea na level ya Extraction Unayofanya

Kibatala: Ni sahihi Kuwa katika kazi Uliyo kuwa unafanya unaunganisha Simu Kwa Kutumia Cable kisha Celebrite inachofanya Kwa kutumia UFEN Kutengeneza Back up

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kuwa physical analyser Inafanya kazi Kwa Ku arrange Taarifa In Chronological Order

Shahidi: Sahihi ila inategemea Level

Kibatala: Jaji akimaliza Ku Rekodi Mwambie Kuwa Kazi ya Physical Analyser Kama Software Ni kuyapanga Mafaili Kwa Mchunguzi ili Ku Make Sense na hiyo Process inaitwa PASSING

Shahidi: Naomba nijibu kwa Maelezo Kuwa Physical analyser, Inafanya kazi 3 ila Kwa Ujumla Ndiyo PASSING

Kibatala: Katika Report Yako Kuna Item Ya PASSING

Shahidi: Kama Software Include hizo Taarifa zake, Basi itaonekana

Kibatala: Basically Physical analyser haina Jipya Zaidi ya kupanga Mafaili

Shahidi: Hapana Physical analyser ni zaidi ya hapo

Kibatala: Tofauti Yake nini, Kama Unaingia Kwenye simu yangu ya Telegram na kisha unapamga Mafaili

Shahidi: Ni zaidi ya hapo kwa sababu ina Uwezo Kuwa Kufanya Back Up Kwa Vitu Vilivyofutwa

Kibatala: Physical ANALYSER inaweza za KubadiliSha Chochote

Shahidi: Hapana

Kibatala Physical analyser Ina extract

Shahidi: Hapana

Kibatala: unapokuwa na Kifaa kama Simu Kutoka Kwa DCI Nini Kilianza Kati ya kutumia UFEN Kufanya Extraction au Physical Analyser Kupamga kazi yako

Shahidi: Nilianza Kutumia UFEN

Kibatala: Wewe Umeletewa 8 applications phones, Je zile Data zilizokuwa katika Hizo phones, Je ni Software gani zilikuwezesha Kuingia Kwenye simu na Kusoma Meseji

Shahidi: Ni Physical analyser

Kibatala: Sasa Mbona Mwanzo Ulikataa, Wacha sasa Ikae Hivyo

Kibatala: Jana Ulizungumzia Kuwa huwezi Ku impose Vitu Vyako Kutoka Nje,

Shahidi: Ndiyo WRITE BLOCK

Kibatala: Unafahamu Kuhusu Software ya CELEBRITE Kuhusu Soft Write Block?

Shahidi: Hiyo sifahamu kwa kweli

Kibatala: Ni kweli au siyo Kweli Kuwa Celebrite Soft Write Block Ndiyo inayomzuia Mtu Kuingilia Mashine ya CELEBRITE

Shahidi: Hiyo sifahamu

Shahidi: Na Bado Ukitaka Kutuaminisha Kuwa Mashine zenu zina Intergrity?

Shahidi: Ndiyo Sijataja

Kibatala: Je ulitaja Jana software zaidi ya Mbili

Shahidi: Sikutaja

Kibatala: Ulizungumzia Forensic Cables,

Shahidi: Sawasawa

Kibatala: Ni Cables kama za USB tuh au Kuna tofauti

Shahidi: Ni Tofauti Kabisa

Kibatala: Inasifa gani Kitaalamu ambayo ni zaidi za USB

Shahidi: Ni Cable Zenye namba pembeni

Kibatala: Je Hapa Umetaja Namba za Cables

Shahidi: Hapana

Kibatala: Hizi Simu ambazo wewe Ulifanyia Extraction, Makers ni Tofauti

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Jana Nilisikia Unasema wewe siyo Mpelelezi ni Mchunguzi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni wapi au Kwenye Instrument ipi Inatofautisha Mpelelezi na Mchunguzi?

Shahidi: Ukija Ofisini Utajua

Kibatala: Mpaka Nije Ofisini kwenu, Vipi PGO Inatambua?

Shahidi: Sijui

Kibatala: PGO ya 8 Sehemu Ndogo ya 4 inasema Kuwa Ofisi Ya DCI inagawanywa katika Divisheni Nne, Mmoja wapo ndiyo hiyo ya Forensic Beaural

Shahidi: Sijui ni PGO gani

Kibatala: zote mbili

Shahidi: Mimi ninachojua Forensic Beaural ni Imtependent Beaural

Kibatala: na Ndiyo Maana ni Kuuliza Unapata wapi Mgawanyo huo

Shahidi: Ukienda Ofisini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi au Dodoma

Kibatala: Mhe Jaji naomba Kielelezo 6,7,

Kibatala: angalia Maneno ya DCI Katika hiyo Barua. Unafahamu Kirefu chake?

Shahidi: nimesahau kidogo

Kibatala: Mimi nikikwambia kwamba kirefu cha hayo maneno uliyoandika wewe kwenye barua yako ni DIRECTOR OF CRIMINAL INVESTIGATION?

Shahidi: Sijui mpaka Nipate Mwongozo Wa Wakubwa zangu

Kibatala: Juu pia maneno ya DFSI kuwa ni DIRECTORATE OF FORENSIC SCIENCE INVESTIGATION?

Shahidi: Sifahamu mpaka Nikumbushwe na wakubwa zangu

Kibatala: Na Bado wewe Unasema ni inspector wa Jeshi la polisi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala Mheshimiwa Jaji muda wetu wa kupumzika umefika, labda nipate mawazo kutoka kwa wenzetu nina maswali mengi bado

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tu' break dakika 45

Wakili Peter Kibatala Saa Saba na Dakika 45

Jaji: Tuna break kwa dakika 45 tutarudi saa saba na dakika 45

====

Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 8 na Dakika 5

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile vile

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi Quorum yetu ipo Vile vile

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Nikumbushwe Nilipo Ishia

Jaji: ulimuuliza Kuwa Bado yeye ni Inspector akajibu Ndiyo

Kibatala: PGO ya 9 inasema Subject to the Direction of the DCI

Je wewe Unapata Mwanga kuwa Ofisi ya Forensic Beaural Bado ni Ofisi inayojitegemea

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji tunaomba tujiridhishe

Kibatala: wacha nibadili swali

Kibatala: Shahidi ulipokea Barua Kutoka Kwa DCI lini

Shahidi: 13 August 2020

Kibatala: Kwakumbu Kumbu yako Version ya PGO ipi ilikuwa Inafanya Kazi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: kwa hiyo nikikusomea PGO ya wakati Unapewa Barua, ilikuwa Inatumika ambayo ni Ile inayosema Mpo Chini ya DCI?

Shahidi: Naomba Kutoa Maelezo, Mimi siyo Msemaji wa Jeshi la Polisi

Kibatala: na hilo nalo ni Jibu, Sijui Kwanini upo Hapa

Kibatala: Katika PGO ambayo ulikuwa unafanyia kazi wakati huo 9(c) Vifaa Kama Simu Vimetajwa?

Shahidi: Mhe samahani wakili NIMEMWAMBIA sifahamu KUHUSU PGO LAKINI NAONA MWENZANGU KAJIKUTA KWENYE PGO TU..

Kibatala: Nivumilie tu, mimi nisipokuuliza swali kuna sehemu nitaulizwa

Kibatala: Katika Majukumu yako Ulifanya Kazi Baada ya Kupata Barua Kutoka kwa DCI

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: na Kilicho Pelekea Wewe Kufanya Uchunguzi yalikuwa ni Maombi Kutoka kwa DCI

Shahidi: Sahihi

Kibatala: na Maombi hayo yalikuwa na Terms of Reference

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Ofisi ambayo inajitegemea Kimamlaka Je Inaweza Kupokea Terms of reference katika Utendaji wake wa Kazi

Shahidi: Sitaki Kujiunga katika Maneno yako, lakini Uchunguzi Ulifanyika Ujue Kuna Sababu ulizopewa

Kibatala: Bado Haujajibu swali, Je Ofisi Ambayo inajitegemea Kimamlaka Je Inaweza Kupokea Terms of reference

Shahidi: Barua Zinapokuja, na Hatujui lolote linaloendelea

Kibatala: Swali langu lipo pale pale Kwamba Je Taasisi ambayo inajitegemea inaweza Kupewa Terms of reference

Shahidi: Kesi husika Inapokuwa kwetu, Kuomba Kufanya Uchunguzi, Lazima. Ije na Barua na Lazima isema Vitu ambavyo inaomba Ichunguze

Jaji: Taasisi ambayo inajitegemea inaweza Kupewa Hadidu za Rejea?

Shahidi: Ndiyo tunavyofanya hivyo hivyo

Kibatala: Wewe Kwa Ufahamu Wako, Taasisi inayofanya Uchunguzi Inaweza Kukusanya Ushahidi

Shahidi: Sijasema Kuku Sanya Ushahidi

Kibatala: Ulisema Nini

Shahidi: nilisema Kuandaa Ushahidi

Kibatala: Taasisi inayofanya Uchunguzi Inaandaa Ushahidi au Findings

Shahidi: inaandaa Findings kwa ajili ya a Kutumika kwenye Ushahidi

Kibatala: Wewe in Inspector Wa Forensic au Inspector Wa Jeshi la Polisi

Shahidi: Ni Inspector Wa Jeshi la Polisi

Kibatala: Unapofanya Uchunguzi, unafanya Uchunguzi wa akosa la Jinai au Uchunguzi Wa Vifaa

Shahidi: Nafanya Uchunguzi wa Vifaa

Kibatala: Kwa hiyo Unafanya Uchunguzi Wa tuhuma Za Jinai au Hufanyi

Shahidi: Sisi Kazi yetu ni Kuchunguza Vile Vifaa Vilivyotumika katika Jinai

Kibatala: Katika kesi hii wewe ulichunguza tuhuma Za Jinai au Lah

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Vifaa Vinavyo kuja Ofisini, is a must Vifaa Vile na Namba ya Kesi husika, Kwa hiyo Jinai Wanaopeleleza Ni Wa pelelezi

Kibatala: kwa hiyo wewe Unachaguza tuhuma Za Jinai au Lah

Jaji: amesema anachunguza Vifaa ambavyo Vinahusishwa na Jinai

Kibatala! Okey any way, Twende Kwenye Barua ya Tigo Soma

Shahidi: "Ofisi Inafanya Uchunguzi Wa Tuhuma Za Jinai....."

Kibatala: kwa Mujibu wa Barua hiyo uliyoandika Wewe Mwenyewe Ulikuwa unachunguza Tuhuma Za Jinai

Shahidi: Ofisi yangu hai Chunguzi Tuhuma Za Jinai

Kibatala: hiyo Barua uliyoandika wewe Kwenda Tigo, na Majibu ya Barua ya Tigo na Vielelezo Kutoka Tigo ni sehemu ya Riport Yako au Siyo sehemu Riport yako

Shahidi: Ni sehemu ya Riport yangu

Kibatala: Ile Originating letter Kutoka Ofisi ya DCI ipo au Haipo Hapa Mahakamani

Shahidi: Hapa Mahakamani Haipo

Kibatala: Shahidi hapa Kuna namba zimeandikwa CD IR 2020..... Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa hizo ni Reference kutoka Forensic au Kutoka Kwa DCI

Shahidi: Hizo ni Reference namba Kutoka Ofisi ya DCI

Kibatala: ambazo hizo hizo Uliwaandikia Tigo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Shahidi Ni sahihi Ume nukuu Sheria ya Makosa ya Mtandao Kifungu cha 34

Shahidi: Ndiyo Niliandika

Kibatala: Tigo walikuwa na nafasi ya Kukataa

Shahidi: Ukisoma Sheria Utajua

Kibatala: Hii Barua Kaandika nani?

Shahidi: Mimi Mwenyewe

Kibatala: Je unafahamu hicho Kifungu ni Kifungu Pelelezi?

Shahidi: Sijui

Kibatala: Kama Tigo Wasingewapa hizo Taarifa Mgewachukilia Hatua?

Shahidi: Kwanini uongee Kitu ambacho akijatokea

Kibatala: Je Mahakama Ikuchukulie wewe ni Afisa Wa Polisi Makini?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Barua Kutoka Tigo ambayo Ulitoa kama Kielelezo hapa Mahakamani, Uliwahi Kuiona?

Shahidi Ndiyo Niliwahi Kuiona

Kibatala Na Ukafanyia Uchunguzi Wako

Shahidi ndiyo

Kibatala Nenda Kielelezo namba P7 some Kumbukumbu namba iliyotajwa hapo

Shahidi CD/ IR/ 2007/ 2020

Kibatala Hilo ndiyo Jalada Mama Kutoka Ofisi ya DCI

Shahidi Ndiyo

Kibatala Kama Usingeona hii namba ya Jalada ungefanyia Uchunguzi?

Shahidi: kimyaa

Kibatala: Nenda Barua ya Tigo, Soma Jalada walilo kujibu pale

Shahidi: CD/IR/2097/2021

Kibatala: Inafanana au Inatofautiana?

Shahidi Inatofautiana sababu ya Typing Error

Kibatala: Sijakutuma utaje sababu hala, Wewe sema Imefanana au haijafanana

Shahidi: haijafanana

Kibatala: Katika Barua Yako inasema 2020 na Barua ya Tigo inasema 2021, Je Ipo wapi Barua ya DCI Kuondoa huu Mtanziko?, Umetoa Mahakamani Kama Kielelezo

Shahidi: Barua sijaitoa Mahakamani

Kibatala: Hii Barua Kutoka Tigo ya Tarehe 01 July 2021, ulipokea wewe Binafsi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Jaji Nani alipokea pale Ofisi ya Forensics

Shahidi: Hapana Sikusema

Kibatala: Wewe ni Inspector wa Jeshi la Polisi unafahamu Chain of Custody?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala Ulimwambia Jaji ulipoitoa hii barua?

Shahidi: Nishajibu hilo

Kibatala: Huyu NAFTALI J MANTAMBA yupo au alikufa?

Shahidi: Yupo

Kibatala: yule Kamishina Wenu anaitwa Nani Vile?

Shahidi CP SHABANI HITI

Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kwamba, Wakati Unaandika Barua, Yeye Kamishina Alikuwa anafahamu au hafahamu?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Jaji Wakati Bwana NAFTALI J MANTAMBA Wakati unasaini Barua hii SHABANI HIKI ALIKUWA Magonjwa au Lah

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kuwa upo familiar na Sahihi ya Bwana NAFTALI MANTAMBA, JE Ulimwambia Hukumwambia

Shahidi: Sikusema Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Shahidi Kuan Kielelezo namba P8, Ambapo Kuna Rekodi ya Mihamala Kutoka Namba Fulani Kwenda Namba fulani Ambapo wewe Uliombea namba 0719931389

Shahidi: Naweza Kuelezea kama Nimavyoona

Kibatala: Kwenye Rrport yako Umesemaje

Shahidi: Kwa Mujibu wa Report ya Tigo

Kibatala: Nini primary Source kati Mhamala Wa Tigo au Riport yako wewe

Shahidi: Mimi sijaelewa

Jaji: liweke Vizuri Swali

Kibatala: Ipi ni Primary source kati ya Taarifa ya Tigo na Report Yako

Shahidi: Primary Source ni Report Kutoka Tigo

Kibatala: Kwa Maana hiyo ufahamu Kiasi cha Fedha TSh 500,000 pesa hiyo ilipotoka?

Shahidi: Sender na Receiver anaonekana

Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa Collection Akaunti au Wallet?

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: kwa hiyo Kwenye Muamala Huo wanaoweza Kuzungumzia zaidi ni Airtel?

Shahidi: Airtel ndiyo wanaweza Kuzungumza

Kibatala: Hiyo namba, Ilikuwa ni sehemu ya Terms of reference Uliyopewa na DCI?

Shahidi: Ndiyo Kutaka Miamala Ya Fedha

Kibatala: Katika originating later ilisema Pamoja na Taarifa zingine, ilikupa wigo Mpana

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa katika Uchunguzi Wako wa Vifaa, ambacho wewe Uliona ni Kiashiria cha Kutenda Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Nilichokiona Ndicho nilichokitoa

Kibatala: Katika Uchunguzi Wako Uliona Mawasiliano yoyote yanamtaja Mtu anaitwa Sabaya
Shahidi: Terms of reference Hazikuelekeza Kumtafuta Sabaya

Kibatala: Katika Uchunguzi Wako Uliona Popote Watu wanapanga Kufanya Ugaidi

Shahidi: Mimi sikuelekezwa Kutafuta hilo

Kibatala Katika Uchunguzi Wako wote, Uliwahi Kuona au Kusoma Wakati Wa Extraction Watu wakipanga Kulipua Madaraja

Shahidi: Kimya

Kibatala: Wakati Unafanya Extraction Kuna Mahala Popote uliona Mawasilisho watu wamepamgwa Kuandaa Maandamamo Nchi Nzima

Shahidi: Sikuelekezwa

Kibatala: Uliwahi kuona mawasiliano katika Subject Phones wakizungumzia bunduki aina ya A5340 aina ya Luger?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ananiuliza mambo ambayo sijafanyia kazi

Kibatala: Nakuuliza kuhusu miamala, Je Kuna Telegram text, WhatsApp, au SMS Umeona meseji kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kutenda ugaidi?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Katika meseji zako kuna sehemu ina neno SABAYA?

Shahidi: HAKUNA

Kibatala: Tuambie Muamala upi wewe kama Inspector uliona watu wanapanga tendo la kihalifu....

Shahidi: Hakuna terms of reference yenye Jambo hilo

Kibatala: Kwa uchunguzi wako wewe ungekuta taarifa za kupanga uhalifu, ungeacha kuandika kwenye report yako kwa sababu haujaambiwa kwenye terms of reference?

Shahidi: Mimi ni Askari Polisi, kama ningekuta meseji za kupanga uhalifu ningeweka kwenye report yangu.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba nipewe Kielelezo namba 24,25, 26 na 27

Kibatala: Shahidi Nakuonyesha Kielelezo namba P25

Kibatala: Unakumbuka Siku Unaandika Covering Letter

Shahidi: ilikuwa Tarehe 09 July 2021

Kibatala: Ilikuwa Saa ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Kwa Mujibu Ushahidi Wako Wa awali ulisema Vifaa Vilichukuliwa Tarehe ngapi?

Shahidi: Tarehe 10 July 2021

Kibatala: alikuja Kuchukua nani

Shahidi: Inspector Swila

Kibatala: ulimkabidhi Vipi.?

Shahidi: Alifika pale Nikamkabidhi

Kibatala: Je Uliandika item Moja Moja akasaini au alichukua Zote akaondoka?

Shahidi: Kwenye Kitabu Kuna sehemu anajaza Pale, kina Items Zote.

Kibatala: Wewe Uliandika wakati Unamkabidhi?

Shahidi: Utaratibu Wa Kwetu Lab Namba, Unapoingia Unasaini, Kuna entry Maalum

Kibatala: Hizi Simu Nane, ambazo zilizokuwa na Taarifa Ulipokea Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 13 August 2020

Kibatala: na ulipozipokea kwa Utaratibu wenu wa Forensic Ukaandika Kwenye Hicho Kitabu. Kwenye Kitabu Cha Maabara ulisaini?

Shahidi: Utaratibu Ndivyo Ulivyo

Kibatala: Nani alileta Hizo Simu Maabara

Shahidi: Goodluck

Kibatala: Goodluck alipokabidhi alisaini au Hakusaini?

Shahidi: anatakiwa Kusaini Siku anapokuja Kuchukua

Kibatala: na aliyekuja Kuchukua ni nani

Shahidi: Inspector Swila

Kibatala: Na Kuchukua anakuja Kufuata Mtu yoyote au Aliyekabidhi?

Shahidi: aliyekabidhi

Kibatala: Na bado ulimpatia Inspector Swila Pamoja na Kuletwa na Goodluck?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Register Ya Siku hiyo Ipo wapi?

Shahidi: Ipo Ofisini Maaabara

Kibatala: umemuonyesha Jaji

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Register Ile imeungua au ni Kubwa sana? Ulimwambia?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji report Creation time ilikuwa Muda gani?

Shahidi: Ilikuwa Tarehe 09 July 2020

Kibatala: Wakati Wa Ushahidi Wako Ulisema Kuwa Ulifanya Kazi hadi Saa Ngapi

Shahidi: Sikuulizwa

Kibatala: Kwa kuwa Hukuulizwa Jaji anajua au Hajui?

Shahidi: Hajui

Kibatala: Extraction ikifanyika lini?

Shahidi: Tarehe 07 July 2020

Kibatala: Extraction time ilikuwa Lini

Shahidi: Tarehe 09 July 2020

Kibatala: Kuna Tofauti ya Siku Ngapi

Shahidi: Kama Siku Moja

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Kuna Delay ya Siku Moja na Data ikiwa Secured

Shahidi Sikueleza hilo

Kibatala: Tafuta Item 89 Mahala imeandikwa ICCID, Je ni Kitu gani

Shahidi: ID ya Kwenye Simu

Kibatala ID ya Kwenye Simu au ID ya Sim Card

Shahidi : ID ya sim Card

Kibatala: Je Ipo Katika Riport Yako au Haipo

Shahidi anatafuta.

Kibatala: angalia Ukurasa Wa Pili

Kibatala: Hiyo ICCID Unakubaliana ni ya Zain?

Shahidi: Nimeona Ndiyo

Kibatala: Katika Kielelezo Cha P25 ni Kweli imeishia na F Ndogo?

Shahidi: Ndiyo ipo

Kibatala: angalia na Kielelezo Kinachofuata, Kipo?

Shahidi: Hakipo

Kibatala: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa ICCID ni Namba siyo Herufi?

Shahidi: Sikuulizwa

Kibatala: Kwa mujibu wa ICCID yako hapo, Ni ya Simcard la mtandao gani

Shahidi: Ni ZAIN..

Kibatala: Tangu uanze kutoa ushahidi hakuna sehemu umetaja neno ZAIN

Shahidi: Kimya

Shahidi MTN

Kibatala Unajua NI Mtandao wa Nchi Gani

Shahidi: Sijui

Kibatala: hujui Kwamba ni Mtandao Wa South Africa?

Shahidi: Hapana Sijui

Kibatala: Ulimtajia Mheshimiwa Jaji, kuhusiana na MTN

Shahid! i Hapana Sijamwambia

Kibatala: Je ulitoa ufafanuzi Kuhusu Crossing references namba za Divices Dhidi ya Namba ya Kwenye Simu

Shahidi: Si Kuulizwa Swali

Kibatala: Kama Hukuulizwa ulitoa Ufafanuzi au Hukutoa

Shahidi: Si Kuulizwa Kama Ningeukizwa Ningetoa

Kibatala: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulisema UFEN Version auliyotolea Ushahidi Ilikuwa namba Ngapi

Shahidi: UFED 7:4:4

Kibatala: Soma Ukurasa Wa 26 Chini Kwenye File system One, UFED ngapi

Shahidi: 7:4:0

Kibatala: Ulizungumzia hiyo jana

Shahidi: Ndiyo Nilitaja Jana

Kibatala: Leo Nimekuuliza Ukataja Version Ngapi

Shahidi 7:4:4

Kibatala: na Hizo Version Mbili Ulimfafanulia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Si Kutoa Ufafanuzi

Kibatala Kwakuwa hii Taarifa ni Self Generated, Soma Extraction Process Discription pale Imaposema Kuwa Application...............

Unakumbuka Nilikuuliza hili swali Mwanzo

Shahidi Nakumbuka

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Application ilifanyiwa Kwa Back Up Android

Shahidi: Ndiyo Ilifanyika

Kibatala: Ulitoa Ufafanuzi Kuhusu Down Graded Area ya Version

Shahidi: Hapana Sikutoa Ufafanuzi

Kibatala: Baada ya Kufanyika Down Grading Ilikuweza EFED na Celebrite Physical Analyser, Je ulifafanua Kwa Jaji Kuhusu Storation

Kibatala: Twende Kwenye Plug inns, Contacts and References Je Ulifafanua kuhusu hilo

Shahidi: Hapana Sijaelezea

Kibatala: Nilikuuliza Kuhusu Forensic Cables, Ukasema Inategemea nini

Shahidi: Nilisema Inategemea

Kibatala: Shika Vielelezo Hivi Vinne, Mwambie Mheshimiwa Jaji Ulifanya Kwa Kutumia Device

Shahidi: Cable namba 100, Techno DA2

Kibatala: Nenda Kielelezo na P25 Ulitumia Forensic Cables zipi na Device Ilikuwa Ipi

Shahidi: Hapa Mheshimiwa Hakutaja Cable iliyotumika

Kibatala: ilikuwa Simu gani

Shahidi: Ilikuwa ni simu ya Tecno

Kibatala: Nenda Kwenye Exhibit P26 aina Ya Simu ni Ipi

Shahidi: Tecno V6 na Cable iliyotumika ni Namba 100

Kibatala: Nenda P27 ni simu aina Gani

Shahidi: Nakumbuka Ilikuwa Techno

Kibatala: Aina ya Simu Haitajwi??

Shahidi: Kimya

Kibatala: hapo ambapo aina ya Simu Haitajwi Ulitumia Forensic Cable gani

Shahidi: Haijataja Cable Iliyotumika

Kibatala: Hizo Simu zinafanama au Tofauti

Shahidi: Ni aina Tofauti

Kibatala: Je Ulimfafanulia Mheshimiwa Jaji siala la Utofauti Wa matumzi ya Tofauti ya Cable

Shahidi: Hapana Siku Mfafanulia

Kibatala: aliyeleta Masuala la Forensic Cables hapa Mahakamani

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Ethical Hacking Maana yake ni Udukuzi wa kimaadili.?

Shahidi: Sijui Kiswahili Chake

Kibatala: Nani anasimamia hiyo Ethical Hacking

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Katika Ushahidi wako wote zile simu 8, zinatakiwa Kufanya Extraction zikiwa Off au On

Shahidi: Inategemea Mashine

Kibatala: Unaweza Kufanya Extraction Simu Ikiwa Off?

Shahidi: Ndiyo unaweza

Kibatala: Chini ya Kiapo Kwamba Unaweza Kufanya Extraction simu zikiwa Off

Shahidi: Ndiyo Unaweza

Kibatala: Haya Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Unaweza Kufanya Extraction simu ikiwa Off

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Katika zile simu Nilisikia Unasema Kuwa Matokeo positive, Maana ya Positive ni nini

Shahidi: Pale ambapo Nilichoombwa Hakijapatika ni Negative

Kibatala: Kwa Ushahidi Wako zile simu Nne zilikuwa hazina Mawasiliano

Shahidi: Hapana Zilikuwa hazina Mawasiliano Zinazo wasiliana na Hizi namba

Kibatala: Nenda Kwenye Terms of Reference, Je Terms of reference Inataja Kwamba Ufanye Uchunguzi Kuanzia Tarehe hii Mpaka Tarehe hii

Shahidi: Hapana Sijaandika

Kibatala: Na Mawasiliano Je

Shahidi: Hakuna Muda wa Limit

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji suala la Kutoa Miamala Na Mawasiliano Kutoka Tarehe fulani Mpaka Tarehe fulani

Shahidi: Kwenye Barua ambayo Ilikuwa Kwangu, Hapa Haipo

Kibatala: Kwanini tusiseme wewe ni miongoni mwa kikundi ndani ya Jeshi la polisi ambacho kilihusika na kupanga njama za Kumpa Freeman Mbowe Kesi ya Ugaidi Ndiyo Maana mlifanya uchunguzi kipindi fulani hadi fulani?

Shahidi: Hapana siyo sahihi

Kibatala: Naishia hapo

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Shahidi Umeulizwa Mambo Mengi sasa ni Muda Wa + Kufanya Ufafanuzi

Wakili wa Serikali: Jana Wakati Uliulizwa Swali hapa Ukasema, Siyo Kweli Kwamba tulifanya Extraction Tupo wengi, Hebu Tufafanulie Ulikuwa na Maan Gani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Pia Kuhusiana Na Extraction Data Ukasema Ulikuwa nazo wewe

Shahidi: Kama Nilivyosema Awali, Kwenye Hizo Mashine tunaingia kwa Akaunti na Username

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali, Ukasema Kwenye Analysis, Ukajibu siyo Sahihi Kwenye Analysis

Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Napinga Namna ya Maswali Kwa Mr. Hilla

Jaji: Kwa Maana anatakiwa kuweka swali na Jibu na vipi Kama aliweka Jibu pekee yake?

Kibatala: Bado Nitapinga

Jaji: Nafikiri sheria inasema kinachofafanuliwa ni Jibu

Wakili wa Serikali: Pius Hilla Mheshimiwa Basi tutafanya hivyo

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa na Wakili Msomi Nashon Nkungu Kuhusiana na Analysis, Ulieleza Vitu VITATU ikiwemo , Extraction na Analysis, Maan yake nini.

Shahidi:Report Yako Ita Include Kile ambacho Umekipata tu.. Haito Include Kile ambacho haujakipata

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kwamba Kwakuwa umepata Kozi Kuhusiana Na Terrorism, Wewe Ukasema Unafahamu Kuhusu Terrorism Kwa Perspective Ya Kiuchunguzi, Maana yake nini.

Shahidi: Software Yenyewe Ina Components ambazo Zina Jijaza Zenyenwe Kwa Pamoja

Nashon Nkungu: OBJECTION Mheshimiwa Jaji naomba Kupinga Jibu na Kinachoendelea, System Kwamba Yenyewe Ina Pick hizo Ingridients na Elements

Wakili wa Serikali: Tuache Shahidi ajibu Mheshimiwa Jaji kisha tupime Kama Linaendana na Jibu lake

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa Pia na Wakili Mallya hapa, Mheshimiwa Jaji naomba P1, P23, P28

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa na Malya, Kwenye Riport ya Kingai akamwambia Usome Kwenye IMEI namba

Alikuonyesha Pia simu na pia Kwenye Report yako, Akakuuliza Swali Kuwa IMEI namba zinatofautiana, wewe Ukasema kuna Digits Mbili Zina Miss, Ulikuwa na Maana Gani?

Shahidi: Kwenye hicho KIELELEZO D Kielelezo P31 zina Tally ila Kwa IMEI namba ya Pili Zina Miss namba mbili inaweza kama amesahau namba kadhaa

Kibatala: HAYO SIYO MAJIBU YA Re:Examination

Shahidi: Katika Report yangu Ipo ya Kwanza hii IMEI namba ya Kwanza ya Kingai 353736289120273 ila IMEI ya Pili Kwangu ni tofauti Inasomeka 3537289120273

WS: Je Zipo Namba Ngapi

Shahidi: Namba 15 au 13

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuwa Kuna Uwezekano wa IMEI Namba Kufanana

Shahidi: Hazifanani Sababu ni Unique Identification ya Kifaa Cha Mawasiliano

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Owenership Za Simcard

Shahidi: Taarifa Zote zinazo husika na Usajili au Taarifa Ya Simu Kadi Zinapatikana kwa watoa huduma

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusiana na software ambazo Ulizitumia kufanya Extraction, ukasema zilikuwa developed na microsoft na celebrite

Kibatala: OBJECTION Hakuna swali wala Hapaawzi kuwa na Jibu, sababu Haiwezekani microsoft a' develop software za celebrite

Wakili wa Serikali: Nimeachana na hilo swali

Wakili wa Serikali: Bado nina maswali mengi naomba Niletee maombi tumalizie kesho

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa sasa ni Saa 11, Tunaomba hairisho Mpaka kesho Tarehe 20 Mwezi January

Wakili Peter Kibatala: Hatuna Pingamizi, Ila tunaomba Waje na Shahidi Mwingine, Ili tulimalizane na Shahidi huyu tuingie Kwa Mwingine

Jaji: Je kuna shida Katika Kumpata Shahidi Kesho?, Siamini Mtatumia Utaratibu wa Utetezi wa Kuuliza Maswali Siku Nzima

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tutajitahidi, Kulingana na Muda Wenyewe Huu

Jaji anaandika Kidogo.

Jaji: Shauri linahailishwa hadi Kesho 20.1.2022, Shahidi ataendelea Kutoa ushahidi wake

Upande wa Jamhuri naelekezwa kuja na shahidi mwingine

Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho asubuhi saa 3 kamili

Jaji anatoka
 
... Shukran Mkuu. Najua shughuli ya leo sio ya kitoto; Adv. Mallya jana aliomba kesi iahirishwe kwa hoja kwamba "ana maswali mengi" kwa shahidi. Bado kamanda wa kikosi cha utetezi Adv.

Kibatala na wengie wa upande wa haki nao hawajashusha nondo zao; jana waliieleza mahakama wangehitaji hadi saa 7 kum-cross-examine shahidi. Usiache yodi wala nukta tafadhali.
 
Wakuu,

Nimepita hapo mawasliano kwenye mahakama ya uhujumu uchumi,nami nina ndugu yangu ana kesi hapo,ila nimeshuhudia hali ya tofauti kidogo.nimeona askari magereza wengi sana wamemzingira mheshimiwa mbowe pale ndani mahakamani,awali nilidhani labda mheshimiwa anaumwa ila nilivyomcheck vizuri ninemuona yuko fit tu.sasa sijaelewa lengo la hao askari ni nin mpaka sasa.

Kuna anaejua kinachoendelea hapo ndani?
 
Wakuu
Nimepita hapo mawasliano kwenye mahakama ya uhujumu uchumi,nami nina ndugu yangu ana kesi hapo,ila nimeshuhudia hali ya tofauti kidogo.nimeona askari magereza wengi sana wamemzingira mheshimiwa mbowe pale ndani mahakamani,awali nilidhani labda mheshimiwa anaumwa ila nilivyomcheck vizuri ninemuona yuko fit tu.sasa sijaelewa lengo la hao askari ni nin mpaka sasa.
Kuna anaejua kinachoendelea hapo ndani?
Vita vya kisaikolojia tu.
 
Wakuu
Nimepita hapo mawasliano kwenye mahakama ya uhujumu uchumi,nami nina ndugu yangu ana kesi hapo,ila nimeshuhudia hali ya tofauti kidogo.nimeona askari magereza wengi sana wamemzingira mheshimiwa mbowe pale ndani mahakamani,awali nilidhani labda mheshimiwa anaumwa ila nilivyomcheck vizuri ninemuona yuko fit tu.sasa sijaelewa lengo la hao askari ni nin mpaka sasa.
Kuna anaejua kinachoendelea hapo ndani?
Wanamfurahisha Hangaya
 
Wakuu
Nimepita hapo mawasliano kwenye mahakama ya uhujumu uchumi,nami nina ndugu yangu ana kesi hapo,ila nimeshuhudia hali ya tofauti kidogo.nimeona askari magereza wengi sana wamemzingira mheshimiwa mbowe pale ndani mahakamani,awali nilidhani labda mheshimiwa anaumwa ila nilivyomcheck vizuri ninemuona yuko fit tu.sasa sijaelewa lengo la hao askari ni nin mpaka sasa.
Kuna anaejua kinachoendelea hapo ndani?
... ana pingu?
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 10/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
=======
Mh Replica Mungu akupe nguvu utupe uhondo siku ya Leo. Tukiamini Mwenyezi Mungu wa Mbinguni yuko na wanawe Akina Mbowe na wenzake. Na Hakika Hatawaacha kamwe.
 
... Shukran Mkuu. Najua shughuli ya leo sio ya kitoto; Adv. Mallya jana aliomba kesi iahirishwe kwa hoja kwamba "ana maswali mengi" kwa shahidi. Bado kamanda wa kikosi cha utetezi Adv. Kibatala na wengie wa upande wa haki nao hawajashusha nondo zao; jana waliieleza mahakama wangehitaji hadi saa 7 kum-cross-examine shahidi. Usiache yodi wala nukta tafadhali.
Naona kwa Mallya tu anaruka viunzi, bado hajakutana na Kibatala, huyu jamaa hii match ya leo kazi anayo
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 10/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
Duuh siku ya leo imeanza kwa gia kubwa sana...
Tutarajie maajabu! Shahidi na mawakili wake wanayokazi
 
Back
Top Bottom