Elections 2010 Kituo feki cha kura chagundulika Shinyanga

Kweli siyo masihara NEC imeamua kuchakachua uchaguzi hata hapa dar kata ya Tabata hilo limetokea kunakituo kimehamishwa kutoka kituo halisi cha awali zahanati hapo karibu na Tabata Shule na kupelekwa Umoja Road na kupewa jina la Tushikamane lengo likiwa nikuwahangaisha wapiga kura hatimae mwisho wasiku wasipige kura wito naomba wananchi kwa maeneo yao husika wafanye uhakiki wakina kubaini mapungufu yote.
 
Jamani chama tawala na Nec kwa nini wanataka kutuchagulia mtu ambaye sie.waache watu wafanye maamuzi sahihi.
 
Jamani Acheni masihara. Watu walio karibu na tukio wachukue ushahidi wa kutosha, kama ni ukweli vyama vya upinzani washinikize Uchaguzi uhairishwe ili chombo cha NEC kiwe dissolved na mchakato uanze upya. Coz huu ni undumi wa kuwili hatuwezi kuendele kufanya mambo kienyeji hivi.
 
SHINYANGA, 28 OKTOBA, 2010*

WAKATI mchakato mzima wa zoezi *la upigaji kura likifika ukingoni imebainika kuna vituo hewa vya kupigia kura vilivyoandaliwa katika Jimbo la Shinyanga mjini.

*

Hali hiyo isiyokuwa ya kawaida imewafadhaisha wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani kutokana na kutumika kwa baadhi ya majina ya wapiga kura wa vituo vingine kwenye vituo hivyo hewa.

*

Kutokana na kubainika kwa mapungufu hayo yenye kila sura ya kuvuruga au kuiba kura katika zoezi la uchaguzi wa Oktoba 31, baadaye wiki hii Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Shinyanga kimemwandikia barua msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika jimbo la Shinyanga.

*

Kituo kimoja kati ya vitu vilivyothibitishwa na waandishi wa habari kubeba mapungufu hayo ni kile cha namba 00018940 cha Chekechea Misheni ambapo wapiga kura walioorodheshwa katika daftari la kupigia kura kwenye kituo namba tatu majina 264 yamerudiwa kuandikwa pia katika kituo namba mbili jambo ambalo limewashangaza wengi na kuweka dhana ya kuwepo kwa vituo hewa katika orodha ya Tume ya Taif ya Uchaguzi (NEC).

*

Baadhi ya majina yaliyobainika kuandikwa mara mbili katika vituo tofauti ni yale yanayoanzia na herufi MW mpaka ZU katika kituo namba tatu kikiwa na wapiga kura 334 na yale yanayoanzia herufi KE mpaka ZU katika kituo namba mbili chenye idadi ya wapiga kura 494.

*

Baadhi ya majina yaliyobinika kubeba udanganyifu huu ni pamoja na Bi. Veronica Paulo Nyanda mwenye shahada namba 11037634, Bi. Veronica Michael Shigulu (11061105), Bi. Veronica Philipo Alphonce (46588250) na Bi. Veronica Philipo Massawe (11042211) yakiwa yameandikwa kituo namba mbili na pia kuonekana kama yalivyo katika kituo namba tatu.

*

Wakati huohuo Katibu wa CHADEMA mkoani Shinyanga, Bw. Nyangaki Shilungushela akizungumzia hali hiyo alisema kitendo hicho kimewapa wasiwasi kuwa kuna mpango muovu wa kuchakachua kura au kuongeza idadi ya kura hewa mara baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika kwa kutumia namba na idadi ya wapiga kura vituoni ambao majina yao yameandikishwa mara mbili.

*

Alisema tayari wamekwisha kumwandikia msimamizi wa uchaguzi kulalamikia kitendo hiki kinachoonesha kuna vituo hewa vilivyoandaliwa.

*

“Hali hii imejitokeza hapa mjini je, huko vijijini hali ikoje ambako wananchi wengi si wafuatiliaji wa mambo?” alihoji Shilungushela.

*

Kwa upande wake msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika Jimbo la Shinyanga mjini, Bw. Festo Kang’ombe amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kueleza kuwa tayari ofisi yake imeishawasiliana na NEC ambao wanashughulikia tatizo hilo kabla ya siku ya upigaji kura.

*

Alisema baada ya kubaini mapungufu hayo hawakuwa na jinsi ya kufanya bali kubandika majina hayo vituoni kama yalivyo ili kuwatendea haki watu wengine ambao majina yao hayakuwa na matatizo ya kujirudia kweenye orodha.

*

“Ni kweli tatizo hilo lipo hata sisi tulilibaini mapema, lakini tayari tumeishawasiliana na Tume ya uchaguzi ambao ndiyo wenye dhamana na daftari hilo la wapiga kura, hivi sasa wanalifanyia kazi, na marekebisho yatafanyika kabla ya siku ya upigaji kura, lakini hata siku hiyo patakuwepo na watu maalum wa kutoa maelekezo,” alieleza Bw. Kang’ombe.

*

Kama itashindwa kufanyiwa marekebisho, ambayo hakuna shaka kuwa yatahitajika baada ya kuchunguza pia vituo vyote vya kupigia kura nchini, hii itakuwa kashfa ya aina yake kwa NEC ambayo itaondoa imani ya wananchi na hata Mataifa kwa NEC.Mwisho
 
Ili kuweka Pressure ya kweli kwa NEC saa hizi ni vema kuwahabarisha watazamaji wa kimataifa ili nao waulizie huko NEC.

Naona mwaka huu mbinu za wizi za CCM na NEC za miaka yote zinafunuliwa. Tumshukuru Mungu.
 
Hamna haja ya kulifanyia kazi, hiyo tume iwe dissolved kwisha kazi. Huu ni uzembe na uchakachuaji wa hali ya juu, wanachezea maisha ya watanzania and at this time we dont need these kind of people. We only have 2 days left watarekebisha vituo vingapi. Hao watu waachie ngazi huu mchakato uanze upya.
 
Jamani watu wa vyama visivyo vya kiserikali, haki za binadamu na vyama vya upinzani tunaomba ushirikiano wenu wa kuufichua huu uhuni wa nec na chama tawala. Hakikisheni waangalizi wa kimataifa wanajulishwa na kuonyeshwa hii mikakati miovu ya kupora haki ya raia kujichagulia viongozi wao. Msilale jamani kwani sasa umefika wakati muafaka wa haja ya kuwa nanyi ndani ya taifa letu. Na Mungu awatangulie na kuwapa ujasiri wa kufuatilia.
 
NEC wapumzike, let smart peole do the job!! wazalendo, wapenda haki na wenye uchungu na nchi yetu wafanye kazi. NEC ondokeni hapo hakuna mnalofanya ni utata mtupu, mtamwaga damu bure kwa vijisenti vya ccm.
 
Asante sana kwa kuleta hii evidence hapa, ndo niliyokua naisema jana, sasa naona kila mtu ameamini taarifa hii kinachofuata ni hatua, naombeni mwongozo
 
Unajua ikiwa wewe wa kushindwa wakushindwa tu, jiandaeni kusikia mengi ila tu niambie WATANZANIA MUngu yuko nyuma yetu katika kuwatoa hawa mafisadi
 
Unajua ikiwa wewe wa kushindwa wakushindwa tu, jiandaeni kusikia mengi ila tu niambie WATANZANIA MUngu yuko nyuma yetu katika kuwatoa hawa mafisadi

Mie ningetaka Mungu awe mbele yetu, yaani tumfuate na sio atufuate. Au sio?

Kwa wale wenye uwezo wa kumwachia Mungu (DETACHMENT) WAFANYE HIVYO. He never disappoints.

Wengine wafanyeje? Wakubali kuhujumiwa demokrasia na mafisadi? CCM iwe macho. Wananchi wengi wakiona wamehujumiwa wanaweza kwenda wenyewe kuwatoa mkuku huko Magogoni. Hata Abdulrahaman Shimbo hatawaweza.
 
Mie ningetaka Mungu awe mbele yetu, yaani tumfuate na sio atufuate. Au sio?

Kwa wale wenye uwezo wa kumwachia Mungu (DETACHMENT) WAFANYE HIVYO. He never disappoints.
.
Mi naona ni heri awe juu yetu, awe nasi sio mbele wala nyuma!!!! You can fool some ppl sometime but you can not fool all people all the time!!!!
 
Kura zimeshaibiwa, Kikwete 80% inawezekana!

CCM tayari wameshajihakikishia ushindi kwa vile tayari wameshakamilisha kazi yao. Katika uchaguzi wamekuwa wakitimiza ratiba tu lakini matokeo ya uchaguzi yanatambulika na mpango kamili wa kukamilisha matokeo hayo ni huu.

A). Upangaji wa vituo
NEC imekuwa ikiendesha zoezi la upangaji wa vituo chini ya uangalizi maalum wa watalaam wa IT (kama ambavyo imekwsiha kuelezwa na baadhi ya wadau hapa JF, ambao ni wa 16 na MBWA MKALI katika Post zilizopita).

i).Utaratibu wa awali ulikuwa ni kuandaa vituo halali ambavyo viliandaliwa na kukamilika.
ii). Utaratibu wa pili ulikuwa ni kuandaa vituo hewa ambavyo viliandaliwa baada ya vituo vya kwanza kukamilika (Hii ni kwa lengo la kutambua vituo awali na kutofautisha vile vya kuchahachulia).

Vituo Hewa:
Jambo hili limekuwa likiwatatiza wengi sana na wengine kushindwa kuamini iwapo jambo hili linawezekana. Ukweli linawezekana na hapa natoa mmoja ya kituo hewa.
· Hapa kwa mujibu wa tume vituo vimepangiliwa kwa majina/namba.
· Kituo ambacho nawatolea mfano hai ni Na. 00020941. Ama kwa jina kinaitwa Kituo cha Shule ya Msingi Kapangaja. Kipo katika Kata ya Bugongwa wilaya ya Ilemela na jimbo la Ilemela.
-Eneo hili la shule ya msingi limegawanywa na kuzaa jumla ya vituo 5.
-Tatizo lipo katika vituo viwili ambavyo ni kituo namba 4 na namba 5.
· Kituo Na. 4: Orodha ya majina ya wapiga kura imebandikwa ikiwa na kurasa 21. Kurasa hii inajumla ya wapiga kura 490. Kwa mujibu wa rekodi za Computer kituo hiki (kwa maana ya orodha yake) kilichapishwa Septemba 16, 2010.
-Ukiangalia kwa makini utakuna majina yake ambayo yamebainishwa kuwa ndiyo ya wapiga kura katika kituo hicho yanajirudia katika kituo namba 5.
-Tofauti iliyopo ni kuwa katika orodha hiyo ya namba 5 majina huku yamepunguzwa toka 490 na kuwa 402 hivyo kuwa na kurasa za majina 17 toffauti na 21 za kituo namba 4.
-Lakini orodha ya majina ya wapiga kura hiyo inaonyesha kuwa imechapishwa katika Computer Oktoba 16, 2010. (Maana yake ni kuwa hiki kimezalishwa baada ya kuwa vituo vyote vine vimekamilika hiyo Septemba 16, 2010). Hivyo ni kipya.

B). Upigaji Kura.
Kwa vile zoezi la upangaji kura limekamilika, kazi imebaki katika kupiga. Ukweli tukubali kura kwa sasa haziibiwi kwa kupiga, ingawa njia hii pia imeandaliwa kama njia ya dharula, lakini ni kwamba kura zitapigwa hivi.
· Kwa vile orodha ya majina iliyoonekana katika kituo namba 4, ndiyo yaliyojirudia kituo namba 5, basi watu hao (ambao ni wana CCM damu ama Polisi au JWT kama watakavyokuwa wameandaliwa) watajihimu kupiga kura na kukamilisha taratibu zote kituo namba 4.
· Kwa vile kila unapopiga kura kidole huwekwa wino maalum kama alama ya kumtambua aliyekwisha piga, basi wakitoka hapo watakwenda kufuta wino huo na kasha kubadili nguo zao na muda wa kurudi kituoni tena kwa ajili ya kupiga kura nyingine. Kura hii itakuwa kura ya pili kwa mtu mmoja kwa idadi ya watu 402 kituo namba 5 kati ya watu 490 wa idadi ya kituo namba 4.
· Watu hao watakuwa wakitumia shahada zao zile zile na kwa kuwa majina yao yamo katika daftari la kudumu la wapiga kura, na wino katika vidole vyao umefutwa kitaalam, basi watapiga kura bila ya wakala kulipwa hela kumshinikiza akubali au kumzuia kwa vile anachoangalia yeye ni shahada na kama imo katika daftari vitu ambavyo ni kweli vipo.
· Kwa vile wakali aliyewaona wakipiga kura katika kituo namba 4 hatotoka kuingia katika kituo namba 5, basi mamluki hao hawatabainika na hivyo watakuwa wamepiga bao la kisigino.
C). Kujumuisha matokeo.
Uchaguzi ukiisha kazi ya kujumuisha matokeo itakuwa imekwisha kwani wakifanikiwa hapo hawatakuwa na haja ya kuongeza kura nyingine juu yake kwani jambo hili litaleta utata na kuwafanya wabainike kama ambavyo ilitokea Kenya kwa kula kuzidi kutokana na ujumuishaji wake.
Hivyo Kikwete atashinda kwa 80% na CCM wataingia mtaani kushangilia wakati Chadema wakilia na kusaga meno na hapo uchaguzi utakuwa umeisha.

NJIA NYINGINE ZA WIZI ZINAZOTANGAZWA:
Kwa hakika mpaka sasa njia zote hizo zinatangazwa sitaki kuzipuuza kwa vile zote zinaweza kutumika lakini nyingi ambazo zimejulikana sasa zimetangazwa kwa makusudi kwa ajili ya kuwazubaisha wakazanie kuangalia huko huku wakitoa akili zao katika katika njii hii ambayo ilikomboa Jimbo la Busanda na Biharamulo.
 
Hii ni kali zaidi lakini kama tulivyosema sisi tuendeleee kuomba na kuendelea kuziba mianya inayojulikana.Tunaamini Mungu yuko upande wetu na tayari ametuonyesha mengi sana.TUMTUMAINIE MUNGU TUTASHINDA TU
 
Back
Top Bottom