Kituko kingine cha Pinda

Lowasa alikuwa ni simba anayeongoza kundi la kondoo, ilhali pinda ni kondoo anayeongoza kundi la simba
kweli nchi inapitia kwenye hali ngumu saaana, pinda si mtoto wa mkulima bali ni mtoto wa mafisadi, pm muoga ka kunguru analialia tuuuuu, jamani tuikomboe hii nchi otherwise tutaangamia milele.
 
Usikurupuke kuhukumu ndg, ukisoma majukumu ya CAG ni pamoja na kuishauri serikali kwenye mambo ya fedha, PM kumwomba CAG ni sawa kabisa make yeye si mtaalam wa mambo hayo. Ndiyo kazi ya kuwa na watu kama CAG, akisema tubadili sheria au tuongeze adhabu serikali inatakiwa ifanyie kazi ushauri. PM hawezi jua kila kitu.

Hivi, kwani hakuna sheria? Kama CAG anajua kuwa kutoa ushauri kuhusu nini cha kufanya na wafujaji angeweka hiyo ndani ya ripoti yake. Kama haipo itakuwa ni kwa sababu anajua kuwa serikali inajua nini cha kufanya. Hivi kweli huyu Pinda, kichwa yake imepinda kiasi ambacho hajui afanye nini na wafujaji wa pesa za wananchi? Mbona aliwahi kuwasimamisha kazi wafujaji fulani Bagamoyo? Je, alitumia sheria gani? alipata ushauri toka kwa nani? Mizengwe kanzi Pinda aache kufikiri watz ni wajinga?
 
Something is very wrong in Pinda's head (bent mind)! Hivi kama mhasibu wangu in my private company, ananisababishia hasara ya 2m na internal auditors wanaconfm mhasibu aliziiba kwa kufoji risiti, je sitamsimamisha kazi mara moja na kutoa taarifa polisi? Shame on you, bogus PM!
 
Jamani mbona tunachekesha - viongozi wetu sasa wametuloga hatuoni hata yale ya wazi - Je, serikali inahitaji ushauri wa CAG juu ya wezi?
Mwanzo nilijua mwizi ni mahakamani haraka na sheria kuchukua mkondo wake. Niliamini hivi mpaka nilipopata style mpya ya EPA kuwa mkiwa mwizi mheshimiwa unaombwa kurudisha na yanaisha.

Ukweli ni kuwa 'Hatuna anayetaka kuwajibika'
 
Kwani hukumjua kwamba ni crying baby?
...Si ndio huyu aliyedai kuwa walioiba fedha za EPA kule BoT ni watu wa kuwaogopa maana ni hatari kwa hiyo kuwafatilia si jambo rahisi!!?? naona naye ni ziro fulani tu hana lolote!
 
Viongozi wa serikali wanazungumza tu kama vile wao hawajui ni nini kinaendelea hapa nchini.
 
Back
Top Bottom