Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,071
- Thread starter
- #21
Nimeona Kitine amemfagilia sana Gideon Cheyo, John Chiligati na Anna Tbaijuka kuwa ni viongozi wasafi. Mzee naona hana cha ku loose. Yaani kamchana Membe ki aina, yaani JK amesahau kutoa kasa lingine kwenye system.
Wazee wamesisitiza kuwa vetting ni muhimu sana katika uteuzi wa nafasi kama hizo za kisiasa na utendaji serikalini hasa kwa kuzingatia rekodi ya mtu katika uadilifu.
Wameoneshwa kutatizwa sana na namna ambavyo viongozi wa sasa wanafanya kazi katika mazingira ambayo wana confilct of interest za wazi sana katika kila wanachofanya. Kibaya zaidi ni pale wanaposhindwa kumudu kuepuka mgongano huo wa maslahi binafsi, hivyo wanaweka mbele maslahi yao na kuacha ya watu wanaotakiwa kuwatumikia. Uongozi/utumishi wa umma imekuwa ni nafasi ya watu kuchuma na kujitajirisha wao, huku wananchi wakiangamia.