Kikwete: Hakuna wa kumshinda Rais Samia 2025 iwe CCM au Upinzani, yule aliyesema kuna Waziri anatafuta Fedha za Urais nje ni muongo na mpuuzi mkubwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,145
Rais mstaafu Mzee Kikwete amesema Chama kisiwavumilie wazushi na waongo wanaokigawa chama.

Kikwete amesema kuelekea 2025 uzushi na Uwongo utakuwa mwingi lakini hakuna wa kumshinda Rais Samia iwe ndani ya CCM au Upinzani.

Kikwete amesema hata ile taarifa ya Waziri kwenda kutafuta Fedha nje ili agombee Urais wa JMT ni za Uwongo na aliyesema akome na ikiwezekana aitwe na chama kuhojiwa.

Kikwete amesema mzushi huyo anafanya na yule Mwanahabari Huru aliyekivuruga sana Chama kwa uzushi.

Chanzo: TBC
 
Mama achuje mchele na chuya sasa. Ataamua mwenyewe amuamini Bushman ama Borntown.

Ila akae akijua ni vigumu sana kwa mtu mdogo kudanganya hadharani vile.

Na kwa namna Borntown alivyoweweseka inaonesha ni wazi yeye alikuwa behind the scene kuucheza mchezo mzima wa huyo waziri kusaka pesa huko nje za nchi.

Kwa sababu kama kweli hahusiki basi siamini kama hajui kwamba kwenye siasa hata tetesi zinapaswa kuchukuliwa kwa uzito wake.

Sasa kitendo cha yeye kubwabwaja hivi ina maana "He Knew".
 
Rais mstaafu Mzee Kikwete amesema Chama kisiwavumilie wazushi na waongo wanaokigawa chama.

Kikwete amesema kuelekea 2025 uzushi na Uwongo utakuwa mwingi lakini hakuna wa kumshinda Rais Samia iwe ndani ya CCM au Upinzani.

Kikwete amesema hata ile taarifa ya Waziri kwenda kutafuta Fedha nje ili agombee Urais wa JMT ni za Uwongo na a
Kikwete anaintelijensia gani ya kujua nani anahusika na nani hausiki na hiyo intelijensia yake ni kwa mawaziri wote?

Nasisi huwa tunasikia chala ni kitengo kule kagera, kigoma na sasa mtwara huwa hawaendi raia.
 
Kwa hiyo kauli ya JK kimsingi nae ni chawa wa Samia pia, hana tofauti yoyote na Chalamila, kwani Chalamila alisema vile kwa lengo la kumpigia debe Samia, na leo JK anampinga Chalamila wakati kimsingi nae anampigia debe Samia, hawa hawachekani.

Huu uchawa naona upo kwenye DNA huko CCM, Samia ni nani hata asipingwe?! ikiwa kuna mjumbe mmoja ambaye hakumpigia kura ya NEC, hii maana yake sio kila mtu mwenye mawazo kama ya wengine.

Mbaya zaidi hata hawa wazee nao wanapokuwa na mawazo ya sampuli hii ndio wanakidumaza chama kabisa, kwa haya mawazo ya kina JK na Mzee Makamba wanaonesha vile hawatakiwi kushirikishwa kwenye hivyo vikao, hawana tena mawazo mapya.

Inashangaza zaidi JK anapojigeuza mahakama ya kumhukumu Chalamila, kusema hakuna aliyekwenda nje bila kumsikiliza Chalamila, huyu nae amelewa mvinyo wa madaraka kama aliolewa Mzee Makamba, siku hizi wao ni kuropoka tu.
 
 
Hawa wazee wanadhani watoto watukutu wa enzi hizi ni wale wa enzi zao wa kukanywa ba kuacha.

Watukutu wa enzi hizi, ukireact ndio wanakuwa wakali zaidi.

Wanajua kumbe imemuuma basi kanyagia hapo hapo.
😀😀😀😀😀😀😀.

Nadhani pia wameata matokeo ambayo hawakutegemea.
 
Back
Top Bottom