Kitine: Kuna waziri ameiba fedha za nchi huko nje ametia mfukoni mwake kutafutia urais

Huyu Hassy Kitine alivyotuhumiwa kutapeli dola elfu 60 za kimarekani kwa matibabu hewa ya mke wake enzi zile za 2004-2005, jee anafikiri watu tumeshasahau hadi kujifanya kiranja wa kukemea ufisadi wa CCM kwa vile labda waliokuja baada yake wamemzidi kwa ujanja na kiasi cha pesa walichofaidika kupitia utapeli na ufisadi wa Serikali ya CCM? Jee, zile dola elfu 60 alizolipwa kwa minaajili ya mkewe kutibiwa "maumivu ya kichwa" kwenye clinic feki Marekani, alizirudisha Hazina?
Kitine paid the price for the mistakes of his wife. He has the moral authority to speak of corrupt practices.

In Christianity Saul was a beast killer of anyone who professed to follow Jesus. Until one day a light shone on him on the way to Damascus. Today, Saul, who became Paul is a saint in the Christian religion.

Kitine made a mistake, paid for it but that does not mean that he cannot be a soldier in this battle against corruption. Let him speak. Kama zile dola elfu sitini ndizo zinazokuumiza, alizirudisha hazina.

Next question?
 
Wazee wawili wastaafu wa nchi hii wako Channel Ten kwenye kipindi cha Je Tutafika. Nafikiri leo ndiyo siku yake (kama si marudio). Ni Dkt. Hansy Kitine na Dkt. Kiwanuka
Huyo jamaa kwenye RED nae kilaza pia....tulimpa ubunge makete kachezea
 
Kama Membe amekwapua asemwe ingawa akisemwa kwa mafumbo ujumbe haufiki vizuri. Kimsingi, hakuna waziri safi chini ya utawala wa CCM. Hili lilijitokeza pale wabunge walipopaswa kusaini karatasi ya kutokuwa na imani na Pinda. Ni Filikunjombe pekee aliyeonyesha kuwa safi ingawa kuna fisadi mmoja Mkono alisaini kutokana na ima kunyimwa fursa kama mwanzo au kutafuta kuungwa mkono na kufikiriwa tofauti na alivyo.
 
Nimeona Kitine amemfagilia sana Gideon Cheyo, John Chiligati na Anna Tbaijuka kuwa ni viongozi wasafi. Mzee naona hana cha ku loose. Yaani kamchana Membe ki aina, yaani JK amesahau kutoa kasa lingine kwenye system.

Huyu mzee naona anapiga porojo tu na kutaka tu kulipiza visasi kwa Membe kumtoa kwenye uwaziri kipindi chake. Gideon Cheyo wakati akiwa waziri wa ardhi, wizara ile ilikuwa imeoza mpaka Magufuli alipoenda pale akanyosha mambo. Hizo pesa ambazo Membe alipewa huko Comoro, Morocco na Libya ziliingizwa kwenye akaunti yake binafsi au? Hamna cha maana hapa.
 
Uthibitisho wa picha litakuwa jambo muhimu sana ikiwezekana na vibali/vyeti vya umiliki kama vitapatikana kwa usahihi zaidi. Wadau nawasilisha.

Picha kila mtu anaweza kupiga ama aka google na kuweka. Hapa inatakiwa kama issue ya Ngeleja na Maige, docs za kuthibitisha kwamba mmiliki ni nani. Ama data na melezo yaliyoshiba. Otherwise hakuna haraka hapa, ukweli kama upo utajulikana tu, hata mtu ajifiche wapi, lakini tusitoe nafasi ya watu kuanza kuchomeka ajenda zao na kuharibu hadhi na heshima ya JF ya kuwa wakweli. Kuna mtu humu aliweka mambo ya Nundu, wakaja watu wakasema katumwa na Naibu wake, jamaa akasema kama wote ni wezi hakuna wa kuachwa na kweli, hakuna aliyebakia wamezolewa na mafuriko ya ZZK70.... na Invisible akamwaga hapa ya Ngeleja na Maige naye zikamwagwa data za uhakika..... mambo yakawa... hii ndio heshima ya JF si maneno matupu.

Mfano hii hoteli tutasema ni ya nani?

pool-area.jpg
 
Kitine paid the price for the mistakes of his wife. He has the moral authority to speak of corrupt practices. In Christianity Saul was a beast killer of anyone who professed to follow Jesus. Until one day a light shone on him on the way to Damascus. Today, Saul, who became Paul is a saint in the Christian religion. Kitine made a mistake, paid for it but that does not mean that he cannot be a soldier in this battle against corruption. Let him speak. Kama zile dola elfu sitini ndizo zinazokuumiza, alizirudisha hazina. Next question?
What we know is that Hassy Kitine, through his wife, willingfully embezzled $60,000 through false pretences, from the Government of Tanzania. What we don't know is how this Criminal and Common Thief so to speak, came to avoid legal consequences of his criminal activities through allegedly making up for crimes by merely "paying back" whatever he stole from the People of Tanzania, and thus by doing so, avoiding any legal consequences and/or punishment according to relevant Laws of the Republic. In other words, there's absolutely no evidence to back up your claims to the contrary.
 
Yale ya Kitine tayari yalishathibitika kwamba ni kweli kwavile hata ushahidi ulitolewa! Hili la Membe, time will tell. Lakini kama asemayo Kitine ni sahihi basi ni sahihi vile vile ku-conclude kwamba Membe na Dr. Kitine hawana tofauti!!
Hili nalo neno, lakini:
Kitine aligunduliwa wizi wake na kulazimika kujiuzulu au kufukuzwa, Membe je, yupo wa kufichua madudu yake? Na kama yakifichuliwa, atajiuzulu/atafukuzwa?
 
What we know is that Hassy kitine, through his wife, willingfully embezzled $60,000 through false pretences from the Government of Tanzania. What we don't know is how this criminal and common thief came to avoid legal consequences of his criminal activities through allegedly making up for crimes by merely "paying back" whatever he stole from the People of Tanzania. In other words, there's absolutely no evidence to back up your claims to the contrary.
OneManArmy,
Believe me I know more about this saga than anybody else in this forum. The word willingfully would not come into play if you knew the whole episode. If Kitine is a thief, he is a repented thief who has paid the price by losing his ministerial position and paying back the money. You cannot say the same of the same fisadis we are talking about in Tanzania today. Unless you have a personal beef with Kitine calling him a criminal and common thief does not do him justice.
 
Ziara ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama nchini Moroco inaanza kuonyesha matunda yake, Big Up Mzee Mvi... Soon tutaambiwa Nyerere si MALAIKA alikosea na wenzake kina Mandela kuitambua Polisario na soon Kamati ya Mvi itaishinikiza Serikali na waziri wa Nje kukubaliana na Moroco kuichukua Polisario, na serikali kwa kuwa sasa imekua haina meno imeelemewa itanywea na mambo yatakua bwerereee!! Na lile dau walilovuna siku mbili zilizopita litakuwa limefanya kazi.. Najua watu hawataelewa lakini soon watapata Poicha... Hiki ni kizunguzungu na jana ndio wakubwa walitua Dar na leo mambo yanaanza!!

picha%2Bnamba%2B3%2B.jpg
picha%2Bnamba%2B2.JPG
 
The said Hotel building is owned by one Shabby....... kama kuna mtu anaweza kutusaidia kuunganisha dots atuwekee, lakini Membe aliwahi kumwambia mtu "huo ujinga wanaoueneza nawasubiri watoke hadharani niwashitaki... hiyo ni hotel ya Shabby, na kuwapo kwake kusini haimaanishi ni ya viongozi wa kusini"........
 
OneManArmy,
Believe me I know more about this saga than anybody else in this forum. The word willingfully would not come into play if you knew the whole episode. If Kitine is a thief, he is a repented thief who has paid the price by losing his ministerial position and paying back the money. You cannot say the same of the same fisadis we are talking about in Tanzania today. Unless you have a personal beef with Kitine calling him a criminal and common thief does not do him justice.

Mkuu Jasusi, mind telling us what you know? It surely won't hurt anyone by doing so, plus it would go a great length in exonerating Hassy Kitine from the the kind of pending allegations he's still facing.
 
Kibanga Ampiga MKoloni,

Ziara ya Morocco wamerejea jana wazee hawa na leo Kitine kaibuka na fedha za Moroco za Polisario!!! duh!! Tusubiri tuone Kamati ya Bunge iliyorejea ikija na azimio la kutaka Tanzania ibadili msimamo na kuitosa Polisario. Tanzania na Polisario, PLO etc si maamuzi ya leo ama jana.... wanaojua historia watuambie

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anzania-haijavunja-uhusiano-na-gadaffi-4.html
Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.

Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).

Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.

Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?

Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?
By Mzee Mwanakjiji
 
Haswa nafikiri anamzungumzia Membe. Watu wa mambo ya nje mliopo humu tuleteeni data hapa JF.

Yupo morocco tokea Jana na kaja baada ya kuona kamati ya mambo ya nje iko morocco,but bahati mbaya kamati imeshajua mpaka pesa alizokula Morroco kwa miaka minne.Nasikia anakula na mkuu WA Kaya pasu kwa pasu...kweli nchi hii inaliwa na wenye Meno na kujengwa na wenye Moyo.
 
Yupo morocco tokea Jana na kaja baada ya kuona kamati ya mambo ya nje iko morocco,but bahati mbaya kamati imeshajua mpaka pesa alizokula Morroco kwa miaka minne.Nasikia anakula na mkuu WA Kaya pasu kwa pasu...kweli nchi hii inaliwa na wenye Meno na kujengwa na wenye Moyo.

Hahaaaaa!!! Thats nice>>>>>> Tupe picha kama hizo hapo juu!!!!
 
Asante kwa maelezo mazuri. Lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa then Kitine hakuwa waziri full. Alikuwa Naibu Waziri (I stand 2 b corrected). Je tuhuma hizo zilitosha kuondoa moral authority yake kuzungumzia masuala ya kuijenga nchi kwa kuweka sawa uongozi huu. Ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa kiongozi wa sekta nyeti na muhimu (tena wakati huo kumbuka ilivyokuwa nyeti kweli).

Lakini suala muhimu hapa, kwa hiyo ni sawa kusema kuwa Membe (kama ni yeye aliyemaanishwa katika kauli hiyo) na Kitine hawana tofauti. Maana ukiziweka vyema sentesi zako katika inferences unapata conclusion hiyo kuwa Membe (kama ni yeye waziri mhusika) na Kitine hawana tofauti, hivyo unakubali kuwa waziri aliyezungumzwa kweli siyo mwadilifu eeh?

Mkuu Tumaini Makene,

Tuweke kumbukumbu sawa: Hapo kwenye RED, Dr. Kitine alikuwa ni full Minister. Ofisi ya Rais - Utawala Bora huwa hakuna Naibu.
 
Last edited by a moderator:
Hahaaaaa!!! Thats nice>>>>>> Tupe picha kama hizo hapo juu!!!!
Picha ngumu kupata sababu ana deal na mtu ambaye alideal na kamati,na akamwambia huyo mtu akikutana na kamati asiseme Kama Yuko morocco,kamati iko marakesh na kesho inaondoka kurudi dar.Yeye anahamia casablancaaaa! Atahangaika but he is responsible to the kamati,nasubiri kwa hamu recommendations za kamati.Maana kila kitu kamati imeambiwa,schoolarship kibao kazikalia hajatoa kwa WA tz...
 
Unapoona mpaka "Usalama wa Taifa" wanageukana wenyewe kwa wenyewe, ujue hapo kazi nene.
 
Hahaaaaa!!! Thats nice>>>>>> Tupe picha kama hizo hapo juu!!!!

Mkuu Halisi,

Siku hizi umekuwa mchoyo wa 'ma-news', yaani 'ma-news' makubwa namna hiyo ulikuwa umegoma kuyavunja hata kwa kutupa dondoo kiduchu?

Hapa kuna agenda ya Mamvi kumshusha jamaa au ni nini kinaendelea? Maana huu mwelekeo unavyokwenda unaashiria makubwa.

Mamvi na Kamati yake walienda kama kikosi cha kufuatilia maswala fulani au nini haswa kilichoifanya Kamati yake iende Morocco. Naona hapa kunaweza kuwa na kete inarushwa kiaina.

CCM ninaipenda bure .... ngoja nikae mkao wa kusubiri kuona watu wanavyomwagiana matope na kuvuana nguo hadharani.

Ila kama "dili" linaenda mpaka kwa Mkulu, hapo naona "imbombo ngafu" tunaweza kuona some sort of Richmond? Maana mambo ya Ekelege na TBS yalianza ivi ivi kwa Kamati kwenda Far East!
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa maelezo mazuri. Lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa tehn Kitine hakuwa waziri full. Alikuwa Naibu Waziri (I stand 2 b corrected). Je tuhuma hizo zilitosha kuondoa moral authority yake kuzungumzia masuala ya kuijenga nchi kwa kuweka sawa uongozi huu. Ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa kiongozi wa sekta nyeti na muhimu (tena wakati huo kumbuka ilivyokuwa nyeti kweli).

Lakini suala muhimu hapa, kwa hiyo ni sawa kusema kuwa Membe (kama ni yeye aliyemaanishwa katika kauli hiyo) na Kitine hawana tofauti. Maana ukiziweka vyema sentesi zako katika inferences unapata conclusion hiyo kuwa Membe (kama ni yeye waziri mhusika) na Kitine hawana tofauti, hivyo unakubali kuwa waziri aliyezungumzwa kweli siyo mwadilifu eeh?

Mkuu tunapozungumzia moral authority tunazungumzia morals. Huwezi kuwa kahaba ukamlaumu mtu mwingine kwa ukahaba, huwezi kuwa mwizi ukamshutumu mwingine kwa wizi. Kama Membe ni mwizi au fisadi kama tunavyodhani anasema Hamisi Kitine, ni vizuri wasiowezi na mafisadi wakasema hivyo. Inatia shaka kusikia mwizi anapiga mayowe ya mwizi, kwenye hali kama hiyo tunaoachwa kwenye mataa ni sisi tunaofisadiwa. Bahati mbaya sijaona kipindi hicho, kama topic ilikuwa "ufisadi na wanaotafuta urais" basi ingekuwa vema azungumzie issue nzima na sio kugusa juu juu ambako hakuna hata wizi, ila kupokea pesa toka nje.

Mzee kama Hamisi Kitine alitakiwa kutumia uzoefu wake kutusaidia watanzania kudeal na mzizi wa ufisadi na sio kutumia issue ya ufisadi kuonesha chuki binafsi kwa waliofichua ufisadi wake.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom