SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amesema hoja zote binafsi zilizositishwa katika Bunge la 10, sasa zitajadiliwa katika Bunge lijalo litakaloanza Aprili 9. Makinda alisema wahusika wa hoja, wanatakiwa kujipanga upya na kuwasilisha hoja zao.
Makinda kwa sasa anahudhuria Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Dodoma. Hata hivyo, ni hoja pekee ya Joshua Nassari kuhusu mwenendo wa Baraza la Mtihani la Taifa (Necta) unavyoathiri elimu ya Tanzania ndiyo haikusomwa kutokana na kuzuka kwa vurugu katika mkutano huo wa Bunge.
Hoja binafsi ziliwasilishwa ni ya Mwigulu Nchemba iliyokuwa ikihusu mikopo ya elimu ya juu, James Mbatia iliyohusu mitalaa ya elimu kwa shule za msingi, sekondari na elimu ya awali.
Hamisi Kigwangala aliwasilisha hoja yake ya kuanzishwa mpango wa kusaidia vijana ikiwamo kuanzisha benki,wakati John Mnyika aliwasilisha hoja kuhusu maji na majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.Hoja zote binafsi sasa kujadiliwa Bunge lijaloHoja zote binafsi sasa kujadiliwa Bunge lijalo
Hata hivyo, hoja za Kigwangala na Nchemba ndizo zilizopita wakati hoja ya Mbatia na Mnyika zilitupwa baada ya mijadala ya hapa na pale kwa wabunge.
Kwa upande mwingine, hoja za Mbatia na Mnyika ndizo zilizowasha moto Bungeni na hata kusababisha Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuamua kuondoa hoja zote kutokana na vurugu hizo ambazo Spika alisema sehemu kubwa zimesababishwa na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.
Makinda alisema pia kuwa pamoja na kuahirisha Bunge, lakini wabunge wametia aibu kubwa ndani ya taasisi hiyo ambayo ni moja ya mihimili ya dola.
Source: Hoja zote binafsi sasa kujadiliwa Bunge lijalo - Habari - mwananchi.co.tz
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Rais dhaifu!Duuuuuuuuu!!!!!!!!!!
Ina maana matusi ya nguoni 400 yametosha huyu mama kubadili msimamo.
Ama kweli nimeamini, Serikali ya tanzania ni LEGELEGE, CCM ni LEGELEGE, na........ ni LEGELEGE, na .......ni LEGELEGE...
maamuzi yao daima ni ya kukurupuka tu...
MIZAMBWA
NABII MTARAJWA!!!
Naibu Spika Ndugai na Spika Makinda kwa kweli walibanwa sana na baada ya mashitaka kufikishwa ktk mahakama za wananchi 10/02/2013 imebidi wajirudi , tutizame jinsi hali ya ubabe wa Naibu Spika na wabunge wa CCM ilivyokuwa wakihaha kutafuta 'kanuni' kubana wabunge wa upinzani kiaina hapo 04/02/2013
source: subi nukta