TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 23,914
- 23,079
Nashauri ipelekwe Hoja Binafsi Bungeni(kwa mujibu wa taratibu za Bunge) -Bunge libatilishe Azimio lile na kisha, Makubaliano yaangaliwe upya pale ambapo panapigiwa kelele na wananchi hasa kipengere cha 23(4), na pengine pia parekebishwe na wananchi waridhike kuwa Sasa makubaliano yapo sawa. Kisha Bunge lipitishe Azimio lililorekebishwa ili serikali iendelee na mchakato unaofuata.
Hili jambo lisitupotezee muda tufanye marekebisho tusonge mbele. Tuna Mambo mengi ya kufanya kwa Kila mtu kwa nafasi yake alipo kuwawezesha watanzania wote kujiletea maendeleo kiuchumi na kiteknolojia.
Naamini viongozi wetu wote Wana kiu ya kuiletea maendeleo halisi ya kiuchumi na kiteknolojia Tanzania kwa manufaa ya watanzania wote. Na kwa msingi huo hoja yangu hii wataitazama na kuifikiria kwa uzito ambao wao wanaona inastahili.
Naomba kutoa hoja.
- - -
TUJITEGEMEE 25/06/2023.