Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,655
- 14,699
Kwa Watu waliolelewa maadili ya Kiuanaume au Kiumeni kamwe picha ya Deo sio tu hadhi yake ya Ubunge bali pia kwa hadhi yake kama Mwanaume ni aibu kwa Mwanaume Mzima lijari kusimama akilumbana na wakina Mama wengine ni hadhi ya Mama yake kama yule Mama Kaihula [Mbunge Viti Maalumu Chadema] aliyekuwa anamwambia akashughulikie matatizo ya Wananchi wake juu ya mradi wa makaa ya mawe na chuma Linganga na Mchuchuma ambako mpaka sasa hawana majibu ya tatizo hilo.Nimeona aibu mimi kama Mwanaume kuona Mwanaume Mwenzangu akipewa Ukweli kupitia mipasho ya kinamama kwa kutumia lugha ya Mwili ya wakina Mama wanyotumia wakiwa wanalumbana mitaani yaani kwa kiswahili KUSUTANA.
Wabunge aina ya Deo ndio hao ambao tuanasema CCM ilifanya makosa kuwapa dhamana ya kugombe ubunge kupitia tiketi ya CCM.Sijui ana elimu ya kiwango gani.Anajua dhahili kuwa wabunge wa Chadema walitoka nje wakiwa wametoka na ghadhabu kisha yeye pasipo fikra na busura anawafuta akiwa na ile ile akili ya VIONGOZI walio wengi ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI kuwa daima wao wako sahihi,na si vinginevyo na kuwaongezea kejeri za kuwatuhumu kuwa ni wakolofi na wasiofuata kanuni.
Ingekuwa imetokea mafichoni tungesema hatujui ila Watanzania wameona kupitia Luninga nini kimetokea.Kwa ujumla Deo alichofanya ni kuwazodoa [Provoke].Ni tendo lisilo la kiungwana tena limemzalilisha sana kwa watu waelevu [Intellectual] wamempimia kijiko na si koleo.
Hatimae tunamuona kwenye televisioni yuko na kinamama ambao ukiwangalia wanavyolumbana nae dhahili katika lugha ya mwili ya wakina Mama [Body language] unaona dhahili ni kama wakina mama wanavyosutana na Mwanamke Mwenzao mitaani kwetu.
CCM Jamani maadili yenu yanapolomoka kupitia viongozi wenu aina ya DEO ni picha chafu isiyopendeza kuiona kati ya kijana DEO mbunge wa Wananchi kupitiia tiketi ya CCM akilumbana na Wakina Mama.
Kisaikolojia picha ile ya DEO na Wakina Mama wale, Wanawake mitaani wanamuona DEO kama kiwakilishi cha Wanaume Waongo wanaosutana na wanawake.
Natoa challange kwa CCM,wachukue Picha zilizopigwa kati ya Deo na kinamama wazipeleke kufanya maojiano kupitia Picha zile [A Picture Speek athousands words] haswa wakina Mama waulizwe wanatafsiri nini kwenye picha hizo zilizombele yao.Majibu yatakayotoka hapo Ndio impact ya kuwa na viongozi type ya Deo ndani ya CCM na Serikalini.Wabunge wapenda vijembe,majungu na ujuaji usio na tija vilivyopelekea kuiponza CCM mpaka kufika hapo ilipo sasa ya KUCHOKWA NA BAADHI YA WANANCH.
Wabunge wa CCM wanaitaji mafunzo ya mahusiano [Public Relation] na miongozo mingine ya jamii kimahusiano juu ya muuonekano [Bahaviour].Na mafunzo hayo yasifanye na watu ndani ya CCM bali yafanywe na makampuni au taasisi zenye kujua mapokeo ya umma dhidi ya matendo ya kiongozi au mwakilisha wa wananchi mbele ya umma yasio ndani ya CCM.Kwa kuwa yanayoendelea ndani ya Watendaji wa CCM ni matokeo ya Mafunzo ya ndani kwa ndani.lakini wakifundishwa kutoka nje watajiona mapungufu yao na hivyo watajifunza kwa faida yao na faida ya CCM kama chama.
Mkuu hapa umepigilia msumari kwenye kidonda tena ule wa inch 6, Magamba yako wapi mbona hayajitokezi kwenye hili thread?
Ritz-Omr-Rejao-FF-