ARUSHA: A HOME FOR NO BODY?
Hi Friends,
Naomba niulize Swali: Hivi Arusha kuna nini?
Huu ni mji wa ajabu sana, kwani inaelekea kila uongozi serikalini ukitaka kula basi ni Arusha. Hivyo wakurugenzi wengi hupangwa kwa ajili ya kufanikisha hilo (mtizamo wangu). Haingii akilini , kwa mji wenye vivutio vingi vya utalii kama Arusha kuwa katika hali kama ilivyo. Ni mchafu, hauna barabara (zaidi ni ile moja tu iliyoachwa na wakoloni), na hakuna juhudi zozote za kuundeleza.
Kila kitu ni ghali, si kwa sababu panatakiwa hivyo, ila ni kwa mji kukosa miundo mbinu , mipango na ulafi uliokithiri. Wabunge na viongozi wa siasa ni wale wale , au walio na mahusiano yaleyale.Ili kudhibiti mabadiliko ya uongozi, huwa wanajitahidi kutoandikisha wanachama wapya wa CCM bila kujua kama watawasaidia au la. Hivyo, mji kama huu ambao una wamasai wengi wanaoheshimu maboma yao, ukidhibiti wanachama walio nje ya zile Boma zinazokupenda, umefanikiwa kupita ngwe nyingine , kiasi kwamba mtandao wao huwezi kuuingilia kamwe. CCM inabidi itafakari haya. Hii ndio moja ya siri ya jeuri za kina Mrema. Wana jeuri isiyo kifani.
Unashangaa mji kama huu hauna viwanja vilivyopimwa zaidi ya Njiro na Ngaramtoni. Na hata vilivyopimwa havigawiwi kwa wananchi, bali viongozi hugawana wenyewe kwa wenyewe wakitumia majina ya bandia ili kuonekana kama vimegawiwa wananchi. Matokeo yake, hawaviendelezi, bali husubiri mtu anayehitaji kujenga ili wamuuzie kwa bei ya kuruka. Na hata kuuza kwenyewe ni mpaka huyo aliyehodhi atake, kwani hawauzi mpaka awe na shida!
Matokeo yake, viwanja hivyo hununuliwa na watu wenye pesa tu, kiasi kwamba eneo la Njiro linaitwa eneo la matajiri wakati si maana yake. Kwanini kuitwe kwa matajiri wakati lengo ilikuwa wanachi wauziwe? Inaingiaje akilini hata raisi wa nchi anathubutu kusema Njiro ni eneo la matajiri, wakati anajua halikutakiwa liwe hivyo? Au kwa vile nyumba nyingi ni za mawaziri na maktibu wa wizara? Nini maana ya yote haya? Mbona miji mingine hupima viwanja tena huvitangaza ili watu wapeleke maombi, lakini si kwa Arusha?
Matokeo yake ni watu kutafuta viwanja visivyo pimwa na kujenga holela , maana serikari inawapimia viwanja matajiri tu. Hivi kweli tumefikia hapo?
Mpaka Arusaha inanyimwa hadhi ya jiji ni kwa sabau ya huo ubovu na kukosekana kwa miundo mbinu. Na tatizo moja ni kwa sabau ya Jumuiya y Afrika Mashariki.
Kila bajeti ikija, watu hupiga dana dana, wakigawana hizo pesa, kwan i wanategemea EAC itatoa pesa siku yoyote ili wafiche maovu yao huko. Ni jambo la aibu sana.
Naomba mnisaidei: Nini tatizo la Arusha?
Ina kuwaje mji mdogo kama huu maji hayatoshelezi wakati kuna maji mengi mno mlima Meru?. Inaingiaje akilini sehemu zingine zinapata maji kila siku , lakini sehemu zingine mgawo mara moja kwa wiki au mwezi? Ni vigezo gani hutumika? Ili watu wakatoe pesa idara ya maji wachimbiwe visima? Hivi nini kinaendelea hapo.
Tanesco -Arusha Bomu, Maji Bomu, Halmashauri Bomu, kweli? Hivi Kenya wangepewa Kisumu iwe ndio EAC ingezembea kiasi hiki? Mji wa kimataifa , uongozi wa kihuni.
No, Let us say NO!!!!