Jeriko Palestine mji mkongwe zaidi duniani

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,917
1. JERICHO -PALESTINE
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa huu ndio mji mkongwe zaid duniani...mji huu ulikuwepo zaidi ya miaka 6800 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Wataalamu wanasema kuwa hapo awali watu waliishi kwa kuhamahama kwahyo mji wa Jericho ndio ulikuwa wa kwanza duniani kwa watu kuanzisha makazi na kutoka kuishi maisha ya uwindaji na kuanza maisha ya kulima Kwahyo tunaweza kusema ndio mji ulioanzisha USTAARABU WA DUNIA

Ndani ya mji huu ndio pia kuna vilima ambavyo Yesu kristo alijaribiwa na shetani (mount of temptation) Lakini pia ndani ya mji huu ndio inasemekana kuna kaburi la Nabii Musa

Pia mji wa Jericho ndio mji wa kwanza duniani kuzungushiwa ukuta (walled city)

Licha ya kuharibiwa na kutengenezwa tena zaidi ya mara moja lakini mji huu hadi leo hii bado unakaliwa na watu... Inasemekana ni makazi ya WAtu zaidi ya elfu 20
 
Brother mimi ni mtu wa maana kishenzi.
 

Attachments

  • Jericho_cityscape_from_wall_ruins.jpg
    Jericho_cityscape_from_wall_ruins.jpg
    9.9 MB · Views: 5
  • images (10).jpeg
    images (10).jpeg
    81.3 KB · Views: 5
Kuta za Yeriko ziliangushwa kwa sauti za tarumbeta na shangwe. Tena kuanguka kwa Kuta hizo hakukuwa kwa kawaida, Kuta zilididimia na kujifukia ardhini.
Hizi ni story zisizoweza kuthibitishwa Kisayansi na hazina ukweli wowote. Bila shaka ni among the fake news zilizoingizwa ktk bible sawa na kila kisa cha Joka na Ever.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom