Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,165
- 30,505
KITABU KINGINE CHA SHEIKH PONDA KIMEZINDULIWA: WALIOPOTEZWA TANZANIA.
Katika kipindi cha miaka mitatu nimekuwa nikipokea vitabu kutoka kwa waandishi wakiniomba nifanye pitio yaani, "book review," kwa nia ya kuvitambulisha vitabu hivi kwa wasomaji na wananchi kwa jumla.
Kitu kinachojitokeza kwa haraka na wazi katika vitabu hivi ni kuwa hivi si vitabu vya kawaida.
Hivi vyote ni vitabu vya kuogofya.
Hivi ni vitabu vya kutisha.
Si vitabu utakachosoma na moyo wako ukawa umetulia.
Hivi ni vitabu unasoma na moyo ukabadilisha mapigo ukawa unadunda kwa haraka.
Hivi ni vitabu vilivyojaa simanzi kila ukurasa unaopindua.
Vitabu vya aina hii si vyepesi kuviandikia pitio ingawa pitio limeandikwa lipo.
Kuna msomaji mmoja alisoma pitio langu la moja ya vitabu hivi vinavyotisha.
Kamaliza pitio langu hakukuta maelezo ya kitabu kinasema nini.
Kahamaki akaniandikia, "Hivi vitisho vya nini tueleze mwandishi kaandika nini?"
Tayari nilikuwa nishawaweleza wasomaji kuwa wasome kitabu waone wenyewe yaliyomo ndani ya kitabu hicho.
Lakini kinyume na wasomaji waandishi wa vitabu hivi wote wameniandikia kunishukuru kwa kufanya pitio la kitabu chake na kuniambia kuwa nimetenda haki kwa kalamu zao.
Ninachoweza kusema kuhusu kitabu hiki cha Sheikh Ponda, "Waliopotezwa Tanzania," ni kuwa kitabu hiki kinatisha sana.
Swali linalozunguka akilini kwangu ni imekuwaje kuwa Tanzania vitabu vyake muhimu kutoka kwa baadhi ya waandishi wake vimekuwa vitabu kurasa zake zinachuruzika damu?
Kitabu hiki kinauzwa Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue na maduka ya vitabu ya Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani.
Bei ya kitabu ni T. Shs: 10,000.00.