Kitabu Kipya: "Waliopotezwa Tanzania " Mwandishi: Sheikh Ponda Issa Ponda

KITABU KINGINE CHA SHEIKH PONDA KIMEZINDULIWA: WALIOPOTEZWA TANZANIA.

Katika kipindi cha miaka mitatu nimekuwa nikipokea vitabu kutoka kwa waandishi wakiniomba nifanye pitio yaani, "book review," kwa nia ya kuvitambulisha vitabu hivi kwa wasomaji na wananchi kwa jumla.

Kitu kinachojitokeza kwa haraka na wazi katika vitabu hivi ni kuwa hivi si vitabu vya kawaida.

Hivi vyote ni vitabu vya kuogofya.
Hivi ni vitabu vya kutisha.

Si vitabu utakachosoma na moyo wako ukawa umetulia.

Hivi ni vitabu unasoma na moyo ukabadilisha mapigo ukawa unadunda kwa haraka.

Hivi ni vitabu vilivyojaa simanzi kila ukurasa unaopindua.
Vitabu vya aina hii si vyepesi kuviandikia pitio ingawa pitio limeandikwa lipo.

Kuna msomaji mmoja alisoma pitio langu la moja ya vitabu hivi vinavyotisha.
Kamaliza pitio langu hakukuta maelezo ya kitabu kinasema nini.

Kahamaki akaniandikia, "Hivi vitisho vya nini tueleze mwandishi kaandika nini?"

Tayari nilikuwa nishawaweleza wasomaji kuwa wasome kitabu waone wenyewe yaliyomo ndani ya kitabu hicho.

Lakini kinyume na wasomaji waandishi wa vitabu hivi wote wameniandikia kunishukuru kwa kufanya pitio la kitabu chake na kuniambia kuwa nimetenda haki kwa kalamu zao.

Ninachoweza kusema kuhusu kitabu hiki cha Sheikh Ponda, "Waliopotezwa Tanzania," ni kuwa kitabu hiki kinatisha sana.

Swali linalozunguka akilini kwangu ni imekuwaje kuwa Tanzania vitabu vyake muhimu kutoka kwa baadhi ya waandishi wake vimekuwa vitabu kurasa zake zinachuruzika damu?

Kitabu hiki kinauzwa Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue na maduka ya vitabu ya Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani.

Bei ya kitabu ni T. Shs: 10,000.00.
Nitakitafuta
 
Msanii,
Hakika ni muhimu tukajiuliza tumefikaje katika hali hii?
Mzee Mohamed Said, kumbuka ama fahamu kwamba mtu anapofanya jambo lenye kuhusisha hadhira huwa anapata washabiki. Mfano mzuri ni timu za soka ambapo zinavutia washabiki na hakika mvumo wa washabiki ni hamasa ya timu kufanya vyema zaidi...

Waliopotezwa walimetuachia huzuni kubwa lakini wapo ambao mpaka kesho wanashabikia kupotezwa kwao hao waliopotezwa.

Jamii ndiyo zao la uhalifu wote. viongozi wakatili ni zao la jamii. Tujenge misingi ya kuimarisha jamii iliyostaarabika na yenye hofu ya Mola
 
Nimeshtushwa na niliyosoma katika kitabu hiki.
 
Maalim, naomba ukipata muda uje utuelezee kuhusu suala la wamanyema kula nyama za watu kabla waarabu hawajafika maeneo ya congo ya mashariki, maandiko kadhaa yanasema hivyo, je ni ukweli au uongo? Kwa nini wanaitwa wamanyema?

Kama ni kweli simlaumu Nyerere kwa kufuta historia za wahamiaji katika kupigania uhuru wa nchi hii, wangetumeza, akina Sykes watakumbukwa JF pekee
 
Jabulani,
Sijui historia hiyo ndiyo naisikia leo.
Tuwekee taarifa zaidi.
 
Msanii,
Nimeshtushwa na niliyosoma katika kitabu hiki.
Umefanya utafiti na wewe kidogo kujiridhisha kwa nini watu wapotezwe.? Pengine ukajiuliza mbona wewe pamoja na kuandika yote hujapotezwa?

Jambo lolote huwa na sababu. Yes kuna haki na sheria ila pia ujue dunia ina kanuni zake. Siku ukiwa kwenye nafasi nyeti za juu kabisa utaelewa hili.

Kuna wakati kuna mambo ya hovyo hutokea na huwa na influence kubwa katika jamii na yakiachwa huwa na madhara makubwa mno mbele. Si kila jambo hushughuliwa kwa level ya kimahakama. Mengine kanuni za dunia huwa zina apply tu. Na kisha maisha yanarejea katika ustaarabu wake.

Mfano leo Kibiti na Mkuranga inakalika. Yaani maisha yamerejea katika ustaarabu wake, lakini mambo yale yangeachwa leo wangekuwa wameshaichukua hadi sehemu ya Dar Salaam.
 
Sheiza,
Unaniuliza kama nimefanya utafiti kwa nini mimi sijapotezwa kwa kuandika.

Labda nikuulize wewe kama mtu Tanzania anaweza kuuliwa kwa kuandika vitabu na makala.

Niuliwe kwa kifungu kipi cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia?
Unasema kuna sababu ya watu kuuawa.

Sababu zipi hizo za kuua watu ovyo na anaetoa hukumu ya kuua ni nani na kwa sheria ipi ya nchi?

Unasema kuna mambo ya hovyo (ovyo) yanatokea na hayo ndiyo yanasabibishwa watu kuuwa.

Mambo gani ya ovyo hayo yasiyoweza kufikishwa mahakamani?
Unaweza kuyaeleza ili yafahamike na jamii?

Unasema mambo haya hayashughulikiwi na mahakama.
Haya umepata wapi?

Kama hayashughulikiwi na mahakama nani anayetoa maamuzi hayo ya kutoa roho za watu na anatumwa na nani na anaongozwa na taratibu zipi?

Hili la kuwa nafasi za juu ndiyo nielewe mbona unazidi kunishangaza?
Umejuaje kuwa mimi niko nafasi za chini?

Wewe unaenadika hapa unazungumza kwa niaba ya hao walio katika nafasi nyeti za juu?

Ikiwa ni hivyo kwa nini hili ulizungumze JF tena ukiwa umejificha?

Toka lini serikali ya Tanzania ikajificha ikawa inazungumza huku imefunika uso wake?

Umehitimisha kwa Kibiti Mkurunga.
Waliouliwa huko ni Waislam na wanafahamika vizuri sana.

Soma kitabu cha Sheikh Ponda kimewaeleza watu waliopotezwa kwa ukamilifu.

Soma kitabu kisha ndiyo njoo unikabili na majibu kutoka yale yaliyoelezwa ndani ya kitabu hicho.

Ninachokutahadharisha ni kuwa usitake kuiingiza serikali katika jinai iliyofanywa na watu binafsi.

Soma uamuzi wa Nuremberg Trials utaelewa kuwa wale walioua Wayahudi katika kambi za mateso na mauaji Auschwitz na kwengineko hawakusalimika kwa kusingizia kuwa walikuwa wametumwa na serikali kuua watu wasio na hatia.
 
Father...
Wote hao ni Watanzania ingawa ni Wamanyema.

Wamanyema wana historia kubwa sana katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nitakuonjesha kidogo:

View attachment 2649364
Kulia ni Hamisi Taratibu Muasisi wa TANU Dodoma Central Province, (Mmanyema), Saadan Abdu Kandoro (Mmanyema) katika waasisi 17 wa TANU, Julius Nyerere (Mzanaki), Sheikh Mohamed Ramiyya (Mmanyema) kiongozi wa TAA na TANU Bagamoyo na Iddi Faiz Mafongo (Mmanyema) Mweka Hazina wa Kwanza wa TANU kati ya watu wasiozidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo na mkusanyaji wa fedha sasfari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955.

Picha imepigwa Dodoma Railway Station mwaka wa 1955 wakati wa kuisambaza TANU majimboni na kupigania uhuru.

Mzee unafeli wapi? Kila siku picha zile zile 😂 😂 😂 😂 😂
 
KITABU KINGINE CHA SHEIKH PONDA KIMEZINDULIWA: WALIOPOTEZWA TANZANIA.

Katika kipindi cha miaka mitatu nimekuwa nikipokea vitabu kutoka kwa waandishi wakiniomba nifanye pitio yaani, "book review," kwa nia ya kuvitambulisha vitabu hivi kwa wasomaji na wananchi kwa jumla.

Kitu kinachojitokeza kwa haraka na wazi katika vitabu hivi ni kuwa hivi si vitabu vya kawaida.

Hivi vyote ni vitabu vya kuogofya.
Hivi ni vitabu vya kutisha.

Si vitabu utakachosoma na moyo wako ukawa umetulia.

Hivi ni vitabu unasoma na moyo ukabadilisha mapigo ukawa unadunda kwa haraka.

Hivi ni vitabu vilivyojaa simanzi kila ukurasa unaopindua.
Vitabu vya aina hii si vyepesi kuviandikia pitio ingawa pitio limeandikwa lipo.

Kuna msomaji mmoja alisoma pitio langu la moja ya vitabu hivi vinavyotisha.
Kamaliza pitio langu hakukuta maelezo ya kitabu kinasema nini.

Kahamaki akaniandikia, "Hivi vitisho vya nini tueleze mwandishi kaandika nini?"

Tayari nilikuwa nishawaweleza wasomaji kuwa wasome kitabu waone wenyewe yaliyomo ndani ya kitabu hicho.

Lakini kinyume na wasomaji waandishi wa vitabu hivi wote wameniandikia kunishukuru kwa kufanya pitio la kitabu chake na kuniambia kuwa nimetenda haki kwa kalamu zao.

Ninachoweza kusema kuhusu kitabu hiki cha Sheikh Ponda, "Waliopotezwa Tanzania," ni kuwa kitabu hiki kinatisha sana.

Swali linalozunguka akilini kwangu ni imekuwaje kuwa Tanzania vitabu vyake muhimu kutoka kwa baadhi ya waandishi wake vimekuwa vitabu kurasa zake zinachuruzika damu?

Kitabu hiki kinauzwa Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue na maduka ya vitabu ya Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani.

Bei ya kitabu ni T. Shs: 10,000.00.
Mzee Said unazungumziaje bandari kuuzwa kwa mwarabu?
 
Mzee unafeli wapi? Kila siku picha zile zile 😂 😂 😂 😂 😂
Tangawizi,
Somo linapokuwa ni la historia usitegemee kuwa utaona picha mpya.
Kila siku picha zitakuwa zile zile.

Angalia picha za Pyramid za Giza Egypt.

Ukizungumza historia ya Giza utaweka picha zile zile kwani hakuna Pyramid mpya inayojengwa.

Si swali la mimi kufeli.
Angalia hiyo hapo chini nilipiga Giza mwaka wa 1988 kuna Pyramid.

Nikienda leo kupiga picha nitakuta Pyramid hiyo hiyo na picha zitakuwa zile zile.

1686513465696.png
 
Sheiza,
Unaniuliza kama nimefanya utafiti kwa nini mimi sijapotezwa kwa kuandika.

Labda nikuulize wewe kama mtu Tanzania anaweza kuuliwa kwa kuandika vitabu na makala.

Niuliwe kwa kifungu kipi cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia?
Unasema kuna sababu ya watu kuuawa.

Sababu zipi hizo za kuua watu ovyo na anaetoa hukumu ya kuua ni nani na kwa sheria ipi ya nchi?

Unasema kuna mambo ya hovyo (ovyo) yanatokea na hayo ndiyo yanasabibishwa watu kuuwa.

Mambo gani ya ovyo hayo yasiyoweza kufikishwa mahakamani?
Unaweza kuyaeleza ili yafahamike na jamii?

Unasema mambo haya hayashughulikiwi na mahakama.
Haya umepata wapi?

Kama hayashughulikiwi na mahakama nani anayetoa maamuzi hayo ya kutoa roho za watu na anatumwa na nani na anaongozwa na taratibu zipi?

Hili la kuwa nafasi za juu ndiyo nielewe mbona unazidi kunishangaza?
Umejuaje kuwa mimi niko nafasi za chini?

Wewe unaenadika hapa unazungumza kwa niaba ya hao walio katika nafasi nyeti za juu?

Ikiwa ni hivyo kwa nini hili ulizungumze JF tena ukiwa umejificha?

Toka lini serikali ya Tanzania ikajificha ikawa inazungumza huku imefunika uso wake?

Umehitimisha kwa Kibiti Mkurunga.
Waliouliwa huko ni Waislam na wanafahamika vizuri sana.

Soma kitabu cha Sheikh Ponda kimewaeleza watu waliopotezwa kwa ukamilifu.

Soma kitabu kisha ndiyo njoo unikabili na majibu kutoka yale yaliyoelezwa ndani ya kitabu hicho.

Ninachokutahadharisha ni kuwa usitake kuiingiza serikali katika jinai iliyofanywa na watu binafsi.

Soma uamuzi wa Nuremberg Trials utaelewa kuwa wale walioua Wayahudi katika kambi za mateso na mauaji Auschwitz na kwengineko hawakusalimika kwa kusingizia kuwa walikuwa wametumwa na serikali kuua watu wasio na hatia.
Umeandika vitu vingi mzee Said. Ila najua unajua. Katika kanuni za dunia si kila kesi inapelekwa mahakamani. Nyingine mnamalizana tu.
Nitakuambia, kuna watu miaka kadhaa walikamatwa msituni huko Tandahimba wakifanya mazoezi ya kivita na wamevaa kama wapo Jihad. Walipelekwa mahakamani wakashinda kesi. Miaka mitano badae watatu kati yao walidakwa kwenye mauaji ya mkuranga. Tena mmoja wao ndio alim snipe mkuu wa kituo.

Huyu na wenzie waliokamatwa wanapelekwaje tena mahakamani. Wakikataa mna vidhibiti gani tena.

Ndio maana nakuambia kuna mahali ukifikia utaelewa. Kama ungekuwa huko usingeongea haya. Kuna nyakati ili nchi au dunia iendelee kuwa na utulivu ni lazima kanuni fulani zi apply.
 
Mbona hayo unayosema hayaingii akilini?
Tandahimba ndiko walipokamatwa na wamevaa kama wako jihad.

Kuvaa kama ''kijihad'' kukoje?
Naomba maelezo.

Walikuwa wangapi na silaha zao zilikuwa zipi na ziliingiaje Tanzania?

Wamepelekwa mahakamani wakashinda kesi.
Walipekekwa mahakama gani?

Nipe ushahidi wa jambo hili kwani mimi sijasikia kesi hiyo kuandikwa popote.
Siwezi kuamini maneno yako.

Na haya maneno yako nitayazungusha kwa wengine wanipe taarifa kama wao wanaijua kesi hii.

Sasa nisikilize na mimi nikueleze yangu.

Kwa kulinda faragha ya huyu mtaalamu wa ugaid aliyekuja kunihoji sitatumia jina lake halisi ninampa jina la kupanga, ''Red Fox.'':

SUALA LA UGAIDI TANZANIA
Red Fox kulia ni Mzungu na mtaalamu wa masuala ya ugaidi.
Ameishi Tanzania kwa miaka 15.

Amefanya utafiti katika ugaidi Tanzania, Kenya na Mozambique.
Amefika kwenye matukio yote ya ugaidi katika nchi hizo.

Jana tarehe 2 Julai 2020 alinitembelea nyumbani kwangu kwa mazungumzo.
Amesoma kila nilichoandika kuhusu Waislam na hali yao Tanzania.

Amesoma utafiti niliofanya katika suala la ugaidi na mauaji yaliyotokea Kilindi na Handeni mwaka wa 2013 na amesoma pia ‘’paper,’’ niliyowasilisha Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria mwaka wa 2006 kuhusu ugaidi.

Red Fox anazungumza Kiswahili kizuri na kanieleza kuwa kajulishwa kwangu na Prof. James Brennan wa Chuo Kikuu Cha Illinois at Urbana Champaign Marekani ambae mimi ni rafiki yangu wa miaka mingi.

Prof. Brennan ni mtaalamu wa historia ya Tanzania na kaandika vitabu na ‘’paper’’ kadhaa kuhusu Tanzania.

Nilimfahamisha Red Fox kuwa wazee wetu walipigania haki yao ya kuwa huru kutoka ukoloni chini ya TANU hawakunyanyua silaha bali waliwaunganisha wananchi wote bila ya kujali dini zao kuondoa dhulma ili haki na usawa ipatikane kwa wote.

Hawakumbagua Julius Nyerere kwa Ukristo wake na walimchagua kuwa kiongozi wao Nyerere akianza siasa Dar es Salaam katika mji wa Waislam.

Huu nikamweleza ndiyo msimamo wa Waislam wengi wa Tanzania na ikiwa haki itaonekana inatendeka kwa wote itakuwa vigumu kwa mbegu ya ugaidi kumea katika ardhi ya Tanzania.

Red Fox alinifahamisha kuwa utafiti wake umeonesha kuwa chokochoko zote alizokutananazo katika suala la ugaidi hazina chanzo kutoka wa kwa Waislam ndani ya Tanzania.

Nilimfahamisha Red Fox kuwa katika kudumisha amani muhimu sana kwa serikali kusikiliza nini Waislam walio nje ya BAKWATA wanasema na serikali isijidanganye kuwa hakuna ubaguzi dhidi ya Waislam Tanzania.

Mimi na Red Fox kwa pamoja tulirejea historia ya BAKWATA.
Mazungumzo yetu yote tulifanya kwa Kiswahili.

Tuombe dua kuwa taarifa yake popote inapokwenda itaakisi fikra hizi nilizomweleza na itasaidia katika kutafuta haki kwa Waislam na kwa kila anaehisi anadhulumiwa kwa nia ya kudumisha amani katika nchi yetu.

Allah ndiye mjuzi.
 
Kuna kitabu kinaitwa THE FAITHFUL SPY mtunzi ni Alex Berenson, sio mpenzi wa novel lakini hiki kitabu mwandishi yaelekea alifanya tafiti ya hali ya juu, Kinazungumzia uislamu, ugaidi na serikali ya US inavyopambana na ugaidi.

Huyo faithful spy ni kachero aliyekuwa akifanya kazi CIA akiitwa John Wells, CIA ilimuagiza walimpa jukumu kwenda ku spy kundi la Taliban huko Afghanistan, baada ya kukaa muda mrefu huko akabadili dini na kuwa muslim, siku anarudi kwao US wenzie hawamuamini tena wanaona amekuwa ni mmoja wa magaidi, Wells anachukia ugaidi lakini amesoma kuhusu uislamu na kapenda kuwa muslim, CIA wanamkamata na kumpeleka chumba cha mahojiano.

Mwisho Wells anakuja kupambana vikali na magaidi na kupelekea kuzuia ugaidi mkubwa uliotaka kujitokeza na kuwashangaza CIA.

Kitabu kinaelezea ugaidi ni kitu tofauti kabisa na uislamu, hapana mahusiano yeyote.
 
Sheiza,
Mbona hayo unayosema hayaingii akilini?
Tandahimba ndiko walipokamatwa na wamevaa kama wako jihad.

Kuvaa kama ''kijihad'' kukoje?
Naomba maelezo.

Walikuwa wangapi na silaha zao zilikuwa zipi na ziliingiaje Tanzania?

Wamepelekwa mahakamani wakashinda kesi.
Walipekekwa mahakama gani?

Nipe ushahidi wa jambo hili kwani mimi sijasikia kesi hiyo kuandikwa popote.
Siwezi kuamini maneno yako.

Na haya maneno yako nitayazungusha kwa wengine wanipe taarifa kama wao wanaijua kesi hii.

Sasa nisikilize na mimi nikueleze yangu.

Kwa kulinda faragha ya huyu mtaalamu wa ugaid aliyekuja kunihoji sitatumia jina lake halisi ninampa jina la kupanga, ''Red Fox.'':

SUALA LA UGAIDI TANZANIA
Red Fox kulia ni Mzungu na mtaalamu wa masuala ya ugaidi.
Ameishi Tanzania kwa miaka 15.

Amefanya utafiti katika ugaidi Tanzania, Kenya na Mozambique.
Amefika kwenye matukio yote ya ugaidi katika nchi hizo.

Jana tarehe 2 Julai 2020 alinitembelea nyumbani kwangu kwa mazungumzo.
Amesoma kila nilichoandika kuhusu Waislam na hali yao Tanzania.

Amesoma utafiti niliofanya katika suala la ugaidi na mauaji yaliyotokea Kilindi na Handeni mwaka wa 2013 na amesoma pia ‘’paper,’’ niliyowasilisha Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria mwaka wa 2006 kuhusu ugaidi.

Red Fox anazungumza Kiswahili kizuri na kanieleza kuwa kajulishwa kwangu na Prof. James Brennan wa Chuo Kikuu Cha Illinois at Urbana Champaign Marekani ambae mimi ni rafiki yangu wa miaka mingi.

Prof. Brennan ni mtaalamu wa historia ya Tanzania na kaandika vitabu na ‘’paper’’ kadhaa kuhusu Tanzania.

Nilimfahamisha Red Fox kuwa wazee wetu walipigania haki yao ya kuwa huru kutoka ukoloni chini ya TANU hawakunyanyua silaha bali waliwaunganisha wananchi wote bila ya kujali dini zao kuondoa dhulma ili haki na usawa ipatikane kwa wote.

Hawakumbagua Julius Nyerere kwa Ukristo wake na walimchagua kuwa kiongozi wao Nyerere akianza siasa Dar es Salaam katika mji wa Waislam.

Huu nikamweleza ndiyo msimamo wa Waislam wengi wa Tanzania na ikiwa haki itaonekana inatendeka kwa wote itakuwa vigumu kwa mbegu ya ugaidi kumea katika ardhi ya Tanzania.

Red Fox alinifahamisha kuwa utafiti wake umeonesha kuwa chokochoko zote alizokutananazo katika suala la ugaidi hazina chanzo kutoka wa kwa Waislam ndani ya Tanzania.

Nilimfahamisha Red Fox kuwa katika kudumisha amani muhimu sana kwa serikali kusikiliza nini Waislam walio nje ya BAKWATA wanasema na serikali isijidanganye kuwa hakuna ubaguzi dhidi ya Waislam Tanzania.

Mimi na Red Fox kwa pamoja tulirejea historia ya BAKWATA.
Mazungumzo yetu yote tulifanya kwa Kiswahili.

Tuombe dua kuwa taarifa yake popote inapokwenda itaakisi fikra hizi nilizomweleza na itasaidia katika kutafuta haki kwa Waislam na kwa kila anaehisi anadhulumiwa kwa nia ya kudumisha amani katika nchi yetu.

Allah ndiye mjuzi.
Ni sawa kabisa mzee Said haya nisrmayo kutoingia akilini mwako sababu una vyanzo vya taarifa ambavyo wewe unaviamini na ambavyo huwezi kuviamini. Ila hiyo taarifa hata sasa bado ipo mitandaoni we google tu. Ilikuwa mwaka 2013.

Then hakuna mahali nimetaja Uislam. Uislam hauingii kwenye andiko langu hata kama kuna baadhi ya wakosaji hufanya vitu kwa kujiweka karibu na dini fulani wakiamini watapata uungwaji mkono..naomba tuongee tu bila kuutaja Uislamu.
 
Ukiondoa Uislam na Waislam katika suala la ugaidi hakuna kitu kitabaki ila makosa ya kawaida ya jinai.

Hapa ndipo sasa nimegundua na kuthibitisha kuwa huna ulijualo katika suala hili.

Ama kuhusu ushahidi niliokuomba na kunielekeza mwaka wa 2013 hivyo sivyo watu wanavyopeana taarifa mitandaoni.

Toa link ya taarifa yako weka hapa sote tusome.
 
Tangawizi,
Somo linapokuwa ni la historia usitegemee kuwa utaona picha mpya.
Kila siku picha zitakuwa zile zile.

Angalia picha za Pyramid za Giza Egypt.

Ukizungumza historia ya Giza utaweka picha zile zile kwani hakuna Pyramid mpya inayojengwa.

Si swali la mimi kufeli.
Angalia hiyo hapo chini nilipiga Giza mwaka wa 1988 kuna Pyramid.

Nikienda leo kupiga picha nitakuta Pyramid hiyo hiyo na picha zitakuwa zile zile.

Kipindi hicho ulikuwa wa mjini haswaa
 
Father...
Wewe ni Mtanzania wa kawaida.
Tuanze na Watanganyika wa kawaida.

Waasisi wa harakati za kupigania Tanganyika alikuwapo Kleist Sykes (Mzulu), Ibrahim Hamisi (Mnubi), Mzee bin Sudi (Mmanyema), Sheikh Mohamed Ramiyya (Mmanyema), Saadan Abdu Kandoro (Mmanyema), Iddi Tosiri, (Mmanyema) Denis Phombeah (Mnyasa), Dome Budohi, (Mkenya), Rashid Kheri Baghdelle (Mnubi), Aoko (Mkenya), TANU Tabora ilijaa Wamanyema wengi sana.

Nimekuonyesha majina machache ili uwajue Watanganyika ambao baadae wakawa Watanzania.

View attachment 2650670
Babu yangu Salum Abdallah (mshale) mmoja wa waasisi wa TANU Tabora Mmanyema na kulia kwake ni Kasanga Tumbo Mnyamwezi na viongozi wengine wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee wangu Said, huchoki na ngonjera za wapigania Uhuru? John Okelo alishiriki mapinduzi kule Zanzibar, je, nae ni Mzanzibar? Swala hapa si kuasisi chama wala kupigania Uhuru, hisipokuwa ni kwamba kuna Watanzania wenye asili ya Wamanyema wa Kongo. Kuwa Mmanyema hakuwezi kukuondoleeni Utanzania wenu kama ilivyo kwa Wamasaai, wako Kenya na wengine Tz, Wamakonde, Wajaruo nk.

Issue kubwa hapa ni maudhui ya vitabu mnavyoviandika. Kama vinahubiri udini na chuki bora usitueleze hapa jf, kaelezaneni uko misikitini. Title tu ya kitabu chenyewe na aina ya uwasilishaji wa maelezo yako, vinatosha kujua nini kimeandikwa ndani ya hiki kitabu. Yaleyale.......kama kawaida yenu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom