Kitabu Kipya: "Waliopotezwa Tanzania " Mwandishi: Sheikh Ponda Issa Ponda

Wakongo gani waliouzwa Zanzibar?
Unaweza kuwatambua?

Tatizo lako ni Waarabu tu?
Unaijua vizuri historia ya Zanzibar?

Huna tatizo na Wahindi Zanzibar?
Unajua kwa nini nimekuongezea Muhindi?

Ikiwa wewe ni mjuzi wa siasa za Zanzibar haraka utakuwa ushatambua kuwa umejiingiza mwenye dema sasa hujui utatokea njia gani.
Maalim siwezi kukupinga kuhusu historia, kuna mengi nimejifunza kutoka kwako, naomba utufahamishe hata kwa uchache kuhusu Wahindi Zanzibar
 
Akiwa mtu mkongomani alafu tena mrundi akawa mwenzake vipi? wewe utakuwa ndo wale wale wanyarwanda
Hapana mie ni mtanzania wa kawaida. Sina tatizo na mataifa mengine ila waache kuja na uchafu toka kwao hasa uchochezi na uchonganishi.
 
Jabulani,
Labda nikuulize.

Vipi migodi ya dhahabu wanayo Waarabu?
Mbona uko kimya?
migodi iliuzwa na rais mtanganyika hatuwezi kulalamika Sana, ila sasa rais mzanzibari anauza rasilimali za Tanganyika hauzi za Zanzibar, na kila kitu kwa waarabu wajomba zake, lazima tupaze sauti, anapiga mnada Tanganyika.
Katiba mpya mambo ya mapato ya Tanganyika yaamuliwe na Watanganyika. Tusiumizwe kwa sababu wazanzibari wachache wamepewa rushwa na waarabu
 
Kwa nini unatumia neno, "Waarabu," badala ya Dubai?

Wewe una chuki?
Sina haja ya kukuuliza usahihi wa taarifa zako.

Hili utalifahamu taratibu kila siku zitakaposonga mbele.
 
Maalim siwezi kukupinga kuhusu historia, kuna mengi nimejifunza kutoka kwako, naomba utufahamishe hata kwa uchache kuhusu Wahindi Zanzibar
Jabulani,
Zanzibar imetawaliwa na marais wawili ambao wamechanganya damu mmoja ya Kihindi na Mwingine Kiarabu.

Katika uteuzi wao ndani ya CCM hakuna yeyote aliyegusa asili za wagombea hawa hadi wakachaguliwa na Wazanzibari kuwa marais.

Hiyo ndiyo Zanzibar toka enzi na enzi.
Sasa unapoleta ubaguzi wa rangi kwa kuangalia Waarabu kuonyesha chuki...
 
Hiiyo ni geresha bwege. Anaitumia kama uchochoro kubaki relevant na kuendeleza uchonganishi wake. Uzuri ni kwamba Ukonga siku zote kupo atapata anachotafuta as soon as possible. Kwanini wasimrudishe kwao DRC
Father...
Nakushauri usome kitabu kwanza ujue kilichoandikwa baada ya kusoma ikiwa utaona ipo haja unaweza ukaleta hoja zako hapa zijadiliwe.

Sheikh Ponda hata mimi kanishangaza.
Kalamu yake ni nzuri.

Hiki ni kitabu chake cha pili na kama cha kwanza ukianza ukurusa wa kwanza hutokiweka chini hadi umekimaliza.

Kama kurudishwa Congo si Sheikh Ponda peke yake.
Hata mimi ni Mmanyema nirudishwe.

Wajukuu wa Mzee bin Sudi warudishwe Congo.
Huyu ni Mmanyema muasisi wa African Association 1929 iliyokuja kuzaa TANU 1954.

Wajukuu wa Iddi Faiz Mafongo huyu Mmanyema ndiye alikuwa Mweka Hazina wa TANU 1954 na ndiye aliyekusanya fedha za safari ya Julius Nyerere UNO 1955 wajukuu zake wapo nao warudishwe.

Nimeweka hapa picha ya Wamanyema wanne wako na Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru wajukuu zao wapo Tanzania watafutwe warudishwe Congo.

Sijataka kukutajia wajukuu wa Wazulu, Wanubi na Wanyasa ambao wako Tanzania hadi hii leo.

Ndugu yangu huu ubaguzi kakufunza nani?

1686282918794.png

Aliyesimama kulia kwa Julius Nyerere ni Iddi Faiz Mafongo uwanja wa ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955.​
 
Hapana mie ni mtanzania wa kawaida. Sina tatizo na mataifa mengine ila waache kuja na uchafu toka kwao hasa uchochezi na uchonganishi.
Father...
Wewe ni Mtanzania wa kawaida.
Tuanze na Watanganyika wa kawaida.

Waasisi wa harakati za kupigania Tanganyika alikuwapo Kleist Sykes (Mzulu), Ibrahim Hamisi (Mnubi), Mzee bin Sudi (Mmanyema), Sheikh Mohamed Ramiyya (Mmanyema), Saadan Abdu Kandoro (Mmanyema), Iddi Tosiri, (Mmanyema) Denis Phombeah (Mnyasa), Dome Budohi, (Mkenya), Rashid Kheri Baghdelle (Mnubi), Aoko (Mkenya), TANU Tabora ilijaa Wamanyema wengi sana.

Nimekuonyesha majina machache ili uwajue Watanganyika ambao baadae wakawa Watanzania.

1686283843750.png

Babu yangu Salum Abdallah (mshale) mmoja wa waasisi wa TANU Tabora Mmanyema na kulia kwake ni Kasanga Tumbo Mnyamwezi na viongozi wengine wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

View attachment 2650670
Babu yangu Salum Abdallah (mshale) mmoja wa waasisi wa TANU Tabora Mmanyema na kulia kwake ni Kasanga Tumbo Mnyamwezi na viongozi wengine wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hubadiliki dogo. Kila siku ngonjera ile ile. Wimbo ule ule vibwagizo vile vile wakati dunia inasonga mbele. Najua wewe na Ponda ni watu wenye udini na uchochezi vinavyonuka au kiwango cha lami so to speak. Hivyo, sina ninachoambua hapa. Sorry about saying so my dear son
 
Father...
Nakushauri usome kitabu kwanza ujue kilichoandikwa baada ya kusoma ikiwa utaona ipo haja unaweza ukaleta hoja zako hapa zijadiliwe.

Sheikh Ponda hata mimi kanishangaza.
Kalamu yake ni nzuri.

Hiki ni kitabu chake cha pili na kama cha kwanza ukianza ukurusa wa kwanza hutokiweka chini hadi umekimaliza.

Kama kurudishwa Congo si Sheikh Ponda peke yake.
Hata mimi ni Mmanyema nirudishwe.

Wajukuu wa Mzee bin Sudi warudishwe Congo.
Huyu ni Mmanyema muasisi wa African Association 1929 iliyokuja kuzaa TANU 1954.

Wajukuu wa Iddi Faiz Mafongo huyu Mmanyema ndiye alikuwa Mweka Hazina wa TANU 1954 na ndiye aliyekusanya fedha za safari ya Julius Nyerere UNO 1955 wajukuu zake wapo nao warudishwe.

Nimeweka hapa picha ya Wamanyema wanne wako na Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru wajukuu zao wapo Tanzania watafutwe warudishwe Congo.

Sijataka kukutajia wajukuu wa Wazulu, Wanubi na Wanyasa ambao wako Tanzania hadi hii leo.

Ndugu yangu huu ubaguzi kakufunza nani?

View attachment 2650662
Aliyesimama kulia kwa Julius Nyerere ni Iddi Faiz Mafongo uwanja wa ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955.​
Kumbe wale wale. Mnaweza kujirudisha ili kuepuka kututia hasara kuwagharimia kurejea kwenu
 
Mtu kaona fursa hapa. Mbona hajaandika waaarabu wajerumani walipoteza wangapi lakini hapa Tanzania.
Na wajinga wapo watakaonunua utadhani hakuna nchi ama raisi asiyepoteza weenye kukifanya wanajua kuongea ama mdomo wao unawasha
Na wajinga wengi watakinunua hasa wale wanaopenda umbea wa udini na chokochoko
 
Huyu mkongomani ni mchonganishi na msaka tonge kama yule mrundi mwenzake Khalifa Hamis. Ni bahati mbaya hata hao waarabu wenzao wanawaunga mkono katika uchonganishi wao wasijue kikinuka wana kwao pa kwenda
Khalifa khamisi ana silaha ya moto kitambo,pengine ni kitengo
 
KITABU KINGINE CHA SHEIKH PONDA KIMEZINDULIWA: WALIOPOTEZWA TANZANIA.

Katika kipindi cha miaka mitatu nimekuwa nikipokea vitabu kutoka kwa waandishi wakiniomba nifanye pitio yaani, "book review," kwa nia ya kuvitambulisha vitabu hivi kwa wasomaji na wananchi kwa jumla.

Kitu kinachojitokeza kwa haraka na wazi katika vitabu hivi ni kuwa hivi si vitabu vya kawaida.

Hivi vyote ni vitabu vya kuogofya.
Hivi ni vitabu vya kutisha.

Si vitabu utakachosoma na moyo wako ukawa umetulia.

Hivi ni vitabu unasoma na moyo ukabadilisha mapigo ukawa unadunda kwa haraka.

Hivi ni vitabu vilivyojaa simanzi kila ukurasa unaopindua.
Vitabu vya aina hii si vyepesi kuviandikia pitio ingawa pitio limeandikwa lipo.

Kuna msomaji mmoja alisoma pitio langu la moja ya vitabu hivi vinavyotisha.
Kamaliza pitio langu hakukuta maelezo ya kitabu kinasema nini.

Kahamaki akaniandikia, "Hivi vitisho vya nini tueleze mwandishi kaandika nini?"

Tayari nilikuwa nishawaweleza wasomaji kuwa wasome kitabu waone wenyewe yaliyomo ndani ya kitabu hicho.

Lakini kinyume na wasomaji waandishi wa vitabu hivi wote wameniandikia kunishukuru kwa kufanya pitio la kitabu chake na kuniambia kuwa nimetenda haki kwa kalamu zao.

Ninachoweza kusema kuhusu kitabu hiki cha Sheikh Ponda, "Waliopotezwa Tanzania," ni kuwa kitabu hiki kinatisha sana.

Swali linalozunguka akilini kwangu ni imekuwaje kuwa Tanzania vitabu vyake muhimu kutoka kwa baadhi ya waandishi wake vimekuwa vitabu kurasa zake zinachuruzika damu?

Kitabu hiki kinauzwa Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue na maduka ya vitabu ya Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani.

Bei ya kitabu ni T. Shs: 10,000.00.
Ni muhimu sana hizi kumbukumbu zikaishi hadi kizazi na kizazi ili makosa yasirudiwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom