FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,211
Sasa wewe unaniuliza mimi Mbatu nitashidwaje kujua maana ya BANTU ikiwa neno lenyewe ni la Kibatu umekunywa nini leo au bado una search ktk site kujua maana yake?. Bantu, Abantu ni WATU nalitumia sana katika lugha yangu.. Wewe uliye mwarabu kwa kiarabu maana yake nini?
Unajua kuna Myahudi mmoja hapa niliwahi bishana naye akisema Waarabu they are Anti Semitics, nikamuuliza kwani Waarabu sio jamii ya Semitics, akajibu ooh they are. Nikamuuliza kwa nni Semitics imekuwa leo ni Wayahudi tu sio WATU wote wenye asili hiyo? tukabisha wee nikamwona mpuuzi tu. Ndio haya...
Kwanza kabisa mimi si Mwarabu. Bali nnakijuwa Kiarabu - Kumbuka hilo. Halafu kama umenisoma vizuri post zangu nimeelezea juu huko ni nini maana ya Arab au Waarabu. Rudi, unaonesha amma husomi tunachojadili amma una kumbukumbu finyu.
Halafu nnafurahi sana kuwa unajuwa maana ya Abantu kuwa ni watu, Wallahi nimefurahi sana kwani inaonesha labda unajuwa kweli maana ya Bantu ila inakuwa vigumu sana kwako kukiri na au kuielezea au hauijuwi na unakisia tu. Kwani umeilezea nusu maana tu tena umeitoa nilivyouliza mimi "Bantu" ukaiongozea "A"bantu". Hiyo inaitwa "manipulation".
Jee hukusoma juu nimekuwekea kipande kutoka Makerere University wanavyofundisha chuoni hapo maana ya Bantu? naomba urudi ukasome ujuwe maana sahihi ya Bantu, unaweza kuwa ni Mbantu lakini pengine maana ya Bantu huijuwi.