Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Kapwila...
Kuna kitu nimekiona nimeona nikurudie nikuonyeshe ili upate yakini
kuwa kitabu changu kilikuja na taarifa muhimu sana katika historia
ya uhuru wa Tanganyika.

Soma hapo chini:

Haya ninayoweka hapo chini nimetoa katika kitabu changu kuhusu:

''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold
Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,
'' Minerva Press, London 1998.​

''In June, TAA headquarters announced its executive committee
with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President;
J.P. Kasella Bantu, General Secretary;
Alexander M. Tobias and
Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were
Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z.
James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1] The composition
of the TAA leadership showed East African solidarity that existed
during the struggle for independence. Kenyan patriots were elected
as office bearers side by side with Tanganyikans. It is said that it
was about that time, in the last months of 1953, that Abdulwahid
talked to Nyerere seriously about forming an open political party to
replace TAA.''​

Kapwila,
Huyu Alexander M. Tobias alifukuzwa chama kwa usaliti katika mkutano
wa kuunda TANU July 1954 kwa sababu alichukua majalada ya TAA
akawapa Special Branch.

Habari hizi alinipa marehemu Mzee Germano Pacha mmoja wa wale
waasisi 17 wa TANU.

Kapwila,
Bado unaamini kitabu hiki ni cha kupuuzwa?​

[1]Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
Mohamed Said ni ukweli ulio wazi kwamba Historia inaweza kuthibitisha chochote kutegemea na yule anayetafiti na malengo pamoja na msukumo ulioko moyoni mwake
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said ni ukweli ulio wazi kwamba Historia inaweza kuthibitisha chochote kutegemea na yule anayetafiti na malengo pamoja na msukumo ulioko moyoni mwake
Nkwesa...
Hilo usemalo si kweli.
Wewe uliyajua haya kabla?

Msukumo wa moyo ungekuwa ndiyo wa kuamua basi tungebaki na historia
ya TANU ya Chuo Cha Kivukoni.

Usitishike ni historia tu niliyoelezwa na wazee wangu.
Huenda wale waliokuja TANU baadae hawakuyajua haya.
 
Kwa kuwa umeambiwa na wazee wako na kuamini na mwingine atakuja kuambiwa na wazee wake akaamini na yale mliyoambiwa wote na wazee tofauti na nyakati tofauti kila mmoja ataamini ya wazee wake ni kweli kutegemea nini alitaka kuamini au kuaminishwa.

Nimesema Historia MTU anaweza kuthibitisha chochote. Kama huutaki ukweli huo kwa kuwa umetengeneza habari ya kihistoria na hutaki watu waitilie Shaka kwa kujua ukweli kwamba si kila kitu kisemwacho ndiyo historia isemavyo ni cha kweli sawa.
Lakini ukikataa kuwa ninaongopa ninaposema kwamba kwa kutumia historia binadamu anaweza kuthibitisha chochote anachotaka watu waamini, nakuwa sikuelewi kwa kuwa najua wewe ni msomi na Una exposure ya kutosha kujua hili.
 
Faiza, nimekundikia mtiririko mzima ili kukurahisishia; nikiandika nambari za post itakupotezea muda wa kutafuta. Hebu kanusha, au kuna mtu ametumia ID yako?

Vv

Kwa kuwa sitaki kwenda huko unapopataka, jibu langu hapo juu limejitosheleza, ukitaka maelezo zaidi na kujadili hilo, funguwa nyuzi yake.
 
Sadoliki,
Usiulize vyeti vya Maalim Faiza.
Inaelekea wewe ni mgeni hapa Majlis.

Faiza kajipambanua sana kama msomi makini si wa vyuo alivyosoma akiwa
keshakua bali hata vile vyuo alivyosoma akiwa na miaka 5/6.

Fanya utafiti mdogo.
Rejea nyuma humu Majlis soma michango yake utamjua.

Hapa Majlis ukileta habari ya vyeti utatufukuza wengi ingawa hatuna vyeti lakini
kwa kweli kwa namna yetu tunachangia kama mnavyochangia wasomi kama wewe
wenye vyeti.

Mtu hafukuzwi hapa barzani kwa kukosa cheti wala hakatazwi kuchangia kwa kukosa
cheti.
Kaka mohammed with all respect to you, i believe mtu anaye waambia wenzio "unazungumza pumba" "acha ujinga" "wewe ulisoma kweli" kwangu mimi siyo sign ya good and progressive conversation, i believe kama wewe katika honest dilagoeus hata kama sikubaliani, siyo kupondana kwa speliing mistakes au kama above, which to me is a sign of inferiority complex
 
Lugha ni lugha inaweza kuongelewa na watu wasokuwa waarabu, na sio kweli kuwa asili ya Waarabu wote wanaongea kiarabu toka kina Ismail, mtu mweusi huwezi kuwa mwarabu kwa asili unachanganya sana. Hivyo usiliseme kabila kuwa ndio asili ya watu maana hata WaTutsi wanaongea lugha ya Kibantu japo sii Wabantu.

Hapo umejichanganya sana. Mara lugha mara rangi.

Unafanya kusudi kujichanganya ili utuchanganye wote au ni upeo tu?

Tuanze na lugha:

Kiarabu ni lugha ya Waarabu, ikitokea mwengine ambae si Mwaarab kukiongea basi haimaanishi na yeye kawa Mwaarabu.

Kama vile wewe ukivaa tai na koti na kucharaza Kingereza hakukufanyi uwe Mwingereza.

Hebu jisomee kidogo kuhusu Waarabu labda utawaelewa:

Arabs (Arabic: عرب‎, ʿarab) are a major panethnic group.[SUP][14][/SUP] They primarily inhabit Western Asia, North Africa, parts of the Horn of Africa, and other areas in the Arab world. Arabic-speaking populations in general are a highly heterogeneous collection of peoples, with different ancestral origins and identities. The ties that bind the Arab peoples are a veneer of shared heritage by virtue of common linguistic, cultural, and political traditions. As such, Arab identity is based on one or more of genealogical, linguistic or cultural grounds,[SUP][15][/SUP] although with competing identities often taking a more prominent role,[SUP][16][/SUP] based on considerations including regional, national, clan, kin, sect, and tribe affiliations and relationships. If the Arab panethnicity is regarded as a single population, then it constitutes one of the world's largest groups after Han Chinese.

The Arabian Peninsula itself was not entirely originally Arab. Arabization occurred in some parts of the Arabian Peninsula. For example, the language shift to Arabic displaced the indigenous South Semitic Old South Arabian languages of modern-day Yemen and southern Oman. These were the languages spoken in the civilisations of Sheba, Ubar, Magan, Dilmun, and Meluhha-which were spread via migrants from the Arabian peninsula, together with written script, in the 8th and 7th centuries BC to the Horn of Africa (Ethiopia, Eritrea, Djibouti, and Somalia).

Chanzo: Arabs - Wikipedia, the free encyclopedia

Hapo ni crystal clear, sijuwi hapo kama kuna cha kujadili zaidi kuhusu Waarabu?
 
Kaka mohammed with all respect to you, i believe mtu anaye waambia wenzio "unazungumza pumba" "acha ujinga" "wewe ulisoma kweli" kwangu mimi siyo sign ya good and progressive conversation, i believe kama wewe katika honest dilagoeus hata kama sikubaliani, siyo kupondana kwa speliing mistakes au kama above, which to me is a sign of inferiority complex

Ukija na pumba usiambiwe?

Ukiwa unaambiwa Mbantu kahamia Afrika ya Mashariki na kakuta wenyeji na unaoneshwa historia za wana historia waliobobea na wewe bado unabisha tu bila ushahidi wowote, basi kwa kuwa unaamini tu ulichofundishwa cha kujazwa ujinga.

Hakuna mahala nimeuliza "wewe ulisoma kweli?", huwa nnauliza, jee shule ulienda kusomea ujinga? kumbuka hilo.
 
Ukija na pumba usiambiwe?

Ukiwa unaambiwa Mbantu kahamia Afrika ya Mashariki na kauta wenyeji na unaoshwa historia za wana historia waliobobea na wewe bado unabisha tu bila ushahidi wowote, basi kwa kuwa unaamini tu ulichofundishwa cha kujazwa ujinga.

Hakuna mahala nimeuliza "wewe ulisoma kweli?", huwa nnauliza, jee shule ulienda kusomea ujinga? kumbuka hilo.
you are trying to write history, with semantics, haiwezekani hata kama ulizqaliwa kariakoo, justification ya kuwa mtu wa kutoka kenya kahamia tanga na kawakuta wenyeji waarabu ni theory yako na wenzako unewajua , kwangu mimi it make no sense na sitaki kupoteza muda ku argue on it, people might not notice the difference
 
Jee, umekisoma kitabu Tanzania na Propaganda za udini cha Professor Ibrahim Noor Shariff?
 
Umechanganya mambo mengi sana mpaka nnashindwa ku "concentrate", sasa kama hautaki kujuwa North na South na wanahistoria walioboobea wanatumia "terminology" hiyo itakuwa wewe huna haja ya kujuwa asili za watu bali unataka ubishi wa kijinga.

Hilo la Makabila ya kibantu kufika 1,000 si muhali hata yakifika 2,000 lakini Wabantu watabaki kuwa Wabantu na Watabaki kuwa Walikuja Afrika ya Mashariki.

Unajuwa maana ya Bantu?

Nnakuwekea hizo "proofs" usome mwenyewe ili usije ukauliza "source". Hakuna aliyezaliwa anajuwa kila kitu, tunasoma, tunajifunza, tunajuwa, unless uwe ni mjinga wa kuzaliwa ndiyo utakataa kusoma waanazuoni waliobobea fani zao na proofs zao, unaweza kuwapinga walichoandika ukaja na chako chenye mashiko zaidi lakini huwezi kuwacha kuwasoma waliyoyaandika watu wengine. Sidhani kama wewe uko huko.

Nnankushangaa sana unapoona kuwa ni kituko mimi kuweka links za maandiko ya wanahistoria ujisomee mwenyewe ili yakuingie.

Unajaribu kufanya "character assassination" ya kijinga. Hunipati huko.
Unajua wewe unachekesha sana yaani unauliza maswali ambayo majibu yake unayatoa Google. Unauliza kuhusu Iraqw wakati wewe mwenyewe unatoa majibu yako Google,halafu unaona umeuliza swali gumu sana watu wanapokupuuza..

Hapa hatushindani, nimekuuliza tu vizuri na ushahidi wako wa Google ya kwamba Ikiwa hayo makabila (Sandawe na Baruge) ulodai kwamba ndiyo Makabila yenye asili ya Tanganyika, nilipokuuliza kama makabila hayo sio Wabantu ukanionyesha sio kwa sababu Asili yao wametoka North na South ina maana hata wao sio wenye asili ya Tanganyika.

Na kutoka North au South haina maana sio Wabantu ikiwa wewe unaamini Wabantu walitoka West Afrika iweje kutoka South au North sio wabantu. Huoni kama unajichanganya, huku unakubali hiki huku unakataa kingine chenye maana ile ile. Ni record gani inaonyesha West Afrika kulikuwa na Wabantu kabla ya Tanganyika na ndio asili yao isiwe Waarabu pia maana unawapenda sana.

Sasa kwa wewe msomi tuambie kina nani wenye Asili ya Tanganyika maana hata hao Wa Iraqw ambao ni Wambulu ambao pia ni Wahamiaji kutokana na asili yao ya wachungaji kuhama kutafuta nchi za malisho ya mifugo yao. Na kuhusu waarabu wewe mwenyewe umeweka kipande hicho hapo juu na kimesema nini baada ya highlight yako kuwa:- Arab Identity is based on one or More genealogical, Linguistic or Cultural.

Sasa wewe unataka kunambia mwarabu ambaye hajui kiarabu sio Mwarabu maana hapa Canada wapo wengi tu. Na hata watoto wa kibantu wasojua lugha hata moja ya Kibantu. Wajamaica, Wahaiti, Wamarekani weusi hawa ni wa asili gani? Wapo waswahili hapa hapa Dar hawajui hata lugha moja zaidi ya kiswahili hawa wana asili gani?

Hakuna record yeyote iliwahi kuonyesha Wabantu sio wenyewe wa Tanganyika kwa sababu Tanganyika sio Manyara wala Arusha peke yake na haiwezekani kabila dog lilohamia likawa ndio kabila kubwa Tanganyika pasipo kupigana vita na kuwaua wenyeji.

Na halafu kumbuka waloipa Zanzibar jina la ZenjBar sio Wa Oman wala Saudia ila Washihir, Washiraz na Waburush walokuja kwanza kabisa kufanya biashara ya viungo, dhahabu na vito. Kwa hiyo huwezi kutumia lugha moja kutafsiri neno kwa sababu wewe unakijua kiarabu cha Karne ya 21. Your very wrong na wewe pitia hapa:- The name Zanzibar came from a combination of two Arabic words, 'Zinj', meaning black, and 'barr', being the Arabic word for land, the result meaning 'Land of the Blacks'.
 
Mohammed Said,
Mimi nakukubali sana katika maelezo yako wala sii kwamba hakuna ukweli wowote isipokuwa Historia ya Nchi huandikwa WATU walohusika na kwa minajiri gani. Kama ni UHURU wa Tanganyika kina AbdulWahid hawakuutaka UHURU wa Waislaam wa Tanganyika isipokuwa UHURU wa WATU wote wa Tanganyika haikubagua dini wala Kabila. Kwa hiyo unapoandika kuhusu wazazi wako ungewataja tu majina yao na michango yao, basi kitabu chako kingepata sifa kubwa sana nchini pengine hata kusomwa mashuleni.

Kosa ullifanya ni kupeleka Udini zaidi ya kuonyesha michango yao isipokuwa mchango wa Uislaam katika Uhuru wa Tanganyika kiasi kwamba ukawaweka hata watu walopingana na TANU juu ya Uhuru wa Tanganyika kina Takadir na AMNUT kuwa katika mashujaa walosahaulika. Kama kweli kweli waislaam walitaka Uhuru wao basi wangekiunga chama hiki cha AMNUT mkono badala ya TANU kilichochanganyikana na watu wa makabila mbali mbali.

Kwa nini unapenda sana kumshusha Nyerere pamoja ya yote alotutumikia? kwa sababu Mkristu au kwa sababu wazee wako hawakupewa nafasi. Mzee Ali Sykes hadi anatutoka alikataa siasa kabisa yeye mwenyewe na historia inatuonyesha wazee wengi waliacha siasa baada ya kutimiza wajibu wao wakafanya biashara zao.

Wewe ni mwandishi mzuri sana na unajua kuzitafuta habari lakini unakumbwa na hili jinamizi la Udini ambalo kama nilivyokwambia wazungu wanapenda sana kuwasoma watu kama wewe kwa sababu wanajua upeo wa fikra zako na utaweza kuwa hatari kiasi gani. Na katika hali kama ya leo ya Ugaidi unaweza kuwepo katika list ya watu wanaotazamwa sana kwa sababu wanaamini watu kama wewe ni hatari na je umeweza vipi kuwalaghai wengine kuwajaza chuki dhidi ya wakristu au watu wengine.

Haya yalifanyika sana Uingereza wakiwaachia masheikh wakizungumza wazi Trafalgar Square, kumbe wakiwachunguzana kuchukua picha za watu wanaohushulia mara kwa mara mihadhara ile, Ilipoanza tu habari za Ugaidi wakakusanywa hata wasokuwemo na kwa sababu kama hizi usidhani unafanya la maana sana ikiwa ncjhi yako yenyewe kitabu chako kimepigwa marufuku. Think big mkuu wangu nakuasa tu.
 
Mkandara,
Niwie radhi.
Hilo "kosa" ni hukumu ya nani?

Wanahistoria gani waliochambua kitabu changu na kukuta kuna makosa?

Nani kakuambia kuwa kitabu changu hakina "sifa kubwa?"
Nani kakuambia kuwa niliandika ili kitabu kisomwe shule?

Hivi unajua kuwa nina kitabu "The Torch on Kilimanjaro" (2007)kimechapwa
na Oxford Unnversity Press (OUP), Nairobi kwa ajili ya shule za Tanzania.

Hivi unajua nini kimetokea kuhusu kitabu hiki?
Kimepigwa "conspiracy of silence."

Usinambie kuwa OUP wanachapa kitabu ndani kina udini.
Hakisomeshwi shule za Tanzania lakini kinasomeshwa Kenya na Uganda.

the%20torch%20on%20kilimomanjaro.jpg

Nani kakuambia kama kitabu cha Abdul Sykes kina udini?
Unaweza kuonyesha huo udini ulipo?

Unataka niamini kuwa walopotosha historia ya TANU walikuwa
wanaongozwa na udini wao?

Wapi nimemshusha Nyerere.
Nionyeshe kwenye kitabu changu mahali nilipomshusha.

Nami nakuahidi In Sha Allah nitarejea hapa Majlis kukupa jibu.

Nani alikwambia wazee wangu walitoa mali na nguvu zao katika
TANU ili wapewe nafasi?

Unajua utajiri alokuwanao Dossa Aziz?
Mdini nani?

Umemsoma Bergen (1981) na Sivalon (1992)?
Unajua kwa nini kitabu cha Njozi (2002) kilipigwa marufuku?

Hawa ndiyo waloeleza nani mdini.
Panapofanyika mazungumzo si Trafalgar Square bali ni Hyde Park.

Mimi sina taarifa kuwa kitabu changu kimepigwa marufuku.
Nenda Tanzania Publishing House (TPH) kipo pale kinauzwa.

Unaniasa mimi.
Unaniasa kwa lipi?

Hivi unajua Taifa lilipoamua kutoa medali kwa Abdul Sykes na mdogo
wake Ally baada ya kuwapuuza kwa miaka 50 unajua "text" iliyosomwa
viwanja vya Ikulu kwenye sherehe ilitoka wapi?

Acha kujitisha na kuwatisha wengine.
Nilichoandika ndiyo ukweli wenyewe.

Kama kuna msomi yeyote anaona mimi nimesema uongo na aandike
kitabu chake aeleze ukweli.

Mimi nimeandika baada ya kusoma historia ya TANU iliyoandikwa na
Chuo Cha Kivukoni.

Historia ile imepotoshwa pakubwa na kukosewa mwisho wa kukosewa ndipo
nikaandika hii historia kama nilivyokuwa nikiwasikia wazee wakihadithia.

''The Torch on Kilimanjaro''

''The Torch on Kilimanjaro'' Kitabu Kilichofitiniwa Kisiingizwe Katika Mtaala wa Shule za Msingi za Tanzania

20140104_205335.jpg

Aliyesimama juu ya boneti ya Land Rover akihutubia wananchi ni Mwalimu Nyererena picha ya pembeni ni
Nyerere na Kenyatta.

20140104_122755.jpg

Mwandishi akitoa maelezo kuhusu kitabu "The Torch on Kilimanjaro."

20140104_115839.jpg
Mohamed Seif Khatib katika Uzinduzi wa Kitabu, ''The Torch on Kilimanjaro''
Kilimanjaro Kempinski Hotel kulia kwake ni Sheikh Abdillah Nassir

5npAjxqx_GzvDTbRG-IwdF5kg_LJr6O9mM4hw7zuGeqm=w773-h541-no
Mwalimu akikiangalia kitabu

20140113_171728+%25281%2529.jpg

20140113_171810.jpg

20140113_171839.jpg

20140113_171902.jpg

''The Torch on Kilimanjaro,'' ni kitabu kilichochapwa na Oxford University Press (OUP) Nairobi.

Kitabu hiki kilikuwa katika mradi wa kuchapa vitabu kwa ajili ya shule za msingi madhumuni yakiwa ni kumsomesha mwanafunzi lugha ya Kiingereza na wakati huo huo ajifunze na historia ya nchi yake ili kujenga uzalendo.

Waandishi kutoka Afrika ya Mashariki waliandika vitabu kiasi ya 15 isipokuwa Tanzania.

OUP walimfuata mwandishi na kumuomba aandike kitabu kimoja ili angalu Tanzania na wao wawemo katika orodha ya nchi zilizoshiriki katika mradi ule wa kusomesha lugha ya Kiingereza Afrika ya Mashariki.

Mwandishi akapeleka mswada Nairobi.
Baada ya muda alikwenda Nairobi kuonana na mhariri ili kurekebisha mswada.

Mhariri akasafiri hadi Dar es Salaam baada ya kupata marekebisho na kazi ikakamilika.
Kitabu kikachapwa.

OUP wakafanya dhifa kubwa sana ya kukizindua kitabu Kilimanjaro Kempinski Hotel ambako wakuu wa Wizara ya Elimu walikaribishwa pamoja na vyombo vya habari.

Mgeni wa heshima alikuwa Mohamed Seif Khatib.

Waalikwa wote walipewa nakala moja ya kitabu na mwandishi alikieleza kitabu mbele ya hadhira ile.

Kwa upande wao OUP walikisifia kitabu kile kuwa kitachangia katika watoto wa shule za msingi kujifunza Kiingereza na historia ya nchi yao hususan historia ya Mwalimu Nyerere alipoanza kudai uhuru wa Tanganyika mwaka 1954 hadi uhuru ulipopatikana mwaka 1961.

Aliposhuka tu kutoka kwenye jukwaa watu wa televisheni na magazeti wakamzunguka kumhoji kuhusu kitabu kile.

Tanzania kitu chochote kinachomuhusu Nyerere kinauzika.

Mwandishi na mchapaji OUP walitegemea makubwa kutoka kitabu kile.
Haikuwa hivyo.

Kitabu hiki kimepigwa chenga kuanzia mwaka 2007 licha ya juhudi nyingi za OUP kuwaandikia Wizara ya Elimu kuwaomba wakiingize katika mtaala wa kusomesha lugha ya Kiingereza.

OUP walimweleza mwandishi kuwa wao hawajui kwa nini kitabu hiki chenye historia ya Mwalimu Nyerere hakitakiwi wakati kule Kenya kitabu cha Jomo Kenyatta ''The Kapenguria Six'' kilicho katika mradi huu kipo katika mtaala wa shule za msingi na kinasomeshwa.

36-alfred-eisenstaedt-kenya-story-mau-mau-leader-jomo-kenyatta-posing-with-five-of-his-staff-members-during-trial.jpg

The Kapenguria Six

Mswada mpya 'The School Trip'' ambao mwandishi aliwapa OUP na wakaupokea kwa ajili ya uchapaji baada ya kuona uzuri wa kitabu kile cha kwanza, OUP wameghairi kukichapa kitabu na maelezo ni kuwa mwandishi hauziki nchini kwake lau kama ana kipaji cha uandishi wa hadithi za watoto.

Hata hivyo OUP walimshirikisha mwandishi katika mradi mwingine kwa ajili ya vitabu Afrika ''The Mermaid of Msambweni and Other Stories'' (2007) kitabu cha mkusanyiko wa waandishi kutoka nchi tofauti za Afrika Tanzania ikiwakilishwa na mwandishi huyu.

OUP wala hawakushughulika kukitangaza kitabu hiki hapa Tanzania.Ndiyo maana husikika minong'ono kuwa kuna kitu katika uendeshaji wa serikali kinaitwa ''Mfumokristo.''

Huu mfumo inasemekana una watu wake unaowapenda na kuwatumikia.
Je, Wizara ya Elimu ni moja ya taasisi zinazoongozwa na ''Mfumokristo?''

DSC04002.JPG
 
Unajua wewe unachekesha sana yaani unauliza maswali ambayo majibu yake unayatoa Google. Unauliza kuhusu Iraqw wakati wewe mwenyewe unatoa majibu yako Google,halafu unaona umeuliza swali gumu sana watu wanapokupuuza..

Hapa hatushindani, nimekuuliza tu vizuri na ushahidi wako wa Google ya kwamba Ikiwa hayo makabila (Sandawe na Baruge) ulodai kwamba ndiyo Makabila yenye asili ya Tanganyika, nilipokuuliza kama makabila hayo sio Wabantu ukanionyesha sio kwa sababu Asili yao wametoka North na South ina maana hata wao sio wenye asili ya Tanganyika.

Na kutoka North au South haina maana sio Wabantu ikiwa wewe unaamini Wabantu walitoka West Afrika iweje kutoka South au North sio wabantu. Huoni kama unajichanganya, huku unakubali hiki huku unakataa kingine chenye maana ile ile. Ni record gani inaonyesha West Afrika kulikuwa na Wabantu kabla ya Tanganyika na ndio asili yao isiwe Waarabu pia maana unawapenda sana.

Sasa kwa wewe msomi tuambie kina nani wenye Asili ya Tanganyika maana hata hao Wa Iraqw ambao ni Wambulu ambao pia ni Wahamiaji kutokana na asili yao ya wachungaji kuhama kutafuta nchi za malisho ya mifugo yao. Na kuhusu waarabu wewe mwenyewe umeweka kipande hicho hapo juu na kimesema nini baada ya highlight yako kuwa:- Arab Identity is based on one or More genealogical, Linguistic or Cultural.

Sasa wewe unataka kunambia mwarabu ambaye hajui kiarabu sio Mwarabu maana hapa Canada wapo wengi tu. Na hata watoto wa kibantu wasojua lugha hata moja ya Kibantu. Wajamaica, Wahaiti, Wamarekani weusi hawa ni wa asili gani? Wapo waswahili hapa hapa Dar hawajui hata lugha moja zaidi ya kiswahili hawa wana asili gani?

Hakuna record yeyote iliwahi kuonyesha Wabantu sio wenyewe wa Tanganyika kwa sababu Tanganyika sio Manyara wala Arusha peke yake na haiwezekani kabila dog lilohamia likawa ndio kabila kubwa Tanganyika pasipo kupigana vita na kuwaua wenyeji.

Na halafu kumbuka waloipa Zanzibar jina la ZenjBar sio Wa Oman wala Saudia ila Washihir, Washiraz na Waburush walokuja kwanza kabisa kufanya biashara ya viungo, dhahabu na vito. Kwa hiyo huwezi kutumia lugha moja kutafsiri neno kwa sababu wewe unakijua kiarabu cha Karne ya 21. Your very wrong na wewe pitia hapa:- The name Zanzibar came from a combination of two Arabic words, 'Zinj', meaning black, and 'barr', being the Arabic word for land, the result meaning 'Land of the Blacks'.

Tazama unavyojikanganya tena.

Link niliyokuwekea inakuonesha wazi kuwa hao ni Cushite na si Bantu na kama ulikuwa umenisoma vizuri bila kiherehere ungeona na DNA proofs, zinazoleta mkanganyiko wa historia na imefikiwa kusema amma Tanzania au Ethiopia, unajuwa kwa nini? very simple, ni amma hayo makabila yalitokea North kuja South amma yalianzia hapo Tanzania kwenda North.

Hakuna Mbantu aliyetokea North, hakuna historia hata moja inalosema hilo, kama unayo yako tuwekee. Palipoandikwa wametokea North utakuta amma Cushite amma Semite. Kwa hiyo usichanganye mambo.

Mwisho wa yote nikakuwekea link inayoonesha ni nani Waarabu na wapi kwao na hiyohiyo link inaonesha yale yale niliyokuuliza uliyoshindwa kuyajibu. Pole sana.

Nnajuwa hapo ukweli umeuelewa lakini unataka tu, kuchanganya mambo, watu kama wewe nawaelewa sana wala hamnipi shida, mnajifunza kwa kupopowa.

Naam, nnakuwekea link kwa kuwa sasa hivi Library zipo mtandaoni, unataka nini zaidi ya hicho, hata teknolojia hauithamini? Unashangaza sana. Leo hii ni kuna "dream world" kwa wapenda historia kwa jinsi tulivyowekewa maktaba na archives za dunia humuhumu mtandaoni. Cha ajabu hapo nini? au hilo kwako ni kituko?

Huyo aliye translate neno Zinj kutoka hiyo website uliyoiweka haijuwi maana ya Zinj. Na pia haijuwi maana ya "barr", barr nilikuelezea maana yake hususan kwa Kiswahili ambayo haina utata kabisa ni bara. Land kwa kiarabu ni "ardh" ndipo kwa Kiswahili tukapata neno ardhi na si "barr".

Kwa hiyo hukohuko kwenye mtandao ulpoiowa hiyo maana wamepotosha na ndiyo maana nawe umepotoka kwa kuwa Kiarabu ahaujuwi kwa hiyo ulichokisoma ukaona aaah, hiki ndiyo sawa, basi hata hutumii akili yako japo kiduchu ukatumia Kiswahili unachokijuwa ambacho kipo karibu zaidi na Kiarabu kupata tafsiri sahihi? Unashangaza.

Nnaona kwa kuja na maana hiyo uliyoitoa kwa ku google pia mtandaoni, niliyoibomonda hapo juu, ya neno Zinj inammanisha haijuwi maana yake, mimi ntakupa jibu.

Maana ya Zinj ni pua-pana. Zinj Bar - Bara la watu wenye pua pana. Unajuwa kwanini wakawaita hivyo? kwa sababu kama ni weusi hata wao hao Waarabu kwa wingi wao ni weusi (post yangu kuhusu Arabs inafafanuwa hilo) sasa wewe mwenyewe mweusi halafu ukamwite mwenzako mweusi si itakuwa ni kituko? Tofauti ya weusi wa Magharibi na Mashariki ni pua zao, hilo halina shaka kabisa, tazama nchi zilizotajwa kwenye post ya ARABS niliyokuwekea juu, utayakinisha hilo. Na hiyo ni moja ya Tofauti ya Semites na Bantus ni pua za na si rangi zao tu.

Sasa hiki nilichokupa hapa "orijino" changu na nnaku refer kwenye links ili kukuhakikishia tu point yangu.

Kuhusu Wabantu kuwa sio wenyewe Tanganyika ni kosa kusema hivyo, inabidi uelewe, wewe ulivyohamia Dar ulikutana na wenyeji wa Dar. Na ukaishi mpaka ukawa na wewe ni mwenyewe Dar na hilo halikupi haki ya kusema na hao uliowakuta si wenyewe.

Kwa mantiki hiyohiyo Semites na Cushites wapo Tanganyika na wao pia ni wenyewe tena wao ni wa zamani zaidi ya Wabantu kutokana na historia.

Hilo la Wahindi na Washihiri ni mada nyingine kabisa, ndiyo maanaa hapo awali nikakusihi ununuwe kitabu kiitwacho Empires of the Monsoon, cha Richard Hall, ungepata majibu ya yote hayo. Na nnakuhakikishia yule mtu anajuwa kuandika, hutatamni kukiweka chini ukianza kukisoma, utapata kuelewa humo kuwa Vasco Da Gama aliitazama Kilwa kwa mbali kutokea kwenye meli yake hakupato kutia mguu wake Kilwa. Mabaharia wake tu walishuka? Jee, kwanini? jisomee.

Pia utapato kujuwa hili ji bahari kubwa kwanini likaitwa la Hindi? ni nani aliyeliita hivyo?

Kuna uwenyewe na uenyeji. Uafrika si Ubantu pekee na pia Utanganyika si Ubantu pekee ni zaidi ya hapo, sana tu.

Hujajibu bado, Jee unajuwa maana ya Bantu?
 
Tazama unavyojikanganya tena.

Link niliyokuwekea inakuonesha wazi kuwa hao ni Cushite na si Bantu na kama ulikuwa umenisoma vizuri bila kiherehere ungeona na DNA proofs, zinazoleta mkanganyiko wa historia na imefikiwa kusema amma Tanzania au Ethiopia, unajuwa kwa nini? very simple, ni amma hayo makabila yalitokea North kuja South amma yalianzia hapo Tanzani kwenda North.

Hakuna Mbantu aliyetokea North, hakuna historia hata moja inalosema hilo, kama unayo yako tuwekee. Palipoandikwa wametokea North utakuta amma Cushite amma Semite. Kwa hiyo usichanganye mambo.

Mwisho wa yote nikakuwekea link inayoonesha ni nani Waarabu na wapi kwao na hiyohiyo link inaonesha yale yale niliyokuuliza uliyoshindwa kuyajibu. Pole sana.

Nnajuwa hapo ukweli umeuelewa lakini unataka tu, kuchanganya mambo, watu kama wewe nawaelewa sana wala hamnipi shida, mnajifunza kwa kupopowa.

Naam, nnakuwekea link kwa kuwa sasa hivi Library zipo mtandaoni, unataka nini zaidi ya hicho, hata teknolojia hauithamini? Unashangaza sana. Leo hii ni kuna "dream world" kwa wapenda historia kwa jinsi tulivyowekewa maktaba na archives za dunia humuhumu mtandaoni. Cha ajabu hapo nini? au hilo kwako ni kituko?

Huyo aliye translate neno Zinj kutoka hiyo website uliyoiweka haijuwi maana ya Zinj. Na pia haijuwi maana ya "barr", barr nilikuelezea maana yake hususan kwa Kiswahili ambayo haina utata kabisa ni bara. Land kwa kiarabu ni "ardh" ndipo kwa Kiswahili tukapata neno ardhi na si "barr".

Kwa hiyo hukohuko kwenye mtandao ulpoiowa hiyo maana wamepotosha na ndiyo maana nawe umepotoka kwa kuwa Kiarabu ahaujuwi kwa hiyo ulichokisoma ukaona aaah, hiki ndiyo sawa, basi hata hutumii akili yako japo kiduchu ukatumia Kiswahili unachokijuwa ambacho kipo karibu zaidi na Kiarabu kupata tafsiri sahihi? Unashangaza.

Nnaona kwa kuja na maana hiyo uliyoitoa kwa ku google pia mtandaoni, niliyoibomonda hapo juu, ya neno Zinj inammanisha haijuwi maana yake, mimi ntakupa jibu.

Maana ya Zinj ni pua-pana. Zinj Bar - Bara la watu wenye pua pana. Unajuwa kwanini wakawaita hivyo? kwa sababu kama ni weusi hata wao hao Waarabu kwa wingi wao ni weusi (post yangu kuhusu Arabs inafafanuwa hilo) sasa wewe mwenyewe mweusi halafu ukamwite mwenzako mweusi si itakuwa ni kituko? Tofauti ya weusi wa Magharibi na Mashariki ni pua zao, hilo halina shaka kabisa, tazama nchi zilizotajwa kwenye post ya ARABS niliyokuwekea juu, utayakinisha hilo. Na hiyo ni moja ya Tofauti ya Semites na Bantus ni pua za na si rangi zao tu.

Sasa hiki nilichokupa hapa "orijino" changu na nnaku refer kwenye links ili kukuhakikishia tu point yangu.

Kuhusu Wabantu kuwa sio wenyewe Tanganyika ni kosa kusema hivyo, inabidi uelewe, wewe ulivyohamia Dar ulikutana na wenyeji wa Dar. Na ukaishi mpaka ukawa na wewe ni mwenyewe Dar na hilo halikupi haki ya kusema na hao uliowakuta si wenyewe.

Kwa mantiki hiyohiyo Semites na Cushites wapo Tanganyika na wao pia ni wenyewe tena wao ni wa zamani zaidi ya Wabantu kutokana na historia.

Hilo la Wahindi na Washihiri ni mada nyingine kabisa, ndiyo maanaa hapo awali nikakusihi ununuwe kitabu kiitwacho Empires of the Monsoon, cha Richard Hall, ungepata majibu ya yote hayo. Na nnakuhakikishia yule mtu anajuwa kuandika, hutatamni kukiweka chini ukianza kukisoma, utapata kuelewa humo kuwa Vasco Da Gama aliitazama Kilwa kwa mbali kutokea kwenye meli yake hakupato kutia mguu wake Kilwa. Mabaharia wake tu walishuka? Jee, kwanini? jisomee.

Pia utapato kujuwa hili ji bahari kubwa kwanini likaitwa la Hindi? ni nani aliyeliita hivyo?

Kuna uwenyewe na uenyeji. Uafrika si Ubantu pekee na pia Utanganyika si Ubantu pekee ni zaidi ya hapo, sana tu.

Hujajibu bado, Jee unajuwa maana ya Bantu?
Ok naona twenda moja baada ya jingine. Nionyeshe mahala panaposema maana ya Cush sio Weusi. na Cush ties sio lugha ya watu weusi. Neno weusi walimaanisa kundi gani? Hiyo website ya Wazanzibar wenyewe utasemaje mwandishi hajui maana, ikiwa wewe mwenyewe unatoa ushahidi wako ktk website kutupinga sisi Wabantu tunaoijua Asili yetu. Kama huyo Mzenji hajui, kwa nini na wewe usiwe hujui unapopingana na Wabantu!...
 
Mohammed Said,
Mimi nakukubali sana katika maelezo yako wala sii kwamba hakuna ukweli wowote isipokuwa Historia ya Nchi huandikwa WATU walohusika na kwa minajiri gani. Kama ni UHURU wa Tanganyika kina AbdulWahid hawakuutaka UHURU wa Waislaam wa Tanganyika isipokuwa UHURU wa WATU wote wa Tanganyika haikubagua dini wala Kabila. Kwa hiyo unapoandika kuhusu wazazi wako ungewataja tu majina yao na michango yao, basi kitabu chako kingepata sifa kubwa sana nchini pengine hata kusomwa mashuleni.

Kosa ullifanya ni kupeleka Udini zaidi ya kuonyesha michango yao isipokuwa mchango wa Uislaam katika Uhuru wa Tanganyika kiasi kwamba ukawaweka hata watu walopingana na TANU juu ya Uhuru wa Tanganyika kina Takadir na AMNUT kuwa katika mashujaa walosahaulika. Kama kweli kweli waislaam walitaka Uhuru wao basi wangekiunga chama hiki cha AMNUT mkono badala ya TANU kilichochanganyikana na watu wa makabila mbali mbali.

Kwa nini unapenda sana kumshusha Nyerere pamoja ya yote alotutumikia? kwa sababu Mkristu au kwa sababu wazee wako hawakupewa nafasi. Mzee Ali Sykes hadi anatutoka alikataa siasa kabisa yeye mwenyewe na historia inatuonyesha wazee wengi waliacha siasa baada ya kutimiza wajibu wao wakafanya biashara zao.

Wewe ni mwandishi mzuri sana na unajua kuzitafuta habari lakini unakumbwa na hili jinamizi la Udini ambalo kama nilivyokwambia wazungu wanapenda sana kuwasoma watu kama wewe kwa sababu wanajua upeo wa fikra zako na utaweza kuwa hatari kiasi gani. Na katika hali kama ya leo ya Ugaidi unaweza kuwepo katika list ya watu wanaotazamwa sana kwa sababu wanaamini watu kama wewe ni hatari na je umeweza vipi kuwalaghai wengine kuwajaza chuki dhidi ya wakristu au watu wengine.

Haya yalifanyika sana Uingereza wakiwaachia masheikh wakizungumza wazi Trafalgar Square, kumbe wakiwachunguzana kuchukua picha za watu wanaohushulia mara kwa mara mihadhara ile, Ilipoanza tu habari za Ugaidi wakakusanywa hata wasokuwemo na kwa sababu kama hizi usidhani unafanya la maana sana ikiwa ncjhi yako yenyewe kitabu chako kimepigwa marufuku. Think big mkuu wangu nakuasa tu.

Mpaka leo wanazungumza sana lakini si Trafalgar Square ni Hyde Park Speakers Corner. Tena nnakuwekea link umsikilize sana Blagrove, huyu ni favorite wangu wa Hyde Park: https://youtu.be/wZN2eAe_iuY

Ni favorite wangu kwani ana high capacity ya general knowledge.

Kitabu cha Alama Mohamed Said kipo, mimi nimekinunuwa Dar.

Vipi unataka kutuaminisha bila "nukuu: hata moja kutoka kwenye kitabu unachokisema? hautuoneshi Alama Mohamed Said kaandika "uchochezi" huu ukanukuu? Tujionee wenyewe? Tukuamini vipi? Unakuja na kubwabwaja na kuhororoja bila kuleta ushahidi? sitaki kuamini na wewe capacity yako ndiyo iko hivyo. Unanshangaza!
 
Ok naona twenda moja baada ya jingine. Nionyeshe mahala panaposema maana ya Cush sio Weusi. na Cush ties sio lugha ya watu weusi. Neno weusi walimaanisa kundi gani? Hiyo website ya Wazanzibar wenyewe utasemaje mwandishi hajui maana, ikiwa wewe mwenyewe unatoa ushahidi wako ktk website kutupinga sisi Wabantu tunaoijua Asili yetu. Kama huyo Mzenji hajui, kwa nini na wewe usiwe hujui unapopingana na Wabantu!...

Kwanza ungeanza kwa kujibu swali langu ingekuwa raha sana.

Swali lako ni irrelevant kabisa tena, kwa kuwa hakuna sehemu niliyoandika kuwa Cushites ni weupe au weusi, sijagusa kabisa hilo.

Lakini ntakujibu hilo swali baada ya wewe kujibu swali langu unalolikwepa.

Jee unajuwa maana ya Bantu?

Halafu kuhusu website kuwa ni ya Wazanzibari si tatizo au si dalili ya kuwa wanaijuwa maana Zinj Bar, sasa wewe mswahili mtu anakwambia maana ya "barr" ni "land" na wewe unakuballi tu? wakati kila siku unatumia neno bara na unalijuwa maana yake ni nini. Na kila siku unatumia neno Ardhi na unajuwa limetokana na Kiarabu Ardh? ikiwa hata hicho kitu kipo wazi kabisa unashindwwa ku "contemplate" unaniweeka katika wwakati mgumu sana kukufundisha, lakini sitichoka, nnakuhakikishia.

Sasa kwa kukufaidisha tu, nnakupa kionjo kimoja; Hata neno "Earth" la Kingereza linatokana na neno "Ardh" la Kiarabu.

Nimekuelezea maana ya Zenjbar kwa Kiswahili fasaha kabisa, nalo pia unashindwa kuelewa? na nikakuuliza jee hilo bara la Zinj lilikuwa wapi? kwani Zanzibar ni visiwa na si bara na Mwarabu hawezi kufanya kosa la bara na kisiwa, lugha yake ni pana sana. Nalo pia umekwepa kujibu.

Pata kionjo kingine, jee, unajuwa huko kwa Washihiri ulipopataja awali pia kuna Zenjbar enzi na enzi hadi leo hii? nacho si kisiwa.

Wallahi naona raha sana, unanipa wasaa wa kumwaga vitu adimu sana.

Kuna msomaji kanitumia ujumbe ananambia niandike kitabu. In Sha Allah ntafanyia kazi na ntakapokianza ntamtumia "draft" Alama Mohamed Said anipe muongozo.

Hapo sasa!
 
Mpaka leo wanazungumza sana lakini si Trafgar Square ni Hayde Park Speakers Corner. Tena nnakuwekea link umsikilize sana Blagrovr, huyu ni favorite wangu wa Hyde Park: https://youtu.be/wZN2eAe_iuY

Ni favorite wangu kwani ana high capacity ya general knowledge.

Kitabu cha Mohamed Said kipo, mimi nimekinunuwa Dar.

Vipi unataka kutuamnisha bila "nukuu: hata moja kutoka kwenye kitabu unachokisema? hautuoneshi Mohamed Said kaandika "uchochezi" huu ukanukuu? Tujionee wenyewe? Tukuamini vipi? Unakuja na kubwabwaja na kuhororoja bila kuleta ushahidi? sitaki kuamini na wewe capacity yako ndiyo iko hivyo. Unanshangaza!
Ni ushauri tu nilompa Mohamed Said, yeye anaweza uchukua ama kuuacha. Wewe una haki na kila sababu ya kufuata, kusoma unalolitaka sijakukwaza. Tuendee la mada yetu acha hizi habari za kubwabwaja maana wewe ndio unabwabwaja hovyo na Uarabu wa kupaka na haki ya Mungu... nakushangaa sana...
 
Kwanza ungeanza kwa kujibu swali langu ingekuwa raha sana.

Swali lako ni irrelevant kabisa tena, kwa kuwa hakuna sehemu niliyoandika kuwa Cushites ni weupe au weusi, sijagusa kabisa hilo.

Lakini ntakujibu hilo swali baada ya wewe kujibu swali langu unalolikwepa.

Jee unajuwa maana ya Bantu?
Sasa wewe unaniuliza mimi Mbatu nitashidwaje kujua maana ya BANTU ikiwa neno lenyewe ni la Kibantu, umekunywa nini leo au bado una search ktk site kujua maana yake?. Bantu, Abantu ni WATU nalitumia sana katika lugha yangu.. Wewe uliye mwarabu kwa kiarabu maana yake nini?

Unajua kuna Myahudi mmoja hapa niliwahi bishana naye akisema Waarabu they are Anti Semitics, nikamuuliza kwani Waarabu sio jamii ya Semitics, akajibu ooh they are. Nikamuuliza kwa nini Semitic imekuwa leo ni Wayahudi tu sio WATU wote wenye asili hiyo? tukabisha wee nikamwona mpuuzi tu. Ndio haya...
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom