Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
Tanzania na Propaganda za Udini
"Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenye kupendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala."

Ibrahim Noor Shariff

2015%2B-%2B1

Prof%2BIbrahim%2Bphoto.jpg

C:\Users\yemen\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.jpg

Prof. Ibrahim Noor Shariff
Mwanachuoni wa Chuo Kikuu Cha Rutgers, New Jersey, Marekani, Ibrahim ni msomi wa Sanaa, Tarikh (Historia) na Fasihi ya Kiswahili.

Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu "Udini na Ugozi," Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali, wanasiasa, mapadri na mashekhe.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.

Kitabu hiki "Tanzania na Propaganda za Udini" kina milango mitatu na sahifa 152.

  1. Mlango wa Kwanza unahusu "Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki." Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatalika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.
  2. Mlango wa Pili unazungumzia "Propaganda za Siasa za Chuki na Athari Zake."Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizowatuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata, kuuza na kumiliki watumwa. Propaganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bure bila ya sababu ilipovamiwa Zanzibar, nchi yenye Waislamu wengi, na kumezwa na Tanganyika 1964.
  3. Katika Mlango wa Tatu "Tanzania na Propaganda za Udini Shuleni" mwandishi, ambae ni Profesa wa Sanaa, anaonesha ubingwa wake wa kuchambua picha. Anatunakilia picha za kuchorwa kutokana na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswahili Waislamu wanawakamata, kuwapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa. Hapohapo Profesa Ibrahim anaonyesha uzushi wa picha hizo zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba bila ya shaka picha nyingine zimebuniwa na wachoraji na hazina ukweli. Prof. Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taarikh (historia) katika shule za Tanzania. Anataka masomo haya yajengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli, sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukoloni.

Prof. Ibrahim Noor ana hadharisha Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na khasa Waislamu katika mipango ya masomo Tanzania. Hizi chuki za udini zitaleta balaa kubwa kuliko mauwaji ya Zanzibar ya 1964. Watakaoumia na chuki hizi ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini Tanzania. Kitabu hiki kinahitajia kimfikie kila mwenye uwezo wa kubadilisha mambo Tanzania, kwa mfano:

a) Wahishimiwa Memba /Wabunge Tanzania

b) Memba wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

c) Mawaziri wa Serikali ya Muungano wa Zanzibar

d) Wakubwa wa Makanisa na Wakubwa wa Vyama vya Kiislamu

e) Wakubwa wa Vyama vya Siasa

f) Wakubwa wa Magazeti

g) Wakubwa wa TV na Radio

h) Na kabla ya wote hao waliotangulia ni mimi na wewe wananchi ambao tunapiga kura kuwachagua viongozi wema

Kinauzwa:

DAR ES SALAAM
Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema, Phone: 0773 777 707

TAMPRO, Magomeni Area along Morogoro Road, Adjacent to Kinondoni Municipal, Plot no. 169 Block R, Kinondoni Dar es Salaam.Phone: 0222172182

KEF "Kalamu Education Foundation", Magomeni– Kinondoni District, Dar es Salaam.

Phone: 0776 525 268

ZANZIBAR
Masomo Bookshop, behind the Central Market, Zanzibar, Phone: 0242 232652
 
Inafurahisha kuona wako watu mashujaa na wenye kupenda nchi yao wanasema kweli. Tanzania hayendi mbele kama kweli haisemwi na kushikilia maovu kuondoshwa. Hapana hatari kubwa kwa nchi kuliko kupoteza akili za vijana na wanafunzi kwa kujaza akili zao chuki za kubaguana. Profesa Ibrahim Noor Shariff ahsante sana.
 
Ndugu Jembepori,
Ninasikitika unakiponda kitabu kabla hujakisoma Kwaza wewe unakosa faida pia unawakosesha wengine faida. Je huu ndio ustaarabu mpya wa wataalamu waTanzania?
 
Ndugu Jembepori,
Ninasikitika unakiponda kitabu kabla hujakisoma Kwaza wewe unakosa faida pia unawakosesha wengine faida. Je huu ndio ustaarabu mpya wa wataalamu waTanzania?

Madafu,
Katika mambo ambayo mimi binafsi nimekutananayo na hakika yamenisikitisha
ni jinsi jamaa zetu walivyoathirika na propaganda.

Hicho kitabu wala si cha dini lakini kilichomkera ni hilo jina la mwandishi.
Kitabu hicho mathalan kingekuwa na jina la John Esposito asingejali.

Juu hayo ningependa ajue kuwa, "Islam," hivi sasa ni "Field of Enquiry,"
muhimu katika vyuo vingi sana hasa Marekani.

Aingie kwenye Google ataona mengi.

Kitabu changu kimepata umaarufu mkubwa sana katika vyuo vya Marekani
kwa kuwa nilikuja na, Islamic movement in nationalist politics ..." katika
Tanganyika ya 1950s.
 
Hivi kile kitabu kilichoandikwa na Salman Rushdie kinachoitwa "Aya za Shetani" kwanini kisiruhusiwe tu watu wengi wakapata kukisoma?au hata hapa jamii forum kikawekwa hadharani....ni katika kupanua maarifa tu!
 
Madafu,
Katika mambo ambayo mimi binafsi nimekutananayo na hakika yamenisikitisha
ni jinsi jamaa zetu walivyoathirika na propaganda.

Hicho kitabu wala si cha dini lakini kilichomkera ni hilo jina la mwandishi.
Kitabu hicho mathalan kingekuwa na jina la John Esposito asingejali.

Juu hayo ningependa ajue kuwa, "Islam," hivi sasa ni "Field of Enquiry,"
muhimu katika vyuo vingi sana hasa Marekani.

Aingie kwenye Google ataona mengi.

Kitabu changu kimepata umaarufu mkubwa sana katika vyuo vya Marekani
kwa kuwa nilikuja na, Islamic movement in nationalist politics ..." katika
Tanganyika ya 1950s.

Kama nimemisunderstand i take back my word, kimsingi sinashida na uislam hata jina kiweje so long as theme haiki biased ila kinacho nisikitisha huwa kila kitabu ama maandishi wanayoandija kuhusu uislam huwa ni malakaniko tu, utasikia historia ya waislam imepotoshwa, mara mambo ya waislam yalinyanganywa kitu ambacho binafsu sikiamini kwani naamini hao waislqm wakipindi hicho nao walikuwa na akili timamu,

Kama kuna mambo waislam wa sasa wanatakiwa kuyafanya ni kurekebisha kasoro walizofanya waislam waliotangulia kwa kuweka vitu kwenye maandishi......

Na hili lilitokea pale walipopuuzia kusoma elimu ya hii ya maisha ya kawaida kwani kwenye elimu hii ndipo watu wanapopata fulsa hata ya kuandika maishayao kabla hata ya kuwa historia.....

Nampongeza sana mwandishi kwa kusoma vizuri mpaka ngazi aliyofikia na pia natiwa moyo na waislam wa siku hizi kwan wengi sana wanapeleka watoto wao shule na pia wao wanasoma.....

That great for future peace of the world.
Mbarikiwe
 
Mohamed Said

Kwanini kiuzwe misikitini? Inaleta picha mbaya kuwa kina lengo au ajenda maalumu.... Nitakitafuta kwa kuwa nimesoma kazi za huyu Ibrahimu Nuru Sharifu, ni mwanazuoni wa lugha pia, naamini humo ndani amejenga hoja kuntu na zenye utafiti wa kutosha!
 
Last edited by a moderator:
Tanzania na Propaganda za Udini
"Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenyekupendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala."
Ibrahim Noor Shariff

2015%2B-%2B1

Prof%2BIbrahim%2Bphoto.jpg

Prof. Ibrahim Noor Shariff
Mwanachuoni wa Chuo Kikuu Cha Rutgers, New Jersey, Marekani, Ibrahim ni msomi wa Sanaa, Tarikh (Historia) na Fasihi ya Kiswahili.

Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu "Udini na Ugozi," Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali, wanasiasa, mapadri na mashekhe.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.
Kitabu hiki "Tanzania na Propaganda za Udini" kina milango mitatu na sahifa 152

Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu "Udini na Ugozi," Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali, wanasiasa, mapadri na mashekhe.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.
Kitabu hiki "Tanzania na Propaganda za Udini" kina milango mitatu na sahifa 152.

Mlango wa Kwanza unahusu "Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki." Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatalika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.

Mlango wa Pili unazungumzia "Propaganda za Siasa za Chuki na Athari Zake."Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizowatuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata, kuuza na kumiliki watumwa. Propaganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bure bila ya sababu ilipovamiwa Zanzibar, nchi yenye Waislamu wengi, na kumezwa na Tanganyika 1964.

Katika Mlango wa Tatu "Tanzania na Propaganda za Udini Shuleni" mwandishi, ambae ni Profesa wa Sanaa, anaonesha ubingwa wake wa kuchambua picha. Anatunakilia picha za kuchorwa kutokana na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswahili Waislamu wanawakamata, kuwapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa.

Hapohapo Profesa Ibrahim anaonyesha uzushi wa picha hizo zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba bila ya shaka picha nyingine zimebuniwa na wachoraji na hazina ukweli. Prof. Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taarikh (historia) katika shule za Tanzania. Anataka masomo haya yajengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli, sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukoloni.

Prof. Ibrahim Noor ana hadharisha Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na khasa Waislamu katika mipango ya masomo Tanzania. Hizi chuki za udini zitaleta balaa kubwa kuliko mauwaji ya Zanzibar ya 1964. Watakaoumia na chuki hizi ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini Tanzania. Kitabu hiki kinahitajia kimfikie kila mwenye uwezo wa kubadilisha mambo Tanzania,

kwa mfano:
a) Wahishimiwa Memba /Wabunge Tanzania
b) Memba wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
c) Mawaziri wa Serikali ya Muungano wa Zanzibar
d) Wakubwa wa Makanisa na Wakubwa wa Vyama vya Kiislamu
e) Wakubwa wa Vyama vya Siasa
f) Wakubwa wa Magazeti
g) Wakubwa wa TV na Radio
h) Na kabla ya wote hao waliotangulia ni mimi na wewe wananchi ambao tunapiga kura kuwachagua viongozi wema

Kitabu kinauzwa:
DAR ES SALAAM
Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema, Phone: 0773 777 707
TAMPRO, Magomeni Area along Morogoro Road, Adjacent to Kinondoni Municipal, Plot no. 169 Block R, Kinondoni Dar es Salaam.Phone: 0222172182
KEF "Kalamu Education Foundation", Magomeni– Kinondoni District, Dar es Salaam.
Phone: 0776 525 268

ZANZIBAR
Masomo Bookshop, behind the Central Market, Zanzibar, Phone: 0242 232652

by Mohamed Said​
 
Mohamed Said

Kwanini kiuzwe misikitini? Inaleta picha mbaya kuwa kina lengo au ajenda maalumu.... Nitakitafuta kwa kuwa nimesoma kazi za huyu Ibrahimu Nuru Sharifu, ni mwanazuoni wa lugha pia, naamini humo ndani amejenga hoja kuntu na zenye utafiti wa kutosha!

Mdau...nadhan tatizo ni neno msikitini....lakin kikwel kabsa ni maduka ya vitabu yaliyoko karibu na msikiti....hiii haimananishii ni ndani ya msikiti. Either way...kuna vitabu vingi ambavyo vinapatikana katika aina flan.ya maduka na si mengineyo
...hii inaweza kuwa ni kwa sabb za kiitikadi au kukipinga aina flan ya vitabu...mfano...kitabu kama keys of this blood japo kimeandikwa na mtumishi wa miaka mingi wa vatikan...huwez kikuta hiki kitabu kwenye maduka mengi ya kanisa...so nadhan hofu yako isikufunge sana kuyaendea maduka yaliyoko misikitin....after all si mahali hatari sana kama inavofanywa kuonekana....just a thought...!
 
Last edited by a moderator:

Hizi habari ya watuhumiwa kujisafisha huku wahanga wakiendelea na makovu ya miaka nendarudi siyo nzuri hata kidogo.
Msiendelee kututiua machungu na madhila waliyotufanyia Wazungu na Waarabu.
Ujinga huu wa eti Uprof na mahistoria iko siku mtasababisha vizazi vijavyo kulipa kisasi.

Ukristo na Uislam wote ni Watuhumiwa wa Biashara ya Utumwa -ila ilikupotoisha waafrika wameamua kutupiana mipira na kutugawa.

Mwafrika jitambue linapokuwa suala la Utumwa Si-Mwarabu wala Mzungu aliyemsafi hata kidogo-na hili ndiyo madharau na ubaguzi ambao wengi wao Wazungu na Waarabu umewakaa Mioyoni mwao.rejea hapo chini na fanya tafiti hata sasa utagundua uhai wa alichokuwa anazungumza huyu bwana.

Botha speech 1985: How do you feel it? Imeniuma sana - JamiiForums

[h=3]The Arab slave trade: 200 million non-Muslim slaves from all ...[/h]
Under Islamic laws, slavery is explicitly permitted.[SUP][145][/SUP] As Saudi Sheikh Saleh Al-Fawzan, a member of the Senior Council of Clerics had said in 2003, those who argue that slavery is abolished are “ignorant, not scholars. They are merely writers. Whoever says such things is an infidel.” [SUP][146][/SUP] Muhammad himself was a slaver. He not only owned many male [SUP][147][/SUP][SUP][148][/SUP] and female [SUP][149][/SUP] slaves, but he also sold, captured, and raped [SUP][150][/SUP] his slaves. Even his wives owned slaves.

The manual also gave indications that Arabs actually created the entire slave export trade in Africa. Bits and pieces from history indicate that Muslims enslaved over 150 million African people and at least 50 million from other parts of the world. They also converted Africans into Islam, causing a complete social and financial collapse of the entire African continent apart from wealth attributed to a few regional African kings who became wealthy on the trade and encouraged it. This is a claim that is not well presented in Western information or education on slavery. You can find a lot of very interesting and original historical materials in Asia and the East which have never found its way to the West.

Kitabu kama hiki kinaonesha kikisomwa na mjinga ataamini 100%
Kwa mwenye akili atachanganya na zake kujuwa mbivu na mbichi..
Ningependa nikipate online nikisome maudhui haswa ni kinakuja kutatatua kero ipi katika jamii yetu
 
Natumai atakuwa ametoa tafsiri sahihi ya neno "udini", pia kitabu ambacho kimeazimiwa kisomwe na watz wote, kisambazwe kwenye bookshop mbali mbali.......

Asante kwa mchango wake na ameitendea haki taaluma yake.
 
kwa muhtasari huo uliowekwa kitabu ni one-sided na kimelenga kujenga kuwa uislam unangamizwa kwa propaganda nchini, mbaya zaidi kinauzwa sehemu za misikiti hii maana yake hadhira iliyolengwa ni waislamu wasome waanzishe chokochoko zisizo na mashiko.

Kwa maoni yangu Prof kachemsha sana na anachembechembe za udini zaidi hafai kuwa fani katika hadhira
 
Tanzania na Propaganda za Udini
"Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenyekupendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala."

Ibrahim Noor Shariff

Mkuu Maalim , kwanza asante kutupatia taarifa hizi, sisi wapenzi wa kusoma vitabu, tutakinunua na kukisoma hiki kitabu cha Tanzania na Propaganda za Udini, ila hata kabla sijakinunua na kukisoma, kiukweli kabisa toka ndani ya nafsi yangu, the sixth sense inanieleza the 'motive behind' mwandishi wa kitabu hiki, Prof. Ibrahim Noor Shariff, ni 'ill motive!'. Tangu Mlango wake wa Kwanza unaohusu "Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki." ameanza na maurongo yaliyokubuhu!, hapa anadanyanya wazi mchana kweupe kwa maushahidi yake ya uongo kwamba eti Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita kabla ya Wabantu, tangu karne ya 16 B.K!. The ill motive ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa kwenye Pwani ya Afrika Mashariki sawa na wenyeji wengineo.

Yaani hapa huyu Mwarabu, anataka kuwafanyia Afrikanization hawa wavanizi wa Kiarabu ili kuwahalaliasha eti na wao, ni wenyenyeji halali wa Afrika Mashariki, na wakati huo huo, kuwaondolea Wabantu, uenyeji wao wa asili, kwa kuonyesha kuwa hata hao Wabantu, Afrika ya Mashariki sio kwao asili bali nao pia ni wahamiaji tuu kama Waarabu!. Huu ni uongo uliokubuhu wa mchana kweupe!.

Lengo ni kuzuia kinachoweza kuja kuwapata Waarabu wa Afrika Mashariki na sana sana Waarabu wa Zanzibar ambao wametoka kwao Omani juzi juzi tuu mwaka 1832 wakiongozwa na Sultan Seyyed Said aliye yahamisha makao yake makuu toka Oman hadi Zanzibar!. Huyu sio tuu ni mvamizi bali pia ndiye mporaji mkuu, aliyejitwalia visiwa hivyo kama ameviokota as if hakumkuta mtu yoyote ili hali wenyeji walikuwepo!. Siku ile ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, siungi mkono mauaji yoyote ya Waarabu, bali wangeambiwa tuu kistaarabu, wafungeshe kilicho chao, wao na wazalio wao, wajirudie kwao Omani walikotoka na kutuachia visiwa vyetu!.

Hili swali la Waarabu wamekujaje Pwani ya Afrika Mashariki, litakuja kurudi tuu mbele ya safari hivyo ushauri wangu, ni kujituliza tuu na kuishi kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana kwa kujihesabu wanaishi hapo kwa hisani tuu, vinginevyo watatimuliwa warudi kwao Oman walikotoka, wao na vizalia vyao!.

Hizi historia za kutunga tunga kutaka kuwahalalisha madhalimu hawa waliowauza mababu zetu kama bidhaa!, hazitasaidia kitu!, no wonder kila siku wanashinda uchaguzi lakini kamwe hawatakabidhiwa nchi, na 2015 watashinda tena na moto ni ule ule!. Mwarabu atoke kwao, aje akutawale, babu zako awauze, kisha mumpindue halafu leo mumrudishe eti kisa amechaguliwa!, hii haitakaa itokee!.

Kesho ni sikukukuu ya Muungano, tutakukumbusheni hiyo Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika, hivyo huu muungano ni wa milele.

As long as hii ni lilterally work, ngoja nikitafute na kukisoma halafu turudi humu kumwaga mbichi na mbivu!, ila kiukweli lazima hata mtoto wa darasa la 4 akiisikia hii acheke, ati Waarabu nao kwao ni Afrika Mashariki, na Wabantu nao pia ni wageni!. OMG!.

Pasco
 
Mohamed Said

Kwanini kiuzwe misikitini? Inaleta picha mbaya kuwa kina lengo au ajenda maalumu.... Nitakitafuta kwa kuwa nimesoma kazi za huyu Ibrahimu Nuru Sharifu, ni mwanazuoni wa lugha pia, naamini humo ndani amejenga hoja kuntu na zenye utafiti wa kutosha!

Mphamvu,
Hiki kitabu hakiuzwi msikitini.

Kitabu hiki kinauzwa na Ibn Hazm Media Centre na maduka yake mawili ya
vitabu moja liko Mtaa wa Mahiwa karibu na Msikiti wa Mtoro na lingine lipo
Mtaa wa Mafia karibu na Msikiti wa Manyema.

Nikupe mfano labda utauelewa.

Cathedral Bookshop iko ndani ya St. Joseph Cathedral hali kadhalika Ukombozi
Bank.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom