Maktaba Imepokea Wageni Kutoka Mbali na Karibu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,922
30,271
IMEPOKEA WAGENI KUTOKA MBALI NA KARIBU

Maktaba leo imepokea wageni kutoka mbali na karibu.

Kulia ni Mwalimu Juma Nyuni kutoka MUM, Prof. Kai Kresse wa Zentrum Moderner Orient, Berlin, Ujerumani, Mohamed Said, Prof. Ibrahim Noor Shariff kutoka Muscat, Oman na Afisa wa MUM Mohamed Ali.

Ndugu zangu wamepita kwangu wakielekea MUM kwenye Tamasha la Kimataifa la Mswahili na Kumbukizi za Shaaban Robert linaloanza kesho Jumapili tarehe 31 Desemba na kumalizika Jumatatu tarehe 1 Januari, 2024.

Hivyo vitabu nilivyoshika ni baadhi ya zawadi nyingi pamoja na lebasi na vinginevyo nilizopokea kutoka kwa hawa ndugu zangu kutoka mbali.

Mgeni njoo mwenyeji apone.
Lakini ni nani hawa Prof. Ibrahim Noor Shariff na Prof. Kai Kresse?

Hapa hapatoshi ila nitawafunulia pazia kidogo mchungulie.

Kwanza ni rafiki zangu wa siku nyingi na wote nimewatembelea makwao ofisini na majumbani.

Hawa ndugu zangu na wote kalamu zao zinakata mithili ya wembe.
Kama nilivyotangulia kusema hapa hapatawatosha.

Nasimama hapa.

Picha chini kushoto ni Prof. Ibrahim Noor Shariff na picha ya kulia Prof. Kai Kresse akizungumza katika Kongamano la Taasisi ya Confucius Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Oktoba 2019.

1703968760775.jpeg

Kulia Mwalimu Juma Nyuni, Prof. Kai Kresse, Mwamdishi, Prof. Ibrahim Noor Shariff na Mohamed Ali
1703968904452.jpeg

Prof. Ibrahim Noor Shariff
1703969024154.jpeg

1703969056401.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom