mlolongo wa matukio yaliyoonekana jana kwenye luninga dunia nzima ni ya kusikitisha.
Leo na wakati huu kila mtu akili ikiwa imepoa ni lazima post mortem ya yaliyotokea ifanyike.
Lakini kati ya yote lilonisikitisha ni hili la mbunge wetu wa mbeya mjini, nd mbilinyi a.k.a sugu.
Pamoja na kutokubaliana naye kisiasa lakini hili la kitabia linaanza kuleta uvundo wa harufu kali wa kujiuliza huyu mtu ametoka wapi na kulikoni?
Kutofautiana kisiasa ni jambo la kawaida , lakini tabia za mhe sugu zinatudhalilisha mbele ya jamii.
Haijapita muda mrefu , kwenye kikao cha bajeti, sugu alisikika akimtusi waziri mkuu, mtu aliyemzidi kiumri na hata kimadaraka.
Najua fika kuwa mh pinda ni mvumilivu sana, akini sina uhakika kama angetukanwa kongozi mwingine angelichukulia hilo swala lightly.
Sasa hili la jana, la kutaka kupigana hadharani mtu wa kawaida atajiuliza kama huyu sugu amkuwa bodi gadi wa mbowe ndani ya bunge?
Bodi gadi asiyetumia akili kisi cha kujua kuwa anaweza kuumizwa vibaya na vyombo vya dola vilivyomo bungeni-kama mashindano ni ya msuli?
Je sugu ana akili timamu kweli , au kuna vitu vinamsukuma kichwani kufanya kama yale aliyofanya jana kwenye luninga, na kuishia kudhalilishwa kwa kubebwa msobe msobe na kutupwa nje ya ukumbi wa bunge kama kibaka!
Na hapo ndo nasema pamoja na kuwa sugu ni wa chama cha upinzani lakini kuna tabia ambazo zinakera. Kuna vijana wa upinzani kama zito na mnyika ambao kwa leo hata kwa vijana wamekuwa role models kwa misimamo yao ya akili na kujenga hoja ambazo hata ccm inazikubali.
Sugu ametuaibisha wana mbeya.
Sioni ni kwa jinsi ipi mtu huyu atakaa meza moja na kujadiliana mambo ya maana wa watu kama kina prof mwandosya, frof. Mwakyusa, dr mwakyembe na kina zambi , sichone na wengine wengi kwenye rcc za mkoa.
Nimalize tu kusema we are ashamed of you mhe. Mbilinyi a.k.a. Sugu.
sijawahi ona spika m.p.u.m.b.a.v.u kama ndugai,yeye hapimi mazingira kama yataleta aibu kwa nchi au la,anachokifanya ni kulinda maslahi ya chama chake hata kama yana athari