Kitabia, huyu Sugu hatuwakilishi watu wa Mbeya , anatutia aibu!!

Status
Not open for further replies.
mlolongo wa matukio yaliyoonekana jana kwenye luninga dunia nzima ni ya kusikitisha.
Leo na wakati huu kila mtu akili ikiwa imepoa ni lazima post mortem ya yaliyotokea ifanyike.

Lakini kati ya yote lilonisikitisha ni hili la mbunge wetu wa mbeya mjini, nd mbilinyi a.k.a sugu.
Pamoja na kutokubaliana naye kisiasa lakini hili la kitabia linaanza kuleta uvundo wa harufu kali wa kujiuliza huyu mtu ametoka wapi na kulikoni?

Kutofautiana kisiasa ni jambo la kawaida , lakini tabia za mhe sugu zinatudhalilisha mbele ya jamii.
Haijapita muda mrefu , kwenye kikao cha bajeti, sugu alisikika akimtusi waziri mkuu, mtu aliyemzidi kiumri na hata kimadaraka.
Najua fika kuwa mh pinda ni mvumilivu sana, akini sina uhakika kama angetukanwa kongozi mwingine angelichukulia hilo swala lightly.

Sasa hili la jana, la kutaka kupigana hadharani mtu wa kawaida atajiuliza kama huyu sugu amkuwa bodi gadi wa mbowe ndani ya bunge?
Bodi gadi asiyetumia akili kisi cha kujua kuwa anaweza kuumizwa vibaya na vyombo vya dola vilivyomo bungeni-kama mashindano ni ya msuli?
Je sugu ana akili timamu kweli , au kuna vitu vinamsukuma kichwani kufanya kama yale aliyofanya jana kwenye luninga, na kuishia kudhalilishwa kwa kubebwa msobe msobe na kutupwa nje ya ukumbi wa bunge kama kibaka!

Na hapo ndo nasema pamoja na kuwa sugu ni wa chama cha upinzani lakini kuna tabia ambazo zinakera. Kuna vijana wa upinzani kama zito na mnyika ambao kwa leo hata kwa vijana wamekuwa role models kwa misimamo yao ya akili na kujenga hoja ambazo hata ccm inazikubali.

Sugu ametuaibisha wana mbeya.
Sioni ni kwa jinsi ipi mtu huyu atakaa meza moja na kujadiliana mambo ya maana wa watu kama kina prof mwandosya, frof. Mwakyusa, dr mwakyembe na kina zambi , sichone na wengine wengi kwenye rcc za mkoa.

Nimalize tu kusema we are ashamed of you mhe. Mbilinyi a.k.a. Sugu.

sijawahi ona spika m.p.u.m.b.a.v.u kama ndugai,yeye hapimi mazingira kama yataleta aibu kwa nchi au la,anachokifanya ni kulinda maslahi ya chama chake hata kama yana athari
 
Mlolongo wa matukio yaliyoonekana jana kwenye luninga dunia nzima ni ya kusikitisha.
Leo na wakati huu kila mtu akili ikiwa imepoa ni lazima post mortem ya yaliyotokea ifanyike.

Lakini kati ya yote lilonisikitisha ni hili la mbunge wetu wa Mbeya Mjini, Nd Mbilinyi a.k.a Sugu.
Pamoja na kutokubaliana naye kisiasa lakini hili la kitabia linaanza kuleta uvundo wa harufu kali wa kujiuliza huyu mtu ametoka wapi na kulikoni?

Kutofautiana kisiasa ni jambo la kawaida , lakini tabia za mhe Sugu zinatudhalilisha mbele ya jamii.
Haijapita muda mrefu , kwenye kikao cha bajeti, Sugu alisikika akimtusi Waziri Mkuu, mtu aliyemzidi kiumri na hata kimadaraka.
Najua fika kuwa Mh Pinda ni mvumilivu sana, akini sina uhakika kama angetukanwa kongozi mwingine angelichukulia hilo swala lightly.

Sasa hili la jana, la kutaka kupigana hadharani mtu wa kawaida atajiuliza kama huyu Sugu amkuwa bodi gadi wa Mbowe ndani ya Bunge?
Bodi gadi asiyetumia akili kisi cha kujua kuwa anaweza kuumizwa vibaya na vyombo vya dola vilivyomo bungeni-kama mashindano ni ya msuli?
Je Sugu ana akili timamu kweli , au kuna vitu vinamsukuma kichwani kufanya kama yale aliyofanya jana kwenye luninga, na kuishia kudhalilishwa kwa kubebwa msobe msobe na kutupwa nje ya ukumbi wa Bunge kama kibaka!

Na hapo ndo nasema pamoja na kuwa Sugu ni wa chama cha upinzani lakini kuna tabia ambazo zinakera. Kuna vijana wa upinzani kama Zito na Mnyika ambao kwa leo hata kwa vijana wamekuwa role models kwa misimamo yao ya akili na kujenga hoja ambazo hata CCM inazikubali.

Sugu ametuaibisha wana Mbeya.
Sioni ni kwa jinsi ipi mtu huyu atakaa meza moja na kujadiliana mambo ya maana wa watu kama kina Prof Mwandosya, Frof. Mwakyusa, Dr Mwakyembe na kina Zambi , Sichone na wengine wengi kwenye RCC za mkoa.

Nimalize tu kusema we are ashamed of you Mhe. Mbilinyi a.k.a. Sugu.

mmh mie napita tu!
 
Busara haifundishwi,hairisishwi,haiigwi wala hainunuliwi.kwa tukio zima jana ilionyesha wapiga kura tulivyo wepesi kutekwa na hali ya kimazingira(situation),kama ni viongozi wa bunge tulio wachagua hawakutumia busara(yaani ndugai),ili paswa Mbowe,sugu na wenzake waonyeshe busara zao.lakin kila mmoja alitaka aonyeshe uwezo wake kwa nafasi yake.ACHENI USHABIKI WA HASARA,IFUATEN KWELI NA MTAMILIKI
 
wewe mleta hoja nadhani si mkazi mbeya sisi sugu tunamkubali kwani haki haiombwi na ukapewa na miccm kirahisi hivyo basi sugu atabaki kuwa mb
unge wetu.
 
Asante mkuu kwa hekima uliyoitoa.

Nimejaribu kuwaelewesha wanaJF-CDM kuwa unaweza kupinga uamuzi bila kujidhalilisha kama alivyofanya Sugu lakini wengi ni wazito wa kutumia busara na hekima kama hii.
Na kwa mara ya kwanza hata Mbowe alipungukiwa katika kuongoza mob psycology.
 
hivyo ni kwa mtazamo wako binafsi, wa kuwajibishwa ni Ndugai na ndiye chanzo cha vurugu zile. Hauko sawa ukimlenga Sugu au wewe nawe ni walewale!!!!
 
wewe mleta hoja nadhani si mkazi mbeya sisi sugu tunamkubali kwani haki haiombwi na ukapewa na miccm kirahisi hivyo basi sugu atabaki kuwa mb
unge wetu.

kwa wazarendo,wanao penda mabadiliko ya kisiasa,kisera ,kiuchumi na kimtazamo hatumshabikii mtu kwa sababu binafsi,wanambeya tunasema Chadema mtiwekee mtu mwingine,Suga anatuaibisha,hebu mlinganishe na wengine toka mbeya
 
hoja yako ni mfu.wote uliowataja ni magamba na watu wa mbeya hawahitaji vikao na watu wa ccm wamekuwepo miaka yote.kwa matendo na maonevu ya wabunge wa ccm wewe kwa uzuzu wako umeona hoja ya sugu kupigwa ni sawa badala ya kuwalaumu wabunge wa ccm unalalamikia kamanda sugu?pole fikiria upya.
Kwa kawaida wewe nisingejisumbua kukujibu kama wakora wengine , lakini kwa watu kama ninyi, Wancholi na Wanchoka, kupigana na kutoana ngeu ni jadi yenu.
 
ile kauli ya kuamru KUB atolewa, mlitegemea nini kitokee ndiyo maana tunawaambia hamfirii what will happen tomorrow. Mnatuaibisha sana kulikuwa na tatizo gani kama Job angetoa nafasi kwa KUB aongee, mbona Anne anamheshimu sana
 
Mlolongo wa matukio yaliyoonekana jana kwenye luninga dunia nzima ni ya kusikitisha.
Leo na wakati huu kila mtu akili ikiwa imepoa ni lazima post mortem ya yaliyotokea ifanyike.

Lakini kati ya yote lilonisikitisha ni hili la mbunge wetu wa Mbeya Mjini, Nd Mbilinyi a.k.a Sugu.
Pamoja na kutokubaliana naye kisiasa lakini hili la kitabia linaanza kuleta uvundo wa harufu kali wa kujiuliza huyu mtu ametoka wapi na kulikoni?

Kutofautiana kisiasa ni jambo la kawaida , lakini tabia za mhe Sugu zinatudhalilisha mbele ya jamii.
Haijapita muda mrefu , kwenye kikao cha bajeti, Sugu alisikika akimtusi Waziri Mkuu, mtu aliyemzidi kiumri na hata kimadaraka.
Najua fika kuwa Mh Pinda ni mvumilivu sana, akini sina uhakika kama angetukanwa kongozi mwingine angelichukulia hilo swala lightly.

Sasa hili la jana, la kutaka kupigana hadharani mtu wa kawaida atajiuliza kama huyu Sugu amkuwa bodi gadi wa Mbowe ndani ya Bunge?
Bodi gadi asiyetumia akili kisi cha kujua kuwa anaweza kuumizwa vibaya na vyombo vya dola vilivyomo bungeni-kama mashindano ni ya msuli?
Je Sugu ana akili timamu kweli , au kuna vitu vinamsukuma kichwani kufanya kama yale aliyofanya jana kwenye luninga, na kuishia kudhalilishwa kwa kubebwa msobe msobe na kutupwa nje ya ukumbi wa Bunge kama kibaka!

Na hapo ndo nasema pamoja na kuwa Sugu ni wa chama cha upinzani lakini kuna tabia ambazo zinakera. Kuna vijana wa upinzani kama Zito na Mnyika ambao kwa leo hata kwa vijana wamekuwa role models kwa misimamo yao ya akili na kujenga hoja ambazo hata CCM inazikubali.

Sugu ametuaibisha wana Mbeya.
Sioni ni kwa jinsi ipi mtu huyu atakaa meza moja na kujadiliana mambo ya maana wa watu kama kina Prof Mwandosya, Frof. Mwakyusa, Dr Mwakyembe na kina Zambi , Sichone na wengine wengi kwenye RCC za mkoa.

Nimalize tu kusema we are ashamed of you Mhe. Mbilinyi a.k.a. Sugu.

Mkuu unataka awe anagonga meza tu na kusema Ndiooooo? Kwanza kura yako hukumpa unachowashwa ni nini?
 
Asante mkuu kwa hekima uliyoitoa.

Nimejaribu kuwaelewesha wanaJF-CDM kuwa unaweza kupinga uamuzi bila kujidhalilisha kama alivyofanya Sugu lakini wengi ni wazito wa kutumia busara na hekima kama hii.
Na kwa mara ya kwanza hata Mbowe alipungukiwa katika kuongoza mob psycology.

nakuunga mkono,kwa Mbowe naweza sema it was just a badluck,maana huwa namuamin kwa kiasi fulan,samahan huu ni mtizamo wangu
 
Nawahurumia sana wanaoongozwa na watu aina ya sugu, heshima, adabu hawana halafu ndio etu waje wawe viongozi wa baadaye. hivi wanaposusa na kutoka nje na zile posho wanazisusa maana kila siku fujo, ili mradi hali isitulie je hizo posho vipi.

Miaka mitano ndio hiyo tutafakari maendeleo waliyotuletea kama sio propaganda wakati wamebaki kuandamana, kususia vikao vya bunge kutembelea magari ya kifahari lakini posho hawwachi wazisuse tuone kweli wanatutetea. sio propaganda maana kama ufisadi umekuwa wimbo, kama rusha imekuwa wimbo, ingekuwa vyema watuoneshe wao sio mafisadi kwa kuchukua posho wasizozitumikia.
 
Sugu ametuaibisha wana Mbeya. Nimalize tu kusema we are ashamed of you Mhe. Mbilinyi a.k.a. Sugu.
avatar47580_3.gif
masopakyindi, mbona solution is so simple...kaitishe mkutano wa wana Mbeya halafu useme haya maneno kama wewe kweli ni mwanamme! Unaruhusiwa kuufanya huo mkutano popote pale ulipozamia kama alivyojaribu "role model" wako Lameck Mwigulu Nchemba hapo Dar es Salaam kwa wana Iramba, are you game?
 
Mkuu kwa tuliokwenda shule tabia hiyo inatukera kweli kweli maana hata ukitofautiana na hasimu wako, mtu ukitumia akili bado ujumbe utafika kisawasawa.
Huyu Sugu is an intellectual misfortune kwa Mbeys inyojulikana kwa wasomi.
Masopakyindi. Ndugu yangu kama wewe unavojiita umekwenda shule hata wenzako wemekwenda shule,ila sema wewe unaweza ukawa unaamini 2+2=22.Utakuwa uko sawa kulingana na mwalimu wako alivokufundisha, na mwingine anaamini 2+2=4 naye yuko sawa kutokana na mwalimu wake.Kwenda shule sio hoja,hoja ni je uko sahihi?.Tembea vijijini uone na upime wananchi sasa wanataka nini kutokana na elimu ya uraia wanayopewa kila kukicha,2015 sio mbaliutaamini Watanzania walivoichoka ccm.
"Sio ushabiki, hutaki unaacha"
 
Mbeya inaonekana wazi kuwa kitovu cha mageuzi kama ilivyo Arusha, Kigoma, nk. Usiiongelee Mbeya ya leo tu bali waulize wanaozijua siasa za taifa hili na wakwambie kundi la Mwakitwange miaka hiyo lilimfanyaje Kawawa.
Kwanza tuna bahati kumpata mtu asiye mwoga na anayetaka kuiona haki ikitendeka kama Mh. Mbilinyi kwa nyakati hizi maana ndiye anaweza kudeal na idadi ya wapuuzi bungeni inayoonekana kuongezeka kuliko nyakati zilizopita.

wapuuzi walioongezeka ni wa chadema, mbona bunge la miaka mitano nyuma haliakua hivi?
 
Nkiripoti toka uhasibu mbeya hapa n hiv,tunaandaa maandamano ya kumtoa Mh Sugu bungeni,bora kiti kibaki waz kuliko kudhalilishwa vile,anaacha kutuwakilisaha sisi anaenda kuwa mlinz wa mbunge mwenzake???hyo n aibu kubwa kwa mnyaki,msafa na wengneo tuiopo huku,JM rudi kwenye mzik siasa waachie wengne.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom