Naomba msaada wa meneno yafuatayo:
- Hujasikia au Ujasikia - mfano, "Inaweza kuchukua miezi kumi kabla hujasikia/ujasikia kutoka kwetu."
- Histahili au Istahili - mfano, "ili familia yako histahili/istahili, unahitaji kufanya a, b, na c"
- Yahitajio au Yahitajiwo - mfano, "tafadhali elezea marekebisho makuu yahitajio/yahitajiwo kwenye nyumba yako."
- Unaipa au Hunaipa - mfano, kwa kutia sahihi hapo chini, unaipa/hunaipa XYZ ruhusa zote kubomoa nyumba yako."
Pia, naomba tafsiri ya maneno haya kwenda kiswahili:
- Inspirational
- Show
- Widow
- Widower
Natanguliza shukhrani~
QM, naomba kujaribu.
Maneno sahihi kwa maoni yangu kama vile ulivyo orodhesha ni:
1. hujasikia
2. istahili
3. yahitajiyo
4. unaipa
Tafsiri:
Inspirational - Yakutia mori/morali. Au kutia moyo, kuriwaza mtima.
Show - onyesha, jidai, funua, fichua, hadhara
Widow - mjane (mwanamke)
Widower - ....sijui
Widow - Is a female who lost her husband (mjane mwanamke)
Widower - I a man who lost his wife (mjane mwanaume)
Have a pleasant weekend.
Thanks Steve!
Hapo kwenye "Show" nilikuwa na maanisha term inayotumika kwenye vipindi vya Tv.
Mfano, Ze Comedy Show.
Hili neno la Show unalitafsiri vipi
Oh kwa hiyo wote wanaitwa wajane!
Asante
Wakuu, nimeulizwa ghafla na mtu ambaye hakijui vema kiswahili maana ya neno SHUBIRI kwani aliambiwa kuna dawa chungu kama shubiri hakuelewa shubiri ni nini kwa kiswahili wala kiingereza, binafsi nimechemsha!
Naweza kueleweshwa maana yake?
Nimeenda hapa sikupata msaada:
shubiri
Karibu.
Wote wanaitwa wajane isipokuwa katika kiswahili tumezoea kumwita mwanamke pekee ndio mjane. Ila katika kiingereza yote yapo na yanatumika sawa.
Nilisema hivi mkuu:Mkuu ushasema kuwa Shubiri ni dawa sasa unataka tafsiri gani tena?
Nimekuwa nasikia maneno haya lakini yananichanganya kujua matumizi yake sahihi.
Vukiza au fukiza?
Vundika au vumbika?
Compyuta?
Mtandao
ila
ingawa
msanii
puchu
mkwara
mwake
chuna
mbongo
Ninayo maneno lukuki lakini nashindwa kuyaainisha yote hapa. Naomba wataalam wa lugha hii adhimu mnisaidie nitoke niliko walau hatua moja mbele katika kujifunza Kiswahili.
Ahsanteni
Aloe vera is the English word for Shubiri.